Tuhuma za kutisha za Dr. Munga Askofu KKKT -DKMS

Tuhuma za kutisha za Dr. Munga Askofu KKKT -DKMS

Status
Not open for further replies.
Munga alipomteua mke wake kuwa provost wa SEKOMU, mwanamke ambaye hana sifa ya kuwa mkuu wa chekechea nilijua tu. SEKOMU kwisha.

Sasa atakua amebaki na ule mradi wa ile Lodge pale Lushoto. Mbona ni DKMS tu ndio kuna dinari.
Nimesoma hapo huyo mama mpuuzi sana aliwahi kusema chuo kikifungiwa majengo atafugia kuku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba Munga ni mtu makini msomi anayependa uwazi demokrasia uongozi bora na uwajibikaji.....
Cha msingi asianze kutafuta wahusika ila ajibu kwa hoja ikiwezekana kuomba msamaha kuweka wazi maovu yake..kuwaomba msamaha familia za wahusika ambao amewaumiza kwa njia moja au nyingine. Kuwarudisha kazini wachungaji wali hoji mapato ya chuo yamepelekwa wapi na hata wale ambao majimbo yao yalikataa kuchanga pesa za madeni hewa pasipo ufafanuzi.
Kuwapongeza wale wenye misimamo walomwambia akiendelea kuuza mali za kanisa hasa ile la tanga mjini awe amekiacha kiti wazi.
Pia hata yule aliekusimamia ndoa kamuombe msamaha umempa adhabu kubwa kumbe alikua na nia nzuri tu.
Mwisho ikikupendeza ili mambo yaende basi rekebisha katiba isomeke mpaka utapofariki ili kupunguza kero za wanaoulizwa katiba zimevunjwa.
Maana wenzako hawakuwa na Phd ila umekuta miradi na mashule na vituo na mashamba kibao....unaondoka hakuna kilichisimama vyote vimekufa ...waambie wakuongezee muda labda unaweza ukafufua hata kimoja .naamini baba watakuelewa .
Baba pole.


Katika hili
Huu ujumbe upo makini sana... kama hataelewa...(Munga).. Basi nitaendelea kuamini lengo lake si jema kwa wana Dayosisi ya DKMS... Niseme ukweli maamuzi ya kujitoa TUMAINI UNIVERSITY (SEKUCO) na kuwa SEKOMU ilikuwa ni haraka sana... kwani maandalizi yalikuwa bado sana... kusimama kama chuo.. Munga nikuambie ukweli wakufunzi wengi walikuwa wanalalamika sana... Prof Nwaogu.. Zigler... H. Moshi... hicho chuo kilikuwa kinaitwa MUNGA'S UNIVERSITY... bro Mke wako amekuangusha sana... Kingazi... hayupo pamoja na ww.... Mwinuka kuwa naye makini.... (akiwa Lwandai kuna mwaka flani Alitembea na magongo) muulize atakuambia ilikuaje... ha ha... mm naishi misheni mlalo... ha ha ha... Any way *RIP Dr Sechambo*.. ulikuwa na maono ya mbali sana.
 
Binamu yangu alinambiaga kuwa kuna prof wa elimu maalum alinyanyaswa akanyimwa haki zake ...ikabidi auze mali zake aondoke kumbe ni huyo
Nwaogu yule Mnigeria bila shaka. Yule babu alikua anapendwa mnoooo and ue knew what he was doing lakini treatment alokua anapata chiniya "uongozi" wa maza ulimfanya aondoke bila kuaga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nwaogu yule Mnigeria bila shaka. Yule babu alikua anapendwa mnoooo and ue knew what he was doing lakini treatment alokua anapata chiniya "uongozi" wa maza ulimfanya aondoke bila kuaga

Sent using Jamii Forums mobile app

Nwaogu, moja ya ishu iliyo muudhi kabisa, mbali na nyingine, ni swala la work permit, chuo kiligoma kumshughulikia mbali na madhila aliyokuwa akiyapata kutoka kwa uhamiaji.

Nyendo zote za Munga na mkewe katika maisha mengine, ambayo siyo ya kiroho, jumlisha na picha tutaziweka tu hapa kumsaidia mshana jr..
 
[emoji120][emoji120][emoji120]nasubiria kwa hamu
Nwaogu, moja ya ishu iliyo muudhi kabisa, mbali na nyingine, ni swala la work permit, chuo kiligoma kumshughulikia mbali na madhila aliyokuwa akiyapata kutoka kwa uhamiaji.

Nyendo zote za Munga na mkewe katika maisha mengine, ambayo siyo ya kiroho, jumlisha na picha tutaziweka tu hapa kumsaidia mshana jr..

Jr[emoji769]
 
Nimesoma hapo huyo mama mpuuzi sana aliwahi kusema chuo kikifungiwa majengo atafugia kuku

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuh kumbe ulikuwepo eeh
Siku ile tunamshupalia apunguze ada akajifanya kutoa majibu ya kunya..
Sasa mwambie aje nimfundishe namna ya kufuga kuku...

Halafu hawa wajinga wametudhulumu hela zetu ngoja nitawafungulia uzi.
 
Hii migogoro ya kuwakataa viongozi wenu nyie KKKT ni ya miaka yote, jitafakarini kwanza.

Lakin kwa sisi watanzania wa kawaida Dr. Munga tunamkubali sana na tunajua uwezo wake wa akili, hayo mengine mnayajua nyie wanadayosisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hajapingwa kwa uwezo wake wa akili anapingwa kwa kwenda kinyume na katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua hapa jukwaani wanamfahamu Munga wa mitandaoni mkosoaji wa serikali hii.. Hawamjui Munga katika uhalisia wake

Jr[emoji769]
Nakumbuka nilipokua mdogo nikiendaga likizo kwa babu huko bumbuli lushoto kuna msitu mkubwa wa kanisa, nilikua nikiwasikia wazee wakilalamika msitu mkubwa vile umevunwa halafu wanaambiwa mbao zinaenda kupaulia hospitali, sasa naanza kuhusianisha na haya uliyoyaandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natural n planted forests are the beauty of Usambara mountains... Tje The monster has harvested them all and without replacing
Nakumbuka nilipokua mdogo nikiendaga likizo kwa babu huko bumbuli lushoto kuna msitu mkubwa wa kanisa, nilikua nikiwasikia wazee wakilalamika msitu mkubwa vile umevunwa halafu wanaambiwa mbao zinaenda kupaulia hospitali, sasa naanza kuhusianisha na haya uliyoyaandika

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr[emoji769]
 
Unaweza sema ni lini Roman Catholic wameingia kwenye mgogoro?? Mgogoro wa pesa?? Achana na migogoro ya kina Privatus Karugendo na Kina Fr Kwela
Migogoro ipo popote sema KKKT huwa hawafichi kitu wanaweka wazi ndio maana inaonekana kama wana migogoro MsemajiUkweli,

Jr[emoji769]

Sent using, Mashikoro Mageni
 
Basi KKKT ni ina waumini dhaifu na wasio na maono. Mtu mmoja anayeendekeza dunia anawasumbua vipi?
Tatizo anataka kutumikia mabwana wawili. Lazima afeli sehemu moja.
20200413_164846.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama inafichwa mimi nitajuaje? RC sio anointed kuwa ni wakamilifu ni mara ngapi tumeona migogoro ya mapadre kuwachagulia waumini viongozi? Mgogoro wa hivi karibuni kabisa ni wa Kanisa la Kawe
Unaweza sema ni lini Roman Catholic wameingia kwenye mgogoro?? Mgogoro wa pesa?? Achana na migogoro ya kina Privatus Karugendo na Kina Fr Kwela

Sent using, Mashikoro Mageni

Jr[emoji769]
 
Pole
Hizi ndio sababu ambazo zilinifanya nikaacha kwenda kwenye kanisa la kilutheri.
Nilifikia usharika moja wa hapa Tanga kila siku ni kuchangia hela kwenda makao makuu.
Nikakaa chini nikawaza kama Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ina waumini 300000 tu na kila mmoja akalipa kwa mwezi mmoja shs 20000

300000 X 20000 = 6,000,000.
6 Billion!!!!!

Hilo deni lingekuwa limelipwa zamani ila inavyoonekana walikuwa wana kula hizi hela haiwezekani miaka na miaka mnalipa tu deni.
Huu ni wizi wa wazi kabisa.

Please watanzania wote sio wajinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilimwambiaga mtu alieniletea kadi kuchanga kwa mara ya nne nikamwambia kwa kuwa wameshindwa kujisimamia basi iteuliwe bodi ya kukusanya pesa na kulipa na kutoa update deni kiasi gani kuliko kuwaambia watu changeni tu hawajui wanalipa mpaka mwaka gani.
Nikamshauri mwl mmoja nikamwambia km chuo kilikua na wanafunzi kimefurika mpaka pakukaa tabu km wanavyosema wenyeji ilikuaje wasilipe madeni ya tra na mengine ambayo tangu kinaanza hawajawai kulipa na pesa zilikua zikikusanywa zinaenda wapi?
Mwisho nikamwambia yule mwl kuwa poleni msimsingizie magufulu.tcu waliwaambia mjrekebishe tangu eni za jk. Mkachukulia poa..anko jpm hajaongeza hata sharti gumu zaidi ya yale ambayo enzi za mjomba jk aliwaambia hamkutimiza...msije mkasingizia siasa. Akasema sio sisi ni baba ndo hataki mashart yafuatwe.na bora mseme nyie waumini sie ukiongea asubuh kazi huna
 
Wapendwa Wana DKMS - KKKT, Salaam katika Kristo Yesu Mkombozi wa wanadamu = Redemptor Hominis!

SABABU ZA KUFANYA MATENGENEZO DKMS - KKKT.

"Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua"
Mithali 29:2.

Inawezekana wengi wenu hamjui kwanini kunahitajika kufanyika matengenezo ya haraka DKMS - KKKT; ni kwamba zipo sababu nyingi sana zilizopelekea jambo hilo:

1. Kuinusuru Dayosisi isiendelee kuongewa madeni.
Kwamba; Uongozi uliopo sasa ambao hauamini kuwa muda wao Kikatiba umemalizika unaendelea kulimbikiza madeni, na hawawezi kufanya muujiza wowote. Deni la SEKOMU tu ni kizungumkuti. Tumshukuru Mungu Ripoti ya Kamati ya Reweta imeshapatikana yote mtayaona kwa uso na macho; hamtaamini jinsi Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu cha Sebastian Kolowa kilivyohujumiwa na kuleta adha kwa Wafanyakazi na Washarika.

2. Kwamba pia Watumishi wengi wa DKMS - KKKT, wanaishi maisha ya dhiki sana, Mishahara na posho zao hawajapata kwa muda mrefu sasa, sijui na janga hili la Corona wataishije maskini ya Mungu. Watumishi hawa wanaogopa kupaza sauti zao; lakini Jipeni moyo Mtetezi wenu yu hai: Msiogope!

3. Kwamba Vituo vingi vya Dayosisi viko hoi(ICU). Vuga Press imefungwa, Bangala Seminary hoi, Lwandai hoi, Hospitali ya Kilindi yachechemea, Bumbuli Hospital nayo ni tia maji tia maji. Hali ni mbaya, kama husadiki tembelea Vituo hivyo utajionea mwenyewe.

4. Kuvuruga uhusiano wa DKMS na marafiki wa Ujerumani.

Hayati Baba Askofu Dkt Sebastian Ignatius Kolowa, ThD, alianzisha Urafiki baina DKMS na Makanisa ya Ujerumani, na mashirika mbalimbali ya Kitume ya Ulaya. Urafiki ulikuwa na manufaa makubwa sana katika Dayosisi hii. Marafiki hao walisaidia sana katika uwanja wa? huduma za kijamii; kama vile, Lutindi Mental Hospital, Irente School for the blind, Irente Children's Home, Usambara Technology Center, ATIFA, Irente, Irente Rehabilitation Center, Rainbow School. Vituo hivyo vilisaidiwa sana kutokana na Urafiki huo. Baada ya Kifo cha Mzee Askofu Kolowa, Dayosisi ikaongozwa na Mt Petro Baba Askofu Joseph Jally, tunamuita Mtume Petro kwakuwa hana makuu, ni? mpole, mnyenyekevu, mwenye upendo, ni mtu wa sala na maombi, alizifuata nyayo za Mtangulizi wake. Akaicha Dayosisi katika hali njema.

Sasa huyu baada ya Askofu Jally, ndio kaiweka Dayosisi kitanzini.

5. Mahusiano ya DKMS na Serikali.

Tokea enzi ya Askofu Dkt Sebastian Kolowa, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ilikuwa na mahusiano mazuri na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wala hakukutokea chokochoko yoyote. Ushirikiano ulijengwa katika huduma za kijamii, kutembeleana, kushauriana na kuombeana kwa amani. Hata Mzee Askofu Jally, alidumisha mahusiano mazuri.

Sasa kiyangayanga ni kwa huyu Mwanaharakati Askofu wa DKMS asiyetaka kustaafu, kosoa weee Serikali, mapovu yakimtoka, huko yeye mwenyewe akiwa na boriti limemzinga, (Mathayo 7:5). Ukiishi kwenye nyumba ya vioo usiwarushie wengine mawe: Ona sasa kwa matumizi yako mabaya ya madaraka (Mr Mkuu wa Chuo SEKOMU, Mrs Makamu Mkuu wa Chuo, na huku Katibu Mkuu wa DKMS ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha SEKOMU, aah majanga): umeleta janga la kutolipa Kodi ambayo Dayosisi inadaiwa, mamilioni na mamilioni, ujanja wako uko wapi?. Ubadhilifu ndio ulioifikisha DKMS hapa, TRA, WFC, NSSF kote wanadai.

Usijidanye kulipa Kodi ni Amri halali tena ni agizo la Mungu: Soma Injili ya Luka 20:21 - 26.

6. Kuvuruga uhusiano wetu na Madayosisi mengine.

Kama hujui Askofu, DKMS imekuwa na mahusiano ya kihistoria na kindugu; nikuingize darasani kidogo pamoja na hiyo PhD yako, kwa kukupa mfano wa Madayosisi ya Kanda ya tu: Tumekuwa ndugu, udugu wetu ulijengwa na Mababa Askofu Moshi, Askofu Kolowa, Askofu Kweka na Askofu Mshana wa Pare, Askofu Jally na Askofu Msangi. Jamii yetu imechanganyika mno, tunaoshirikiana mno. Uliza siku mwili wa Mzee Askofu Kolowa, uliposafirishwa toka KCMC kwenda Lushoto, mji mzima wa Moshi na Pare ulisimamisha shughuli zao kwa kumuenzi Mzee Askofu Kolowa, walimwona kuwa ni Baba yao. Sisi Waumini wa DKMS hakuelewi kwanini unamshambulia Mkuu wetu wa Kanisa? Halafu unawaeleza washarika Kanisani ili iweje?

Ukome kabisa na uache tabia hiyo. Tena Baba Askofu Charles Mjema wa Dayosisi usimfuate Askofu Munga atakuingiza chaka.

7. Kuwafukuza na Kuwasimamisha Uchungaji baadhi ya Watumishi.

Kama Baba Askofu Kolowa asingemsihi Mkuu wa Chuo cha Makumira Mch Dkt Hans Mwakabana asikufukuze Chuo cha Uchungaji kutokana na uliyoyatenda ukiwa usingefikia hapo ulipofikia (kisa chenyewe tunakitunza).
Umefukuza Mch Dkt Kopwe, Dean Mch Mwamboza, Mch Crispus Kanju, umewasimamisha Mch Peter Zakaria na Mch Dickson, bila sababu za msingi . Aliyekuwa na Katibu Mkuu Mch Godrey Hermann umemfanyia figisu figusu, akaamua kukuachia ofisi. Ulishamsimamisha Mch Shekifu na Dean Mmaka pia. Wote hao umewaumiza, tunajiuliza ni jiroho gani lililokukamata.

8. Kutowathamini Watumishi Wastaafu.

Hivi Askofu Dkt Stephen, unapata muda wa kuwajulia hali Wastaafu pamoja na wajane!. Huna muda huo uko bize. Pension pia huwapi, wakati unataka maslahi makubwa.

9. Mafao ya Askofu Munga atakapostaafu.

Ulipeleka madai ya mafao ya kustaafu kwako kuwa:

a.Ujengewe Nyumba kubwa ya kuishi,

b.Ujengewe Nyumba ya vyumba vitatu (3), kwa ajili ya Watumishi.

c.Uwekewe Watumishi wataolipwa na Dayosisi yaani Dereva, walinzi, wapishi na mfanyakazi wa bustani.

d. Ununuliwe gari kubwa la kifahari V8 au VX

e. Ujengewe bwawa kubwa la samaki, ili uepuke kula RED MEAT(nyama nyekundu), aloo rahaa utamu!

f. Alipwe mshahara unaotosheleza, na kutunzwa hadi ukamilifu wa dahari.

Je, watangulizi wako walifanyiwa hivyo? Wafanyie kwanza halafu wewe ndio ufuate.

Mwisho Wachungaji, Watumishi na Washarika wote wa DKMS msidanganyike; Muda wa kipindi cha Uaskofu wa Munga umemalizika, hana mamlaka ya kuongoza Mkutano Mkuu wala Kikao chochote kabisa.

Bado anaendelea kutumia Gari la Kanisa na Posho, yuko DSM na Wasaidizi wanapanga mkakati wa kujinasua.

FAHAMUNI KANUNI YA 6 ya Katiba ya DKMS - KKKT ya Mwaka 2000:

E.
1. Askofu
c. Askofu atatakiwa kustaafu Kikatiba akiwa na umri wa miaka sitini na tano (65) ya kuzaliwa, lakini anaweza kustaafu kwa hiari yake akiwa na miaka sitini (60).

Habari ndiyo hiyo.

Tena Kanuni hiyohiyo ya 6:

F. Ukomo wa Uongozi.

Kiongozi anaweza kuacha kazi, kuachishwa, kujiuzulu ama kufukuzwa ikiwa;

1. Hatatimiza wajibu wake au akivunja Kanuni na Sheria za Dayosisi.
4.Kustaafu akitimiza umri wa kustaafu kisheria.
5. Kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe.
6. Kujiuzulu kwa kuwajibika.

Jiulize anatokaje hapo?

Ni jukumu lake kutafakari na kuchukua hatua kwani Neno la Mungu lasema:

"Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;
Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 22:3

Wakatabahu,

+++ Sauti ya Kijito Kedroni.

Jr[emoji769]
 
Ni wakati sasa wa kusikia kutoka upande wa Askofu pia.Ni muhimu sana kusikia kutoka kwake ili tuweze kupima kama tuhuma hizi ni za kweli au ni siasa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom