Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Tufanyeje tuweze kuirejesha Tanganyika?

Kama halikuwa ndilo lengo hasa la muungano wetu unafikiri kwanini nyerere haliitowesha tanganyika?

Kitendo cha kuchanganywa kwa udongo wa Tanganyika na Zanzibar kuliashiria kuyazika completely mataifa haya na MOJA na siyo kuamasisha uwepo wa serikali 3 au utengano, mwisho wa siku divide & rule ni faida ya politicians.
Undava King hivi unajua muungano wa sasa umeshikiliwa na kiuzi kimoja chembamba cha siasa? Zenji kwasasa wana kila kitu kasoro chama cha siasa
 
Kwenye miungano mingine huko Duniani haindoi zile nchi mama kufutika kwenye ramani.

Huendelea kutajwa tu kama vile Wales, Scottish, Australia, N.k

UK nchi jumuia zimekuwa zikitumia majina kama kawaida,

Hata kwenye uraia wamekuwa watu wao wakirejea nchi zao mama,

Sasa Tanganyika Kwanini ifutike mazima kwenye ramani ya Dunia?

Hivi aliyeturoga ni nani ?
 
Hoja dhaifu sana, ni sawa na wale ambao eti tuu kwa kuwa wamezaliwa na kukulia mijini basi eti hawaoni umuhimu wa kujua chimbuko la ukoo wao huko kijijini.
Chimbuko la ukoo linakusaidia nini? Wewe juwa baba yako na mama yako halafu jikite na kutafuta hela. Mnajipa kazi nyingi ambazo hazina tija
 
Sema kwamba tuanzie na rasimu ya katiba ya mzee Warioba lakini tuibireshe zaidi.
Hapo kwenye kuiboresha ndipo chama tawala wanapopataka, wanapitia humohumo kuweka mambo yao. Rasimu ya Warioba si imekusanya maoni ya wananchi, ipite kama ilivyo ikapigiwe kura na wananchi haohao waliotoa maoni. Bunge libariki tu mchakato au ikibidi, sheria ielekeze tu Rasimu ikapigiwe kura moja kwa moja, kusiwe na bunge la katiba.
 
Ule uhuru 9 December , Muingereza aliipa Tanzania ??
Kusema ukweli Zanzibar ni kupe Tanzania

Wanaleta wafanyakazi Bara
Wanaleta wabunge Bara
Wanaleta mawaziri Bara
Wananunua ardhi Bara

Ila Watanzania hawawezi pata chochote kule kwao
Yaani hawa Watanganyika waliojaa huku Zanzibar ni hatari, karibu kisiwa kitazama . Kuna wengine kwa mamia wanalala mpaka kwenye mapaa ya Nyumba Za Michenzani , Wamasai wameacha mifugo yao wamekuja kuchunga samaki , maana ng'ombe wamewashinda, wamejaa.
 
Undava King hivi unajua muungano wa sasa umeshikiliwa na kiuzi kimoja chembamba cha siasa? Zenji kwasasa wana kila kitu kasoro chama cha siasa
Ni kweli muungano wetu kiunganishi chake kwa sasa ni 'CCM' na wako radhi kumpitisha wamtakae hata kinguvu kutoka chama chao hili ahimarishe utawala kule visiwani, hili ile idea ya kuuvunja muungano iwe under control na mapungufu yaliyopo yasizungumziwe lakini huu ni ujinga wa kushindwa kuandaa suluhisho la kudumu.

Nakuunda serikali tatu haitokuwa na utofauti na muunganiko wenye mfanano na ule wa kijumuiya kama Afrika ya mashariki yaani kiufupi muungano wetu utavunjika tu iwe isiwe kwa sababu akutokuwa na strong bonds kati yetu na pia gharama za uendeshaji wa serikali zote tatu ni mzigo mkubwa kwa wananchi.

Kama kweli wanajali maslahi ya Tanzania waitane waketi meza moja waunganishe serikali zote mbili pamoja, wavunje mihimili yote ya kidola na tuwe wamoja tukipambania nafasi za uongozi na uchumi kwa usawa kama nchi moja na Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mikoa inayounda Tanzania.

Ila kutokana na suala la pride, maslahi ya kisiasa na ignorance watu hawatokuwa tiyari kuachia identity ya taifa lao ipotee, basi kama hawataki tuumane 'jino kwa jino' zichapwe tu atakayeshinda atatanua ukubwa wa territory yake,

Ni bora hasara ya vita kuliko malipo ya fidia ya kuvunja muungano pamoja na mambo ya kiusalama ukichukulia zenji ni taifa la kiislamu na lina washirika wengi arabuni na bado litatumiwa na mataifa ya magharibi kutufanya tusiwe stable kama Kenya na Somalia.
 
Nipe faida walau 3 tuu za Muungano, hasa kwa mtanzania wa kawaida kabisa kule Namanyere, Likawage, Nanjirinji, Nakapanya, Nanguruwe na kwingineko.

Sio mpaka muungano ukufaidishe wewe , hao wanaofaidika nao na wao ni WATANZANIA
 
d33ec815e4023a3b64a72e0a05dc8e30.jpg
 
habari yako kiongozi

samahan mi toka nmetoka chuo nmesomea excavator sjapata ata pakujishkiza kaka kama una hints zozote labda unaeza nsaidia
 
habari yako kiongozi

samahan mi toka nmetoka chuo nmesomea excavator sjapata ata pakujishkiza kaka kama una hints zozote labda unaeza nsaidia
Ngoja mwaka upinduke usijali tutaona cha kufanya
 
Sababu kificho iliyofanya tuungane na Zanzibar ilikuwa ni kwasababu ya vita baridi ya dunia kati ya wajamaa na mabepari.. Sisi watanganyika tulitumika tuu, ishu ya kusema ni kwasababu za kiusalama na matisho ya kigaidi ilikuwa ni sababu kwepeshi ya kuficha ukweli

Vita baridi ilikwisha kwa anguko la Soviet Union USSR.. Mabepari yaliibuka washindi na kuweza kuitawala dunia yatakavyo lakini madhara yaliyotuachia si haba!

Muunganiko uliopaswa kuwa na usawa umefeli pakubwa.

Mamlaka moja jina lake asilia limenyongelewa mbali huku nyingine ikitamaki na la kwake.

Mamlaka moja pamoja na kupokwa madaraka hapo kwanza lakini sasa iko hatua za mwisho kujitwalia mamlaka kamili, bado kipengele kimoja tu dhaifu cha kisiasa!

Tunapoelekea tamati ya huu mwisho wa iliyokuwa ndoa ya mkeka ninini hatima ya Tanganyika kwa utambulisho?
Siku CCM ikitoka madarakani itakua ndio mwanzo wa kufufuliwa kwa Tanganyika yeyu
 
MAONI YANGU KUHUSU SULUHISHO LA KUDUMU LA KERO ZA MUUNGANO ULIOPO

TUNAPOIKUMBUKA APRILI 26, YA MWAKA 1964 TUJIKITE ZAIDI KATIKA KUEPUKANA AU KUMALIZA KABISA ZINAZOITWA KERO ZA MUUNGANO KWA KUFANYA YAFUATAYO:

MOSI, TUWE NA NCHI MOJA NA SERIKALI MOJA, YAANI MUUNGANO KAMILI (COMPLETE UNION). TUACHANE KABISA NA MUUNGANO HUU WA KUBANANA, KUFINYANA, KUPUNJANA NA KULAUMIANA.

PILI, TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZIWE NCHI KAMILI ZENYE MAMLAKA KAMILI NA KUBAKIA MAJIRANI WEMA WA KIHISTORIA NA KINDUGU.

HILI NDILO SULUHISHO BORA NA LA KUDUMU LA MUUNGANO HUU USIOISHA KERO.
Credit: brother Gwappo Mwakatobe
 
Tufanye "mojawapo" ya hayo mawili: kuwa na nchi moja na serikali moja, au kuwa na nchi na serikali 2 tofauti zenye ujirani mwema na wa kistoria na kindugu.
 
Sababu kificho iliyofanya tuungane na Zanzibar ilikuwa ni kwasababu ya vita baridi ya dunia kati ya wajamaa na mabepari.. Sisi watanganyika tulitumika tuu, ishu ya kusema ni kwasababu za kiusalama na matisho ya kigaidi ilikuwa ni sababu kwepeshi ya kuficha ukweli

Vita baridi ilikwisha kwa anguko la Soviet Union USSR.. Mabepari yaliibuka washindi na kuweza kuitawala dunia yatakavyo lakini madhara yaliyotuachia si haba!

Muunganiko uliopaswa kuwa na usawa umefeli pakubwa.

Mamlaka moja jina lake asilia limenyongelewa mbali huku nyingine ikitamaki na la kwake.

Mamlaka moja pamoja na kupokwa madaraka hapo kwanza lakini sasa iko hatua za mwisho kujitwalia mamlaka kamili, bado kipengele kimoja tu dhaifu cha kisiasa!

Tunapoelekea tamati ya huu mwisho wa iliyokuwa ndoa ya mkeka ninini hatima ya Tanganyika kwa utambulisho?
Ni aibu kuendelea kuishi enzi za miaka ya 1960 na ambayo uhalisia wake haupo kwa sasa. Ili tuishi kisasa ni kuzirejeshea mamlaka kamili Tanganyika na Zanzibar sasa hivi!
 
Hazijawahi kukoma labda tu pengine hufuatilii historia.. Unakumbuka kundi la G55?
Ni vema watu wajue kuwa Tanganyika bado ipo na Watanganyika bado tupo. Hata Wazanzibar ni vivyo hivyo, wakiwa nje ya nchi hujitambulisha kuwa ni Wazanzibar, si Watanzania.
 
Kwani hata kuuvunja kuna ubaya gani?
Kumevunjwa , Soviet Union, Czechoslovakia , Senegambia nk na dunia inaenda Itakuwa huu uvamizi wa Nyerere uliopewa jina Muungano. Wazanzibari tume suffer vya kutosha tumechoka na jinamizi hili
Sawa kabisa!
 
Back
Top Bottom