Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Sio nilitaka Bali hata mtoto mdogo wa kiarabu akikuona Kyle yemeni atajua wewe ni mwafrika!
we Kwa mambo hayo ya michezo ya kisilamu hupo salama🙆🙄
Labda Padri wako ndivyo anavyoona na Kanisa lako , kuna weusi kwa mamilioni huko Yemen , Saudi Arabiia, Kuwait , Oman , Emirates wala sijasikiapo kuitwa waafrika , ukienda wewe hii Leo of course utaitwa mwafrika na passport yako ya tz. Kule kila mtu ana kabila lake. Sio huku kumejaa watoto wa Mapadri na Makardinali hata wazee wao hawawajui
 
Kuitaka Tanganyika sio kutaka kuuvunja.
Kwani hata kuuvunja kuna ubaya gani?
Kumevunjwa , Soviet Union, Czechoslovakia , Senegambia nk na dunia inaenda Itakuwa huu uvamizi wa Nyerere uliopewa jina Muungano. Wazanzibari tume suffer vya kutosha tumechoka na jinamizi hili
 
Nyerere alihusika kumuua Karume ili muungano udumu na yote hayo ni kutokana na uoga wa Tz kuvamiwa enzi hizo
 
Heri nusu mkate kuliko kuukosa kabisa, ukiwa na tamaa ya kupitiliza kuupata mkate mzima uwezekano mkubwa ni kuukosa wote kabisa.
Kwani hata kuuvunja kuna ubaya gani?
Kumevunjwa , Soviet Union, Czechoslovakia , Senegambia nk na dunia inaenda Itakuwa huu uvamizi wa Nyerere uliopewa jina Muungano. Wazanzibari tume suffer vya kutosha tumechoka na jinamizi hili
 
Heri nusu mkate kuliko kuukosa kabisa, ukiwa na tamaa ya kupitiliza kuupata mkate mzima uwezekano mkubwa ni kuukosa wote kabisa.

Mkate gani wa kuukosa na mumeweka majeshi kila mtaa na uslama wa Taifa. Kwa hali mliyotufikisha huo mkate mbona tulishaukosa zamani . kila uchaguzi ni kuuliwa watu na kunajisiwa wanawake na kutiwa vilema watu na kubambikiziwa kesi za kigaidi. , kisa kulinda uvamizi uliopewa jina la muungano usio na tija yoyote zaidi kulinda viongozi wachache waendelee kuiba na kutekeleza maagizo ya kanisa katoliki la kuwakandamiza waislamu
 
Zanzibar ina raia milioni moja na ushee ila wanatungoza Tanganyika wenye raia milioni sitini.

Pia watu milioni moja wanapata mgao wa asilimia 30 huku watu milioni 60 wakipata 70 asilimia.

Mikopo ikija tunagawana.

Ni rahisi kwa Mzazibar kuwa DC au RC au Waziri ila jambo hilo katu haliwezekani kwa Mtanganyika kufanya hivyo huko Zanzibar.
 
Sijui sana

Ila ingekuwa vizuri tuuache muungano ila tuwaache wajitegemee yaani wawe na katiba yao na kila kitu chao kiuchumi na vitu vingine vyoote wajitegemee kama haiwezekani kabsa tuuache tu huu muungano na kila kitu kiendelee vile vile

Kiasili hatutofautiani sana
Nipe faida walau 3 tuu za Muungano, hasa kwa mtanzania wa kawaida kabisa kule Namanyere, Likawage, Nanjirinji, Nakapanya, Nanguruwe na kwingineko.
 
Makabila yaliyopo Tanzania yenyewe kama yenyewe hayajawahi kuungana na kupigania maslahi yao kwa pamoja kabla ya uhuru. Mapigano yao yote yalichochewa na msukumo wa mkoloni aliyetawala wakati huo.
Makabila hayakupigana yenyewe kwa yenyewe ili kujiumarisha? Someni history vijana...
 
Hamna haja ya kurejesha Tanganyika kwa sababu 85% ya raia waliopo sasa wamezaliwa Tanzania. Hivyo kuanza kuwaletea hoja ya Tanganyika ni sawa na kumywesha mtu dawa ambayo hajui inatibu ugonjwa gani!!
Hoja dhaifu sana, ni sawa na wale ambao eti tuu kwa kuwa wamezaliwa na kukulia mijini basi eti hawaoni umuhimu wa kujua chimbuko la ukoo wao huko kijijini.
 
Ufitini huu mbona akiwa ofisini Magufuli au Mkapa hakunaga harakati kama hizi za Tanganyika
Acha kuabudu waliotangulia mbele za haki. Tumia akili yako aliyokupa Mungu hao walikuwa binadamu kama wewe tuu na pengine ukiachana na bahati ya kuwa Marais pengine wewe una akili kuwazidi..
 
Kuirudisha Tanganyika ilikuwa ni kwa kumuunga mkono Hayati Mchungaji Christopher Mtikila, muasisi wa UKAWA. Sema ndio vile vyama vyetu hivi huwa havijui lipi jambo la maana na muhimu kwa wakati husika. Aliachwa kuipambania Tanganyika yeye peke yake na hata kurudishwa nyuma na vyama vingine vya siasa.

Tukiachana na hayo, katiba ya Warioba ndio ilikuwa inairudisha Tanganyika, kwa hiyotu hiyo tuanzie kwa Katiba ya Warioba, irejee kwenye bunge maalum la Katiba na ije kupigiwa kura. Bunge la Katiba lisibadilishe chochote libariki tu ije kwenye kura za maoni
Sema kwamba tuanzie na rasimu ya katiba ya mzee Warioba lakini tuibireshe zaidi. Pili bunge maalum la katiba lisiwe na hata mbunge mmoja wa bunge la sasa hivi, kwani hawa wakiwepo tuu basi jua mchakato utakufa tena.
 
Makabila hayakupigana yenyewe kwa yenyewe ili kujiumarisha? Someni history vijana...
Yenyewe kama yenyewe
Vs
Yenyewe kwa yenyewe.


Uwe unasoma ili uelewe, usisome ili ujibu. Sawa kijana
 
La kukubali kuwa nchi moja hilo tusahau kabisa na halitakuja litokeee.. Kuuvunja muungano ni rahisi zaidi kuliko hilo la kutaka kuunda nchi moja
Kama halikuwa ndilo lengo hasa la muungano wetu unafikiri kwanini nyerere haliitowesha tanganyika?

Kitendo cha kuchanganywa kwa udongo wa Tanganyika na Zanzibar kuliashiria kuyazika completely mataifa haya na kuanza upya kama taifa moja lakini kutokana na dosari ya kuiachia Zanzibar mamlaka ya ki-nchi kuliufanya muungano huu uwe meaningless.

Tunajua fika wananchi wa Tanganyika na Zanzibar hawana shida hata leo hii ukiwaambia waachane na tofauti zao wawe wamoja katika nchi moja isiyo na mipaka hawatoona ajabu sababu nchi zote mbili ni ndugu wa damu, wanashare utamaduni na lugha.

Tatizo ni wanasiasa ambao daima ufanya mambo kwa FAIDA ZAO BINAFSI KWA KIVULI CHA WANANCHI siku zote politicians wako after "POWER" kufanikisha GREEDY AND MONEY.

(Trust me wanaohamasisha tujitoe kwenye muungano na wanaoimiza muungano uendelee both ni politicians na hawafanyi hivyo kwa maslahi ya majority bali themselves)

Ukiwa nje ya box utaelewa kuwa kuuvunja muungano au kuuendeleza ulivyo hivi sasa ni pande mbili za sarafu zisizo na faida yeyote kwa mtanzania,

Kitakachofanya muungano usiendelee na kukomaa ili kufikia lengo la umoja kamili kama walivyoanzisha waanzilishi ni Wanasiasa na sababu kuu si kingine bali hofu ya kupoteza 'POWER' (u-mimi au ubinafsi)

Haijalishi mageuzi haya wahamasishi watayaita kwa majina mazuri kiasi gani iwe ni mamlaka kamili, uhuru wa kiuchumi, kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar, kuikomboa nchi, kurejesha utambulisho wa utaifa n.k jua kuwa wanapambania vyeo vyao na maslahi ya matumbo yao na si kwa ajili ya nchi.

Ni rai yangu kuwa kama Great thinkers tuanzishe kampeni ya kuamasisha umma kwa kuwajenga wananchi katika idea na saikolojia ya kuwa na TAIFA MOJA na siyo kuamasisha uwepo wa serikali 3 au utengano, mwisho wa siku divide & rule ni faida ya politicians.
 
Back
Top Bottom