Tufanye nini ili TBC iwe na mvuto kwa watazamaji?

j kisumu

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
289
236
Ni muda mrefu sana tokea mpira wa VPL uanze kurushwa na azam TV na baadae kundi la orijino komedi kupotea na tena bunge live lilivyositishwa TBC imeonekana kukosa washabiki wengi.

Kiukweli ndio maana nimeona tusaidiane namna ya kuwashauri hawa ili waweze kuwa na mvuto kwa watanzania.

Hii imeonekana kukosa mvuto pamoja na kwamba inaoneshwa bure kabisa lakini mtu yuko radhi anunue kifurushi ili tu aangalie Shilawadu.
 
1. Wapunguze wazee wastaafu.
2. Waache kuwaza kuteuliwa sijui u-DC, RCnk ambayo inaleta kujipendekeza mpaka unakuwa mpumbavu
3. Ubunifu zero
4. Utaifa na uzalendo zero (timu ya taifa inacheza wao wanarusha chereko sijui choroko
5. Picha mbaya nyeusi hazina mvuto.
6. Against upinzani hata akitoa hoja nzuri kiasi gani
7. Waondoe matangazo ya biashara, hii ni TV ya taifa sio binafsi
8. Wasipangiwe cha kurusha, kusoma, nk
 
Wafanye kazi kwa weledi kwa ushindani na waache siasa hiyo TV Inaendeshwa kwa kodi zetu watanzania
Wamewahi kufanya kazi kwa weledi mkubwa na ushindani kipindi cha Tido Mhando, wakavutia sana watazamaji. Kilichofuata wakaingia MGOGORO Mzito na Mengi kwasababu ya kunyang'anyana MATANGAZO YA KIBIASHARA. Kina Mengi wakawa wanaipiga vita kwamba TBC inatumia ruzuku ya serikali hivyo haitakiwa kuweka ushindani mkali hususani wa kibiashara kwenye media

- Kwahiyo mambo mengine jamani ni zaidi ya myajuavyo
 
Iache uoga wa serikali
2. Istopishe upesi HABARI za madereva
3. Irudishe ze komedi na kututolea wapuuzi wanaoshindwa kuchekesha na kuishia kuwasifia wadhamini(Coca-Cola)mpaka inakuwa kero
4. Watoe kipindi cha bango
5. Waajiri vijana
Watoe kipindi cha lile jamaa lenye sifa linadhaminiwa na redbull
6. Waboreshe urushaji wa picha na sauti Uwe wa kisasa
7. Waache kutangaza habari wawili wawili pia wawe wanasoma comment zote za watazamaji sio zinazosifia serikali tu.
 
Ni muda mrefu sana tokea mpira wa vpl uanze kurushwa na azam TV na baadae kundi la orijino komedi kupotea na tena bunge live lilivyositishwa TBC imeonekana kukosa washabiki wengi.

Kiukweli ndio maana nimeona tusaidiane namna ya kuwashauri hawa ili waweze kuwa na mvuto kwa watanzania, hii imeonekana kukosa mvuto pamoja na kwamba inaoneshwa bure kabisa lakini mtu yuko radhi anunue kifurushi ili tu aangalie shilawadu.
of what use? let it die!
 
Watangazaji tu sura zao kama kituo cha tv cha kijeshi!!mtu anatangaza taarifa ya habari amekuja uso kama anatangaza hali ya hatari?!!
Doh! Tbc kama chombo cha umma kinapaswa kwenda na wakati! kwa bahati nzuri sana Mwl. Ryoba ana experience na exposure na suala la mabadiliko si la mtu wala siku moja!

:Kwa kuwatazama tu hao presenters hawana hata wardrobe /make up allowance ndin maana watu wengi mnawazungumzia sana! ukiwa mfuatiliaji utawagundua mpk tai wanazo ngapi!

:Mkurungenzi wa habari na matukio (Nadhani mama Suzie Mungy bado ana hudumu) abadilike kwakweli! haiwezekani kuna tukio kubwa la kitaifa limetokea nchini hulioni kwenye taarifa ya habari kisha habari kuu unakuta "Mwnyekiti wa Ccm Nkasi atembelea wafungwa" au "Wakulima wa pareto wataka pembejeo"

:Kuna mambo ya kiufundi yanatokea hewani unajiuliza hivi hakuna news editor? eg: kwenye link ya habari zao za biashara na imekua ikimtokea sana Vumilia Mwasha wote tunafaham hua ile segment ni recorded lakini hata kuziondoa zile take one! two! nazo ni shida!

:Camera sasa! kituko! wide shot ina rangi ya orange close up brown! unajiuliza hata white balancing nayo niya kuhoji? tunafaham camera hajatengenezewa mtu mweusi ndio mana hakuna "black balancing" lakini wapi!

:Ningalipata nafasi ningalifumua Programming yote ya Tbc! Ninge invest kwanza kwenye news bulleting kwa kuweka "Commanding personalities tu" kuna wale watu wakikaa kwenye Tv wanakufanya tu utazame! si kila mtu anacho hicho kitu! Tbc hawazidi 4!

Mwl,Ryoba ana kazi nzito! tumuunge mkono!
 
Back
Top Bottom