Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Kitendo aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Michael Retzer cha kupitia mtandao wa Wikileaks, kumtuhumu Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa amehongwa pair 5 za Suti za Savile Row, sio tuu ni cha udhalilishaji wa hali ya juu kwa mkuu wetu wa nchi, bali pia ni matukano kwa Watanzania kwa ujumla wetu kwani Rais wetu ni kama baba wa familia kwenye nyumba yetu, hawezi baba yetu kudhalilishwa sisi watoto ambao tunaishi kwenye nyumba hii tukakaa kimya.
Kukanusha peke yake hakutoshi, hoja kuwa kwa vile Ikulu inafungu la kunvisha rais, sio defence kuwa hawezi kuhongwa suti, haswa ukizingatia suti zenyewe sio suti tuu ili mradi ni suti, suti zenyewe ni Savile!. Tunataka Marekani imuombe radhi rais Kikwete na Watanzania kwa ujumla kwa kadhia hii ya Wikileaks.
Mara baada ya JF kutundika bandiko la kadhia hii, Ikulu ilikurupuka kutoa taarifa ya kukanusha. Nimesema Ikulu ilikurupuka kukanusha vipengele vya rushwa tuu kwa kukanusha yaliyonukuliwa na JF badala ya kuifuata ile link na kuyakanusha yote yanayohusiana na Tanzania.
Kwa vile source mama ipo na tuhuma zinazidi kushuka kila kukicha, ilikuwa ni busara kwa Ikulu kukanusha yote in details once and forall, hivyo na tusubiri kuona ni mangapi yatakayofuatia, Ikulu itakuwa inasafisha kila kukicha!.
Mengi yaliyokanushwa na Ikulu, sio yale ya Wiki leaks, bali ya Wiki Leaks yaliyoandikwa JF. Kufuatia kanusho hilo, yule mtoa taarifa kwa Balozi wa Marekani, Bi. Lisa Pile, naye ametumiwa sio taarifa ya Wiklleaks, bali ametumiwa ile thread ya JF ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Matokeo yake, Bi. Pile anakanusha kuwa yeye hajui Kiswahili na wala hakuwahi kukutana na JK hivyo wanamsingizia.
Ilitakiwa huyu Bi Lisa atumiwe ile link ya WikiLeaks na sio hiyo ya JF waliomtumia. Alitakiwa akanushe kukutana na balozi wa Marekani au akiri walikutana na Michael Retzer lakini akanushe hakumwambia kile balozi huyo alichoripoti nchini kwao ambacho ndicho kilichonukuliwa na Wikileaks ili tujue Balozi Michael Retzer ndie muongo wetu hivyo kutupa haki Tanzania kuombwa radhi na JK kutendewa haki sio tuu kwa kuombwa radhi, bali pia hata kufidiwa kwa madhara aliyoyapata kwa kuchafuliwa reputation yake.
Badala ya kukanusha kilichoandikwa na Wikileaks yaani alichoongea na Balozi wa Marekani, hiyu bibie amekanusha hajui Kiswahili na hajawahi kukutana na rais Kikwete wala rais yoyote. Nani kamwambia bibi huyu kuwa kaongea Kiswahili au kakutana na JK?.
Hebu soma hilo kanusho hapo chini lenye headline ya thread ya JF!. Kufuatia kanusho hilo la Bi. Pile, mmiliki wa Kilimanjaro hotel Albawadry naye ametoa statement ya kanusho akimtetea Bi. Pile kuwa kweli hajui Kiswahili hivyo yote yaliyosemwa na JF ni uwongo! lakini hawazungumzii kilichoandikwa na Wikileaks!.
Kwa vile chanzo cha uwongo wote huu ni taarifa ya Balozi wa Marekani kipindi hicho, Bw.Michael Retzer, Serikali ya Tanzania, kupitia njia za kidplomasia,
1. Kwanza Lisa Pile apelekewa taarifa rasmi za Wikileaks na akanushe hayo aliyomweleza balozi wa Marekani Bw. Michael Retzer maana Pile ndie chanzo kilichonukuliwa na balozi. Hiyo taarifa ya Pile kukanusha kilichoandikwa Jf ni nothing!.
2. Waziri Membe kupitia njia za Kidiplomasia, kuulazimisha ubalozi wa Marekani nchini, kwanza kukanusha taarifa hizo za aliyekuwa balozi wake nchini si za kweli bali ni uzushi wa aliyekuwa balozi wake na pia kumuomba radhi JK na Watanzania kwa jumla.
3.Balozi Michael Retzer popote alipo, ama athibitishe alichoandika ndicho alichoambiwa na Pile, au akiri kuwa kuwa yeye ndiye mzushi aliteutunga uwongo ule hivyo kumuomba rasmi radhi JK na kumpa JK fursa ya kudai fidia na Watanzania tutapoozwa kidogo japo kwa chochote kitu.
4. Wasaidizi wa Rais JK, kuanzia Ikulu mpaka chini, kunapotokea rais kuchafuliwa, muwe mstari wa mbele kumsafisha na kuilinda hadhi na heshima yake instantly na promptly mapema kadri iwezekanavyo, na sio kusubiri mpaka Mtandao wa JF uweke hadharani ndipo mkurupuke na kujibu tuhuma za JF ambazo ni nusu nusu, jibuni tuhuma halisi za Wiki Leaks!.
Mbona ni mengi, mabaya, machafu, ya kudhalilisha na kutia aibu yamesemwa na Wikileaks nanyi mko kimya tuu bila kukanusha lolote, kitendo cha kuibuka na kukanusha hili la hongo kwa JK pekeyake, huku sio kukanusha proper, huku sio kujikomba komba kwa rais ili angalau muonekane nanyi mko kazini wakati in actual fact hamjamsaidia lolote!?. Sasasana ndio kwanza umeutangazia umma kuhusu rais wetu!.
JF ilipoziweka tuhuma zile, iliwawekea mpaka link ya Wiki Leaks, kilichowafanya msifungue hiyo link na kukanusha tuhuma zote moja baada ya nyingine ni nini, hadi kuwapelekea waarabu tuhuma za Kiswahili na Mtoa habari Bi. Pile kupelekewa taarifa ya JF ya kiswahili badala ya kumpa taarifa halisi ya Wiki Leaks?!.
Kwa vile kwenye ile link ya Wikileaks kuna tuhuma lukuki mle, kuanzia ile ya Hosea, itakuwa ni busara na kuwatendea haki Watanzania, sasa kama mtaingia kazini rasmi, na kuanza kupangua tuhuma moja baada ya nyingine kwa, vinginevyo usafishaji huu wa tuhuma za rais peke yake, utaishia kugeuka ni 'Funika Kombe, Mwanaharamu Haramu Apite!'...wenye akili zao watakuwa wameisha pepeta kujua pumba ni zipi na mchele ni upi, na badala ya kumsafisha rais wetu, mnajikuta ndio kwanza mnazidi kumpaka ....!.
Wito kwa Wana jf wenzangu kwenye issues kubwa kama hizi, zinazomhusu kiongozi wetu mkuu wa nchi, nawasihi sana, tuwe wamoja, tuweke maslahi ya taifa mbele. Tuache mambo ya mizaha mizaha. Tuhuma hizi ni mzito na very serious, tunapozijadili, naombeni sana tuwe serious accordingly na kutumia lugha za Staha kwa Viongozi wetu.
Rais Jakaya Kikwete ni rais wa nchi yetu, yeye sio tuu ndiye mtu mwenye jina la JK, bali yeye ndie mkuu wa taasisi ya urais,(presidential insitution) ambayo ndio taasisi yenye hadhi na heshima ya juu kabisa na kubwa kuliko taasisi nyingine zote (isipokuwa katiba) hivyo inastahili heshima yake.
JK ndiye rais wetu, uwe ulimchagua, ua hukumchagua, uwe unamkubali au haumkubali, yeye ndiye rais wetu na ni rais wa wote hata hao alioshindana nao, this is not debetable fact ni hard fact!. Naomba awe addressed kwa heshima stahiki.
Mode: For the sake of this thread, naomba muimoderate effectively na kama mko busy sana naomba nipewe u-mode kwa muda only for the sake of this thread ili post zozote za kipuuzi puuzi zenye lugha isiyo na staha, nizifutilie mbali, ili zisichafue lengo, madhumuni na maudhui ya mjadala kwenye thread hii kwa maslahi ya taifa.
Wasalaam.
Paskali