Rev.Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,552
December 9 1961, Tanganyika ilipata Uhuru wake kutoka kwa Muingereza.
December 1963, Zanzibar ilipata Uhuru wake kutoka kwa Muingereza.
January 12 1964, Mapinduzi ya kuingoa Serikali ya Zanzibar iliyopata Uhuru kutoka kwa Muingereza December 1963 yalitokea.
April 26 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokea na kuundwa kwa Taifa au Nchi mpya, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
February 5 1977, vyama tawala vya Zanzibar ASP na Tanganyika (au kama inavyojulikana sasa Tanzania Bara) TANU viliungana na kuzaa CCM, Chama cha Mapinduzi ambacho kimfumo kina Makamu wawili, Makamu Bara na Makamu Zanzibar chini ya Mwenyekiti. Mgawanyo wa Uongozi na Uwakilishi ni nusu kwa nusu.
Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Zanzibar, alikuwa na Makamu wa Rais ambaye alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania Bara.
Mfumo wa Utawala na Urais unasema Raisi akitoka Bara, ni lazima makamu atokee Zanzibar, na Waziri Mkuu wa Muungano anatokea Bara. Mfumo huo huo unasema Rais wa Muungano akitokea Zanzibar, Makamu wa Rais lazima atokee Tanzania Bara na Waziri Mkuu atatokea ... hapa ni utata, baada ya mabadiliko ya kuondoa nafasi ya Makamu wa Rais kutoka Bara kuwa Waziri Mkuu, nafasi hii sijui kama itakuwa ni ya Zanzibar au itashinikizwa kuwa ya Bara.
Bunge la Muungano, linaongozwa na Serikali ambayo hujenga hoja na bajeti kwa manufaa ya Tanzania bara na hata pamoja na kuwa kuna uwakilishi kutoka Zanzibar, nafasi ya Spika na Naibu siku zote wamepewa Watanzania Bara na si Wazanzibari kwa kisingizio cha kuwepo kwa baraza la Wawakilishi na Serikali yao.
Uhuru tunaosherehekea December 9, ni Uhuru wa Tanganyika na si Uhuru wa Tanzania kwa kuwa Tanzania haijawahi kuwa Koloni na kudai Uhuru. Mbaya zaidi, haijawahi kutamkwa rasmi kuwa Tanganyika, ilibadilisha jina na kuitwa Tanzania Bara. Hivyo si sahihi kabisa kusema kuwa December 9 ni Uhuru wa Tanzania. Tanzania ilizaliwa April 26 1964, itakuwaje tushangilie miaka 47 ya Uhuru wa Tanzania huku ukweli ni Uhuru wa Tanganyika na si Tanzania
Hivyo basi, kuna ubatili mkubwa sana wa mfumo mzima wa Muungano, uendeshaji wa Serikali zetu na hata mazingira mazima yaliyoleta kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yaliinyang'anya haki ya Utaifa na Nchi Tanganyika na kuinyang'anya mamlaka ya Utawala Zanzibar.
Swali langu ni kwa nini wakati lile kundi la G55 ambalo lilipewa nguvu na ushawishi wa kidemokrasia na aliyekuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mzee wetu John Samuel Malecela, maarufu kama Tinga Tinga, lilikosa ushabiki kutoka kwa Watanganyika?
Kwa nini Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akipinga kuundwa na kurudishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya mfumo mzima wa Muungano ambao una Serikali kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?