Anguko la KKKT - DKMs, limesababishwa na nani?
"Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
Mwanadamu, wewe unakaa kati
ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi".
Ezekieli 12:1 - 2.
Wapendwa Wana DKMs, nawasalimu katika Jina la Kristo Mfufuka.
Dayosisi yetu imepatwa na anguko kubwa sana; lakini jambo la kushangaza mpaka sasa wako baadhi ya Wachungaji na Washarika wanaofurahia na kuendeleza anguko hilo.
Swali la kujiuliza ni hili, je, anguko la DKMs limesababishwa na nani?
Jibu ni hili, anguko hilo limesababishwa na Askofu Mstaafu Dkt Stephen Ismail Munga, na Wasaidizi wake bila ya kuwasahau Wachungaji na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi.
Hao kwa kushirikiana na Askofu Munga, ndio wameifikisha Dayosisi hapa ilipo. Na wala hawataki kuamka katika usingizi mzito. Wachungaji na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ndio waliopewa dhamana ya Uongozi, katika kuziwakilisha na kusimamia Sharika. Washarika hupokea maagizo kutoka kwao na kuyateketeza. Wachungaji na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi ndio wanaoingia katika vikao vya maamuzi, na yote yanayotendeka wanayajua; tatizo la wote hao ni woga na hofu, yaani Munga anaogopewa kuliko Mungu. Wameshindwa kumkosoa Askofu Munga na Mkewe pale walipokihujumu Chuo Cha SEKOMU, hatimaye kikapoteza sifa ya kudahili.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu, walinyamaza hata pale Kituo cha Mafuta Mombo kilipouzwa na Askofu Munga akishirikiana na shemejiye aitwaye Mch James Mwinuka.
Kwa wasiojua historia ya Kituo cha mafuta - Mombo, ni hivi kwamba; alikuwepo Mjerumani mmoja anaitwa Schomer (Shoma), huyu alikuwa ni rafiki wa Baba Askofu Dkt Sebastian Kolowa (RIP), huyo ndiye aliyekikabidhi Kituo cha mafuta Mombo kwa Mzee Askofu Kolowa kiwe mali ya Dayosisi; Askofu Kolowa bila ya tashwishwi yoyote akakikabidhi Kituo kwa Dayosisi, ingawa kutokana na urafiki aliokuwa nao kati yake na yule Mjerumani, angeweza kumwambia Bw Shoma, unaonaje Kituo hiki kikiwa changu binafsi? Mr Shoma asingeweza kumkatalia. Bw Dulus naye alitoa jengo lile la gereji karibu na kituo cha mabasi Lushoto, pamoja na nyumba aliyokuwa akiishi Katibu Mkuu Bw Frederick Shebila, iliyoko jirani na European cemetery - Lushoto. Mzee huyu na wenzake hawakuwa na tamaa.
Hebu, kama huyo Askofu Mstaafu Munga ndiye angekabidhiwa mali hizo ( tena hapo tumetaja chache) si angezitafuna? hakuna patano lolote la Halmashauri Kuu ya Dayosisi, amekiuza Kituo cha mafuta Mombo, sembuse Shoma angemkabidhi yeye, si angekifanya mali yake?.
Misitu imevunwa, fedha hazijulikani, hakuna ukaguzi wa Mahesabu si katika Sharika, Dinari wala Dayosisi na Taasisi zake, imekuwa vurugu mechi.
Dayosisi inakabiliwa na madeni mengi sana, tena ina kesi kibao Mahakamani, na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), na kwakuwa ni haki zao Wafanyakazi watashinda tu, tena saa tatu asubuhi.
Wachungaji wamenyamaza, Wajumbe wa Halmashauri Kuu wametulia. Sasa mbio za Uongozi wenu umeifikisha Dayosisi hapa ilipo. Wapo baadhi ya Wachungaji wanaunga mkono udhalimu huo, na wao wenyewe wamesharithi jiroho la pepo badhilifu; na hapa niwataje wachache:
1.Mch Moses wa Kana, Mhasibu na kila kitu kinachohusu fedha ni yeye, hata ile mikataba ya Benki na Hospitali ni yeye. Hatoi ripoti yoyote ya fedha za Usharika na za Dinari.
2. Mch Yambazi Mauya wa Usharika wa Manundu Korogwe, huyu anapokea fedha toka Jimbo rafiki la Floto - Ujarumani, fedha za vifaa vya ujenzi wa makanisa na nyumba za Watumishi, usafiri na hata fedha za msaada wa elimu kwa wasio na uwezo. Je, Mchungaji Mauya unaweza kutokea mezani na kutoa hesabu ya uwakili wako?
3. Mchungaji Paulo Kivatiro wa Usharika wa Muheza, naye huyu ni kiburi na mbabe aliyejaa tamaa, amehamia Usharikani Muheza, kasikia kuna shamba la michungwa linauzwa, kawakusanya baadhi ya Washarika akawalazimisha wamchangie fedha za kununua shamba hilo. Hana matumizi mazuri ya fedha hali inayoleta shida kwa Mhasibu. Ameligawa Baraza la Wazee kwa Uongozi na misimamo yake mibovu; tena mzee mmoja mpigaji ndiye anayemkingia kifua. Patano la Baraza la Wazee, walikubaliana kuwa Mchungaji aliyehama Usharika huo aje afanye makabidhiano kabla ya kumfanyia sherehe za kumwaga ili wahakiki huo ufisadi wa milioni 19 umetokeaje? hata hivyo kwa kiburi na ubabe wa Mchungaji Kivatiro alitangaza hakutafanyika makabidhiano na kwamba Mch N'kanileka Chedi ataagwa na atapewa Shilingi milioni 4, walizochanga Washarika kama zawadi; yaani ni umwamba tu. Bila kushirikisha Halmashauri ya Dinari, yeye na Mchungaji Mauya wamewahamisha Wainjilisti na Wahasibu katika Sharika, wengi wakiwa wanadai mishahara yao. Baraza la Wazee liliposhauri Watumishi hao wasihame mpaka watakapolipwa stahiki zao, walipuuza maoni hayo.
4. Katibu Mkuu Mwinuka, huyu kila kona yumo, Ofisi Kuu yumo, Utume Radio, yumo, Bureau de change, yumo; mfuko mpana, yumo, SEKOMU, yumo; hakuna haja ya kuyarudia .
Huyu Katibu Mkuu James akishirikiana na Mchungaji Chedi, wameuhamisha mradi wa mnara wa simu, ambao Usharika wa Muheza uliwekeana na kampuni moja ya simu. Wameuhamishia Dayosisi na wala hawatoi malipo kwa Usharika kama unavyotaka; hiyo imepelekea Usharika kudai milioni 16, ambazo zingesaidia kulipa madeni ya mishahara ya Watumishi.
Wako wa Mungu walioamka kwa neema ya Kristo kuikomboa DKMs toka mikononi mwa wadhalimu, lakini watu hao wanaonekana kama wajinga. Wachungaji na Wajumbe wa iliyokuwa Halmashauri Kuu wanasapoti ufisadi uliofanyika na unaoendelea kufanyika, kwasababu kwenye vikao wamekuwa mabubu, ndio sababu Dayosisi imefika hapa ilipo.
Haya, TCU, wanahitaji kuhakiki Deni la Mkopo SEKOMU walilokopa CRDB, mtajibu nini, wakati fedha zilishachangwa na Washarika zaidi ya Bilioni moja, kila Usharika ukamkabidhi Mkuu wake wa Jimbo; fedha hizo mmezipeleka wapi?. Ndiyo maana fisadi mwenzenu hamtaki aguswe kwasababu mna maslahi yenu.
Mchungaji Mwarabu wa Usharika wa Soni acha kuwachangisha fedha Washarika wa Soni kwa ajili ya kulipa madeni ya mishahara ya Watumishi wa Usharika, wewe si ulitamka kwamba Dayosisi iko vizuri, Askofu Munga ni msafi, hakuna madeni, iweje sasa unawachangisha Washarika?.
Wanamatengenezo wanapoibua ufisadi na kutaka kuleta uhai, mnawatenga na Kanisa. Mlalo wametengwa Vijana 8, Kana Mzee 1, mwingine kasimamishwa uzee wa Kanisa; kisa wamehoji uharibifu unaoendelea.
Wito: Je, "Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi"
Eze 12:1,2.
Enyi Wachungaji na Washarika, endeleeni kufumba macho na kuziba masikio, kana kwamba hamzioni hujuma zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika chini ya Uongozi wa Askofu Munga.
Subirini rundo la madeni ya mabilioni yatafumuka hivi karibuni, na msiache kuchanga ili yalipwe yote kwa ukamilifu wake, halafu yazalishwe mengine, yalipwe tena na tena.
Kunyamaza kwako kumetufikisha hapa tulipo.
Kwanini Askofu Kolowa na Askofu Jally hawakuwa mafisadi! Ni kwasababu walitunza viapo vya Uchungaji.
Hivi sasa tamaa tu ya mali, Mbuyukenda nayo iliponea tundu la sindano ilibakia nukta moja tu iuzwe.
Mwenye masikio ya kusikia na asikie.
++++ Sauti ya Waebrani: Shime amkeniiii!
Jr[emoji769]