ATC Rekebisheni hili kabla hapajawa jioni

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Kampuni yetu pendwa yenye ndege tulizonunua wenyewe kwa kodi zetu kuna mambo inatakiwa warekebishe kidogo ili waende sambamba na ushindani wa kibiashara.

1.Kuambiwa ndege imeahirisha safari au itachelewa kuondoka kwao ni jambo la kawaida
2.Ndege hata kama imeahirishwa hawana utaratibu wa kuangalia namna wateja wao watakavyolala au hatima yao itakuwaje either kuwapangia hotel au la yaani wanaachwa tu utajiju

Usiku wa kuamkia jana ndege ilitoka sehemu flani siitaji kuwasetiri watu wa shift hiyo.humo ndani kulikuwa na wasafiri ambao walikuwa wanakwenda South Africa kilichotokea ndege ilichelewa sana kuondoka kufika dar ndege yao ya connection wakaikosa kwa maana hiyo wakahesabika ni no show.Ila waliambiwa ndege ya Airlink ambayo ilikuwa wapande wakitaka tena ni Jumatatu hivyo ingebidi waingie gharama mifukoni kutafuta hotel za kulala na bado nauli tena.

Wawili kati ya hao walikuwa na meeting muhimu sana Africa Kusini ilibidi wazame mifukoni mwao wapande Air Malawi kuunganisha hadi Africa Kusini. Huyu mmoja yeye aliamua kupanda KQ hadi Nairobi akafika Africa kusini saa sita usiku na robo.

Nafahamu biashara ya ndege ni pasua kichwa sana ona SAA South Africa Airway wanavyoyumba hata KQ
walishayumba wakakaa sawa.

Raisi aliyepita marehemu na mama wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha serikali yetu nayo inakuwa na ndege zake alidiriki hata kucheza mchezo mmoja wa rafu sana Fastjet wakaondoka yote ni kufanya shirika letu li flourish.

Kwa mtindo huu hao wateja wa jana sidhani kama kwa ridhaa yao watakubali tena kupanda ndege ya ATC kwa adha waliyoipata walikuwa watatu wataambia watu watatu na watatu watawaambia watatu.
Hata upande wangu kwa kweli pamoja na kwamba nina mapenzi na nchi yangu lakini nikiwa na safari yangu ambayo ni ya emergency sana siwezi kukata ticket ya ATC asilani labda kama ni trip ambayo haina ulazima wa tharura kwenda kula starehe mahali.

Rekebisheni haya tafadhali ndege zetu ni nzuri tunazipenda
 
Back
Top Bottom