Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Smiley, Oct 25, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. G

  George Smiley JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  [​IMG]

  Mimi katika vitu vilivyonishinda humu ni mabishani ya nani zaidi kati ya CCM na CHADEMA. Sasa nimeona bora nikufahamisheni Mwakyembe ambaye anajisifia kuwa mpinga rushwa mkubwa alivyokuwa fisadi na ushaidi wote nauweka hapa na kama kuna mtu anabisha aendelee.


  Kwa kifupi wafuatao wanahusika kwenye huu wizi:

  HARRISON MWAKYEMBE
  MANAGEMENT NZIMA YA ATC
  BODI YA ATC
  KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA
  EXTERNAL AUDITORS WA ATC
  LUDOVICK UTUOH AMBAYE NI MKAGUZI MKUU WA SERIKALI  Tuhuma zenyewe ni kama ifuatavyo:

  1. Shirika la ndege la taifa (AIR TANZANIA) waliamua kukodisha ndege yenye umri wa miaka 32 aina ya B737-200 iliyozeeka na mbovu kutoka kampuni ya Africa Kusini inayoitwa Star Air Cargo.


  2. Ndege hii ilianza kufanya kazi mwaka 1980 kule UK, na ilikuwa inatumiwa na kampuni inayoitwa BRITISH AIRTOURS na baada ya hapo ilikodishwa na mashirika zaidi ya 20 Ulaya na Latin America.

  3. Mwakyembe, Menejimenti na bodi mpya ya ATC walikubali na kupitisha ukodishaji wa hii ndege kwa kiasi cha dola laki 2 (200,000 US Dollars) kwa mwezi katika miezi 3 ya awali ya ukodishaji kinyume na ushauri ambao Mwakyembe na maswahiba zake wa ATC walipewa.

  4. Mkataba unaonyesha kuwa itabidi ndege hii itabidi iruke kwa masaa 150 kwa mwezi at a rate of $1,350 (kwa kila saa)

  5. Mkataba unaendelea kusema kuwa ATC LAZIMA wagharimie gharamza zote za ma crew ambayo iko estimated to be in the region of a further $80 – $100 PER DAY & PER INDIVIDUAL !

  (Katika mazingira ya kawaida msomaji utaona gharama ni ndogo lakini ukweli ni kubwa sana uzingatia kuwa ndege yeneyewe inasafiri kwenda sehem 3 tuu yaani kati ya Dar es Salaam – Kilimanjaro – Mwanza na hii yoye iko funded na walipakodi wa Tanzania).

  Sasa ukweli ni kuwa kama kweli Mwakyembe & kundi lake wana nia nzuri wasingekubali dili hii ipitishwe kwa kuzingatia kuwa kwanza ndege inge cost less kuikodisha kuliko gharama ambazo hawa mafisadi wamepitisha, na pia hizi gharama za malipo kwa saa ni kubwa mno na hapa ndipo Mwakwembe na kundi lake la mafisadi wanakula zaidi kwenye huu mgao.

  Suala lingine la kuzingatia hapa ni operating costs ambazo Mwakyembe & his crew wa ATC ni uhuni mtupu kwani ndege ina miaka 32 na gharama za uendeshaji na hasa za matumizi ya mafuta ni kubwa mno ukilinganisha ndege za kisasa.

  Kwa msiojua ni kuwa gharama za mafuta (fuel costs) kwa kawaida zinachukua around 40% ya overall costs lakini kama shirika linatumia ndege za kizamani basi ni wazi kuwa gharama zitaongezeka zaidi. Na uhuni uliofanywa na ATC wakishirikiana na wahuni wenzao pale wizarani kwa Mwakwembe ni kupiga rangi hizi ndege wakati wakijua wazi kuwa walipa kodi wanataka kujua mikataba iko kwa maslahi ya taifa (NATIONAL INTEREST).

  [​IMG]

  Moja kati ya maswali ya kujiuliza ni kwa nini Mwakyembe na ATC walikataa kuchukua ndege kama CRJ ambazo ni ndogo zaidi lakini zina fly economically lakini pia ni kubwa kiasi kiasi cha kurestart hii biashara ya shirika kama ATC. Lakini hii pia ni mfululizo wa uhuni unaoendelea kama ule wa awali wa kukodisha ndege toka kampuni ya Arabuni ambayo intugharimu sana sisi walipa kodi kama ile ya uhuni wa awali wa ukodishaji wa Airbus.

  Sasa huyu Mwakyembe ambaye anajifanya ni kinara wa kupiga vita ufisadi anakubali na amepitisha huu uhuni wa ATC ambao utamgharimu zaidi mlipa kodi. Huu ni uthibitisho kuwa wanaolack vision si wale wa (Pemba + Zimbabwe ) pekee lakini mpaka huyu mwanasheria kama Mwakyembe ambaye anaendeleza uhuni wa stop gap measures.
  [​IMG]

  This half baked measures za Mwakyembe et al zinathibitisha kuwa everything is fundamentally wrong with his ministry and ATCL in particular. Kwa kifupi, they lack leadership, they lack vision, and most of all, they lack planes and money.

  Sasa kaeni mkao wa kuona wanaleta maombi ya kutaka wapewe pesa zaidi ili waendelee kula. Na news zilizopo kwenye corridor za ATC ni kuwa wana haha kama mbwa mwitu ili warejeshe safari za nairobi na hasa baada ya player mpya chini ya (FAST JET) kuingia kwenye soko.  BTW

  Nadhani mnaikumbuka ile ndege ya ATC iliyoanguka kule mwanza? bas ndio model hiyo hiyo aina ya B737-200 kama hii mbovu na iliyozeeka ambayo Mwakyembe & his crew wanatuleta.


  uhondo zaidi uko hapa:  Air Tanzania Company Limited (ATCL) has suspended its contract with the Dubai based aviation company, Aero Vista, that saw the latter lease a Boeing 737-500 plane to embark on domestic flights.

  [​IMG]

  ATCL CEO, Captain Milton Lusajo Lazaro  ATCL leased a Boeing 737- 500 plane with the capacity to carry 108 passengers, which has since then been embarking on the national flag carrier's Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza routes before launching the Dar es Salaam-Hahaya (Comoros) route last month.


  The airline's Acting Chief Executive Officer, Captain Milton Lazaro, said the company had reached that decision to ensure a win-win situation and sustainability from the contract.


  He, however, said the company intends to undertake a contract review with Aero Vista adding that the company may go in for another company if the two sides do not reach a consensus on the matter.  "We had decided to suspend the contract earlier entered upon with Aero-Vista in order to ensure compliance with Government pre-requisite. We may be able to re-enter a new contract with them after discussions on revision of some clauses that do not favour a sustainable outcome.
  [​IMG]

  "Passengers who are holding ATCL tickets have been reallocated alternative flights with other carriers and notified accordingly," he said. He added that the national flag carrier will be able to be back on the routes after the completion of the maintenance exercise of its Dash-8 Q300 plane that is undergoing checks at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salam.


  Captain Lazaro said, however, that only its Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza routes will be temporarily affected by the suspension urging that the airline continue with its three-time weekly flights between Dar Es Salaam and Hahaya (Comoros).


  "We regret the inconveniences that have been caused to our valued customers, we take this opportunity to thank them for their continued support and reassure that, the resumption of these services will take place as soon as possible," he said.

  Source Daily News.


  Wakati sisi tuko bize kukodisha ndege za miaka 32 na kutetea ufisadi wa akina Mwakyembe & Co, Rwanda wao wameamua kufanya kweli na kuwa nchi ya kwanza Africa kununua ndege 4 aina ya CRJ900NG ambayo wataalama wanasema kuwa ni the most economical short and medium range jets toka kwa kampuni ya Bombadier. (wataalam wa mambo ya ndege watakuambieni ubora wa hizi ndege kulinganisha na mtumba wa ATC)

  [​IMG]

  Hawa wa NyaRwanda ambao tumewashinda kwenye kila kitu (kasoro akili). Kwa sababu wakati sisi tuko bize kusifiana upuuzi wao wameopt kununua state of the art modern aircraft ambayo ina gharama za chini sana kulinganisha na mitumba ya akina Mwakyembe & ATC lakini pia wao wameunyesha pride ya KUNUNUA NDEGE MPYA badala ya kukodisha hizo ndege na hii inawapa sense of ownership na muhimu zaidi inawapa abiria confidence abiria wake wa safari zake za Africa na mashariki ya kati

  Ndege hizi zina dual class configuration ya 7 business class seats kwa mpango wa 2×1 layout na 68 economy class seats katika mpango wa 2x layout, ambayo nadhani ni quite ideal for the short and medium distances ambazo Rwanda Air inasafiri.

  Kwa kuonyesha kuwa hawa wa NyaRwanda wako serious, wao hawataki tena mitumba na wanaondoa ndege walizokodisha aina ya Dash 8-100 na badala yake wanaweka ngoma iliyokuwa advanced na kubwa zaidi zaidi toka Bombadier Q400, ambayo kwa sasa zinapatikana kwenye dual class configuration – type ya kwanza ilikuwa delivered kwa Ethiopian Airlines wiki chache zilizopita

  Sasa hivi Air Rwanda inakwenda nchi 14 na wanamipango ya kuongeza frequencies za key destinations zaidi ya 40. Sasa wao hawafkiriii kushindana na ATC wao target ni kuwapiku KQ. Sisi tuko hapa hatujajua bado kama Tanzania ilitokana na Pemba na Zimbabwe au nchi ya kifikirika.

  UPDATES: Ile safari ya akina Mwakyembe Ujerumani nayo inaelekea kuota mbawa kwani bodi ya Lufthasa nao wamechomoa kuwa na JV au kurudisha safari zao Tanzania kwa sababu hazina faida.


   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Umekurupuka kutoa tuhuma kwa Ofisi ya taifa ya ukaguzi , Suala la ukodishaji wa ndege chakavu CAG kapiga kelele sana, rejea taarifa yake kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha unaoishia juni 30, 2010 amebainisha kuwa , kuhusu atcl, serikali itafakari upya juu ya shirika ila tube wavumilivu katika kipindi hiki atcl inajaribu kufufuka, haya mengine unayotuambia Leo hatuyaamini kwa sababu wengine nyie mnaweza kuwa mawakala wa washindani wa atcl yani precision nk.
   
 3. i

  iseesa JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe uloleta uzi huu ni kambi ya EL?
   
 4. S

  Shembago JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ndio kwanza nataka kwenda lunch nttachangia baadae ila nasema "hakuna msafi ccm"
   
 5. ULUMI

  ULUMI Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni mkanganyiko fulani wa mawazo!

  Mleta mada anaonyesha mweelewa kidogo sana wa mambo ya usalama wa anga,Umri wa ndege haupimwi kwa muda iliotengenezwa tuu, bali masaa ya kuruka .

  Pia mwenye chuki binafsi na Mwakyembe, Amezidi kujikanyaga hasa alipomuhusisha CAG.Namshauri kwanza atatue mgogoro wake wa ndani ili aweze kuweka mtiririko unaoeleweka. Atenganishe tuhuma, chuki binafsi na majungu.

  Pia ajifunze na kupokea ushauri kwamba uropokaji hadharani siyo njia muafaka ya kuwakilisha ujumbe.

  Tunataka data!!
  :glasses-nerdy:
   
 6. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Dogo naona ,upo kazini boss wako Mataka hajambo, mwambie sis atcl bado tunadunda kama kawaida. mwambie akupe umbea mwingine ulete humu.
   
 7. K

  Kyatsvapi JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 315
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Taarifa hii imekaa kinafiki nafiki na inaonekana imeletwa mahsusi kushambulia upande wa Mwakyembe.

  Ngoja wenyewe wazione hizi tuhuma. Nina uhakika watakuja na majibu stahiki.
   
 8. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Ili tuondokane na haya mauza mauza katika nchi hii, tunahitaji mambo makuu mawili.

  1. Siasa Safi

  2. Uongozi Bora
   
 9. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,521
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  Ufisadi inawezekana upo lakini nakosa imani unapomhusisha Waziri Mwakyembe,CIG,Bunge,ATCL wenyewe..siamani kama wote hao lao moja.!
   
 10. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ndo wale wa bandarini mmeamua kumwaga mboga eeh:-D
   
 11. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Siamini kama Mwakyembe anaweza kuvishawishi vichwa vyote hivyo ulivyovitaja ndani ya ATCL, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma na ofisi ya CAG wanaweza kushirikiana na Mwakyembe kufanya hujuma ya aina hiyo. Hii imekaa kichukichuki zaidi.
   
 12. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,058
  Likes Received: 6,506
  Trophy Points: 280
  andikeni hata ya uvunguni sie twayasoma tu yakhe.
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  angalia mlivyo na akili kama za mulugo
   
 14. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,202
  Likes Received: 1,332
  Trophy Points: 280
  naona kama personal attack kwa Mwakyembe
   
 15. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Acha chuki Binafsi,isipende kuleta hoja jamvini kwa chuki,ukitumia chuki hutaeleweka jaribu kuondoa chuki ndiyo unaweza kulete hoja yako vizuri mkuu.
   
 16. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,318
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Nimepanda hii ndege inayotuhumia jana tu, from Dar to....! ukweli management ya ATC ime change sana, wapo very serious na biashara, wahudumu ni wazuri na wapo committed hasa, kabla ya uzi huu kubandikwa, kwasababu na mimi ni mTanzania nilifanya mahesabu yafuatayo:-

  Trip moja from Dar to Mwanza ni Tsh 166,000/= kwa abiria anaenda one trip only, lakini kwa wale wanaokata go and return Mwanza to Dar ni Tsh 257,000/= well, let us just assume kwamba abiria wote ni wa go and return, of course nia hapa ni kua na hesabu ambayo ni most minimum, kama kila Trip ndege itabeba abiria 50 tu it mean kwa trip moja ndege hiyo itakua imetengeneza pesa hizi.

  Chukua nusu ya hiyo 257,000/= gawanya kwa 2 itakupa 128500/= then kwa hao abiria 50 itakupa 6425000/= ndege hii hufanya safari sita kwenda na kurudi Mwanza, yaani asubuhi ya saa 12 to Mwanza, then saa 2 to Dar, kisha saa za mchana to Mwanza again, machana huo huo hurudi Dar tena then saa 11 jioni inatia timu Mwanza while mbili usiku inarudi Dar, weka hesabu hiyo mara sita yaani 6425000 kwa 6 sawa 38,550,000/= sasa hiyo ni pesa ya siku moja, weka kwa hiyo miezi 3 ya ukodishwaji, assuming mwezi utakua na siku 90 then jumla ya pesa kama Gross itakazo zipata ATC kwa deal hili ni Tsh 3,469,500,000/= mbona hili deal linalipa sana tu, anyway twende kwenye hiyo bill ya mwezi ya USD 200,000, kama exchange rate ni 1=1550 then USD 200,000 ni sawa 310000000/= wakati siku moja umelala na Tsh 38550000, kumbukeni pia, Distance from Mwanza to Dar kwa ndege ni Km 450 tu.

  Mmmm, wakuu, tuache majungu, Mwakyembe ameweka dira, hata bei za Precion naona kama zimeshuka hivi, i think because of compitetion!
   
 17. k

  kajembe JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Hahahahahaha! Watu wakishikwa pabaya wanakurupuka na mambo.Sasa jamaa kaiba kwa hiyo pendekezo lako ajiuzuru na ashitakiwe mara moja eeee! hao akina mwakyembe wamevuta ngapi hapo? naomba unifafanulie maana sikuelewi vizuri! Unajaribu kueleza jambo ambalo halielezeki!
   
 18. a

  afwe JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mtatueleza madhambi yenu yote hata mliyoyafanya kabla ya Mwakyembe kuingia kwenye hiyo wizara. Muhimu mjue tunataka mabadiliko na taifa lirudishe heshima ya kuwa na shirika lake la ndege
   
 19. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Duh wakuu nadhani hapa cha kuangalia ni kama kuna ukweli wa hii habari na sio motive ya mleta hoja.., who cares kama mleta mada na mtuhumiwa wana chuki binafsi? (cha maana ni Je ni kweli kuna Ufisadi ?) hayo mengine sidhani kama yanatuhusu unless otherwise huu uzi unakuwa ni wa motive ya mleta uzi na sio ukweli wa habari
   
 20. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Hii thread siyo ya LOWASSA? nauliza tu.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...