Tuige hii desturi ya wachaga

Mimi ni Mkuria,Baba yangu alishaniambia ukienda mahali popote hapa Tz ukimkosa mchaga ni siishi hilo eneo halifai.

Mie Watoto wangu niliwaambia ukiingia Course yoyote Chuo ukaona hiyo Course haina Mtoto wa Kichaga omba kubadilisha!
 
~~~>>>Arusha ni ya Wameru na Wamasai....... Je umezunguka Arusha nzima na kila kijiwe unauliza unaowakuta makabila yao¿??

Nenda Ungalimited, Sanawari, Barabara ya İlboru n.k hivi ni Vijiwe vichache.... Kawaulize makabila yao.

[HASHTAG]#Rombo[/HASHTAG] wanaongoza kwa mali za Ushirikina.... Fika pale Tarakea kiongozi wao ni jamaa mmoja anaitwa Maulidi
 
Utakufa hivyo hivyo na roho yako ya kwanini...mpuuzy mkubwa wewe!
 
Mtawananga Wachaga mseme wezi na wachawi lakini ukweli ni wachapa kazi. Kwanza hakuna mchawi tajiri. Na kama Wachaga wezi mbona vyombo vya dola havijawakamata? Kama kweli ni wezi lakini hawakamatiki basi waongezee sifa ingine kwamba wana akili sana kiasi kwamba hata wanaweza kukwepa vyombo vya dola. Lazima mkubali. Huku duniani kuna makabila/mataifa ambao ni wachapa kazi kuliko wenzao. Waisraeli hata muwasemeje wako juu tu kibiashara, na kiakili kulinganisha na wazungu wengine. Wewe utasema Wahaya sio wasomi (japo wana dharau ubaguzi na maringo)? Kuna ukweli ambao lazima uukubali. Wakikuyu wamewazidi Wakenya wenzao kwa uchacharikaji kibiashara na kielimu. Na Wachaga hivyo hivyo kwa upande wa Tanzania

We huoni Kenya wanasonga mbele hatuwapati kiuchumi wao ni developing country na sisi ni least developing country. Wakikuyu walishika madaraka kwanza, hata kama anajua kuiba ila anajua kuzitafuta. Tofauti na wengine wanajua kuiba tu, biashara hawajui, uvivu na madoido yasiyo na kichwa wala miguu. Yaani kwa ujumla wakipata wa naona hakuna kufa.
 
Andiko reeefu kumbe pumba tupu,
wewe wachaga huwajui unawasikia tu.
Wachaga ni wezi
wachaga majambazi
wachaga washirikina,hayo mabiashara yao ni uchawi mtupu.
NENDA kule kwao Romba kila nyumba kuna mtoto taahira ndani.
Wewe ndio taahira kwani huwajua wachaga
 
MTOTO WA KICHAGAA AKIWA NA PESA .... BABA YAKE ANAMWAMKIA " SHIKAMOO MTOTO" HAHAHAHAHAHHAA
 
ELIMU, KUFANYA KAZI, ADABU, HAWAJUI UCHAWI, UBINAFSI...UMEWASAIDI SANA WACHAGGA..
KIKUBWA TEAM WORK NDIO SIRI KUBWA KWAO
 
1691823731319.png
 
Mwaka jana nilibahatika kwenda Arusha kikazi ambako nililazimika kukaa kwa muda wa majuma mawili. Kuna mambo ya maana nimejifunza kutoka kwa kabila la wachaga, ambayo kama watanzania tukiyatilia maanani, yanaweza kutuletea maendeleo kwa haraka.

Katika pitapita zangu sikuwahi kuwaona wachaga wakiwa wamekaa kwenye vijiwe au vikundi vya kupiga sogakila mtu yupo serious na kazi au shughuli inayomuingizia kipato. Kuna baa moja maarufu ambayo nilipenda kwenda kula chakula ambako pia nilijifunza jambo kuhusu kabila hili. Sikuweza kuwakuta wachaga wakilewa ovyo kama watu wa makabila mengine. Mchaga akitoka kazini hupitia baa na kunywa bia zake 2 au 3 na kisha huondoka kwenda nyumbani kujipumzisha ili kesho awahi kazini kwake kuchapa kazi bila kuathiriwa na mninginio (hangover) wa ulevi. Wachaga huwa hawakeshi kwenye mabaa wakilewa chakali. Hawana utamaduni huo hata kidogo.

Aidha, wachaga ni watu ambao wanaheshimu sana kazi. Kazi wanayoiweza na ambayo imewapa sifa sana ni biashara. Sote ni mashahidi jinsi ambavyo watu wa kabila hili wametapakaa nchi nzima wakifanya shuguli za biashara kuanzaia ya duka (Dukani kwa Mangi) hadi biashara kubwa kabisa. Hakuna mtaa katika nchi hii ambako utakosa duka la Mangi. Nadhani mazingira ya mikoa wanayotoka (Arusha & Kilimanjaro) inachangia sana kuwafanya wawe wajasiriamali na watafuta mali/utajiri. Katika mikoa hii, hakuna ardhi ya kutosha kuendesha shughuli za kilimo. Hivyo, inawalazimu kuwa wajasiriamali moja kwa moja tangu wakiwa na umri mdogo.

Wazazi wa kichaga huwarithisha watoto wao ELIMU badala ya ARDHI (ambayo hawana). Mzazi akishamsomesha mwanae hadi akahitimu chuo au kozi fulani, ndio nitolee. Usitegemee kwamba atakupa urithi mwingine zaidi ya huo hata kama ana utajiri wa kutishasahau kabisa! Hili nalo linasaidia kuwafanya watoto wa kichaga wasome kwa bidii na kufaulu vizuri. Ushahidi wa hili ni kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa. Mara nyingi mikoa ya Arusha na Kilimanjaro hufanya vizuri kila mwaka. Ndio maana wachaga wengi hushiikilia nafasi za juu serikalini na katika sekta muhimu hapa nchini. Sio kwamba wanapendelewa au kupendeleana kikabila bali inatokana na juhudi zao za kusaka elimu na maendeleao kwa bidii zao zote.

Ikiwa kila mtanzania akiiga utamaduni huu wa wachaga ni wazi kwamba nchi hii itapata maendeleo haraka kuliko tunavyotarajia. Kwa bahati mbaya makabila mengine wanaweza sana kujikweza na kujisifu (Wahaya), kukatana mapanga na kupigana vita (Wakurya), kucheza ngoma na bao (Wakwere, Wadengereko na Wakwere na baadhi ya makbila ya pwani), kujinyonga (watani zangu Wahehe), kula chamaki nchanga na (watani zangu Wamakonde na Wahehe), n.k.

Utamaduni huu wa maendeleo kutoka kwa watani zangu wachaga nimeupenda sana na ningeomba kila mtanganyika mpenda maendeleo auige.

Nawasilisha.
:yield:
Mimi ni Mchaga, hili taifa lina tatizo la mila na desturi zinazoturudisha nyuma. Ili tufike mbali inabidi tuamke na tusisubirie msaada kutoka nje. Huku uchagani kuna umoja na kuna tough love. Yaani kuna mapenzi au upendo wa kuchanana ukweli. Ndugu yako wa damu atakufanya uhenyeke ili uijue kazi. Lakini ukishajua A to Z ndo unakuja kuelewa alimaanisha nini. Aisee changamoto nilizopitia kwenye kujitafuta kuna muda niliona ndugu zangu hawafai . Vijana wengi wa kizazi cha leo wasingevumilia. Lakini walikuwa wananifundisha maisha. Kuna makabila unakuta kijana anahudumiwa hela mpaka miaka 35. Pia unakuta kijana baba yake anaongeza mke na hana kazi wala uchumi wa kumudu maamuzi yake. Na kijana anahudumia hiyo familia na anatuma hela nyumbani. Ila kwa mwaka huu 2023 naona baadhi ya watu wamefunguka kiakili na wameamka. Huku uchagani kuna kuchanana live haijalishi umri. Hiyo kitu inasaidia sana .
 
Kweli kabisa mkuu. Wachaga nawakubali sana. big p!
 
Andiko reeefu kumbe pumba tupu,
wewe wachaga huwajui unawasikia tu.
Wachaga ni wezi
wachaga majambazi
wachaga washirikina,hayo mabiashara yao ni uchawi mtupu.
NENDA kule kwao Romba kila nyumba kuna mtoto taahira ndani.
Roho mbaya hiyo. Unawaonea wivu tu huna lolote.
 
Mimi ni Mchaga, hili taifa lina tatizo la mila na desturi zinazoturudisha nyuma. Ili tufike mbali inabidi tuamke na tusisubirie msaada kutoka nje. Huku uchagani kuna umoja na kuna tough love. Yaani kuna mapenzi au upendo wa kuchanana ukweli. Ndugu yako wa damu atakufanya uhenyeke ili uijue kazi. Lakini ukishajua A to Z ndo unakuja kuelewa alimaanisha nini. Aisee changamoto nilizopitia kwenye kujitafuta kuna muda niliona ndugu zangu hawafai . Vijana wengi wa kizazi cha leo wasingevumilia. Lakini walikuwa wananifundisha maisha. Kuna makabila unakuta kijana anahudumiwa hela mpaka miaka 35. Pia unakuta kijana baba yake anaongeza mke na hana kazi wala uchumi wa kumudu maamuzi yake. Na kijana anahudumia hiyo familia na anatuma hela nyumbani. Ila kwa mwaka huu 2023 naona baadhi ya watu wamefunguka kiakili na wameamka. Huku uchagani kuna kuchanana live haijalishi umri. Hiyo kitu inasaidia sana .
Mkuu umeongea ukweli tupu. Kuna Mangi mmoja tulimaliza nsye chuo kimoja. Wakati sisi tunarudi kwa wazazi wetu, yeye akawa anafungasha virago vyake kwenda kuanza maisha ya kujitegemea. Baba wa kichaga akishakusonesha tu, amemaliza kazi. Usitegemee urithi wowote kutoka kwake zaidi ya hiyo elimu aliyokusomesha.
 
Back
Top Bottom