Ushirikiano wa kilimo kupitia BRI wasaidia kukabiliana na changamoto za dunia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG31N1239565875.jpg


Ikiongozwa na uelewa kuwa changamoto za dunia zinahitaji ushirikiano wa pamoja, China imefungua milango yake kwa nchi zote na mashirika mbalimbali ya kimataifa na kikanda, kupitia program na mapendekezo mbalimbali, kama Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), na kuboresha ushirikiano wa kimataifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, sekta ambayo ni muhimu sana katika juhudi za kuondokana na umasikini na njaa.

Tangu mwaka 2013, kupitia Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililotolewa na rais wa China Xi Jinping, lenye lengo la kuimarisha muunganiko wa miundombinu, biashara na uwekezaji, China imeanzisha ushirikiano wa kilimo na zaidi ya nchi 90 pamoja na mashirika mbalimbali ya kimataifa. China pia imefanya uwekezaji katika Zaidi ya miradi 650 ya kilimo yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 14 katika nchi zilizojiunga na Pendekezo hilo.

Katika muongo mmoja uliopita, ikiwa ni miaka 10 tangu rais Xi alipotoa Pendekezo hili la Ukanda Mmoja, Njia Moja, China imepeleka Zaidi ya wataalamu wa kilimo 2,000 katika nchi Zaidi ya 70, ambao wametoa mafunzo kwa wataalamu katika nchi husika jinsi ya kulima mpunga chotara na aina nyingine mbalimbali za mazao. Pia, katika kipindi hicho cha miaka 10, Zaidi ya wakulima laki moja wamepata mafunzo, na Zaidi ya wakulima milioni moja wamefaidika kwa njia isiyo ya moja kwa moja, na kukabiliana na mahitaji ya muhimu ya wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani ya kilimo na chakula. Katika ngazi zote nne za mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo, ambazo ni utaalamu, uzalishaji, ufungashaji na kufikisha kwa wateja, juhudi zinazoongozwa na China zinakabiliana na changamoto za miongo kadhaa ambayo imezorotesha ukuaji katika sekta ya kilimo na sekta nyingine husika.

Tangu kuanzishwa kwake, ushirikiano wa kilimo kupitia BRI umezingatia hatua za kitaifa na kimataifa zinazolenga kuondokana na vikwazo katika ukuaji wa sekta ya kilimo, na kujenga miundombinu rahisi na migumu. Miundombinu hiyo ni pamoja na mitandao sahihi ya usafirishaji ili kupeleka bidhaa za kilimo katika masoko, kuboresha uratibu wa utafiti katika sayansi ya kilimo, na kuhuisha viwanda vya hifadhi pamoja na umwagiliaji, na pia kuwatambulisha wakulima kilimo cha kisasa na teknolojia zinazounga mkono kilimo cha kisasa, na hivyo kuboresha kilimo endelevu.

Kwa nchi zilizojiunga na Pendekezo la BRI, ushirikiano huo wa kilimo unasukuma mageuzi ya kiuchumi kwa kuimarisha uwezo wa uzalishaji na kuboresha biashara katika sekta ya kilimo, na kwa njia hiyo, kukabiliana na changamoto za dunia ikiwemo umasikini na njaa. Ushirikiano wa kilimo wa BRI unafungua fursa mpya za ukuaji katika mnyororo wa thamani wa kilimo na chakula, na kuwezesha nchi washiriki, hususan nchi zinazoendelea, zikiwemo za Afrika, kuendeleza ukuaji unaotokana na kilimo ili kutimiza malengo ya maendeleo.

Katika nchi nyingi za kipato cha chini ama cha kati ambako nguvukazi kubwa inajishughulisha na kilimo, na ambazo sekta hiyo inachukua asilimia 25 ya pato la jumla la ndani, ushirikiano wa kilimo wa BRI unaohusiana na uhamishaji wa teknolojia za kilimo, uwekezaji katika kilimo, uwekezaji katika miundombinu na kasi ya sera za uratibu, unatoa fursa ya kipekee kwa nchi hizo zinazoendelea kutimiza ukuaji endelevu unaochochewa na kilimo, kuingia katika masoko mapya na makubwa, kusaidia kutoa fursa za ajira, na kuboresha usalama wa chakula.

Tukichukulia mfano wa Burundi, ambayo ilijiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Mojam waka 2018, ikianzia na ushirikiano wa kilimo, kwa sasa imepata mafanikio makubwa kutokana na juhudi za China. Ikiwa na ardhi nzuri ya kilimo na mvua za kutosha, uwezo mdogo wa Burundi wa kutumia kikamilifu rasilimali hiyo uliodumu kwa miongo kadhaa, ulichangia kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi masikini zaidi duniani ikiwa na hali mbaya ya usalama wa chakula.

Lakini mara baada ya kuanza ushirikiano na China chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ambao unazingatia Zaidi ushirikiano uliopo wa kilimo kati ya nchi hizo mbili, katika miaka mitano iliyopita, Burundi imeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo na ufugaji nchini humo, hususan kilimo cha mpunga, na hivyo kuboresha kidhahiri usalama wa chakula nchini humo. Kupitia ushirikiano wa kilimo wa BRI, Burundi imepokea awamu tano za wataalamu wa kilimo kutoka China, ambao wamefanya utafiti na majaribio kadhaa, na kufanikiwa kuchagua na kutambulisha aina nane za mpunga zinazoendana na hali ya hewa na mazingira ya nchi hiyo. Kutokana na juhudi hizo, mavuno hafifu ya mpunga yaliyokuwa yakisababishwa na magonjwa ya mpunga kwa sasa yamekuwa historia.
 
Back
Top Bottom