Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Status
Not open for further replies.
Sijaenda deep kujua ukweli wa aliyosema mtoa hoja isipokuwa ukiangalia mwenendo wa ATC unaweza kuunganisha points ukapata majibu.
Tatizo la bongo hatuna mipango ya maana. Baada ya ATC kusuasua nilitegemea kuona kipindi cha mpito ambacho kingekuja na mpango mkakati wa miaka 50 mpaka 100. Badala yake tunachokiona sasa ni kesho kutakuchaje!? Hili ndiyo tatizo langu kwa miradi mingi ya bongo. kila siku tunajenga barabara dar ambazo ni short term. hatuna muda mrefu huu mradi wa sasa wa mabasi yaendayo kasi utaonekana umezidiwa na tutasikia flyovers in Dar is inevitable wakati leo inaonekana kama ndoto za alinacha.
Anyway, tusisahau ule usemi usemao "mtu kujamba chooni si ajabu"
 
Dogo naona ,upo kazini boss wako Mataka hajambo, mwambie sis atcl bado tunadunda kama kawaida. mwambie akupe umbea mwingine ulete humu.
Tuache ujinga,tujadili issue na sio mleta uzi,mambo aloeleza ni msingi kiabisa,kwanini tuendelee n a mitumba? badla ya kununua ndege mpya? kichwa ni kwa ajili ya ubongo sio kuoteshea nywele jamani,upuuzi huu mpaka lini?tujadili issue na sio personality,na hapo ndipo tutakuwa great thinkers.namalizia si mwakyembe wala nani ndani ya ccm wote wananuka,hakuna anayestahiki ,au kusawili urais.
 
Wakisoma uzi huu wapuuzi wachache wanaonufaika na ufisadi wa aina hii wanabaki kupindisha mada,ukweli ni kwamba Mwakyembe tusimwamini sana na kumwona ana extra mind.Alipiga makelele ya richmond kumbe alikuwa mmoja wa washika dau wa mpango wa umeme wa upepo kule Makambako.Sasa hili la ndege yenye umri mkubwa kuliko mbunge wa CHADEMA Mhe.David Silinde ni vema tukaliangalia vizuri kwani bila shaka kwa mfumo huu shirika litakuwepo kama picha tu bila mchango wowote katika uchumi maana hakutakuwa na faida ila gharama za uendeshaji...Hivi ni kweli Watanzania tunataka kushiriki biashara ya ushindani au tunaigiza? Sijui CCM imewafanya nini viongozi wake kiasi cha kukosa mipango ya miaka 50 ijayo.Miaka 30 ijayo Wanyarwanda wakitupiku kimaendeleo,wadhaifu wa Tanzania tutawasikia wakisema 'Rwanda ni ndogo kuliko Tanzania' bila kujadili kwamba hata rasilimali zao ni chache ukilinganisha na Tanzania ila watu wake wameamua kuweka upuuzi pembeni.
 
wakati sisi tuko bize kutetea mafisadi, KENYA AIRWAYS wao wanaendelea kupiga hatua kwani wameamua kugeuza ndege zao 6 za aina ya 737-300 ili ziwe zinabeba cargo. Hawa jamaa business plan yao iko sound na hawataki mchezo kabisa.

dCQ6Y.jpg

kwa maneno mengine wao wanasema kuwa wanataka 10% ya revenues zao kwa mwaka zitokane na biashara ya cargo.
Na wamedhamiria kuchukua routes hizi zote kwa ajili ya : Juba (South Sudan), Luanda (Angola), Bangui (Central African Republic), Douala, Yaoundé (Cameroon), Kigali (Rwanda), Entebbe (Uganda), Dar-es-Salaam (Tanzania), Kinshasa (DRC) and Bujumbura (Burundi)
 
Ili tuondokane na haya mauza mauza katika nchi hii, tunahitaji mambo makuu mawili.

1. Siasa Safi

2. Uongozi Bora

P1020053.JPG

Huko sawa kabisa juhudi za dhati zinatakiwa na hazitaletwa na viongozi waliopo madarakani bali na wananchi wa Tanzania kwa ujumla wetu bila kujali itikadi za vyama vya siasa wala dini.
 
Tuache ujinga,tujadili issue na sio mleta uzi,mambo aloeleza ni msingi kiabisa,kwanini tuendelee n a mitumba? badla ya kununua ndege mpya? kichwa ni kwa ajili ya ubongo sio kuoteshea nywele jamani,upuuzi huu mpaka lini?tujadili issue na sio personality,na hapo ndipo tutakuwa great thinkers.namalizia si mwakyembe wala nani ndani ya ccm wote wananuka,hakuna anayestahiki ,au kusawili urais.

unataka wakutukane?
 
Dr-Harrison-Mwakyembe.jpg

Mimi katika vitu vilivyonishinda humu ni mabishani ya nani zaidi kati ya CCM na CHADEMA. Sasa nimeona bora nikufahamisheni Mwakyembe ambaye anajisifia kuwa mpinga rushwa mkubwa alivyokuwa fisadi na ushaidi wote nauweka hapa na kama kuna mtu anabisha aendelee.

Kwa kifupi wafuatao wanahusika kwenye huu wizi:

HARRISON MWAKYEMBE
MANAGEMENT NZIMA YA ATC
BODI YA ATC
KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA
EXTERNAL AUDITORS WA ATC
LUDOVICK UTUOH AMBAYE NI MKAGUZI MKUU WA SERIKALI

Tuhuma zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Shirika la ndege la taifa (AIR TANZANIA) waliamua kukodisha ndege yenye umri wa miaka 32 aina ya B737-200 iliyozeeka na mbovu kutoka kampuni ya Africa Kusini inayoitwa Star Air Cargo.

2. Ndege hii ilianza kufanya kazi mwaka 1980 kule UK, na ilikuwa inatumiwa na kampuni inayoitwa BRITISH AIRTOURS na baada ya hapo ilikodishwa na mashirika zaidi ya 20 Ulaya na Latin America.

3. Mwakyembe, Menejimenti na bodi mpya ya ATC walikubali na kupitisha ukodishaji wa hii ndege kwa kiasi cha dola laki 2 (200,000 US Dollars) kwa mwezi katika miezi 3 ya awali ya ukodishaji kinyume na ushauri ambao Mwakyembe na maswahiba zake wa ATC walipewa.

4. Mkataba unaonyesha kuwa itabidi ndege hii itabidi iruke kwa masaa 150 kwa mwezi at a rate of $1,350 (kwa kila saa)

5. Mkataba unaendelea kusema kuwa ATC LAZIMA wagharimie gharamza zote za ma crew ambayo iko estimated to be in the region of a further $80 – $100 PER DAY & PER INDIVIDUAL !

(Katika mazingira ya kawaida msomaji utaona gharama ni ndogo lakini ukweli ni kubwa sana uzingatia kuwa ndege yeneyewe inasafiri kwenda sehem 3 tuu yaani kati ya Dar es Salaam – Kilimanjaro – Mwanza na hii yoye iko funded na walipakodi wa Tanzania).

Sasa ukweli ni kuwa kama kweli Mwakyembe & kundi lake wana nia nzuri wasingekubali dili hii ipitishwe kwa kuzingatia kuwa kwanza ndege inge cost less kuikodisha kuliko gharama ambazo hawa mafisadi wamepitisha, na pia hizi gharama za malipo kwa saa ni kubwa mno na hapa ndipo Mwakwembe na kundi lake la mafisadi wanakula zaidi kwenye huu mgao.

Suala lingine la kuzingatia hapa ni operating costs ambazo Mwakyembe & his crew wa ATC ni uhuni mtupu kwani ndege ina miaka 32 na gharama za uendeshaji na hasa za matumizi ya mafuta ni kubwa mno ukilinganisha ndege za kisasa.

Kwa msiojua ni kuwa gharama za mafuta (fuel costs) kwa kawaida zinachukua around 40% ya overall costs lakini kama shirika linatumia ndege za kizamani basi ni wazi kuwa gharama zitaongezeka zaidi. Na uhuni uliofanywa na ATC wakishirikiana na wahuni wenzao pale wizarani kwa Mwakwembe ni kupiga rangi hizi ndege wakati wakijua wazi kuwa walipa kodi wanataka kujua mikataba iko kwa maslahi ya taifa (NATIONAL INTEREST).

phpCbr2d6.jpeg

Moja kati ya maswali ya kujiuliza ni kwa nini Mwakyembe na ATC walikataa kuchukua ndege kama CRJ ambazo ni ndogo zaidi lakini zina fly economically lakini pia ni kubwa kiasi kiasi cha kurestart hii biashara ya shirika kama ATC. Lakini hii pia ni mfululizo wa uhuni unaoendelea kama ule wa awali wa kukodisha ndege toka kampuni ya Arabuni ambayo intugharimu sana sisi walipa kodi kama ile ya uhuni wa awali wa ukodishaji wa Airbus.

Sasa huyu Mwakyembe ambaye anajifanya ni kinara wa kupiga vita ufisadi anakubali na amepitisha huu uhuni wa ATC ambao utamgharimu zaidi mlipa kodi. Huu ni uthibitisho kuwa wanaolack vision si wale wa (Pemba + Zimbabwe ) pekee lakini mpaka huyu mwanasheria kama Mwakyembe ambaye anaendeleza uhuni wa stop gap measures.
tzmishapix.jpg

This half baked measures za Mwakyembe et al zinathibitisha kuwa everything is fundamentally wrong with his ministry and ATCL in particular. Kwa kifupi, they lack leadership, they lack vision, and most of all, they lack planes and money.

Sasa kaeni mkao wa kuona wanaleta maombi ya kutaka wapewe pesa zaidi ili waendelee kula. Na news zilizopo kwenye corridor za ATC ni kuwa wana haha kama mbwa mwitu ili warejeshe safari za nairobi na hasa baada ya player mpya chini ya (FAST JET) kuingia kwenye soko.

BTW

Nadhani mnaikumbuka ile ndege ya ATC iliyoanguka kule mwanza? bas ndio model hiyo hiyo aina ya B737-200 kama hii mbovu na iliyozeeka ambayo Mwakyembe & his crew wanatuleta.

uhondo zaidi uko hapa:

Air Tanzania Company Limited (ATCL) has suspended its contract with the Dubai based aviation company, Aero Vista, that saw the latter lease a Boeing 737-500 plane to embark on domestic flights.

Captain-Milton-Lusajo-Lazaro.jpg

ATCL CEO, Captain Milton Lusajo Lazaro

ATCL leased a Boeing 737- 500 plane with the capacity to carry 108 passengers, which has since then been embarking on the national flag carrier’s Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza routes before launching the Dar es Salaam-Hahaya (Comoros) route last month.

The airline’s Acting Chief Executive Officer, Captain Milton Lazaro, said the company had reached that decision to ensure a win-win situation and sustainability from the contract.

He, however, said the company intends to undertake a contract review with Aero Vista adding that the company may go in for another company if the two sides do not reach a consensus on the matter.

“We had decided to suspend the contract earlier entered upon with Aero-Vista in order to ensure compliance with Government pre-requisite. We may be able to re-enter a new contract with them after discussions on revision of some clauses that do not favour a sustainable outcome.
4.jpg

“Passengers who are holding ATCL tickets have been reallocated alternative flights with other carriers and notified accordingly,” he said. He added that the national flag carrier will be able to be back on the routes after the completion of the maintenance exercise of its Dash-8 Q300 plane that is undergoing checks at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salam.

Captain Lazaro said, however, that only its Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza routes will be temporarily affected by the suspension urging that the airline continue with its three-time weekly flights between Dar Es Salaam and Hahaya (Comoros).

“We regret the inconveniences that have been caused to our valued customers, we take this opportunity to thank them for their continued support and reassure that, the resumption of these services will take place as soon as possible,” he said.

Source Daily News.

Wakati sisi tuko bize kukodisha ndege za miaka 32 na kutetea ufisadi wa akina Mwakyembe & Co, Rwanda wao wameamua kufanya kweli na kuwa nchi ya kwanza Africa kununua ndege 4 aina ya CRJ900NG ambayo wataalama wanasema kuwa ni the most economical short and medium range jets toka kwa kampuni ya Bombadier. (wataalam wa mambo ya ndege watakuambieni ubora wa hizi ndege kulinganisha na mtumba wa ATC)

BA-RwandAir_delivery_3.jpg

Hawa wa NyaRwanda ambao tumewashinda kwenye kila kitu (kasoro akili). Kwa sababu wakati sisi tuko bize kusifiana upuuzi wao wameopt kununua state of the art modern aircraft ambayo ina gharama za chini sana kulinganisha na mitumba ya akina Mwakyembe & ATC lakini pia wao wameunyesha pride ya KUNUNUA NDEGE MPYA badala ya kukodisha hizo ndege na hii inawapa sense of ownership na muhimu zaidi inawapa abiria confidence abiria wake wa safari zake za Africa na mashariki ya kati

Ndege hizi zina dual class configuration ya 7 business class seats kwa mpango wa 2×1 layout na 68 economy class seats katika mpango wa 2x layout, ambayo nadhani ni quite ideal for the short and medium distances ambazo Rwanda Air inasafiri.

Kwa kuonyesha kuwa hawa wa NyaRwanda wako serious, wao hawataki tena mitumba na wanaondoa ndege walizokodisha aina ya Dash 8-100 na badala yake wanaweka ngoma iliyokuwa advanced na kubwa zaidi zaidi toka Bombadier Q400, ambayo kwa sasa zinapatikana kwenye dual class configuration – type ya kwanza ilikuwa delivered kwa Ethiopian Airlines wiki chache zilizopita

Sasa hivi Air Rwanda inakwenda nchi 14 na wanamipango ya kuongeza frequencies za key destinations zaidi ya 40. Sasa wao hawafkiriii kushindana na ATC wao target ni kuwapiku KQ. Sisi tuko hapa hatujajua bado kama Tanzania ilitokana na Pemba na Zimbabwe au nchi ya kifikirika.

UPDATES: Ile safari ya akina Mwakyembe Ujerumani nayo inaelekea kuota mbawa kwani bodi ya Lufthasa nao wamechomoa kuwa na JV au kurudisha safari zao Tanzania kwa sababu hazina faida.

Hivi mwaka 1980 Mwakyembe alikuwa ni waziri tayari wa hii wizara ya uchukuzi ama vp mi mbona sielewi kabisa hapa???????????
 
Hello,
Sorry. Your income vs. expenditure accounting theory seems to be informed by, and therefore based on Mama Ntilie rather than airline business economics. It should be more than, but ought to include the number of flying aircrafts, routes, expertise, competent/skilled and professional management and political environment, to mention only a few. Airline business must break-even, not just counting cash, which in most cases (ceteris peribus) takes no less than five years.

What a Bull *hit
At least they help the price to go down, you better go back learn again
 
Kuna watu mna shida sana mjini na hizi NETWORK kuwa za mia mia ndo basi tena! Ni kukurupuka tu na majungu. Fanya kitu kimoja
Tenganisha, chuki, majungu, tuhuma na utaalamu then Uje tena labda utapata wasikilizaji!!
 
ahaaaaa paka mwenye kengele anataka kumkamata panya inawezekana kweli?Tafakari na uchukue hatua.
kuna msemo mmoja wa kingereza unasema the LOUDEST IN THE ROOM IS THE WEAKEST.
 
Huu ni umbeya tu. No evidence. Hizi ni chuki bianfsi tu. Ungeweka documents za kuthibitisha hayo ynayoongea. Otherwise ni zaidi ya upepo.
 
Kwa kifupi wafuatao wanahusika kwenye huu wizi:

HARRISON MWAKYEMBE
MANAGEMENT NZIMA YA ATC
BODI YA ATC
KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA
EXTERNAL AUDITORS WA ATC
LUDOVICK UTUOH AMBAYE NI MKAGUZI MKUU WA SERIKALI
Mkuu yaani watu wote hawa wawe wanaisibiri hiyo $200,000 sasa ishu ndefu kama dowans na EPS si wananchi wote tungepata thumni yetu
kajipange vizuri na wivu wako wa kike halafu uje tena

Tuhuma zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Shirika la ndege la taifa (AIR TANZANIA) waliamua kukodisha ndege yenye umri wa miaka 32 aina ya B737-200 iliyozeeka na mbovu kutoka kampuni ya Africa Kusini inayoitwa Star Air Cargo.

yaani wewe you know jack shit of aviation ndege haina uzee kwa kila kitu kinakwenda kwa time haalafu kinatolewa kuhusu ubovu ni lini imewaacha abiria ? ila tunaona Precision wana cancel kila mara wakikosa watu wa kuwapiga

2. Ndege hii ilianza kufanya kazi mwaka 1980 kule UK, na ilikuwa inatumiwa na kampuni inayoitwa BRITISH AIRTOURS na baada ya hapo ilikodishwa na mashirika zaidi ya 20 Ulaya na Latin America.
sasa unajaribu kuelezea kitu gani ? kwa ndege ikienda latin amerika haifai kuja Tanzania ?
3. Mwakyembe, Menejimenti na bodi mpya ya ATC walikubali na kupitisha ukodishaji wa hii ndege kwa kiasi cha dola laki 2 (200,000 US Dollars) kwa mwezi katika miezi 3 ya awali ya ukodishaji kinyume na ushauri ambao Mwakyembe na maswahiba zake wa ATC walipewa.
Bora hawa ime wainvolve watu wengi lakini ile ya mwanzi iliwa involve watu wawili tuu RIP Nundu na RIP Chizi hata katibu mkuu aliizuia kuruka

4. Mkataba unaonyesha kuwa itabidi ndege hii itabidi iruke kwa masaa 150 kwa mwezi at a rate of $1,350 (kwa kila saa)
sasa tofautisha na hii hapa;
1. Boeing 737-500 itabidi waruke masaa 250 kwa mwezi at a rate of $2100
2. Airbus 320 dry lease kwa mwezi ni $370,000 hapa itabidi uongeze insurance, maintenance reserve na makolokolo memgine kibao

sasa tunaomba utunyumbulishie ki[i ni cha gharama nafuu hapo juu
Serikali ilitakiwa impe Kaptain shirika lile long time lakini walidumisha urafiki

5. Mkataba unaendelea kusema kuwa ATC LAZIMA wagharimie gharamza zote za ma crew ambayo iko estimated to be in the region of a further
$80 – $100 PER DAY & PER INDIVIDUAL !

sasa tatizo lipo wapi Per diem kwao kimekua kitu haramu, mbona wabunge wenu mnawalipa per dem ilhali wanalala tuu bungeni
(Katika mazingira ya kawaida msomaji utaona gharama ni ndogo lakini ukweli ni kubwa sana uzingatia kuwa ndege yeneyewe inasafiri kwenda sehem 3 tuu yaani kati ya Dar es Salaam – Kilimanjaro – Mwanza na hii yoye iko funded na walipakodi wa Tanzania).
jamaa wanaenda Mwanza via JRO mara mbili kwa siku kitu ambacho kinawapa over 180 BH kwa mwezi

Sasa ukweli ni kuwa kama kweli Mwakyembe & kundi lake wana nia nzuri wasingekubali dili hii ipitishwe kwa kuzingatia kuwa kwanza ndege inge cost less kuikodisha kuliko gharama ambazo hawa mafisadi wamepitisha, na pia hizi gharama za malipo kwa saa ni kubwa mno na hapa ndipo Mwakwembe na kundi lake la mafisadi wanakula zaidi kwenye huu mgao.
mkuu unaweza kutuletea quote ya ACMI rate cheaper zaidi ya hii ? kuthibitisha madai yako

Suala lingine la kuzingatia hapa ni operating costs ambazo Mwakyembe & his crew wa ATC ni uhuni mtupu kwani ndege ina miaka 32 na gharama za uendeshaji na hasa za matumizi ya mafuta ni kubwa mno ukilinganisha ndege za kisasa.

hapa tuna nyumbulisha tena kwa mujibu wa mkataba
Boeing 737-200 inatumia 2.6 Tons/hour X150 BH monthly utilization = 390 tons per month
Boeing 737-500 inatumia 2.4 Tons/hour X 250 BH monthly utilization = 600 tonz per month
sasa nani atakuwa na bigger fuel bill

Kwa msiojua ni kuwa gharama za mafuta (fuel costs) kwa kawaida zinachukua around 40% ya overall costs lakini kama shirika linatumia ndege za kizamani basi ni wazi kuwa gharama zitaongezeka zaidi. Na uhuni uliofanywa na ATC wakishirikiana na wahuni wenzao pale wizarani kwa Mwakwembe ni kupiga rangi hizi ndege wakati wakijua wazi kuwa walipa kodi wanataka kujua mikataba iko kwa maslahi ya taifa (NATIONAL INTEREST).
mkuu haya madai yako yatachukuliwa hatua labda uende mwembe yanga ndio wata kuelewa, usichezie na JF home of great thinkers
Labda ndio maana umeleta jukwaa la sihasa
 
3. Mwakyembe, Menejimenti na bodi mpya ya ATC walikubali na kupitisha ukodishaji wa hii ndege kwa kiasi cha dola laki 2 (200,000 US Dollars) kwa mwezi katika miezi 3 ya awali ya ukodishaji kinyume na ushauri ambao Mwakyembe na maswahiba zake wa ATC walipewa.

4. Mkataba unaonyesha kuwa itabidi ndege hii itabidi iruke kwa masaa 150 kwa mwezi at a rate of $1,350 (kwa kila saa)

5. Mkataba unaendelea kusema kuwa ATC LAZIMA wagharimie gharamza zote za ma crew ambayo iko estimated to be in the region of a further $80 – $100 PER DAY & PER INDIVIDUAL !

Kama kinachosemwa hapo juu ni cha kweli, maana yake ni kwamba hiyo ndege itakuwa itakuwa haiingizi faida. Kama ni kweli wameingia mikataba hiyo sitashangaa kusikia hao watu wanamahusiano na popo-bawa
 
Duh wakuu nadhani hapa cha kuangalia ni kama kuna ukweli wa hii habari na sio motive ya mleta hoja.., who cares kama mleta mada na mtuhumiwa wana chuki binafsi? (cha maana ni Je ni kweli kuna Ufisadi ?) hayo mengine sidhani kama yanatuhusu unless otherwise huu uzi unakuwa ni wa motive ya mleta uzi na sio ukweli wa habari
Watu haohao tuhuma kama hizi zikienda kwa JK na Lowasa wanazikubali bila kuomba ushahidi. Lakini leo kaja mtu na data zake za tuhuma kwa Mwakyembe, wao wanakanusha tu bila kuleta data zao. Halafu leo hii Waislamu wakileta fujo wao wanasema waislamu hawatumii logic, wakati wao pia hawatumii logic, kweli nyani haoni. Inabidi tubadilike sio kuwa washabiki wa mtu fulani. TZ bado safari ni ndefu na inawezekana hatujaianza hiyo safari kabisa.
 
Wakisoma uzi huu wapuuzi wachache wanaonufaika na ufisadi wa aina hii wanabaki kupindisha mada,ukweli ni kwamba Mwakyembe tusimwamini sana na kumwona ana extra mind.Alipiga makelele ya richmond kumbe alikuwa mmoja wa washika dau wa mpango wa umeme wa upepo kule Makambako.Sasa hili la ndege yenye umri mkubwa kuliko mbunge wa CHADEMA Mhe.David Silinde ni vema tukaliangalia vizuri kwani bila shaka kwa mfumo huu shirika litakuwepo kama picha tu bila mchango wowote katika uchumi maana hakutakuwa na faida ila gharama za uendeshaji...Hivi ni kweli Watanzania tunataka kushiriki biashara ya ushindani au tunaigiza? Sijui CCM imewafanya nini viongozi wake kiasi cha kukosa mipango ya miaka 50 ijayo.Miaka 30 ijayo Wanyarwanda wakitupiku kimaendeleo,wadhaifu wa Tanzania tutawasikia wakisema 'Rwanda ni ndogo kuliko Tanzania' bila kujadili kwamba hata rasilimali zao ni chache ukilinganisha na Tanzania ila watu wake wameamua kuweka upuuzi pembeni.

Hapo ndipo watanzania wengi hawajui. Walikuwa wanagombania deal sio makambako tu pia kuna sehemu moja karibu na katikati ya Tanzania, deals za umeme wa upepo. Lengo lao lilikuwa kuondoa deal la richmond ili deal lao li pick up.
Wa-TZ walivyokuwa wehu wanadhani hata sumu aliyowekewa aliwekewa kwa sababu anawatetea wananchi, hawajui sababu ilikuwa ni vita vya kupigania ma-deal.
 
Acha chuki Binafsi,isipende kuleta hoja jamvini kwchuki,ukitumia chuki hutaeleweka jaribu kuondoa chuki ndiyo unaweza kulete hoja yako vizuri mkuu.

Ukishindwa kuchambua mada bora unyamaze kimya. Watu wengi JF mmezoea umbea tu na ushabiki. Ikija mada za uchambuzi zero. Sasa wewe umepewa data. Wewe unakuja na tafsiri zako za jumlajumla. Mwakyembe si malaika na kwanza kuwa CCM pamoja na uozo uliopo, unyama aliofanyiwa huku kakaa kimya yatosha tu kuonyesha kuwa ni mchumia tumbo asiyependa kuacha sufuria la ugali hata kama anachapwa viboko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom