Tuhuma za kutisha za Dr. Munga Askofu KKKT -DKMS

Tuhuma za kutisha za Dr. Munga Askofu KKKT -DKMS

Status
Not open for further replies.
SITOSHANGAA KAMA KKKT ITALETA UNAFIKI KATIKA MAZISHI YA ASKOFU MUNGA

Juzi niliandika hapa kuwa kuna umafia, chuki, vinyongo na visasi vya kutisha ndani ya Kanisa la KKKT na hili muwe mnaelewa kuwa namaanisha wala sibagazi wala kumbananga mtu wala Kanisa.

Kuna mipango mingi miovu na ya kutisha ambayo hupangwa, kuratibiwa na kutekelezwa na Kanisa.

Ni bahati mbaya Kondoo wakishalishwa chuki na kisha kupambwa na maneno kuwa ni shetani amejiinua kupinga kazi ya Mungu huamini na kuendelea kutumika kwa maslahi ya viongozi wa dini wachache.

Askofu MUNGA ni miongoni mwa waliobahatika kupitishwa katika moto huu mbaya ndani ya Kanisa hili. Vita ya walioyataka madaraka kwa njia za panya na njia za mkato zilifanya Askofu Munga apitishwe kwenye njia ya kila aina ya matope, matusi, kashfa, kejeli na dhihaka.

Huyu Mzee amepitishwa kwenye mengi na watesi wake waliokuwa na kiu, njaa na uchu wa madaraka, acheni tu apumzike.

Hata baada ya wao kujitwalia madaraka bado wakahakikisha wanaendeleza chuki, visasi, vinyongo na umafia dhidi ya Askofu Munga. Hata tu hadhi ya Askofu na Askofu Mstaafu alibaki nayo kwa tabu sana, walivitaka vyote.

Hebu tafakari tu, huyu ni Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Askofu Mstaafu Dr. Stephen Munga .

Huyu ni Askofu Mstaafu ambaye anastahili kuhudumiwa na Kanisa lakini kwa sababu tu ya chuki, ubinafsi na roho mbaya za viongozi wenye hila na chuki leo Mzee huyu anakosa huduma na haki stahiki kutoka KKKT.

Leo Mzee huyu anahudumiwa na Kanisa la Anglican! Yaani Kanisa lingine linatazama na kushuhudia unyama, ufedhuli na mateso anayotendewa Askofu Munga na Kanisa hili la KKKT hadi wanaona huruma na kujitolea kumsaidia.

Askofu Munga ameishi uzee wake na ustaafu wake kwa upweke wa kutisha ndani ya Kanisa hili la KKKT. Askofu Munga ameishi uzee wake na ustaafu wake ndani ya Kanisa hili la KKKT kama yatima kamili "total orphan".

KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki waliona hii ni sawa na ndio stahiki anayofaa kutendewa Askofu Munga. Askofu Mbilu naye akasimamia unyama na ukatili huu dhidi ya Askofu Munga. KKKT makao makuu na Wakuu wake kwa maana ya Askofu Shoo na sasa Askofu Malasusa wakaona hii ni sawa. Askofu Malasusa akachagua kuwa chawa kuliko kusimamia haki za Watumishi kama hawa wanaonyanyaswa na Kanisa?

Kosa la huyu Askofu huyu ni nini? Na je hata kama kuna kosa ni kosa lipi lisilosameheka? Huu ndio upendo wa Kristo mnaoruhubiria au ni kutulaghai tu mpate chenu kutoka mifukoni mwetu mpite hivi?

Ule msamaha wa saba mara sabini elfu mnaoruhubiria ndio huu au mnatulaghai tu?

Sio ninyi mnaotuambia nduguyo akikukosea muite kwa upendo? Huu ndio upendo wa Agape?

Nimerudia kuyasema haya kwa sababu ni kawaida kwa KKKT kutumia misiba kama platform ya kuonesha UNAFIKI, upendo na mshikamano. Sitashangaa wakiuleta huu unafiki pale Lushoto kwa kwenye mazishi ya Askofu Munga.

Nitashangaa na kuumia kama familia ya Askofu Munga itakubali huu unafiki. Kwa heshima ya Askofu Munga kataeni unafiki wowote wa KKKT katika mazishi haya.

Kanisa la Anglican lililochagua kusimama na Askofu Munga wakati KKKT imemtupa, hawa waliosimama na Askofu Munga wakati wa mapito na hata ugonjwa hadi wapeni nafasi na heshima ya kumzika Askofu Munga.

Nasisitiza familia isikubali ulaghai wa aina yoyote hata kama ni kwa ahadi za kilaghai, hiyo ni rushwa na laana msikubali.

Waliolia na ninyi wakati Askofu akiwa hai ndio hao hao walie nanyi wakati Askofu Munga akiwa mfu. Waliocheka wakati wa mateso ya Askofu Munga na waende wakahitimishe kicheko chao sasa kwa sherehe kubwa wakale na kunywa maana yule waliyemuona ni adui yao sasa amelala mauti.

Muishi kwa raha sasa mkila na kunywa enyi watakatifu. Ikiwa mlitenda kwa haki kwa Askofu Munga mukawe na mwisho mwema lakini ikiwa mlitenda kwa akili, mkamtendea madhila na dhulma hakika Mungu wa Munga aigeuzie vita malangoni mwenu. Hamtaijua amani wala furaha katika maisha yenu.

Naam, Wewe Kondoo jiulize tu ikiwa Kanisa linamtendea hivi Askofu Mstaafu, linawatendea dhuluma Watumishi wake vipi linaweza kukutendea haki wewe? Linaweza kukutendea upendo wewe?

Askofu Stephen Munga usilale salama ni hadi watesi wako wamelipa gharama, Askofu Stephen Munga usipumzike kwa amani hadi vita imegeukia malangoni mwa watesi waliokufanya uishi uzee wa tabu, mateso na upweke.

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
 
IMG-20250920-WA0076.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom