Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Status
Not open for further replies.
CHADEMA yafichua ufisadi wa Mwakyembe
• Adaiwa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari

na Josephat Isango

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuwa amefanya yale aliyoyakataa kwenye Kampuni ya Richmond, licha ya wakati huo kujidai anajua kufuata taratibu.
CHADEMA imefichua kuwa Dk. Mwakyembe amekiuka sheria ya manunuzi ya umma katika mradi wa upanuzi wa bandari kavu unaofanyika katika eneo la Sukita, Tabata jijini Dar es Salaam.
Siri hiyo ilifichuliwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa vikao vya Kamati Kuu ya chama hicho.
Kigaila alidai kuwa Dk. Mwakyembe ni mnafiki, kwani yale aliyoyakataa wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati teule ya Richmond ambapo ripoti yake ilisababisha Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Lowassa ajiuzulu, leo ameyafanya.
“Alilaumu kuwa Richmond ilipewa zabuni bila kuwa na vigezo, bila kufanyiwa upembuzi yakinifu, tena bila zabuni husika kutangazwa.
Hili ni eneo la SUKITA linamilikiwa na CCM na lipo maeneo ya barabara ya Kawawa na Mandela,” alisema.
Alisema mradi huu utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya CCM inayoitwa Jitegemee Trading Company na TPA kwa gharama ya mabilioni ya shilingi.
Kigaila alidai kuwa katika mwaka ujao wa fedha 2013/2014 Mamlaka ya Bandari (TPA) itailipa CCM sh bilioni 10 na kwamba tayari fedha hizo zimetengwa katika bajeti ya serikali.
Kampuni ya SUKITA ilisajiliwa Machi 15, 1978 na Jitegemee Trading Company Limited ilisajiliwa mwaka 1997.
Wakurugenzi wa Jitegemee ni Sam Mapande, Peter Machunde na Diwani wa CCM Kata ya Hananasif, wilayani Kinondoni, Abbas Tarimba. Mapande, ndiye mwanasheria aliyehakiki fomu za Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
“Kwanza mradi huu unaotaka kufanywa na Mwakyembe kwa kutumia kivuli cha TPA haukufanyiwa tathimini, upembuzi yakinifu kiuchumi sawa sawa na ilivyokuwa kwa kampuni ya kitapeli ya Richmond,” alisema Kigaila.
Aliongeza kuwa mradi huu haukufanyiwa uchanganuzi wa kiuchumi ili kubaini pamoja na kulipa sh bilioni 10 ya plot kabla ya kujengwa kwa mradi.
“Mradi huu wa Mwakyembe na chama chake haukufuata sheria ya manunuzi ya umma (PPRA). Hakukuwa na zabuni iliyotangazwa wala ushindani kwa makampuni na mashirika mengine yenye sifa,” alisisitiza.
Kigaila aliongeza kuwa nyaraka zilizopo TPA zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2010, Bodi ya Bandari ilipokea maombi kutoka Manispaa ya Temeke ya kutaka kufanya ubia wa eneo la maegesho, ambapo walitenga eneo huko Kurasini, karibu kabisa na bandari.
Alisema kuwa wazo hilo halijafanyiwa kazi, badala yake Mwakyembe amekuja na mradi wake.
Kigaila alisema vyanzo vyao ndani ya serikali na CCM vinasema mjumbe mmoja wa Bodi ya TPA alihoji kwanini shirika linaingiza fedha hizo kwenye mradi huu katika eneo la SUKITA, lakini mkurugenzi wa bandari alijibu: “Huu ni mradi wa chama tawala, hivyo ni muhimu tukau-sapport”.
Alihoji kama Mwakyembe, serikali na CCM hawaoni umuhimu wa kutumia fedha hizo kuimarisha bandari zilizopo kwenye maeneo ya maziwa kama vile Kigoma, Mwanza, Rukwa na Musoma ikiwa ni kujiweka sawa kwenye ukanda wa biashara na ukuaji wa soko la Afrika Mashariki.
Alisema kuwa siku zote CCM na serikali yake wamekuwa wakijifanya kuwaonea huruma Watanzania na kuwataka wahame mabondeni, lakini hao hao wanatumia mabilioni ya shilingi na kuyaingiza katika bonde la Msimbazi, ambako kuna hatari kubwa ya mvua kusomba magari na makontena ya wateja wa TPA.
“Lakini ukiangalia hii ripoti, utaona kuwa kuna miradi mikubwa 35 ambayo imeombewa fedha si kwa sababu ya kuiendeleza, bali ni kukusanya fedha za kutafuta urais,” alidai.
Kigaila aliongeza kuwa Mwakyembe amekataa mapendekezo yaliyokuwa yamefanywa na uongozi wa bandari kushirikiana na Manispaa ya Temeke kupanua bandari eneo la Kurasini, badala yake ameelekeza upanuzi huo ufanyike katika eneo la SUKITA.
“Kampuni ni ya CCM, kiwanja ni cha CCM, zabuni haikutangazwa wala kufanya upembuzi yakinifu kwa kampuni hii kama imekidhi vigezo. Mwakyembe atuambie ilishindanishwa na kampuni zipi na ilishinda kwa vigezo vipi. Iweje yale aliyoyakataa kwenye Richmond ameyatenda?” alihoji.
Kigaila amelaani tabia ya viongozi wa CCM kuanzisha miradi au kampuni hewa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu kwani ni kwa njia hii huchota fedha kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi kama ilivyofanyika kwa EPA.
“Mwakyembe yupo kwenye kambi ya Samuel Sitta, wanaungana na familia ya Jakaya Kikwete kumsaidia Bernard Membe katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ujao, hivyo wameamua kuanzisha miradi hii kwa njia za kifisadi,” alisema.
Juhudi za Tanzania Daima kuzungumza na Mwakyembe au Naibu wake, CharlesTizeba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye ziligonga mwamba baada ya wote kutotoa ushirikiano.
Waziri Mwakyembe simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipoandikiwa ujumbe mfupi (sms) hakupatikana tena hewani wakati naibu wake, alisema: “Wewe gazeti lenu liliandika nilifukuzwa Mtwara, na sasa unataka kunigonganisha na propaganda za CHADEMA ili upate habari ya kuandika, sitaki gazeti lako na sikutaki wewe.”
Naye Nape alisema: “Andikeni mnavyoandika mimi nitajibu kesho kwa kuwa najua nikijibu sasa mtayaweka ndani kwa udogo.”
Alipoulizwa kwanini asitumie hiyo nafasi kujibu, alimwambia mwandishi: “Kama hutaki kusikia yangu, basi andika ya kwako, mimi nimesema nitajibu kesho.”

CHADEMA yafichua ufisadi wa Mwakyembe
 
sasa jana Mwakyembe kaenda aiport kamkamata mbeba unga mmoja leo anataka kuiambia dunia nzima kuwa yule dogo ndio mmbaya kuliko wote

Kwanza Mwakyembe shughulikia AIR CONDITION na LIFT/ESCALATORS za ule uwanja
 
Mleta uzi aliyeshikwa jana na unga ni kijana wako so nawe umeona ulete hii apunguze spidi nn?
 
CHADEMA yafichua ufisadi wa Mwakyembe

• Adaiwa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari

na Josephat Isango

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuwa amefanya yale aliyoyakataa kwenye Kampuni ya Richmond, licha ya wakati huo kujidai anajua kufuata taratibu.
CHADEMA imefichua kuwa Dk. Mwakyembe amekiuka sheria ya manunuzi ya umma katika mradi wa upanuzi wa bandari kavu unaofanyika katika eneo la Sukita, Tabata jijini Dar es Salaam.
Siri hiyo ilifichuliwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa vikao vya Kamati Kuu ya chama hicho.

Kigaila alidai kuwa Dk. Mwakyembe ni mnafiki, kwani yale aliyoyakataa wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati teule ya Richmond ambapo ripoti yake ilisababisha Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Lowassa ajiuzulu, leo ameyafanya.
"Alilaumu kuwa Richmond ilipewa zabuni bila kuwa na vigezo, bila kufanyiwa upembuzi yakinifu, tena bila zabuni husika kutangazwa.
Hili ni eneo la SUKITA linamilikiwa na CCM na lipo maeneo ya barabara ya Kawawa na Mandela," alisema.
Alisema mradi huu utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya CCM inayoitwa Jitegemee Trading Company na TPA kwa gharama ya mabilioni ya shilingi.
Kigaila alidai kuwa katika mwaka ujao wa fedha 2013/2014 Mamlaka ya Bandari (TPA) itailipa CCM sh bilioni 10 na kwamba tayari fedha hizo zimetengwa katika bajeti ya serikali.

Kampuni ya SUKITA ilisajiliwa Machi 15, 1978 na Jitegemee Trading Company Limited ilisajiliwa mwaka 1997.
Wakurugenzi wa Jitegemee ni Sam Mapande, Peter Machunde na Diwani wa CCM Kata ya Hananasif, wilayani Kinondoni, Abbas Tarimba. Mapande, ndiye mwanasheria aliyehakiki fomu za Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
"Kwanza mradi huu unaotaka kufanywa na Mwakyembe kwa kutumia kivuli cha TPA haukufanyiwa tathimini, upembuzi yakinifu kiuchumi sawa sawa na ilivyokuwa kwa kampuni ya kitapeli ya Richmond," alisema Kigaila.
Aliongeza kuwa mradi huu haukufanyiwa uchanganuzi wa kiuchumi ili kubaini pamoja na kulipa sh bilioni 10 ya plot kabla ya kujengwa kwa mradi.
"Mradi huu wa Mwakyembe na chama chake haukufuata sheria ya manunuzi ya umma (PPRA). Hakukuwa na zabuni iliyotangazwa wala ushindani kwa makampuni na mashirika mengine yenye sifa," alisisitiza.
Kigaila aliongeza kuwa nyaraka zilizopo TPA zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2010, Bodi ya Bandari ilipokea maombi kutoka Manispaa ya Temeke ya kutaka kufanya ubia wa eneo la maegesho, ambapo walitenga eneo huko Kurasini, karibu kabisa na bandari.
Alisema kuwa wazo hilo halijafanyiwa kazi, badala yake Mwakyembe amekuja na mradi wake.
Kigaila alisema vyanzo vyao ndani ya serikali na CCM vinasema mjumbe mmoja wa Bodi ya TPA alihoji kwanini shirika linaingiza fedha hizo kwenye mradi huu katika eneo la SUKITA, lakini mkurugenzi wa bandari alijibu: "Huu ni mradi wa chama tawala, hivyo ni muhimu tukau-sapport".
Alihoji kama Mwakyembe, serikali na CCM hawaoni umuhimu wa kutumia fedha hizo kuimarisha bandari zilizopo kwenye maeneo ya maziwa kama vile Kigoma, Mwanza, Rukwa na Musoma ikiwa ni kujiweka sawa kwenye ukanda wa biashara na ukuaji wa soko la Afrika Mashariki.
Alisema kuwa siku zote CCM na serikali yake wamekuwa wakijifanya kuwaonea huruma Watanzania na kuwataka wahame mabondeni, lakini hao hao wanatumia mabilioni ya shilingi na kuyaingiza katika bonde la Msimbazi, ambako kuna hatari kubwa ya mvua kusomba magari na makontena ya wateja wa TPA.
"Lakini ukiangalia hii ripoti, utaona kuwa kuna miradi mikubwa 35 ambayo imeombewa fedha si kwa sababu ya kuiendeleza, bali ni kukusanya fedha za kutafuta urais," alidai.
Kigaila aliongeza kuwa Mwakyembe amekataa mapendekezo yaliyokuwa yamefanywa na uongozi wa bandari kushirikiana na Manispaa ya Temeke kupanua bandari eneo la Kurasini, badala yake ameelekeza upanuzi huo ufanyike katika eneo la SUKITA.
"Kampuni ni ya CCM, kiwanja ni cha CCM, zabuni haikutangazwa wala kufanya upembuzi yakinifu kwa kampuni hii kama imekidhi vigezo. Mwakyembe atuambie ilishindanishwa na kampuni zipi na ilishinda kwa vigezo vipi. Iweje yale aliyoyakataa kwenye Richmond ameyatenda?" alihoji.
Kigaila amelaani tabia ya viongozi wa CCM kuanzisha miradi au kampuni hewa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu kwani ni kwa njia hii huchota fedha kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi kama ilivyofanyika kwa EPA.
"Mwakyembe yupo kwenye kambi ya Samuel Sitta, wanaungana na familia ya Jakaya Kikwete kumsaidia Bernard Membe katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu ujao, hivyo wameamua kuanzisha miradi hii kwa njia za kifisadi," alisema.
Juhudi za Tanzania Daima kuzungumza na Mwakyembe au Naibu wake, CharlesTizeba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye ziligonga mwamba baada ya wote kutotoa ushirikiano.
Waziri Mwakyembe simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipoandikiwa ujumbe mfupi (sms) hakupatikana tena hewani wakati naibu wake, alisema: "Wewe gazeti lenu liliandika nilifukuzwa Mtwara, na sasa unataka kunigonganisha na propaganda za CHADEMA ili upate habari ya kuandika, sitaki gazeti lako na sikutaki wewe."
Naye Nape alisema: "Andikeni mnavyoandika mimi nitajibu kesho kwa kuwa najua nikijibu sasa mtayaweka ndani kwa udogo."
Alipoulizwa kwanini asitumie hiyo nafasi kujibu, alimwambia mwandishi: "Kama hutaki kusikia yangu, basi andika ya kwako, mimi nimesema nitajibu kesho."

Taarifa hii imekaa kinafiki nafiki na inaonekana imeletwa mahsusi kushambulia upande wa Mwakyembe.

Ngoja wenyewe wazione hizi tuhuma. Nina uhakika watakuja na majibu stahiki.

Nafikiri tuache maneno yale tunayoona hayana faida tujadili yale yenye mantiki. kwa mfano hivi inaingia akilini TZ kuendelea kukodisha ndege wakati Rwanda na wengine wananunua ndege mpya za kwao wenyewe. Rwanda wana nn sisi tusiweze? wana rasilimali gani ambazo ss hatuna?

ni bora hata hizo ndege mtumba tusikodishe bali tununue, ili tujue tuna mandege mabovu kadhaa. Ushauri wangu kwa ATC na Serikali, tusione aibu, kama kukosea kila mtu anakosea, tukbali tulikosea mahali fulani, kosa sio kufanya kosa bali kurudia kosa, cha kufanya sisi tuamue sasa badala ya kukodisha ndege tununue ndege mpya kubwa hata 2 kwa mwaka. tukinunua ndege 2 kila mwaka nin hakika baada ya miaka 5 tutakuwa na ndege zetu mpya 10, ambazo utakuwa ni mtaji tosha kabisa ATC kujiendesha.

kwa safari za ndani ya nchi hata ATC ikinunua Boeing mbili za za watu 150 zinatosha kabisa, kwani uanchofanya unachora ramani ya safari zako, ukiona abiria sio wengi uaanzia dsm-KIA-Mwanza au ZBR- KIA-KGM-Mza lazima ndege itajaa tu. Mbona fastjet wameweza ss tunashindwa nn
 
Umekurupuka kutoa tuhuma kwa Ofisi ya taifa ya ukaguzi , Suala la ukodishaji wa ndege chakavu CAG kapiga kelele sana, rejea taarifa yake kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha unaoishia juni 30, 2010 amebainisha kuwa , kuhusu atcl, serikali itafakari upya juu ya shirika ila tube wavumilivu katika kipindi hiki atcl inajaribu kufufuka, haya mengine unayotuambia Leo hatuyaamini kwa sababu wengine nyie mnaweza kuwa mawakala wa washindani wa atcl yani precision nk.

Kaka hata usipoteze nguvu bure, hata mimi sitegemei wakae kimya kwa kauli kama ile aliyoitoa Mwakyembe. Kumbuka ni ULAJI unabughudhiwa, watajilinda kwa njia nyingi na moja wapo ni hii. Tuombe tu mungu waendelee tu kuandika kila kukicha ili mradi wasije waka muUlimboka wamuache mdingi apige kazi.
 
Blaah blaaah......nyingi sana hapa.unapofananisha ATCL na Rwanda nashindwa kukuelewa.
1.Rwanda safu nzima imejipanga,
2.mwakiembe akileta bajeti ya kununua ndege mpya hata 1 tu nani atapitisha mjengoni?
3.unapotaja ufisadi ktk gharama za kukodi ulipaswa kuonyesha mapato na matumizi ili tujadili profit.
4.ofisi ya CAG inatoa ripoti nzuri sana usitupoze aise,
tuache yote.
KWANINI MLETA MAADA UNAM-ATTACK MWAKIEMBE WAKATI HUU ANAPOANZISHA VITA KUU YA MADAWA YA KULEVYA?
hitimisho
hoja yako haina uzito ingawa umejitahidi sana kujenga hoja.ASANTE
 
.....ni bora hata hizo ndege mtumba tusikodishe bali tununue, ili tujue tuna mandege mabovu kadhaa. Ushauri wangu kwa ATC na Serikali, tusione aibu,.... tuamue sasa badala ya kukodisha ndege tununue ndege mpya kubwa hata 2 kwa mwaka. tukinunua ndege 2 kila mwaka nina hakika baada ya miaka 5 tutakuwa na ndege zetu mpya 10, ambazo utakuwa ni mtaji tosha kabisa ATC kujiendesha....
assuredly4,
Ushauri wako unakinzana na kujipinga. Mwanzo unashauri tusikodi mitumba bali tuinunue. Halafu baadae unashauri tena badala ya kukodi mitumba, bora tununue ndege mbili mpya kila mwaka. Tukichulia ushauri wa Kwanza kununua ndege mpya; sheria za manunuzi zilikuwa haziruhusu. Ndo maana tulishindwa kununua iliyokuwa mitambo ya Dowans kwa kuwa ilikwishatumika na mmiliki mwingine hivyo inaangukia kwenye kundi la mitambo chakavu. Kwenye ushauri wako wa pili tatizo ni uwezo kifedha.
 
Last edited by a moderator:
Uli/Mlikuwa wapi siku zooote hizo kuleta shituma kama hizo, Shutuma yenyewe haina msingi wowote kwetu wanainchi ukizingatia hali duni ambayo inatuzonga, maisha kupanda juu kila siku, Macho na masikio yetu sasa yapo kwa kiongozi ambaye anaguswa na hali ya nchi ilipofikia na tunapoelekea, #Mwakyembe kaonesha ujasiri wa hali ya juu kwenye ishu ya madawa ya kulevya ukizingatia ni miaka sasa imepita toka tusikie tuhuma za madawa ya kulevya si tu nchini mwetu bali hata nchi za nje swali lakujiuliza Je??? KUNA KIONGOZI GANI KAJITOKEZA KUKEMEA AMA KUFUATILIA???? JAKAYA M,RISHO KIKWETE mwenyewe kakaaa kimya kama haoni uozo unaofanyika na BAADHI YA VIONGOZI SERIKALINI, ISIPOKUWA MWAKYEMBE PEKEE....

1. Ulikuwa wapi siku zote kuleta uzi huo wa hizo shutuma??
2. Umekurupuka bro. we si wakwetu katika harakati za kuiokomboa nchi yetu dhidi ya MAFISADI
3. Nina wasiwasi nawe ni mmoja wao.
4. Subiri washiriki wa madawa ya kulevya tuwapate then uje na hizi unthinkable shutuma
5. Watu kama ninyi si wema kwa maana kuwa tunapotaka kumea uhuni wa serikali ya ccm ndipo mnapokuja kutuletea
habari zenu ili tusahau harakati zetu.
 
Mwakiyembe ni tishio
1. mafisadi,
2. wauza unga na
3. chadema, wamekusudia kupunguza credit za Mwakyembe wataweza?
 
Wewe ni mfanyakazi mchafu wa hapo JNIA ambaye Mwakyembe anakukaribia....unamuwahi sio!?Jembe lile!Tafuta jingine basi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom