Tuirudishe Tanganyika Kwanza - Kiini cha Suluhisho

Tuirudishe Tanganyika Kwanza - Kiini cha Suluhisho

rudi Baba yangu aiseee!! nimefundishwa sana historia yako tangu enzi za Kinjekitile Ngwale na akina dr.Fedrick Kyaruzi bila kumsahau Mr.Martin Kayamba wa Tanganyika Civil Servant Association miaka 1922,hata kabla ya Mwl.J.K Nyerere hajaitwa mwalimu,jinsi walivyojitoa ili kukupa uhuru baba yangu Tanganyika,lakini Nyerere pamoja na akina Kawawa na Kleist Sykes wakakamilisha kukupata muheshiwa,kwa sifa zao wakakuzika tena,daah!! pole sana Tanganyika,Mungu amekusikia naye amekufufua,najua sasa tutakusherekea kwa uhalisia,karibu sana Tanganyika,jina lako tu ni utajiri tosha,maana unajulikana kwa kutoa samaki na dagaa watamu wenye gharama.nakupa shikamoo kabla hujakuja.Godbless Tanganyika.
 
Zanzibar ni Nchi hili halina mjadala wala haja ya kupigishana makelele.Kwa mfano rahisi tu Nchi zinapoungana kila kitu huondoka nikimaanisha serikali na hata jina la Nchi ,sasa japo Nyerere alionekana mjanja lakini kwa hili alizidiwa ,yeye kwa ujuaji anaoujua mwenyewe alikubali kuiua Tanganyika na kuiwacha Zanzibar intact (Serikali yake ,majeshi yake).
Anaesema Zanzibar si Nchi huyo anajipendekeza kwa mafisadi ,ni bora ikadaiwa na kurudishwa Tanganyika ili mafisadi wasambaratishwe.
Karume alimzidi Nyerere akili, hilo halina ubishi.
 
Mchakato wa kuandika Katiba ya jamhuri ya muungano Usimamishwe!, Iitishwe kura ya maamuzi(referendum), Watanganyika waulizwe kama wanataka muungano na Wazanzibari na wapemba pia waulizwe kama wanautaka muuangano,majibu yake kama ilivyokuwa Cremea yatakuwa ndiyo msingi wa kujiuliza swali la pili ambalo ni muungano wa aina au muundo gani ndio hapo sasa tuandike katiba.matokeo ya (referendum) yakionyesha kukukataliwa kwa pande zote mbili za muungano BASI kila upande uchukue kilicho chake,wa baharini na aende baharini na mlima arudi mlimani.maana yake uvunjike huo muungano.sijui watu wanaoung'ang'ania wanataka kutuonyesha kitu gani.Nimewasikiliza akina Msekwa na wazee wengine waliokuwepo wakati huo,wote ni aibu tupu walishurutishwa tu hakukuwa na mtu wa kuhoji,walitumika tu kama rubber stamp.:A S 13:
 
Mimi bado ninatetea mfumo wa sasa kuwa ni sahihi kabisa na unaofaa. Hongera kwa walioubuni. Utaifa na Sovereignity haviondoki wala havifi. Hivyo Zanzibar haikupoteza utaifa wake wala sovereignity yake kwa kuingia Muungano. na Tanganyika haikupoteza vile vile vitu hivyo kwa kuingia Muungano. Hata jina halikupotea ila limebadilishwa matamshi tu, Kwani nahakika kuwa na wewe unaitaja kila mara Tanzania Bara (hiyo ndiyo Tanganyika) Aina ya Muungano unaopendeklza wewe haifai ukizingatia vitu unavyotaka kuunganisha Zanzibar na Tanganyika (ambapo Zanzibar kwa hali yoyote ile kieneo, ki-utajiri, ki rasilmali, ) si jui ni marangapi kwa Tanganyika. Aina hiyo yafaa labda pengine kwa Tanganyika na Kenya)Tatizo la Tanzania kwa hivi sasa ni la utekelezaji wa sura na muundo huu tuliouchagua. Na tuangalie mapungufu yaliyopo. Mfumo wa Serikali Tatu hauwafai Wazanzibari. Lakini hawataki kuangalia suala hili kwa undani. Wao mara nyingi huangalia upande wa haki zao tu (kuwa wakiwa katika Serikali tatu basi watazipata inavyostahili) Sawa. Lakini hawafikirii kuwa kuna haki na wajibu. Jee wajibu wao wataweza kuutekeleza vizuri katika mfumo huo wa Serikali tatu. Hilo Jeshi watashiriki vyema?. Watawapata wapi watu wa kuwaingiza Jeshini kulinda mipaka katika kiwango sawa na patner wao. Jee gharama za kukimu vitu hivyo vya pamoja watazipata wapi na kutoa kwa kiwango kinachitakiwa kiuuwiano. Hili suala wananchi tunahitaji taaluma ya kutosha. Wasomi tusaidieni.

Wewe ni kifuu, rais wako tu amekwambia kama znz inafursa nyingi sana ambazo ikiwa na mamlaka kamili inaweza ikajiendesha.

sasa unaleta porojo hapa
 
Mimi siku zote nimekuwa nikiwaza kwamba, kama ni suala la utaifa basi utaifa wa Tanganyika na utaifa wa Zanzibar urudi na kila mmoja abakie na sovereignty yake na Muungano uitwe wa United Republic of Tanganyika and Zanzibar.

Sasa kwanza itabidi katiba zote mbili zipitiwe upya na itungwe katiba mpya ya Muungano na ambayo ni ya sovereignty kwamba itaongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Pili Bunge litakuja kutokana na uongozi wa katiba hiyo na bunge hili Parliament Sovereignty litakuwa na maamuzi yanayohusu sovereignty ya Muungano bila kuathiri bunge la taifa la Zanzibar ambalo hupanga mambo ya Zanzibar tu.

Pia hili bunge la Muungano lilasimamia mambo yote ya msingi likiwemo la foreign policy ambayo ziku zote ni la Sovereign state na sio nation tu.

Ikiwa hivyo basi, hata pasi za kusafiria zibadilishwe na ijulikane hata kule UN na duniani kote kwamba sasa kuna United Republic of Tanganyika na Zanzibar kama "sovereign state".

Pia suala la Muungano litakuwepo kwa basis ya mataifa haya mawili ku-share bahari, bandari, jeshi na polisi.

Kwa kuwa tatizo la kubinywa lipo Zanzibar basi iachiwe baraza lake la wawakilishi ili litoe maamuzi ya taifa la Zanzibar kuhusu maendeleo yake yakiwemo yale ambayo yanaguza kitu kinachoitwa Muungano kama sera ya mambo ya nje.

Huo ndo mtazamo wangu.

Umechambua vizur lakin kitu cha kubaki kwenye serikal ya Muungano ni ulinzi na uraia tu.kama umoja wa kiarabu.
 
Je Zanzibar ni Nchi au si Nchi?

Na. M. M. Mwanakijiji

Nadhani hapa mgogoro wa lugha si wa lazima kabisa.

a. Zanzibar si nchi kwa maania ya sovereign State kama vile Tanzania Bara si nchi. Kuna nchi moja nayo inaitwa TAnzania (ambayo nguvu na mamlaka ya sovereignty yamo).

b. Hii haina maana kuwa huko nyuma Zanzibar haikuwahi kuwa nchi, ndiyo iliwahi kama vile Tanganyika ilivyowahi kuwa nchi. Hili halina ubishi. Zilipokuwa nchi hizi mbili zilikuwa na madaraka sawa ya nchi na uwezo sawa kama nchi. Nguvu hizi za nchi unaweza kuzisoma vizuri katika Azimio la Uhuru la Marekani la 1776.

c. Zanzibar hata hivyo ni Taifa (Nation, State). Mara nyingi tumekuwa tukizungumzia Nations kwa maana ya nchi lakini hasa nation ina maana ya watu wenye historia yao inayowajumuisha pamoja na kuwatofautisha na jamii nyingine. Na ndipo hapa hata neno "State" linapokuja.

Kuna kitu kinaitwa "Arab Nation", huu ni mfano mzuri wa kitu ambacho kinakubalika kuwepo lakini si nchi iliyopo. NI jamii ya watu. Na ni katika maana hii utakuta majimbo ya Marekani kwa mfano ya Magavana wake, Mahakama zake (hadi za Juu) na Majeshi yake (yanayoitwa National Guards).

d. Hivyo Zanzibar ni Taifa kwa maana hii ya pili, kwamba walipopoteza nchi yao kwa kuungana na Tanganyika hawakupoteza utaifa (Statehood with limited sovereignty). Hivyo ndio maana wakaendelea kuwa na Rais, Mahakama, Jeshi (KMKM) na Baraza lao la Kutunga Sheria. Kuwepo kwa vitu hivi hakunamaana Zanzibar kama nchi imerudishwa.

e. Hivyo basi ukiangalia sana utaona kuwa baada ya kuungana mambo makubwa mawili yalitokea ambayo ni kiini kwa kiasi kikubwa cha matatizo tuliyonayo katika Muungano:

Kwanza, Tanganyika ilipoteza nchi na ikapoteza Taifa. Hivyo hakuna nchi ya Tanganyika kama vile hakuna nchi ya Zanzibar, lakini pia hakuna Taifa la Watanganyika ingawa lipo Taifa la Wazanzibar.

Pili, Upande wa Tanganyika ambao walipoteza nchi na taifa lao wao wakavishwa hiki tunachokiita Muungano. Sasa tatizo la Muungano ulivyo sasa ni kama walivyosema ni kama "koti". Sasa koti linatakiwa kuvaliwa na mikono miwili ili likae vyema.

Wakati Zanzibar limeingiza mkono wake sawasawa upande mmoja, Bara inataka kuvaa mkono wake inakatazwa inaambia litundike shingoni tu lakini wakati huo huo mkono mmoja unaweza kuingia hadi katika ule wa Zanzibar na hivyo kunatokea hali ya kubanana. Zanzibar inasema "unanichukulia upande wangu" na bara wanasema "sasa mbona mimi nakatazwa hata kuingiza mkono uliowazi upande wangu?

Hivyo utaona basi koti halijavaliwa sawasawa na hivyo hata kutembea inakuwa matatizo. Hiki ndicho kinachoitwa kero za Muungano.

e. Hizi kero za Muungano zinaonekana sasa kwenye maneno. Zanzibar ni nchi au si nchi? Hili siyo swali sahihi! Swali linapaswa kuwa je katika mfumo wetu huu wa sasa Zanzibar na Bara bado ni nchi na zina utaifa wao? Jibu nimeshalitoa hapo juu.

Ni kwa sababu hiyo, basi utaona kati ya vitu vya kwanza ambavyo vinaweza kufanyika bila kuleta madhara makubwa ni kurudishwa kwa jina la Tanganyika kuelezea Tanzania bara, na hivyo kurudisha Utaifa wa bara japo kuwa haturudishi nchi.

Bara ikishakuwa na utaifa wake tunawarudishia limited sovereignty kwa kuamua kuwa Waziri Mkuu anakuwa ni Waziri Mkuu wa Bara ambaye ni mtendaji. Yaani anapigiwa kura kama kawaida. Tukishafanya hivyo, Bara na wenyewe wanaunda Baraza lao la Wawakilishi na kuwa na mfumo wao wa mahakama, na hili linafanyika kwa kutengeneza parallel judicial system ambapo una State Judiciary kama ilivyo Zanzibar lakini unapia Union Judiciary.

Katika kufanya hivi vyote Serikali ya Muungano bado inakuwa ndiyo sovereign. Sasa mtu anaweza akafikiri nilichosema ni serikali tatu. Hapana, nilichoonesha ni kuendelea na mfumo ule ule wa serikali mbili kwa maana unaserikali ya State na serikali ya Union.

Mahusiano kati ya hizi States mbili (Zanzibar na Tanganyika) yanakuwa katika misingi ya mahusiano ya kidugu ambapo uraia hauko wa Zanzibar au Tanganyika bali wa Tanzania lakini wananchi wake wanaweza kuendelea kujiita Wazanzibari au Watanganyika bila haja ya kujisikia wanausaliti Muungano.

Bila ya shaka utaona vinafanana sana na mfumo wa Marekani. Ndiyo kwa sababu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafanana zaidi na Muungano wa Marekani kuliko nchi nyingine nyingi, kwani States za Marekani zilipokuja kukaa chini na kuungana zile Original 13 zilikuwa ni nchi kamili. Ndiyo maana hata wakati mwingine tunapoyaita "majimbo" ya Marekani siyo tafsiri sahihi, kwani siyo Provinces kama za Afrika ya Kusini bali ni "States" ndani ya Muungano wao, na kila siku tangu waungane wamekuwa wakishughulika kuimarisha.

Naamini na sisi tunaweza kuumirisha muungano wetu kwa njia nyepesi na Rais, hasa tukianza na hili la kurudisha jina la Tanganyika kwanza, na kumrudisha Waziri Mkuu wa Tanganyika na Baraza lake la Mawaziri na Baraza la Wawakilishi.


NB: NImeandika nikiwa namjibu mtu kwa hiyo kuna mambo ambayo nikiamka bila ya shaka nitapanua kidogo, kuyafafanua na kuyaendeleleza. huu ni mwanzo tu.
Hizi hoja sijui kwanini hazifiii...
 
Wanaweza kuichelewesha, lakini hawataweza kuimimya milele haki ya Tanganyika kutambulika kuwa ni nchi.
 
Back
Top Bottom