Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,370
- 39,186
Je Zanzibar ni Nchi au si Nchi?
Na. M. M. Mwanakijiji
Nadhani hapa mgogoro wa lugha si wa lazima kabisa.
a. Zanzibar si nchi kwa maania ya sovereign State kama vile Tanzania Bara si nchi. Kuna nchi moja nayo inaitwa TAnzania (ambayo nguvu na mamlaka ya sovereignty yamo).
b. Hii haina maana kuwa huko nyuma Zanzibar haikuwahi kuwa nchi, ndiyo iliwahi kama vile Tanganyika ilivyowahi kuwa nchi. Hili halina ubishi. Zilipokuwa nchi hizi mbili zilikuwa na madaraka sawa ya nchi na uwezo sawa kama nchi. Nguvu hizi za nchi unaweza kuzisoma vizuri katika Azimio la Uhuru la Marekani la 1776.
c. Zanzibar hata hivyo ni Taifa (Nation, State). Mara nyingi tumekuwa tukizungumzia Nations kwa maana ya nchi lakini hasa nation ina maana ya watu wenye historia yao inayowajumuisha pamoja na kuwatofautisha na jamii nyingine. Na ndipo hapa hata neno "State" linapokuja.
Kuna kitu kinaitwa "Arab Nation", huu ni mfano mzuri wa kitu ambacho kinakubalika kuwepo lakini si nchi iliyopo. NI jamii ya watu. Na ni katika maana hii utakuta majimbo ya Marekani kwa mfano ya Magavana wake, Mahakama zake (hadi za Juu) na Majeshi yake (yanayoitwa National Guards).
d. Hivyo Zanzibar ni Taifa kwa maana hii ya pili, kwamba walipopoteza nchi yao kwa kuungana na Tanganyika hawakupoteza utaifa (Statehood with limited sovereignty). Hivyo ndio maana wakaendelea kuwa na Rais, Mahakama, Jeshi (KMKM) na Baraza lao la Kutunga Sheria. Kuwepo kwa vitu hivi hakunamaana Zanzibar kama nchi imerudishwa.
e. Hivyo basi ukiangalia sana utaona kuwa baada ya kuungana mambo makubwa mawili yalitokea ambayo ni kiini kwa kiasi kikubwa cha matatizo tuliyonayo katika Muungano:
Kwanza, Tanganyika ilipoteza nchi na ikapoteza Taifa. Hivyo hakuna nchi ya Tanganyika kama vile hakuna nchi ya Zanzibar, lakini pia hakuna Taifa la Watanganyika ingawa lipo Taifa la Wazanzibar.
Pili, Upande wa Tanganyika ambao walipoteza nchi na taifa lao wao wakavishwa hiki tunachokiita Muungano. Sasa tatizo la Muungano ulivyo sasa ni kama walivyosema ni kama "koti". Sasa koti linatakiwa kuvaliwa na mikono miwili ili likae vyema.
Wakati Zanzibar limeingiza mkono wake sawasawa upande mmoja, Bara inataka kuvaa mkono wake inakatazwa inaambia litundike shingoni tu lakini wakati huo huo mkono mmoja unaweza kuingia hadi katika ule wa Zanzibar na hivyo kunatokea hali ya kubanana. Zanzibar inasema "unanichukulia upande wangu" na bara wanasema "sasa mbona mimi nakatazwa hata kuingiza mkono uliowazi upande wangu?
Hivyo utaona basi koti halijavaliwa sawasawa na hivyo hata kutembea inakuwa matatizo. Hiki ndicho kinachoitwa kero za Muungano.
e. Hizi kero za Muungano zinaonekana sasa kwenye maneno. Zanzibar ni nchi au si nchi? Hili siyo swali sahihi! Swali linapaswa kuwa je katika mfumo wetu huu wa sasa Zanzibar na Bara bado ni nchi na zina utaifa wao? Jibu nimeshalitoa hapo juu.
Ni kwa sababu hiyo, basi utaona kati ya vitu vya kwanza ambavyo vinaweza kufanyika bila kuleta madhara makubwa ni kurudishwa kwa jina la Tanganyika kuelezea Tanzania bara, na hivyo kurudisha Utaifa wa bara japo kuwa haturudishi nchi.
Bara ikishakuwa na utaifa wake tunawarudishia limited sovereignty kwa kuamua kuwa Waziri Mkuu anakuwa ni Waziri Mkuu wa Bara ambaye ni mtendaji. Yaani anapigiwa kura kama kawaida. Tukishafanya hivyo, Bara na wenyewe wanaunda Baraza lao la Wawakilishi na kuwa na mfumo wao wa mahakama, na hili linafanyika kwa kutengeneza parallel judicial system ambapo una State Judiciary kama ilivyo Zanzibar lakini unapia Union Judiciary.
Katika kufanya hivi vyote Serikali ya Muungano bado inakuwa ndiyo sovereign. Sasa mtu anaweza akafikiri nilichosema ni serikali tatu. Hapana, nilichoonesha ni kuendelea na mfumo ule ule wa serikali mbili kwa maana unaserikali ya State na serikali ya Union.
Mahusiano kati ya hizi States mbili (Zanzibar na Tanganyika) yanakuwa katika misingi ya mahusiano ya kidugu ambapo uraia hauko wa Zanzibar au Tanganyika bali wa Tanzania lakini wananchi wake wanaweza kuendelea kujiita Wazanzibari au Watanganyika bila haja ya kujisikia wanausaliti Muungano.
Bila ya shaka utaona vinafanana sana na mfumo wa Marekani. Ndiyo kwa sababu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafanana zaidi na Muungano wa Marekani kuliko nchi nyingine nyingi, kwani States za Marekani zilipokuja kukaa chini na kuungana zile Original 13 zilikuwa ni nchi kamili. Ndiyo maana hata wakati mwingine tunapoyaita "majimbo" ya Marekani siyo tafsiri sahihi, kwani siyo Provinces kama za Afrika ya Kusini bali ni "States" ndani ya Muungano wao, na kila siku tangu waungane wamekuwa wakishughulika kuimarisha.
Naamini na sisi tunaweza kuumirisha muungano wetu kwa njia nyepesi na Rais, hasa tukianza na hili la kurudisha jina la Tanganyika kwanza, na kumrudisha Waziri Mkuu wa Tanganyika na Baraza lake la Mawaziri na Baraza la Wawakilishi.
NB: NImeandika nikiwa namjibu mtu kwa hiyo kuna mambo ambayo nikiamka bila ya shaka nitapanua kidogo, kuyafafanua na kuyaendeleleza. huu ni mwanzo tu.