Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Status
Not open for further replies.
Hivi wataalm wa Aviation wanasema kuhusu hizi tuhuma?

Lakini kwa Tanzania ya leo sishangai kitu

Hata sijui nililikosa vipi hili dili maana waliokula sasa wanachekelea tuu benki
 
Hivi wataalm wa Aviation wanasema kuhusu hizi tuhuma?

Lakini kwa Tanzania ya leo sishangai kitu

Hata sijui nililikosa vipi hili dili maana waliokula sasa wanachekelea tuu benki
 
Nimepanda hii ndege inayotuhumia jana tu, from Dar to....! ukweli management ya ATC ime change sana, wapo very serious na biashara, wahudumu ni wazuri na wapo committed hasa, kabla ya uzi huu kubandikwa, kwasababu na mimi ni mTanzania nilifanya mahesabu yafuatayo:-

Trip moja from Dar to Mwanza ni Tsh 166,000/= kwa abiria anaenda one trip only, lakini kwa wale wanaokata go and return Mwanza to Dar ni Tsh 257,000/= well, let us just assume kwamba abiria wote ni wa go and return, of course nia hapa ni kua na hesabu ambayo ni most minimum, kama kila Trip ndege itabeba abiria 50 tu it mean kwa trip moja ndege hiyo itakua imetengeneza pesa hizi.

Chukua nusu ya hiyo 257,000/= gawanya kwa 2 itakupa 128500/= then kwa hao abiria 50 itakupa 6425000/= ndege hii hufanya safari sita kwenda na kurudi Mwanza, yaani asubuhi ya saa 12 to Mwanza, then saa 2 to Dar, kisha saa za mchana to Mwanza again, machana huo huo hurudi Dar tena then saa 11 jioni inatia timu Mwanza while mbili usiku inarudi Dar, weka hesabu hiyo mara sita yaani 6425000 kwa 6 sawa 38,550,000/= sasa hiyo ni pesa ya siku moja, weka kwa hiyo miezi 3 ya ukodishwaji, assuming mwezi utakua na siku 90 then jumla ya pesa kama Gross itakazo zipata ATC kwa deal hili ni Tsh 3,469,500,000/= mbona hili deal linalipa sana tu, anyway twende kwenye hiyo bill ya mwezi ya USD 200,000, kama exchange rate ni 1=1550 then USD 200,000 ni sawa 310000000/= wakati siku moja umelala na Tsh 38550000, kumbukeni pia, Distance from Mwanza to Dar kwa ndege ni Km 450 tu.

Mmmm, wakuu, tuache majungu, Mwakyembe ameweka dira, hata bei za Precion naona kama zimeshuka hivi, i think because of compitetion!

:target::target::target:
 
Huu ni umbeya tu. No evidence. Hizi ni chuki bianfsi tu. Ungeweka documents za kuthibitisha hayo ynayoongea. Otherwise ni zaidi ya upepo.
Jinsi siku zinavyozidi kwenda ubongo wa Mtanzania unazidi kuwa mdogo wakati wa jirani zetu kama Kenya na Rwanda unazidi kuwa mkubwa. Lecturer akishakupa hints darasani, nenda kachimbe upate zaidi. Sasa ukitaka kutafuniwa kila kitu hata rangi ya njano itafika hatua tutasema ni nyeupe.
 
Its getting emotional here...

Ishu sio emotional
ishu ni kuwa huyu mwakyembe ni katika kundi la wanasiasa ambao wanapewa chapuo na wana JF ambao wanasema CCM wote ni mafisadi lakini kwa huyu wako tayari kumwaga damu kumtetea

double standards za JF hizo
 
Duuuh, usafiri wa treni ndani ya jiji la DSM umeleta mambo..! acha wivu wewe, mkubali kuwa jamaa anaweza. Au mnaogopa biashara zenu za malori ya mizigo kwenda mikoani zitakufa. Jamaa hataki mchezo reli zote zitafunguliwa, nyinyi endeleeni na majungu yenu.
 
Haaa,,, ahaaaa nimeamini nyie ndiyo mnaotaka kufifisha juhudi za Mwakyembe, Ila Mwakyembe achana na wapiga debe wa Mafisadi,,,,, endelea kuwafumua na kuwasaka popote walipo Bandalini,
 
FAST JET tayari washaanza kukimbia

PW nao wameshusha ndege

sisi huku bado tunamwona Mwakyembe bado safi kwenye hili lindi la ufisadi ATC
 
Kuna mtu kaandika kwenye mtandao kuwa waTz akili zetu zinazidi kusinyaa wakati za wa Kq na na wakagame zinapanuka kadiri muda unavyoenda. Hako kandege kamoja mapovu yanatutoka ndani ya forum! namquote MD wa KQ kwenye gazeti lao la msafiri la November 2012`Despite these challanges (kupanda bei ya mafuta, gharama za uendeshaji nk) we remain committed to improving our service across our network which is approaching 60 destinations. Since August KQ has taken delivery of a new Embraer 190 each month till March 2013." another quote "....plans to increase the number of aircraft from 34 in 2012 to to 115 over 9years. Rwanda airline wameanza 2001 na ndege moja ya kukodi, sasa wana ndege mpya 7. Great thinker tunaja uzi kujadili ndege mmoja ya kukodi kwa national flag carrier. Jamani viongozi wetu wameua utaifa wetu. Nchi nzima imeshindwa kusimamia shirika ambalo lingeuza utalii wetu nje yanchi. Jamani ebu tanze kuthink big. kila siku mawazo madogo madogo yanatumaliza. Tunajadili kandege kamoja, jamaa anapanga ndege 115. Tunajadili Mwanza Dar Mwanza. Jamaa anaongelea destination za miji yote mikuu Afrika. Inakera sana. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kama uliyajua haya ulingoja nini kutoa mapema ? Au ni mmoja wa waathirika wa speed za mwakyembe ? Umechelewa.
 
Taarifa hii imekaa kinafiki nafiki na inaonekana imeletwa mahsusi kushambulia upande wa Mwakyembe.

Ngoja wenyewe wazione hizi tuhuma. Nina uhakika watakuja na majibu stahiki.
Kuna majungu mengine ya kitoto sana,
Mwakyembe amekaa hapo wizarani kwa muda gani???
Naona waliotupwa nje wanasikia baridi sana kwa hiyo wanajaribu kurudi au wawe wengi ili kuwe na ka joto kidogo nje
 
Ni mkanganyiko fulani wa mawazo!

Mleta mada anaonyesha mweelewa kidogo sana wa mambo ya usalama wa anga,Umri wa ndege haupimwi kwa muda iliotengenezwa tuu, bali masaa ya kuruka .

Pia mwenye chuki binafsi na Mwakyembe, Amezidi kujikanyaga hasa alipomuhusisha CAG.Namshauri kwanza atatue mgogoro wake wa ndani ili aweze kuweka mtiririko unaoeleweka. Atenganishe tuhuma, chuki binafsi na majungu.

Pia ajifunze na kupokea ushauri kwamba uropokaji hadharani siyo njia muafaka ya kuwakilisha ujumbe.

Tunataka data!!
:glasses-nerdy:

you are a great Adviser.
 
Mtoa hoja ana hoja ya msingi sana wachangiaji Wengi wanafuata upepo ulipo na siyo hoja ya msingi ufisadi wa mwakiembe
na kukodi Ndege chakavu ,na Rwanda Kununua Ndege mpya 4 jibuni hoja tz wanashindwa nini
 
Mtoa thread ni mmoja wa wale wale e e e e e e e e e e, umeona e e e eh h h.

Hukumu kama hizi zinarudisha nyuma maendeleo, kabla ya kumhukumu mtoa uzi, ungefanyika uchunguzi wa kina kuona ukweli wa tuhuma hizi. Kwa mtazamo huu tunaweza kupinga hata mambo ya msingi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom