Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,433
Wanabodi,

Kitendo aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Michael Retzer cha kupitia mtandao wa Wikileaks, kumtuhumu Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa amehongwa pair 5 za Suti za Savile Row, sio tuu ni cha udhalilishaji wa hali ya juu kwa mkuu wetu wa nchi, bali pia ni matukano kwa Watanzania kwa ujumla wetu kwani Rais wetu ni kama baba wa familia kwenye nyumba yetu, hawezi baba yetu kudhalilishwa sisi watoto ambao tunaishi kwenye nyumba hii tukakaa kimya.

Kukanusha peke yake hakutoshi, hoja kuwa kwa vile Ikulu inafungu la kunvisha rais, sio defence kuwa hawezi kuhongwa suti, haswa ukizingatia suti zenyewe sio suti tuu ili mradi ni suti, suti zenyewe ni Savile!. Tunataka Marekani imuombe radhi rais Kikwete na Watanzania kwa ujumla kwa kadhia hii ya Wikileaks.

Mara baada ya JF kutundika bandiko la kadhia hii, Ikulu ilikurupuka kutoa taarifa ya kukanusha. Nimesema Ikulu ilikurupuka kukanusha vipengele vya rushwa tuu kwa kukanusha yaliyonukuliwa na JF badala ya kuifuata ile link na kuyakanusha yote yanayohusiana na Tanzania.

Kwa vile source mama ipo na tuhuma zinazidi kushuka kila kukicha, ilikuwa ni busara kwa Ikulu kukanusha yote in details once and forall, hivyo na tusubiri kuona ni mangapi yatakayofuatia, Ikulu itakuwa inasafisha kila kukicha!.

Mengi yaliyokanushwa na Ikulu, sio yale ya Wiki leaks, bali ya Wiki Leaks yaliyoandikwa JF. Kufuatia kanusho hilo, yule mtoa taarifa kwa Balozi wa Marekani, Bi. Lisa Pile, naye ametumiwa sio taarifa ya Wiklleaks, bali ametumiwa ile thread ya JF ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Matokeo yake, Bi. Pile anakanusha kuwa yeye hajui Kiswahili na wala hakuwahi kukutana na JK hivyo wanamsingizia.

Ilitakiwa huyu Bi Lisa atumiwe ile link ya WikiLeaks na sio hiyo ya JF waliomtumia. Alitakiwa akanushe kukutana na balozi wa Marekani au akiri walikutana na Michael Retzer lakini akanushe hakumwambia kile balozi huyo alichoripoti nchini kwao ambacho ndicho kilichonukuliwa na Wikileaks ili tujue Balozi Michael Retzer ndie muongo wetu hivyo kutupa haki Tanzania kuombwa radhi na JK kutendewa haki sio tuu kwa kuombwa radhi, bali pia hata kufidiwa kwa madhara aliyoyapata kwa kuchafuliwa reputation yake.

Badala ya kukanusha kilichoandikwa na Wikileaks yaani alichoongea na Balozi wa Marekani, hiyu bibie amekanusha hajui Kiswahili na hajawahi kukutana na rais Kikwete wala rais yoyote. Nani kamwambia bibi huyu kuwa kaongea Kiswahili au kakutana na JK?.

Hebu soma hilo kanusho hapo chini lenye headline ya thread ya JF!. Kufuatia kanusho hilo la Bi. Pile, mmiliki wa Kilimanjaro hotel Albawadry naye ametoa statement ya kanusho akimtetea Bi. Pile kuwa kweli hajui Kiswahili hivyo yote yaliyosemwa na JF ni uwongo! lakini hawazungumzii kilichoandikwa na Wikileaks!.

Kwa vile chanzo cha uwongo wote huu ni taarifa ya Balozi wa Marekani kipindi hicho, Bw.Michael Retzer, Serikali ya Tanzania, kupitia njia za kidplomasia,

1. Kwanza Lisa Pile apelekewa taarifa rasmi za Wikileaks na akanushe hayo aliyomweleza balozi wa Marekani Bw. Michael Retzer maana Pile ndie chanzo kilichonukuliwa na balozi. Hiyo taarifa ya Pile kukanusha kilichoandikwa Jf ni nothing!.

2. Waziri Membe kupitia njia za Kidiplomasia, kuulazimisha ubalozi wa Marekani nchini, kwanza kukanusha taarifa hizo za aliyekuwa balozi wake nchini si za kweli bali ni uzushi wa aliyekuwa balozi wake na pia kumuomba radhi JK na Watanzania kwa jumla.

3.Balozi Michael Retzer popote alipo, ama athibitishe alichoandika ndicho alichoambiwa na Pile, au akiri kuwa kuwa yeye ndiye mzushi aliteutunga uwongo ule hivyo kumuomba rasmi radhi JK na kumpa JK fursa ya kudai fidia na Watanzania tutapoozwa kidogo japo kwa chochote kitu.

4. Wasaidizi wa Rais JK, kuanzia Ikulu mpaka chini, kunapotokea rais kuchafuliwa, muwe mstari wa mbele kumsafisha na kuilinda hadhi na heshima yake instantly na promptly mapema kadri iwezekanavyo, na sio kusubiri mpaka Mtandao wa JF uweke hadharani ndipo mkurupuke na kujibu tuhuma za JF ambazo ni nusu nusu, jibuni tuhuma halisi za Wiki Leaks!.

Mbona ni mengi, mabaya, machafu, ya kudhalilisha na kutia aibu yamesemwa na Wikileaks nanyi mko kimya tuu bila kukanusha lolote, kitendo cha kuibuka na kukanusha hili la hongo kwa JK pekeyake, huku sio kukanusha proper, huku sio kujikomba komba kwa rais ili angalau muonekane nanyi mko kazini wakati in actual fact hamjamsaidia lolote!?. Sasasana ndio kwanza umeutangazia umma kuhusu rais wetu!.

JF ilipoziweka tuhuma zile, iliwawekea mpaka link ya Wiki Leaks, kilichowafanya msifungue hiyo link na kukanusha tuhuma zote moja baada ya nyingine ni nini, hadi kuwapelekea waarabu tuhuma za Kiswahili na Mtoa habari Bi. Pile kupelekewa taarifa ya JF ya kiswahili badala ya kumpa taarifa halisi ya Wiki Leaks?!.

Kwa vile kwenye ile link ya Wikileaks kuna tuhuma lukuki mle, kuanzia ile ya Hosea, itakuwa ni busara na kuwatendea haki Watanzania, sasa kama mtaingia kazini rasmi, na kuanza kupangua tuhuma moja baada ya nyingine kwa, vinginevyo usafishaji huu wa tuhuma za rais peke yake, utaishia kugeuka ni 'Funika Kombe, Mwanaharamu Haramu Apite!'...wenye akili zao watakuwa wameisha pepeta kujua pumba ni zipi na mchele ni upi, na badala ya kumsafisha rais wetu, mnajikuta ndio kwanza mnazidi kumpaka ....!.

Wito kwa Wana jf wenzangu kwenye issues kubwa kama hizi, zinazomhusu kiongozi wetu mkuu wa nchi, nawasihi sana, tuwe wamoja, tuweke maslahi ya taifa mbele. Tuache mambo ya mizaha mizaha. Tuhuma hizi ni mzito na very serious, tunapozijadili, naombeni sana tuwe serious accordingly na kutumia lugha za Staha kwa Viongozi wetu.

Rais Jakaya Kikwete ni rais wa nchi yetu, yeye sio tuu ndiye mtu mwenye jina la JK, bali yeye ndie mkuu wa taasisi ya urais,(presidential insitution) ambayo ndio taasisi yenye hadhi na heshima ya juu kabisa na kubwa kuliko taasisi nyingine zote (isipokuwa katiba) hivyo inastahili heshima yake.

JK ndiye rais wetu, uwe ulimchagua, ua hukumchagua, uwe unamkubali au haumkubali, yeye ndiye rais wetu na ni rais wa wote hata hao alioshindana nao, this is not debetable fact ni hard fact!. Naomba awe addressed kwa heshima stahiki.

Mode: For the sake of this thread, naomba muimoderate effectively na kama mko busy sana naomba nipewe u-mode kwa muda only for the sake of this thread ili post zozote za kipuuzi puuzi zenye lugha isiyo na staha, nizifutilie mbali, ili zisichafue lengo, madhumuni na maudhui ya mjadala kwenye thread hii kwa maslahi ya taifa.

Wasalaam.

Paskali
 
Attachments

  • TARIFA YA LISA PILE KUKANUSA KUWA HAJUI KISWAHILI NA HAJAWAHI KUKUTANA NA JK..doc
    188.5 KB · Views: 380
  • Taarifa ya IKULU KUKANUSHA WIKILEAKS KUHUSU RAIS KUHONGWA SUTI.doc
    57 KB · Views: 237
  • TAARIFA YA ALBAWADRY KUKANUSHA KUMHONGA RAIS JAKAYA KIKWETE .doc
    618 KB · Views: 253
Oops!! I think I was not suppose to lay my eyes on this... sorry... I'm out!!
 
Pasco,
Nimeipenda lugha yako ya uandishi.
Mwanamme anamfuata mwanamke anamwambia "unajua watu wanasema wewe ni mzuri" haina tofauti na kusema "mimi nakuona wewe ni mzuri". Umefuzu katika uandishi wako.
Unadhani kama ingekuwa ni rahisi sana Marekani wangepata kiggugumizi mpaka wa leo?
Ni ishu nzito kama unavyoisema. Tumeaibishwa. Suti?
 
Wakuu wa nchi zingine (zilizoendelea) kwa kashfa km hizi wanakanusha - kwanini unataka waombe msamaha na si KIKWETE akanushe km hakuongwa? Au hujawahi muona JK akiwa ametupia mwilini hizo suit?
 
kwani wikileaks wanakisa gani mpaka wamchukie JK kwa kumtungia uongo.

kwa nini usiitake wikileaks iiombe radhi marekani kwa kuweka taarifa ya uongo (kumsakazia uongo balozi wake) ?

Je ikiwa wikileaks wanatunga kwa nia ya kuigonganisha marekani na Tanzania ni ni ipi hasa faida itakayovuna wikileaks kwenye hii skendo????

Kwa namna IKULU inavyokanusha hata mambo yaliyo na ukweli wa 100% nashawishika kuamini taarifa ya wikileaks
 
@Pasco, hiyo habari ya kwamba bi Lisa Pile amekanusha inahitaji verification na kuna kila dalili it's fake, the provided email could be done by just anyone!!!!! Just for your info! kuna jitihada kubwa mno inafanywa na watu mbali mbali paid and the non-paid kukwepesha aibu hii! Usije kushangaa hata hiyo barua inayodaiwa kutoka kwa msemaji wa mmiliki wa Kempinski nayo ni ya kuchonga!!!!!! Lakini as usual hawa jamaa zetu siku zote huwa wanasahau details ndogo ndogo! Keep watching!!!!!
 
Pasco uko sawa lakini hili tatizo lilishakuwa ni tatizo la kidiplomasia la dunia nzima,kuwa zilizokuwa ni siri za marekani zimewekwa wazi na kuwa madhara yake yametapakaa dunia nzima,kwa taarifa walishaomba lazi kwa yaliyotokea kuwa siri zimevuja.

Naludia tena kusema inasemekana walishaomba samahani kwa Mataifa mengi kuwa SIRI zimevuja [leaky].Hivyo kuvuja kwa siri sio kuwa siri hizo ni za kuunda ila ndio ukwel wenyewe ila kilichofanyika samahani yao wanaomba ni kuvuja kwa siri hizo.Na si uzito wa yaliyomo kwenye siri.Kwani wamarekani wao wanaathirika nini kwa Rais wetu kupewa suti.Ila kununuliwa suti kwa Rais wetu kwetu sisi inaimpact.

Sisi tunaangaika na madhara ya Matendo ya siri husika,Hivyo Wamarekani hawana cha kuomba samahani.
 
Wanabodi,

Kitendo aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Michael Ritze cha kupitia mtandao wa Wiki Leaks, kumtuhumu Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa amehongwa pair 5 za Suti za Savile Row, sio tuu ni cha udhalilishaji wa hali ya juu ya mkuu wetu wa nchi, bali ni matukano kwa Watanzania katika ujumla wetu.

Rais wetu ni kama baba wa familia, hawezi kudhalilishwa sisi tukakaa kimya. Kukanusha peke yake hakutoshi, tunataka Marekani imuombe radhi rais Kikwete na Watanzania kwa ujumla.

Mara baada ya JF kutundika kadhia hiyo, Ikulu ilitoa taarifa ya kukanusha. Mengi yaliyokanushwa na Ikulu, sio yale ya Wiki leaks, bali ya Wiki Leaks yaliyoandikwa JF. Kufuatia kanusho hilo, yule atoa taarifa kwa Balozi wa Marekani, Bi. Lisa Pile, naye ametumiwa sio taarifa ya Wiki Leaks, bali ile thread ya JF ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Matokeo yake, Bi. Pile anakanusha kuwa yeye hajui Kiswahili na wala hakuwahi kukutana na JK hivyo wanamsingizia, badala ya kukanusha kilichoandikwa na Wiki Leaks yaani alichoongea na Balozi wa Marekani.

Mmiliki wa Kilimanjaro hotel naye, Albadadry kupitia kanusho la Bi. Pile, naye ametoa statement kukanusha tuhuma za Wiki Leaks kupitia JF, kwa kusema Pile hazungumzi lugha ya Kiswahili, hiyo yaliyosemwa yote ni uwongo.

Kwa vile chanzo cha uwongo wote huu ni taarifa ya Balozi wa Marekani kipindi hicho, Bw. Michael Ritz, Serikali ya Tanzania, kupitia njia za kidplomasia, iulazimishe Ubalozi wa Marekani, kwanza,
1.Kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli, bali Wiki Leaks wamejitungia, hivyo kumuomba radhi rais wetu na Watanzania kwa ujumla.
2.Balozi Michael Ritz popote alipo, ama akanushe kuwa hakuzungumza hayo na Bi. Pile, wala hakuipeleka taarifa ile ya Uwongo iliyonukuliwa na Wiki Leaks, ama akiri kuwa alichoambiwa na Bi. Pile ndicho alichoripoti nchini kwake, hivyo Watanzania tutamjua mchawi wetu ni Bi. Pile aliyetunga maneno ya uwongo na kumpa balozi wa Marekani.
3. Wasaidizi wa Rais JK, kuanzia Ikulu mpaka chini, kunapotokea rais kuchafuliwa, muwe mstari wa mbele kumsafisha na kuilinda hadhi yake mapema iwezekanavyo, na sio kusubiri mpaka Mtandao wa JF uweke hajarani ndipi muibuke kujibu tuhuma za Wiki Leaks. Mbona ni mengi, mabaya, machafu, ya kudhalilisha na kutia aibu yamesemwa na Wiki Leaks nanyi mko kimya tuu bila kukanusha lolote, kitendo cha kuibuka na kukanusha hili la hongo pekeyake, huku sio kukanusha proper, ni kujikomba komba kwa rais muonekane mko kazini!.

JF ilipoziweka tuhuma zile, iliwawekea mpaka link ya Wiki Leaks, kilichowafanya msifungue hiyo link na kukanusha tuhuma zote moja baada ya nyingine ni nini, hadi kuwapelekea waarabu tuhuma za Kiswahili na Mtoa habari Bi. Pile kupelekewa taarifa ya JF ya kiswahili badala ya kumpa taartifa halisi ya Wiki Leaks!.

Kwa vile kuna tuhuma lukuki mle, kuanzia ile ya Hosea, itakuwa ni kuwatendea haki Watanzania, sasa kama mtaingia kazini rasmi, na kuanza kupangua tuhuma kwa tuhuma, vinginevyo usafishaji huu wa tuhuma za rais peke yake, utaishia kugeuka ni 'Funika Kombe, Mwanaharamu Haramu Apite!", wenye akili zao watakuwa wameisha pepeta kujua pumba ni zipi na mchele ni upi, na badala ya kumsafisha rais wetu, mnajikuta ndio kwanza mnazidi kumpaka ....!.

Wito kwa Wana jf, kwenye issues kubwa kama hizi, zinazomhusu kiongozi wetu mkuu wa nchi, nawasihi sana, tuache mambo ya mizaha. Tuhuma hizi ni mzito na very serious, tunapozijadili, naombani sana tuwe serious accordingly na kutumia lugha za Staha kwa Viongozi wetu.
Rias Jakaya Kikwete ni rais wa nchi, uwe ulimchagua, hukumchagua, unamkubali, haumkubali, yeye ndiye rais, naomba awe addressed kwa heshima stahiki.

Mode: For the sake of this thread, naomba nipewe u-mode ili thread zozote za kipuuzi puuzi zenye lugha isiyo na staha, nizifutilie mbali, ili zisichafue lengu, madhumuni na maudhui ya mjadala kwenye thread hii kwa maslahi ya taifa.

Wasalaam.

Pasco.

Naunga mkono ikiwa kama Rais wetu hahusiki ni vema Serikali ya Marekani ikaomba radhi kwani wametuvunjia heshima watanzania. Wasitudhalilishe na misaada yao ikiwa hatuheshimiani.
 
Katika misemo ya kibantu nayoipenda,ni huu "Ukweli kwa mkubwa kwa mtoto ni uongo, na Ukweli wa mtoto kwa mkubwa ni uongo." Na hii imejidhihirisha kwa serikali yetu ya kishikaji. Mimi ninahisi kuna ushenzi mwingi utaja fichuka kama biashara zenyewe ndo hizi za kununuliana Misuli. Hongera kikwete kwa kununuliwa pamba safi. !! Ziba masikio,ni wivu wetu unatusumbua. Big up!
 
Wanabodi,
Kitendo aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Michael Ritze cha kupitia mtandao wa Wiki Leaks, kumtuhumu Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa amehongwa pair 5 za Suti za Savile Row, sio tuu ni cha udhalilishaji wa hali ya juu ya mkuu wetu wa nchi, bali ni matukano kwa Watanzania katika ujumla wetu.

Rais wetu ni kama baba wa familia, hawezi kudhalilishwa sisi tukakaa kimya. Kukanusha peke yake hakutoshi, tunataka Marekani imuombe radhi rais Kikwete na Watanzania kwa ujumla.

Mara baada ya JF kutundika kadhia hiyo, Ikulu ilitoa taarifa ya kukanusha. Mengi yaliyokanushwa na Ikulu, sio yale ya Wiki leaks, bali ya Wiki Leaks yaliyoandikwa JF. Kufuatia kanusho hilo, yule atoa taarifa kwa Balozi wa Marekani, Bi. Lisa Pile, naye ametumiwa sio taarifa ya Wiki Leaks, bali ile thread ya JF ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Matokeo yake, Bi. Pile anakanusha kuwa yeye hajui Kiswahili na wala hakuwahi kukutana na JK hivyo wanamsingizia, badala ya kukanusha kilichoandikwa na Wiki Leaks yaani alichoongea na Balozi wa Marekani.

Mmiliki wa Kilimanjaro hotel naye, Albadadry kupitia kanusho la Bi. Pile, naye ametoa statement kukanusha tuhuma za Wiki Leaks kupitia JF, kwa kusema Pile hazungumzi lugha ya Kiswahili, hiyo yaliyosemwa yote ni uwongo.

Kwa vile chanzo cha uwongo wote huu ni taarifa ya Balozi wa Marekani kipindi hicho, Bw. Michael Ritz, Serikali ya Tanzania, kupitia njia za kidplomasia, iulazimishe Ubalozi wa Marekani, kwanza,
1.Kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli, bali Wiki Leaks wamejitungia, hivyo kumuomba radhi rais wetu na Watanzania kwa ujumla.
2.Balozi Michael Ritz popote alipo, ama akanushe kuwa hakuzungumza hayo na Bi. Pile, wala hakuipeleka taarifa ile ya Uwongo iliyonukuliwa na Wiki Leaks, ama akiri kuwa alichoambiwa na Bi. Pile ndicho alichoripoti nchini kwake, hivyo Watanzania tutamjua mchawi wetu ni Bi. Pile aliyetunga maneno ya uwongo na kumpa balozi wa Marekani.
3. Wasaidizi wa Rais JK, kuanzia Ikulu mpaka chini, kunapotokea rais kuchafuliwa, muwe mstari wa mbele kumsafisha na kuilinda hadhi yake mapema iwezekanavyo, na sio kusubiri mpaka Mtandao wa JF uweke hajarani ndipi muibuke kujibu tuhuma za Wiki Leaks. Mbona ni mengi, mabaya, machafu, ya kudhalilisha na kutia aibu yamesemwa na Wiki Leaks nanyi mko kimya tuu bila kukanusha lolote, kitendo cha kuibuka na kukanusha hili la hongo pekeyake, huku sio kukanusha proper, ni kujikomba komba kwa rais muonekane mko kazini!.

JF ilipoziweka tuhuma zile, iliwawekea mpaka link ya Wiki Leaks, kilichowafanya msifungue hiyo link na kukanusha tuhuma zote moja baada ya nyingine ni nini, hadi kuwapelekea waarabu tuhuma za Kiswahili na Mtoa habari Bi. Pile kupelekewa taarifa ya JF ya kiswahili badala ya kumpa taartifa halisi ya Wiki Leaks!.

Kwa vile kuna tuhuma lukuki mle, kuanzia ile ya Hosea, itakuwa ni kuwatendea haki Watanzania, sasa kama mtaingia kazini rasmi, na kuanza kupangua tuhuma kwa tuhuma, vinginevyo usafishaji huu wa tuhuma za rais peke yake, utaishia kugeuka ni 'Funika Kombe, Mwanaharamu Haramu Apite!", wenye akili zao watakuwa wameisha pepeta kujua pumba ni zipi na mchele ni upi, na badala ya kumsafisha rais wetu, mnajikuta ndio kwanza mnazidi kumpaka ....!.

Wito kwa Wana jf, kwenye issues kubwa kama hizi, zinazomhusu kiongozi wetu mkuu wa nchi, nawasihi sana, tuache mambo ya mizaha. Tuhuma hizi ni mzito na very serious, tunapozijadili, naombani sana tuwe serious accordingly na kutumia lugha za Staha kwa Viongozi wetu.
Rias Jakaya Kikwete ni rais wa nchi, uwe ulimchagua, hukumchagua, unamkubali, haumkubali, yeye ndiye rais, naomba awe addressed kwa heshima stahiki.

Mode: For the sake of this thread, naomba nipewe u-mode ili thread zozote za kipuuzi puuzi zenye lugha isiyo na staha, nizifutilie mbali, ili zisichafue lengu, madhumuni na maudhui ya mjadala kwenye thread hii kwa maslahi ya taifa.

Wasalaam.

Pasco.

Kwanza kabisa anza wewe kuwaomba radhi Wamarekani kwa kumpa aliyekuwa Balozi wao jina ambalo si lake. Anaitwa Michael Retzer na wala si Ritz. Huonekani pia kuwa na uelewa wa WikiLeaks kiasi cha kudhani hizi taarifa zimeandikwa nao. WikiLeaks ni chombo kilichotumika kubeba na kuweka hadharani mawasiliano ya kidiplomasia ya Wamarekani. Kuanza kuilaumu ni sawa na wewe upokee ujumbe mbaya kwenye sms halafu badala ya kukimbizana na aliyeuandika unakimbizana na handset yako.
Lakini cha muhimu ni kwamba, je unapotaka Watanzania tudai kuombwa radhi na Wamarekani kwa kumdhalilisha Vasco, je wewe una ushahidi kwamba hana tabia ya kupenda vya kupewa? Kuna cable moja ilimnukuu akimueleza Waziri wa zamani wa masuala ya Afrika wa Marekani Jendayi Fraser kuwa angependa kwenda Washington. Hiyo nayo vipi?
Huwezi kudai watu wapiganie kulinda heshima ya mtu ambaye hajui heshima ya taaluma ya diplomasia. Zigo lake la misumari hili acha alibebe mwenyewe au kama vipi nenda kasaidiane na Salva mkamtakatishe.
 
Hizi Wikileaks zilikuwa ni internal correspondence kati ya Balozi na Wizara ya Mambo ya Nje ya US. Nyingi ya hizi zilikuwa pia ni Classified au Secret. Walioziandika hawakuwa wanategemea kuwa zingekuja kuletwa kwenye Public Arena..

Hizi taarifa zimetoka nje kwa bahati mbaya. Hakuna haja ya watu waliotajwa kwenye hizo taarifa kukasirika sana. Laiti watu wangejua makampuni yao ya Bima yanavyowasema kwenye internal correspondence, wangezimia.

In conclussion: Itakuwa ni retro-active kama serikali ikiamua kuchukua hatua za kisheria. Hata hii kujibu shutuma haina haja.
 
Pasco,
Madai ya Rais kuhongwa suti yako nje ya uwezo wetu maana yametolewa na mtu(chombo) ambacho hatuna uwezo nacho no matter tutasema na kutoa mapovu kiasi gani.

Tatizo ni kwa watu waliokanusha hiyo taarifa- hawakuwa smart, wameacha nyufa nyingi sana ambazo kwa namna moja zinaweza kuwa zinasaidia mtu kuamini kuwa tukio hilo ni kweli.

Nashauri.....Pasco ujiunge idara ya mawasiliano Ikulu, utafanya tofauti kubwa sana maana unajua sana ''kuneutralize'' mambo. Kila nikikusoma nakulinganisha na Dr. Mutua
 
Mimi sioni tatizo, hakuna haja ya kutuomba radhi kwani Marekani wametukosea nini. Mbona Kikwete hajawaomba radhi Watanzania kwa kitendo cha IKULU kusafirisha kwa kuwatorosha Twiga kwenda UAE. Yawezekana hao Twiga ndoyalikuwa malipo ya hizo SUTI tutajuaje!!! kwa sababu SUTI hizo zilitokea UAE. Kazi kwelikweli.
 
Wanabodi,

Kitendo aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Michael Ritze cha kupitia mtandao wa Wiki Leaks, kumtuhumu Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa amehongwa pair 5 za Suti za Savile Row, sio tuu ni cha udhalilishaji wa hali ya juu ya mkuu wetu wa nchi, bali ni matukano kwa Watanzania katika ujumla wetu.

Rais wetu ni kama baba wa familia, hawezi kudhalilishwa sisi tukakaa kimya. Kukanusha peke yake hakutoshi, tunataka Marekani imuombe radhi rais Kikwete na Watanzania kwa ujumla.

Mara baada ya JF kutundika kadhia hiyo, Ikulu ilitoa taarifa ya kukanusha. Mengi yaliyokanushwa na Ikulu, sio yale ya Wiki leaks, bali ya Wiki Leaks yaliyoandikwa JF. Kufuatia kanusho hilo, yule atoa taarifa kwa Balozi wa Marekani, Bi. Lisa Pile, naye ametumiwa sio taarifa ya Wiki Leaks, bali ile thread ya JF ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Matokeo yake, Bi. Pile anakanusha kuwa yeye hajui Kiswahili na wala hakuwahi kukutana na JK hivyo wanamsingizia, badala ya kukanusha kilichoandikwa na Wiki Leaks yaani alichoongea na Balozi wa Marekani.

Mmiliki wa Kilimanjaro hotel naye, Albadadry kupitia kanusho la Bi. Pile, naye ametoa statement kukanusha tuhuma za Wiki Leaks kupitia JF, kwa kusema Pile hazungumzi lugha ya Kiswahili, hiyo yaliyosemwa yote ni uwongo.

Kwa vile chanzo cha uwongo wote huu ni taarifa ya Balozi wa Marekani kipindi hicho, Bw. Michael Ritz, Serikali ya Tanzania, kupitia njia za kidplomasia, iulazimishe Ubalozi wa Marekani, kwanza,
1.Kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli, bali Wiki Leaks wamejitungia, hivyo kumuomba radhi rais wetu na Watanzania kwa ujumla.
2.Balozi Michael Ritz popote alipo, ama akanushe kuwa hakuzungumza hayo na Bi. Pile, wala hakuipeleka taarifa ile ya Uwongo iliyonukuliwa na Wiki Leaks, ama akiri kuwa alichoambiwa na Bi. Pile ndicho alichoripoti nchini kwake, hivyo Watanzania tutamjua mchawi wetu ni Bi. Pile aliyetunga maneno ya uwongo na kumpa balozi wa Marekani.
3. Wasaidizi wa Rais JK, kuanzia Ikulu mpaka chini, kunapotokea rais kuchafuliwa, muwe mstari wa mbele kumsafisha na kuilinda hadhi yake mapema iwezekanavyo, na sio kusubiri mpaka Mtandao wa JF uweke hajarani ndipi muibuke kujibu tuhuma za Wiki Leaks. Mbona ni mengi, mabaya, machafu, ya kudhalilisha na kutia aibu yamesemwa na Wiki Leaks nanyi mko kimya tuu bila kukanusha lolote, kitendo cha kuibuka na kukanusha hili la hongo pekeyake, huku sio kukanusha proper, ni kujikomba komba kwa rais muonekane mko kazini!.

JF ilipoziweka tuhuma zile, iliwawekea mpaka link ya Wiki Leaks, kilichowafanya msifungue hiyo link na kukanusha tuhuma zote moja baada ya nyingine ni nini, hadi kuwapelekea waarabu tuhuma za Kiswahili na Mtoa habari Bi. Pile kupelekewa taarifa ya JF ya kiswahili badala ya kumpa taartifa halisi ya Wiki Leaks!.

Kwa vile kuna tuhuma lukuki mle, kuanzia ile ya Hosea, itakuwa ni kuwatendea haki Watanzania, sasa kama mtaingia kazini rasmi, na kuanza kupangua tuhuma kwa tuhuma, vinginevyo usafishaji huu wa tuhuma za rais peke yake, utaishia kugeuka ni 'Funika Kombe, Mwanaharamu Haramu Apite!", wenye akili zao watakuwa wameisha pepeta kujua pumba ni zipi na mchele ni upi, na badala ya kumsafisha rais wetu, mnajikuta ndio kwanza mnazidi kumpaka ....!.

Wito kwa Wana jf, kwenye issues kubwa kama hizi, zinazomhusu kiongozi wetu mkuu wa nchi, nawasihi sana, tuache mambo ya mizaha. Tuhuma hizi ni mzito na very serious, tunapozijadili, naombani sana tuwe serious accordingly na kutumia lugha za Staha kwa Viongozi wetu.
Rias Jakaya Kikwete ni rais wa nchi, uwe ulimchagua, hukumchagua, unamkubali, haumkubali, yeye ndiye rais, naomba awe addressed kwa heshima stahiki.

Mode: For the sake of this thread, naomba nipewe u-mode ili thread zozote za kipuuzi puuzi zenye lugha isiyo na staha, nizifutilie mbali, ili zisichafue lengu, madhumuni na maudhui ya mjadala kwenye thread hii kwa maslahi ya taifa.

Wasalaam.

Pasco.

Umekuja kwa style ya TANU kufanya spinning kwa jamii hii ya mwaka huu 2011. Unatafuta public sympathy kwa nguvu zako zote kwa kutulazimisha eti Watanzania tumezalilishwa na balozi wa marekani,ni kweli tumezalilisha ila aliyetuzalilisha ni JK. Waambie wenzako hapo ikulu kwamba "if you win the youths then you win the future". Sasa uovu ni mwingi umefanyika hapo ikulu na unaanza kugundulika na raia wa kitaifa na kimataifa. Naamini vijana ndo chachu ya mabadiliko sasa serikali ya CCM imelose the youths so they also lose the future. Kiama chenu kimewadia na ukweli utajulikana zaidi na zaidi na adhabu yenu ni kwenye sicret ballot pekee.
6a00d83455d78069e201538f5b75de970b-320wi.jpg
 
Pasco you are not serious I belive so.

Najuwa unatania na una sherehesha mjadala wa kupewa suti, labda yeye Mhe hakuwa na hakuona kama ni fedhehea na ina sura kama ya hongo!

Weekleaks wamevujisha taarifa kama 120 juu ya nchni yetu, hakuna mpumbuvu hata mmoja anayeweza kuwaelewa mkiwa mtaka kutwambia lililo la uongo au linalo waudhi sana kushuparia ni la suti peke yake! Hakuna mpumbuva hambaye atashindwa kujuwa kwanini hilo ndilo linapingwa kwa sauti kubwa na kelele za kila dakika.

Ila kwa mwelevu inaonyesha na kudhiirisha ni kwa jinsi gani tulivyo wapumbavu wa kupoteza muda na mambo ya kipuuzi na kuacha mambo ya msingi ambayo yana madhara kwa Taifa na jamii yetu hadi kizazi na kizazi. Kikwete kununuliwa suti ina madhara gani kwa Mtanzania wa leo na kesho? Kama ni tabia yake ni upuuzi wake ni wake aamue kuupuza au ajiulize alijukwaa wapi na ajifunze kutokana na makosa.

Kuna mambo kama ya Kkwete na Kapuya kupingana na Gen. Waitara juu ya kupereka vikosi vyetu kupewa mafunzo USA bila kuweka wazi nadharia ya mafunzo yenyewe na mipaka ya mwingiliano kijeshi kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo! Unajuwa madhara ya aliyokuwa anafanya huyo Rais wetu na Kapuya wake kwa Mstakabali wa nchni yetu na Taifa letu leo na kesho?

Leteni hoja za kitaifa juu ya habari za weekleaks muache kujikita katika kujenga personality kwa kuuwa utaifa ili mradi mnajenga utu wa mtu mmoja aitwaye Kikwete.
 
Hilo la kuombwa radhi wala halina nafasi maana inaonyesha hujui wikileaks ni nini. Kuna bwana mmoja hapo juu ameeleza hakuna sababu ya kurudia. Kwamba habari ni za uongo nalo linachekesha. How do you know? Wakati JK alikuwa waziri wa mambo ya nje huyo balozi atamsingizia kwanini?

Kwa watu wanaoangalia mambo kwa uchambuzi wa kina, huyu mwarabu alipata hotel ya Kilimanjaro kwa hila na namna inayoacha maswali mengi. Mengi ambaye ni mzawa alikuwa na uwezo wa kuinunua na kuiendeleza ila wakamnyima kwa hila wakampa mwarabu. Namna alivyoipata inaonyesha alikuwa well connected serikalini hivyo alikuwa na mtu mwenye nafasi na ukweli ndio huu kwamba kumbe JK ndie aliyempigia debe akiwa waziri kwenye serikali ya Mkapa baada ya kupatiwa viwalo. sasa unavyosema madai ni ya uongo una maanisha nini? Watuambie basi nani alimleta mwarabu na ni kwanini walimnyima Mzawa hotel wakampa yeye wakati sera yetu ni kuwawezesha wazawa? tafakari
 
Back
Top Bottom