Tuige hii desturi ya wachaga

Tatizo la watanzania wengi ni kwamba wako incomptent na ndiyo maana kila mmoja analilia kuajiliwa serikalini ili asiwe anafanya kazi bali awe analipwa kwa kupiga domo tu na kuto onekana kazini. Yaani utakuta mtu kaajiliwa serikalini, asubuhi anakwenda kazini kusign kuwa yupo kazini, baada ya saa moja anarudi nyumbani kwenda kuuza vitumbua na mwisho wa mwezi analipwa mshahara as mfanya kazi wa serikali. Nimeshuhudia pale wizara ya mambo ya ndani, utakuta umepewa ahadi na fulani umfuate kesho muda wa kazi, yaani asubuhi. Utakwenda pale an hour before na utakaa mpaka jioni jamaa hatokei, ukirudi mitaani unamkuta yuko restaurant na wahindi pamoja na wasomali wakimhonga kuwapa passport. Ila to hell with wachagga, I will never copy them....I am competent and they (wachagga) need to copy me ili wajifunze mawii matatu.
 
Andiko reeefu kumbe pumba tupu,
wewe wachaga huwajui unawasikia tu.
Wachaga ni wezi
wachaga majambazi
wachaga washirikina,hayo mabiashara yao ni uchawi mtupu.
NENDA kule kwao Romba kila nyumba kuna mtoto taahira ndani.
Acha usengerema wewe nyie ndo wale watoto wa kiswahili mnabaki kusema wachaga wachawi.wezi. uku tunazidi kuwaamisha mjini na uko mnako amia baada miaka tunakuja kiwanunua pia kama amtafanya kazi
Kaua mchawi au mwizi na wewe ili ufanikiwe acha mboyoyo za k.....a
 
Rejea somo ulilofundishwa linalohusiana na "DIVISION OF LABOUR". Shoe shine nao wana umuhimu wake katika uchumi wa Taifa letu. Mtu huyu unayemdharau anapata kipato cha kujikimu yeye, familia yake na wazazi wake aliowaacha kule kijijini; na kwa taarifa yako habari sahihi kule kijijini kuwa fulani yuko DSM ni mfanya biashara.

Kama anaingiza TZS 20,000 kwa siku wewe unadhani mfanyakazi wa Urafiki mwenye Diploma anapata kipato hicho kwa siku?
Hii field sio division of Labour ni division of tribe wewe,mbona kazi nyimgine hufanywa na watu wa makabila mbalimbali,zaidi ya hiko kimgine mlichokuwa nacho ni kubebana tu.hamna lolote.
 
Hii field sio division of Labour ni division of tribe wewe,mbona kazi nyimgine hufanywa na watu wa makabila mbalimbali,zaidi ya hiko kimgine mlichokuwa nacho ni kubebana tu.hamna lolote.
sema usemavyo lakini huyo unayemdharau analisha familia yake, anatoa msaada kwa wazazi wake na chanzo kikubwa cha habari kwa wapenda vijiwe kama wewe
 
sema usemavyo lakini huyo unayemdharau analisha familia yake, anatoa msaada kwa wazazi wake na chanzo kikubwa cha habari kwa wapenda vijiwe kama wewe
Hata kobe anafamilia na anailisha, ije kuwa shoe shiner mangi.
 
Andiko reeefu kumbe pumba tupu,
wewe wachaga huwajui unawasikia tu.
Wachaga ni wezi
wachaga majambazi
wachaga washirikina,hayo mabiashara yao ni uchawi mtupu.
NENDA kule kwao Romba kila nyumba kuna mtoto taahira ndani.
Mkuu ni maarifa na kujituma tu,hamna muujiza hapo,kama mchaga,"ubepari & maslahi ya SHILINGI ni KIPAUMBELE CHA KWANZA",Pale tu jua linapokucha...ndio ukweli hapo
 
Andiko reeefu kumbe pumba tupu,
wewe wachaga huwajui unawasikia tu.
Wachaga ni wezi
wachaga majambazi
wachaga washirikina,hayo mabiashara yao ni uchawi mtupu.
NENDA kule kwao Romba kila nyumba kuna mtoto taahira ndani.

Si kwel wachaga wapambanaji sana

Acha akili za kijinga ndugu, huo uchawi huko kwenu sumbawanga, bagamoyo, ukerewe, mbozi, Dodoma, au musoma haupo?
We kalia kupiga domo na kuoa wanawake 4 na kuzaa lundo la watoto halafu usichape kazi uone kama utatajirika.
Utabaki kulia lia na kusema wachaga wachawi sijui wezi wenzako wanapiga kazi mwanzo mwisho na kusonga mbele.
Kwa taarifa yako hakuna mchawi tajiri, sasa jipime mwenyewe nani mchawi kati yako na mchaga..
 
kweli ukiona sehemu mchaga hana mzuka nayo au biashara jifikirie Mara mbili ujipange upya sasa wew kakae sehemu kuna watu wa kigoma, pwani, lingo, mtwara, tanga uone
 
Mtawananga Wachaga mseme wezi na wachawi lakini ukweli ni wachapa kazi. Kwanza hakuna mchawi tajiri. Na kama Wachaga wezi mbona vyombo vya dola havijawakamata? Kama kweli ni wezi lakini hawakamatiki basi waongezee sifa ingine kwamba wana akili sana kiasi kwamba hata wanaweza kukwepa vyombo vya dola. Lazima mkubali. Huku duniani kuna makabila/mataifa ambao ni wachapa kazi kuliko wenzao. Waisraeli hata muwasemeje wako juu tu kibiashara, na kiakili kulinganisha na wazungu wengine. Wewe utasema Wahaya sio wasomi (japo wana dharau ubaguzi na maringo)? Kuna ukweli ambao lazima uukubali. Wakikuyu wamewazidi Wakenya wenzao kwa uchacharikaji kibiashara na kielimu. Na Wachaga hivyo hivyo kwa upande wa Tanzania
 
Andiko reeefu kumbe pumba tupu,
wewe wachaga huwajui unawasikia tu.
Wachaga ni wezi
wachaga majambazi
wachaga washirikina,hayo mabiashara yao ni uchawi mtupu.
NENDA kule kwao Romba kila nyumba kuna mtoto taahira ndani.
n jambo la ajab san kupinga hoja kwa chuki binafs

n sawa na kusema diamond freemason wakt umemfollow insta
 
Mwaka jana nilibahatika kwenda Arusha kikazi ambako nililazimika kukaa kwa muda wa majuma mawili. Kuna mambo ya maana nimejifunza kutoka kwa kabila la wachaga, ambayo kama watanzania tukiyatilia maanani, yanaweza kutuletea maendeleo kwa haraka.

Katika pitapita zangu sikuwahi kuwaona wachaga wakiwa wamekaa kwenye vijiwe au vikundi vya kupiga soga—kila mtu yupo serious na kazi au shughuli inayomuingizia kipato. Kuna baa moja maarufu ambayo nilipenda kwenda kula chakula ambako pia nilijifunza jambo kuhusu kabila hili. Sikuweza kuwakuta wachaga wakilewa ovyo kama watu wa makabila mengine. Mchaga akitoka kazini hupitia baa na kunywa bia zake 2 au 3 na kisha huondoka kwenda nyumbani kujipumzisha ili kesho awahi kazini kwake kuchapa kazi bila kuathiriwa na mning’inio (hangover) wa ulevi. Wachaga huwa hawakeshi kwenye mabaa wakilewa chakali. Hawana utamaduni huo hata kidogo.

Aidha, wachaga ni watu ambao wanaheshimu sana kazi. Kazi wanayoiweza na ambayo imewapa sifa sana ni biashara. Sote ni mashahidi jinsi ambavyo watu wa kabila hili wametapakaa nchi nzima wakifanya shuguli za biashara kuanzaia ya duka (Dukani kwa Mangi) hadi biashara kubwa kabisa. Hakuna mtaa katika nchi hii ambako utakosa duka la Mangi. Nadhani mazingira ya mikoa wanayotoka (Arusha & Kilimanjaro) inachangia sana kuwafanya wawe wajasiriamali na watafuta mali/utajiri. Katika mikoa hii, hakuna ardhi ya kutosha kuendesha shughuli za kilimo. Hivyo, inawalazimu kuwa wajasiriamali moja kwa moja tangu wakiwa na umri mdogo.

Wazazi wa kichaga huwarithisha watoto wao ELIMU badala ya ARDHI (ambayo hawana). Mzazi akishamsomesha mwanae hadi akahitimu chuo au kozi fulani, ndio nitolee. Usitegemee kwamba atakupa urithi mwingine zaidi ya huo hata kama ana utajiri wa kutisha—sahau kabisa! Hili nalo linasaidia kuwafanya watoto wa kichaga wasome kwa bidii na kufaulu vizuri. Ushahidi wa hili ni kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa. Mara nyingi mikoa ya Arusha na Kilimanjaro hufanya vizuri kila mwaka. Ndio maana wachaga wengi hushiikilia nafasi za juu serikalini na katika sekta muhimu hapa nchini. Sio kwamba wanapendelewa au kupendeleana kikabila bali inatokana na juhudi zao za kusaka elimu na maendeleao kwa bidii zao zote.

Ikiwa kila mtanzania akiiga utamaduni huu wa wachaga ni wazi kwamba nchi hii itapata maendeleo haraka kuliko tunavyotarajia. Kwa bahati mbaya makabila mengine wanaweza sana kujikweza na kujisifu (Wahaya), kukatana mapanga na kupigana vita (Wakurya), kucheza ngoma na bao (Wakwere, Wadengereko na Wakwere na baadhi ya makbila ya pwani), kujinyonga (watani zangu Wahehe), kula chamaki nchanga na (watani zangu Wamakonde na Wahehe), n.k.

Utamaduni huu wa maendeleo kutoka kwa watani zangu wachaga nimeupenda sana na ningeomba kila mtanganyika mpenda maendeleo auige.

Nawasilisha.
:yield:
Big up
 
Back
Top Bottom