Tugeuze kilimo kiwe mgodi wa dhahabu

Totozee

Member
Oct 15, 2018
98
69
Nilikuwa nasoma kitabu cha Marehemu Dr.Reginald Mengi kinaitwa

I CAN, I MUST,I WILL nikamnukuu akisema ndani ya kitabu chake tafiti zinaonyesha kwamba;

1. Bonde la mto Ruvu peke yake linaweza kuilisha Afrika Mashariki yote.Eneo la Kilombero linaweza kuilisha Afrika ya Kati yote kwa mchele.

2. Wilaya ya Kyela peke yake inaweza kuzalisha mchele wa kuilisha Afrika Magharibi yote

3. Bonde la Rufiji linaweza kuilisha Afrika ya Kaskazini ikijumuisha Sudan, Ethiopia na Somalia.

4. Maeneo ya Wami na Arusha Chini yanaweza kuzalisha mchele wa kutosha kuilisha Kusini ya Afrika yote.

5. NIKASOMA tena ripoti ya BENKI KUU kuhusu kilimo nikainukuu ikisema:-

A) Tanzania ina hectares millioni 44 ambazo zinafaa kwa kilimo.

B) Lakini ni asilimia 25% tu ya eneo hili lote ndio linatumika hadi sasa kwa shughuli za kilimo.

C) Hectare million 29 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ni asilimia 1% tu ya hectare zote hizi ndio zinatumika kwa kilimo cha umwagiliaji.

D) Asilimia 64% ya wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono kulima sehemu ndogo za mashamba kuanzia acre 0.5 hadi acre 5

E) 6.5% ya wakulima wote ndio wana uwezo wa kupata mikopo ya kilimo, hii inapelekea wengi kukosa mtaji wa kuongea uzalishaji..

6. NIKASOMA ripoti ya wizara ya kilimo chini ya serikali ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan na jinsi alivyoipa kipaumbele sekta nzima ya kilimo ikieleza:-

A) Serikali imepokea zaidi ya dollar za kimarekani million 700+ kutoka kwa wadau mbalimbali wa kilimo duniani zote zikilenga namna gani wanaweza wakachangia katika kuinua sekta ya kilimo

7. Kilimo ni kitatatua matatizo yetu yote.
 
Tutumie na takwimu, si umesikia pia kwamba tupo kwenye top 20 ya nchi zinazopoteza chakula kwa kuharibika?

Kulima tayari tunalima bado tu kwenye kuuza, uuzaji wa hicho tulicholima.

Uchawi ndo upo hapa, na kutoboa kama nchi ni tukazie hapa.

Serikali, wadau na motivation spika wote kazieni kusema kijana unafeli wapi kuuza mazao nje. Msituletee tena swagga za eti tukalime zaidi wakat mazao yanapotea tu
 
Back
Top Bottom