Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Sababu kificho iliyofanya tuungane na Zanzibar ilikuwa ni kwasababu ya vita baridi ya dunia kati ya wajamaa na mabepari.. Sisi watanganyika tulitumika tuu, ishu ya kusema ni kwasababu za kiusalama na matisho ya kigaidi ilikuwa ni sababu kwepeshi ya kuficha ukweli

Vita baridi ilikwisha kwa anguko la Soviet Union USSR.. Mabepari yaliibuka washindi na kuweza kuitawala dunia yatakavyo lakini madhara yaliyotuachia si haba!

Muunganiko uliopaswa kuwa na usawa umefeli pakubwa.

Mamlaka moja jina lake asilia limenyongelewa mbali huku nyingine ikitamaki na la kwake.

Mamlaka moja pamoja na kupokwa madaraka hapo kwanza lakini sasa iko hatua za mwisho kujitwalia mamlaka kamili, bado kipengele kimoja tu dhaifu cha kisiasa!

Tunapoelekea tamati ya huu mwisho wa iliyokuwa ndoa ya mkeka ninini hatima ya Tanganyika kwa utambulisho?
Mshana Jr, tuirejeshe Tanganyika dhidi ya nani, wakati Tanzania ndiyo Tanganyika asili au jina la Zanzibar kuwepo midomoni mwa watu linakutisha!!??
 
Kwa Katiba Gani??
Mpango kaapa Kulinda Serkali ya Muungano!
Hivyo Tanganyika haitambui...
Katiba aliyoiandika Nyerere, Zanzibar ina katiba yake Hiyo katiba aliyoapia Mpango itakuwa ya wapi Kama si Tanganyika iliyovaa koti la muungano?
 
ww ukizaliwa uarabuni na mababu walioishi zaidi ya miaka 200 utaitwa mwarabu??
msikiti ni hatari sanaaa[emoji56]
Ulitaka niwe mwafrika ? Kwani yule mfalme wa Kuwait, aliyekuwa mfalme wa Oman Qaboos, ni waafrika?

Ile michezo ya Mapadri inawatoa akili na kuwatia chuki
 
Sababu kificho iliyofanya tuungane na Zanzibar ilikuwa ni kwasababu ya vita baridi ya dunia kati ya wajamaa na mabepari.. Sisi watanganyika tulitumika tuu, ishu ya kusema ni kwasababu za kiusalama na matisho ya kigaidi ilikuwa ni sababu kwepeshi ya kuficha ukweli

Vita baridi ilikwisha kwa anguko la Soviet Union USSR.. Mabepari yaliibuka washindi na kuweza kuitawala dunia yatakavyo lakini madhara yaliyotuachia si haba!

Muunganiko uliopaswa kuwa na usawa umefeli pakubwa.

Mamlaka moja jina lake asilia limenyongelewa mbali huku nyingine ikitamaki na la kwake.

Mamlaka moja pamoja na kupokwa madaraka hapo kwanza lakini sasa iko hatua za mwisho kujitwalia mamlaka kamili, bado kipengele kimoja tu dhaifu cha kisiasa!

Tunapoelekea tamati ya huu mwisho wa iliyokuwa ndoa ya mkeka ninini hatima ya Tanganyika kwa utambulisho?
Nilitegemea uhubiri suala la Zanzibar kuachana na mambo ya kujiita nchi na badala yake iwe mkoa ndani ya Tanzania hili tusahau tofauti zetu kama tulishawahi kuwa na Tanganyika na Zanzibar.

Kinachofanya muungano wetu uendelee kuwa na mushkeli ni kwa kuwa Tanganyika ili-realise ndoto za muungano kwa kukubali kujisalimisha lakini Zanzibar yenyewe iligoma kumezwa na muungano.

Kiufupi muungano wa kweli kwa mtazamo wangu tutaufikia pale tutakapo kubali kuwa NCHI MOJA yenye mamlaka kamili na siyo nchi mbili au tatu zenye mamlaka tofauti lasivyo makandokando hatuwezi kuyaepuka, na kuvunja muungano ni suala ambalo halitokuwa na manufaa yeyote kwa pande zote mbili.
 
La kukubali kuwa nchi moja hilo tusahau kabisa na halitakuja litokeee.. Kuuvunja muungano ni rahisi zaidi kuliko hilo la kutaka kuunda nchi moja
 
Ulitaka niwe mwafrika ? Kwani yule mfalme wa Kuwait, aliyekuwa mfalme wa Oman Qaboos, ni waafrika?

Ile michezo ya Mapadri inawatoa akili na kuwatia chuki
Sio nilitaka Bali hata mtoto mdogo wa kiarabu akikuona Kyle yemeni atajua wewe ni mwafrika!
we Kwa mambo hayo ya michezo ya kisilamu hupo salama🙆🙄
 
Katiba aliyoiandika Nyerere, Zanzibar ina katiba yake Hiyo katiba aliyoapia Mpango itakuwa ya wapi Kama si Tanganyika iliyovaa koti la muungano?
Aliapa Kuilinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Aliapa Kuilinda Tanganyika?? 👂
 
Tanganyika inafutwa zaidi na watanganyika wenyewe kwa kushindwa kuipigania kama wanavyofanya wazanzibar kwa Zanzibar yao.

Jambo pekee liliobaki kwetu ni kuwaruhusu waondoke bila kuwabugudhi ili waiache...baada ya kuondoka ndio tubadili jina na kurudia Tanganyika yetu.
Sisi wa bara tumelala sana.
Muungano hata ukivunjwa still sisi tutajiita TANZANIA, Tanganyika ndio nini
 
Ufitini huu mbona akiwa ofisini Magufuli au Mkapa hakunaga harakati kama hizi za Tanganyika
 
Tatizo mojawapo la kuzingatia!
Leo Muungano Unalindwa na Rais Aliye Apa Kuulinda Muungano kama Ulivyo!
Ikiwa Muungano Umekufa ghafla Nani Atakuwa Rais wa Tanganyika?
Zenj wataendelea kuwa na Rais Aliyeapa kuilinda zenj!
Raisi wa Tanzania ndio raisi wa Tanganyika,
 
Sababu kificho iliyofanya tuungane na Zanzibar ilikuwa ni kwasababu ya vita baridi ya dunia kati ya wajamaa na mabepari.. Sisi watanganyika tulitumika tuu, ishu ya kusema ni kwasababu za kiusalama na matisho ya kigaidi ilikuwa ni sababu kwepeshi ya kuficha ukweli

Vita baridi ilikwisha kwa anguko la Soviet Union USSR.. Mabepari yaliibuka washindi na kuweza kuitawala dunia yatakavyo lakini madhara yaliyotuachia si haba!

Muunganiko uliopaswa kuwa na usawa umefeli pakubwa.

Mamlaka moja jina lake asilia limenyongelewa mbali huku nyingine ikitamaki na la kwake.

Mamlaka moja pamoja na kupokwa madaraka hapo kwanza lakini sasa iko hatua za mwisho kujitwalia mamlaka kamili, bado kipengele kimoja tu dhaifu cha kisiasa!

Tunapoelekea tamati ya huu mwisho wa iliyokuwa ndoa ya mkeka ninini hatima ya Tanganyika kwa utambulisho?
Kuirudisha Tanganyika ilikuwa ni kwa kumuunga mkono Hayati Mchungaji Christopher Mtikila, muasisi wa UKAWA. Sema ndio vile vyama vyetu hivi huwa havijui lipi jambo la maana na muhimu kwa wakati husika. Aliachwa kuipambania Tanganyika yeye peke yake na hata kurudishwa nyuma na vyama vingine vya siasa.

Tukiachana na hayo, katiba ya Warioba ndio ilikuwa inairudisha Tanganyika, kwa hiyotu hiyo tuanzie kwa Katiba ya Warioba, irejee kwenye bunge maalum la Katiba na ije kupigiwa kura. Bunge la Katiba lisibadilishe chochote libariki tu ije kwenye kura za maoni
 
Wengi wamebaki kushangaa.. wameduwaa.. zama zile walizoea kutaja 'Tanzania Bara' na 'Tanzania Vsiwani' sasa nchi inatajwa 'Tanzania Bara' na 'Zanzibar' .. muungano ule sio huu. Kuna jambo haliko sawa. Kama muungano ulikuwa wa sovereign states mbili Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika i wapi?
Huwa sifatilii lakina naona kama mambo yamebadilika kidogo.
nasoma mimi niliambiwa Tz ina mikoa 26 (21 tz bara na 5 tz visiwani)
lakini sasa hivi mtu akikuuliza tz ina mikoa mingapi, naona anakuwa ana maanisha tanganyika ina mikoa mingapi maana zanzibar ni kama ka nchi fulani kamekamilika.
 
Back
Top Bottom