Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,252
Reaction score
871,783
Sababu kificho iliyofanya tuungane na Zanzibar ilikuwa ni kwasababu ya vita baridi ya dunia kati ya wajamaa na mabepari.. Sisi watanganyika tulitumika tuu, ishu ya kusema ni kwasababu za kiusalama na matisho ya kigaidi ilikuwa ni sababu kwepeshi ya kuficha ukweli

Vita baridi ilikwisha kwa anguko la Soviet Union USSR.. Mabepari yaliibuka washindi na kuweza kuitawala dunia yatakavyo lakini madhara yaliyotuachia si haba!

Muunganiko uliopaswa kuwa na usawa umefeli pakubwa.

Mamlaka moja jina lake asilia limenyongelewa mbali huku nyingine ikitamaki na la kwake.

Mamlaka moja pamoja na kupokwa madaraka hapo kwanza lakini sasa iko hatua za mwisho kujitwalia mamlaka kamili, bado kipengele kimoja tu dhaifu cha kisiasa!

Tunapoelekea tamati ya huu mwisho wa iliyokuwa ndoa ya mkeka ninini hatima ya Tanganyika kwa utambulisho?
 
Sijui sana

Ila ingekuwa vizuri tuuache muungano ila tuwaache wajitegemee yaani wawe na katiba yao na kila kitu chao kiuchumi na vitu vingine vyoote wajitegemee kama haiwezekani kabsa tuuache tu huu muungano na kila kitu kiendelee vile vile

Kiasili hatutofautiani sana
 
Literally Tanganyika ilishakufa tangu 1964 kuifufua it needs a very smart strategic contigency plan by the smartest people who are willing even to die for the sake of their Country

Who are aware knowing when the Country is faltering and helping it to do better..knowing where to start unlike many other

Its not an easy task its matter of been Patriots
 
Tanganyika inafutwa zaidi na watanganyika wenyewe kwa kushindwa kuipigania kama wanavyofanya wazanzibar kwa Zanzibar yao.

Jambo pekee liliobaki kwetu ni kuwaruhusu waondoke bila kuwabugudhi ili waiache...baada ya kuondoka ndio tubadili jina na kurudia Tanganyika yetu.
Sisi wa bara tumelala sana.
 
Tatizo mojawapo la kuzingatia!
Leo Muungano Unalindwa na Rais Aliye Apa Kuulinda Muungano kama Ulivyo!
Ikiwa Muungano Umekufa ghafla Nani Atakuwa Rais wa Tanganyika?
Zenj wataendelea kuwa na Rais Aliyeapa kuilinda zenj!
 
Naomba kuuliza, hivi ili eneo ambalo sasa hivi linaitwa Tanzania bara zamani Tanganyika kabla ya Uhuru wake lilikuwa likitambulika kwa jina gani?
Tanganyika
tanganyikamap%20(1).jpg
220px-Stamp_Tanganyika_1925_10c.jpg
 
Sijui sana

Ila ingekuwa vizuri tuuache muungano ila tuwaache wajitegemee yaani wawe na katiba yao na kila kitu chao kiuchumi na vitu vingine vyoote wajitegemee kama haiwezekani kabsa tuuache tu huu muungano na kila kitu kiendelee vile vile

Kiasili hatutofautiani sana
Kinachounganisha sasa ni uzi mmoja mwembamba wa kisiasa
 
Back
Top Bottom