Tufanye nini ili TBC iwe na mvuto kwa watazamaji?

Simple! Wamrudishe Tido Muhando harafu wasimuingilie kwenye kazi zake na wamuwezeshe kufanya kazi zake? Huyu wa sasa alikuja na fujo nyingi kumbe nguvu ya soda. Kazi kweli kweli
 
Ningalipata nafasi ningalifumua Programming yote ya Tbc! Ninge invest kwanza kwenye news bulleting kwa kuweka "Commanding personalities tu" kuna wale watu wakikaa kwenye Tv wanakufanya tu utazame! si kila mtu anacho hicho kitu! Tbc hawazidi 4!
Mwl,Ryoba ana kazi nzito! tumuunge mkono!
Big Up,

P.
 
Matatizo wameyalimbikiza yamekuwa mengi kiasi kwamba hata pesa za kuyatatua inakuwa ngumu kuzipata. Sijui huwa hawayaoni? Watangazaji wanaonekana ni wasomi sawa lakini ile organisation culture inawaondolea ufanisi wao katika kufanya kazi.
 
Nashukuru kwa ushauri mzuri nadhani wahusika wameelewa wakumbuke kwamba TBC ni ya taifa na hivyo inapaswa kutokurusha matangazo kwa upendeleo na pia waongeze ubunifu kama CMG. Msg sent.
 
Ni muda mrefu sana tokea mpira wa VPL uanze kurushwa na azam TV na baadae kundi la orijino komedi kupotea na tena bunge live lilivyositishwa TBC imeonekana kukosa washabiki wengi.

Kiukweli ndio maana nimeona tusaidiane namna ya kuwashauri hawa ili waweze kuwa na mvuto kwa watanzania.

Hii imeonekana kukosa mvuto pamoja na kwamba inaoneshwa bure kabisa lakini mtu yuko radhi anunue kifurushi ili tu aangalie Shilawadu.


Wawafukuze kazi wote walio na vyeti fake na watoto wa mjomba/shangazi. Walete watangazaji wa ukweli na wenye taaluma.
 
Kwakweli sijui hii TV ina nini. Yaani nikiishiwa kifurushi niko radhi nisiangalie TV kuliko kutazama TBC
 
Yah akili ndio kipindi pekee kinachoangaliwa na watoto kwa idadi kubwa
 
1. Wapunguze wazee wastaafu.
2. Waache kuwaza kuteuliwa sijui u-DC, RCnk ambayo inaleta kujipendekeza mpaka unakuwa mpumbavu
3. Ubunifu zero
4. Utaifa na uzalendo zero (timu ya taifa inacheza wao wanarusha chereko sijui choroko
5. Picha mbaya nyeusi hazina mvuto.
6. Against upinzani hata akitoa hoja nzuri kiasi gani
7. Waondoe matangazo ya biashara, hii ni TV ya taifa sio binafsi
8. Wasipangiwe cha kurusha, kusoma, nk

Hya ni mawazo ya kuiua TBC na si kuiboresha
 
Kila mtu ana uhuru wa kuangalia RUNINGA anayotaka, na kusikiliza REDIO aonayo bora
 
Waache kuegemea upande mmoja, waangalie technical problems mfano habar unakuta sauti inatangulia video, mwisho mkulu nae aiangalie aache kuangalia mawingu
 
Ni muda mrefu sana tokea mpira wa VPL uanze kurushwa na azam TV na baadae kundi la orijino komedi kupotea na tena bunge live lilivyositishwa TBC imeonekana kukosa washabiki wengi.

Kiukweli ndio maana nimeona tusaidiane namna ya kuwashauri hawa ili waweze kuwa na mvuto kwa watanzania.

Hii imeonekana kukosa mvuto pamoja na kwamba inaoneshwa bure kabisa lakini mtu yuko radhi anunue kifurushi ili tu aangalie Shilawadu.
can you make the corpse work?
 
Doh! Tbc kama chombo cha umma kinapaswa kwenda na wakati! kwa bahati nzuri sana Mwl. Ryoba ana experience na exposure na suala la mabadiliko si la mtu wala siku moja!

:Kwa kuwatazama tu hao presenters hawana hata wardrobe /make up allowance ndin maana watu wengi mnawazungumzia sana! ukiwa mfuatiliaji utawagundua mpk tai wanazo ngapi!

:Mkurungenzi wa habari na matukio (Nadhani mama Suzie Mungy bado ana hudumu) abadilike kwakweli! haiwezekani kuna tukio kubwa la kitaifa limetokea nchini hulioni kwenye taarifa ya habari kisha habari kuu unakuta "Mwnyekiti wa Ccm Nkasi atembelea wafungwa" au "Wakulima wa pareto wataka pembejeo"

:Kuna mambo ya kiufundi yanatokea hewani unajiuliza hivi hakuna news editor? eg: kwenye link ya habari zao za biashara na imekua ikimtokea sana Vumilia Mwasha wote tunafaham hua ile segment ni recorded lakini hata kuziondoa zile take one! two! nazo ni shida!

:Camera sasa! kituko! wide shot ina rangi ya orange close up brown! unajiuliza hata white balancing nayo niya kuhoji? tunafaham camera hajatengenezewa mtu mweusi ndio mana hakuna "black balancing" lakini wapi!

:Ningalipata nafasi ningalifumua Programming yote ya Tbc! Ninge invest kwanza kwenye news bulleting kwa kuweka "Commanding personalities tu" kuna wale watu wakikaa kwenye Tv wanakufanya tu utazame! si kila mtu anacho hicho kitu! Tbc hawazidi 4!

Mwl,Ryoba ana kazi nzito! tumuunge mkono!
uyo ryoba experience ameipata wapi?
 
Back
Top Bottom