MATAMKO: Chadema vyuo vikuu/chaso juu ya kuvuliwa uongozi kwa Zitto na Kitila

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,957
1,327
Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa chadema wametoa tamko kali la kulaani hali mbaya kisiasa na mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya chama hicho huku kamti kuu ikiwavua uongozi naibu katibu mkuu zitto kabwe na mjumbe wa kamati kuu kitila mkumbo.

Wamesema kuwa chadema taifa imejipambanua kama kikundi cha wachache wasiotaka kukosolewa wala kuona watu wanaotofautiana nao kimawazo. Wameweka msimamo kuwa wao wanamuunga mkono zitto kabwe na wanakitaka chama hicho kitumie busara kumaliza mgogoro huo kabla haujakiathiri chama..

Chanzo cluods radio habari.

----------------------------------------

TAMKO LA CHASO SAUT

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA .

Tamko la chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) tawi la SAUT Mwanza,kwa kushirikiana na umoja wa CHADEMA vyuo vikuu kanda ya ziwa.

Ndugu zangu watanzania, lifuatalo ni tamko letu kama wasomi wa CHADEMA tawi la chuo kikuu cha mtakatifu Augustino ,(SAUT) juu ya kinachoendelea ndani ya chama hasa kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na kamati kuu ya chama chetu pendwa na kilichobeba matumaini makubwa ya kumkomboa mtanzania.

Sisi wanachama na viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA tawi la SAUT Mwanza ,tunapenda kuunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya chama iliyokutana kuanzia tarehe 20-22/11/2013,kilichoazimia kuwavua nyadhifa zote za kiuongozi waliokuwa viongozi wa chama ndugu Zitto Zuberi Kabwe aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama,Dk Kitila Mkumbo aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama na ndugu Samson Mwigamba aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Arusha.kwani vitendo walivyokuwa wanafanya na walivyokuwa wamepanga kuvifanya ndani ya chama kama vilivyoelezewa vema na wasemaji wa chama vinakiuka katiba ya chama na maadili ya viongozi kuanzia ibara ya 10.1(viii)(ix)(xii) pamoja na ibara ya 10.2(iv)(v).

Pia tunapenda kuwaambia wanachama na wapenzi wote wa CHADEMA Tanzania,Kwamba chama hiki kimejengwa na kuundwa kwa misingi ya sheria na kanuni sahihi ni sharti kila mwanachama na kiongozi azifuate na kuziheshimu. Hivyo basi chama hiki ni taasisi kubwa na maamuzi yake hutokana na vikao halali ndani ya chama. Na atakaye kiuka kanuni na taratibu hizi za chama hana budi kuwajibishwa.

Pia tunapenda kukanusha TAARIFA ZILIZOSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII zikianzia Jamii Forums kwamba sisi wanachama wa CHASO SAUT tunapanga kufanya maandamano kupinga MAAMUZI HALALI YA KAMATI KUU YA CHAMA Hivyo Uongoziwa CHADEMA SAUT na wanachama wake kwa ujumla tunasisitiza kwamba taarifa hizo siyo sahihi na hazina ukweli wowote bali zililenga kupotosha umma na kuzalilisha uongozi wa CHASO na wanachama wake kwa ujumla.

Mwisho uongozi unapenda kumalizia kwa kutoa wito ufuatao.

Tunapenda kuwakumbusha watanzania kwamba CHADEMA ni chama makini,chenye sera,kanuni,taratibu na nia thabiti ya kuikomboa nchi hii kutoka mikononi mwa mafisadi na wezi wa CCM,uongozi unakumbusha kwamba, kuna watu wamefilisika,wamefungwa ,wamefukuzwa kutoka kwenye fursa zao za kimaisha na wengine hata kufariki dunia kutokana na harakati za chama hiki,hivyo kwenda kinyume namaamuzi ya chama ama kupanga kufanya hujuma ama usaliti wa namna yoyote ni kuzisaliti damu za watanzania hao,wanachama tuwe na utaratibu wa KUPENDA CHAMA KAMA TAASISI na si mtu binafsi kwani TAASISI inadumu lakini watu wanakufa,hivyo tujifunze kuheshimu maamuzi ya chama ambayo huamuliwa ndani ya vikao halali vya chama na tusikubali kupotoshwa na propaganda nyepesi nyepesi za watu wasiokitakia mema chama.

LANG'O JACKSON KITALY WILHAD
KATIBU CDM SAUT MKT CDM SAUT
TAREHE 29/11/2013.

TAMKO LA CHASO MOROGORO

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

CHASO MKOA

S. L. P 1976,

MOROGORO

30 November, 2013


TAARIFA RASMI YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA CHADEMA VYUO VIKUU (CHASO) MKOA WA MOROGORO KWA VYOMBO VYA HABARI.


Ndugu Wanahabari,


Ni matumaini yangu kuwa mu wazima na hongereni kwa kazi ya kupasha habari kwa umma wa watanzania.
Tumewaita hapa kuzungumza na umma wa Watanzania kupitia ninyi, na tuna mambo machache ya kuzungumza na kupasha umma kuhusu yanayoendelea ndani ya chama chetu.


Kufuatia kikao cha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHASO Mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 30.11.2013, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi 8.00 mchana katika ofisi za CHADEMA Mkoa wa Morogoro, kilichohudhuriwa na viongozi wa vyuo vikuu vya Mkoa wa Morogoro (Wenyeviti, Makatibu,na makatibu wenezi), wajumbe wa mkutano kwa kauli moja wameunga mkono maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya Chama dhidi ya Zitto Zuber Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama makini na umakini wake umethibitishwa na maamuzi yake dhidi ya wahujumu chama na wanaojiona miungu watu ndani ya chama chenye sura na matendo ya kidemokrasia, na kinachomthamini kila mtanzania.


Kwa mantiki hii na kwa tukio hili lililofanywa mbele ya watanzania, ni dhahiri kwamba CHADEMA kimekomaa na kinafaa kupewa jukumu la kuiongoza nchi kwani maamuzi magumu (na yenye manufaa kwa umma) ndiyo maamuzi stahiki kwa chama chochote cha siasa nchini na kote ulimwenguni.


Vipo vyama vingi vya siasa nchini (mathalan CCM) ambavyo vimekuwa vikiwaingiza wananchi kwenye nyakati ngumu na dimbwi la umaskini kwa kuwa tu, wanawalinda mafisadi, wasaliti, na watu wenye maslahi yao binafsi.
Taswira aliyoionesha Zitto Kabwe ni taswira mbaya na haifai kuigwa na kijana au mtu yeyote kwani kinachoonekana ni kwamba ameyatanguliza mbele maslahi yake binafsi na kuyaacha ya taifa na chama chake.


Zitto Kabwe amehasi chama na taifa kwa ujumla na ameshindwa kutekeleza majukumu yake sawia kama chama kilivyokusudia hadi kumpa jukumu la Naibu Katibu Mkuu Bara, nafasi ambayo ni nyeti sana ndani ya chama kinachokuwa kwa kasi kama CHADEMA.


Kama kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya chama, alikuwa na uwezo wa kuwashauri viongozi wenzake wa ngazi ya juu ndani ya chama pale walipokosea (kama kweli makosa yapo) na siyo kutumia nafasi hiyo kujitafutia mtaji binafsi wa kisiasa (personal political capital).


Kwa misingi ya hoja hii, hata kama kuna makosa yaliyofanywa na viongozi wenzake ndani ya chama, bado Zitto Kabwe hafai kuendelea kupewa jukumu lolote kwani kushauri mfumo (system) unapokosea ni jukumu la mwanachama yeyote na siyo kutafuta umaarufu ndani ya chama kwa kuombea viongozi kufanya kosa.


Wapo wanachama wanaokesha kwenye mitandao ya kijamii kuandika kwenye kurasa (pages) za viongozi waandamizi wa chama, wakiwa na lengo la kurekebisha au kutoa taarifa ya kukikuza chama hiki na kukilinda.


Hii ni kutokana na kutokuwa na ukaribu wa kutosha na viongozi hawa ili wawashauri. Tunamsikitikia ndugu Zitto Kabwe mwenye ukaribu na access ya kuonana na kiongozi mwenzake yeyote anayemhitaji na wakati wowote anayahifadhi mapungufu ya chama mfukoni ili kesho anunue umaarufu binafsi yeye na familia yake.


Pia CHASO Mkoa wa Morogoro kupitia viongozi na wawakilishi wa vyuo vikuu, tunawataka wanachama wa CHADEMA kuwa na subira na utulivu katika kipindi hiki cha mpito ndani ya chama kwani chama kinategemea nguvu ya umma katika kufanya maamuzi yake na CHADEMA ndilo tumaini jipya kwa Watanzania.


Pia tunawasisitiza wanachama na viongozi kutoterereka na kutumika kwa maslahi ya mtu binafsi au kikundi chochote chenye itikadi kinzani na ya chama na kuepukana na propaganda za wapinzani kwamba hoja giza katika maamuzi haya ni Hofu ya uongozi wa juu ndani ya chama (uenyekiti) jambo ambalo halina ukweli wala haliwezi kusadikika kuwa na ukweli wowote kwani yeye (Zitto) siyo mtu wa kwanza kuadabishwa na chama kwa utovu wa nidhamu binafsi na ya umma, wapo wakina David Kafulila, Danda Mjuju na wengine wengi ambao waliwajibishwa pale tu walipokwenda kinyume na chama na matakwa ya kanuni na katiba ya chama.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza,

Wenu katika Mapambano,

Ebenezer F. Kwayu.

Mwenyekiti CHASO, Mkoa wa Morogoro

Na

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa BAVICHA, CHADEMA

0764013330

ekwayu@ymail.com

WASOMI WAMNANGA ZITTO

Jumuiya kadhaa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zimeendelea kutetea uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho ya kuwavua nafasi za uongozi Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake.

Wengine waliovuliwa nafasi zao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo Novemba 22, mwaka huu kwa tuhuma za kukisaliti chama.

Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limemuonya Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini kuacha kuendelea kuzungumzia uaamuzi wa Kamati Kuu kwenye vyombo vya habari kwa maelezo kuwa wanayo mambo mengi yanayomuhusu ambayo wakiyatoa hadharani yatamshushia zaidi heshima yake.

Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa pamoja na Baraza la Vijana Mkoa wa Mbeya na Shirikisho la Umoja wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu wa Chadema (Chaso).

Heche alisema kuna mambo mengi kadhaa aliyoyafanya Zitto ambayo kama Bavicha itaamua kuyaanika hadharani huenda heshima aliyonayo kwenye jamii ikatoweka.
"Namsihi Zitto anyamaze, asiendelee kutumia vyombo vya habari kutaka kujitetea kwa sababu kama ataendelea kuzungumzia suala hili nasi pia tutaanika mambo yake na ninaamini kuwa ataumbuka zaidi," alisema Heche.

Alisema kauli na matendo ya Zitto yaliwatia shaka viongozi wenzake na wanachama kwa ujumla ndani ya chama na ndiyo sababu hawakuacha kumtilia shaka na kumfuatilia kabla ya kupatikana kwa waraka unaonyesha usaliti wa wazi kwa chama hicho.

Heche alisema kuwa kitendo cha Zitto kuvuliwa madaraka kuwaumiza zaidi mahasimu wao Chama Cha Mapinduzi (CCM) badala ya wana-Chedema wenyewe kinaongeza shaka na kuwafanya waamini kuwa uamuzi uliochukuliwa na Kamati Kuu ya Chadema ulikuwa ni sahihi.

"Ukiona unafanya jambo fulani kisha ukalaumiwa na adui yako ujue kuwa uamuzi ulioufanya uko sahihi, nasi kwa kuona kuwa uamuzi wa Kamati Kuu kumvua Zitto nyadhifa zake unawaumiza zaidi wapinzani wetu wa CCM, tunaamini kuwa hatujakosea," alisema Heche.

BAVICHA MBEYA YAUNGA MKONO

Kwa upande wake, Bavicha Mkoa wa Mbeya limetoa tamko la kuunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu kumvua nyadhifa zake Zitto Kabwe na kusema kuwa uamuzi huo ulifanyika kwa maslahi ya chama na Watanzania wote.

Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala, alisema vijana wa Mkoa wa Mbeya wanaunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu kwa vile hata wao walikuwa hawaridhishwi na mwenendo wa Zitto ndani ya chama kwa muda mrefu.

"Sisi kama vijana wa Mkoa wa Mbeya tunaunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu wa kumvua nyadhifa zote ndani ya Chama Zitto Kabwe kwa sababu hata sisi tulikuwa haturidhishwi na mwenendo, kauli na matendo yake ndani ya chama," alisema Kasambala.

Alisema Zitto kwa kipindi kirefu amekuwa akifanya vitendo ambavyo vinaonyesha wazi kukihujumu chama huku akiwa haonekani katika baadhi ya matukio muhimu ya kukitetea chama na wananchi kwa ujumla.

Hata hivyo, Kasambala aliiomba Kamati Kuu kutumia busara zaidi kumrekebisha Zitto badala ya kumfukuza uanachama kwa sababu pamoja na makosa yake yote bado mchango wake wa kuijenga Chadema unahitajika.

CHASO MORO: NI MAAMUZI SAHIHI

Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Chaso) wa Chadema mkoani Morogoro imeunga mkono maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya kuwavua uongozi Zitto na wenzake.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chadema Mkoa, Mwenyekiti wa Chaso, Ebenezer Kwayu, alisema hayo ni maazimio ya kikao cha tarehe Novemba 30 kilichokaa kwa saa nane katika ofisi za Chadema Mkoa wa Morogoro.

Alisema uamuzi wa Kamati Kuu ulifanyika baada ya kutafakari na kubaini uwepo wa mbinu chafu za kisiasa zenye taswira ya ubinafsi kwa badhi ya viongozi ambazo zisipodhitiwa mapewa zitasababisha chama tegemewa kama Chadema kusambaratika.

"Viongozi hawa na wengine wameonyesha taswira ya ubinafsi, siasa chafu za kuviziana na kutafutana makosa pasipo kukumbushana mapema ili kuboresha chama badala yake wamefanya hivyo wakilenga kutengeneza umaarufu ndani ya taasisi kubwa kama hii kwa faida zao binafsi, sisi wasomi Moro tunasema si sahihi na uamuzi wa Kamati Kuu ndio sahihi," alifafanua Kwayu.

Kwayu aliyeongozana na viongozi wa chama hicho wakiwemo wenyeviti, makatibu na makatibu wa uenezi, alisema Chadema ni chama makini na umakini wake umethibitishwa na maamuzi magumu na mazito dhidi ya hujuma zinazofanywa na baadhi ya wanachama wanaojiona miungu watu ndani ya chama.

Alisema mamuzi ya Kamati Kuu yanadhihirisha kwa Watanzania kuwa Chadema kimekomaa na kinafaa kupewa jukumu la kuongoza nchi kwa uwezo wake wa kutomwonea haya mtu, tofauti na vyama vingine kikiwemo chama tawala ambavyo vinawaingiza wananchi kwenye wakati mgumu kwa kuwa hakuna wa kumkea mwenzie kwa ufisadi na ubinafsi.

ZIARA YA DK. SLAA KIGOMA YASITISHWA

Uongozi wa Chadema Mkoa wa Kigoma umemuomba Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, kuahirisha ziara ya kichama mkoani humo iliyiopangwa kuanza keshokutwa.

"Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uweze kwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu.

Hata kama yanamaumivu, "inasema sehemu ya taarifa ya Chadema Mkoa wa Kigoma ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wake, Jafari Kasisiko, na Katibu, Msafiri Wamalwa.

Taarifa hiyo inasema kuwa uamuzi huo unatokana na kutokuwapo na uhakika wa hali ya usalama baada ya maamuzi ya Kamati Kuu.

Alisema ziara hiyo ilitarajia kuanzia Wilaya ya Kakonko Jimbo la Buyungu na kumalizia Kanda ya Magharibi Desemba 14 mwaka huu.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo, juzi walifanya kikao cha Baraza la Uongozi la Mkoa na kuwashirikisha viongozi wa Wilaya Kigoma Mjini, Kusini na Kaskasini ili kujadili na kupanga utaratibu wa ziara hiyo.

Alisema katika kikao hicho waliangalia hali ya usalama kwa sababu Katibu Mkuu ni mtu mkubwa kichama na walijadili suala hilo kwa muda wa saa tatu na viongozi waliwathibitishia kuwa hali siyo nzuri hakuna uhakika wa usalama atakapokuwa katika maeneo hayo kutokana na maamuzi ya kumvua uongozi Zitto.

Aidha, alisema Jimbo la Kasulu, Buhigwe na Muhambwe viongozi wao walidai hali ya usalama siyo nzuri na hawawezi kumhakikishia usalama kiongozi huyo wa kitaifa.
Alisema kutokana na hali hiyo, wameamua kuwashauri viongozi wa kitaifa kuwa ni vizuri katibu mkuu akaahirisha ziara yake mkoani Kigoma ili waweze kufanya uchunguzi wa kina kama kweli amani inaweza kuwapo.

Kasisiko alisema wameshauri makao makuu waahirishe ziara ya Dk. Slaa kwa sasa wakati wanajaribu kufanya ziara katika majimbo ya mkoa kwa kutoa elimu kuhusiana na maamuzi dhidi ya Zitto.

Alisema Kigoma ni ngome ya Chadema na kuwa baada ya muda mfupi vijana watatulia na hali itakuwa nzuri ya kumuwezesha Katibu Mkuu au kiongozi yeyote wa kitaifa kufika wakiwa na uhakika wa usalama wao.

Kuhusu maamuzi ya Kamati kuu, alisema: "Sisi kama mkoa hatujatamka chochote na hatukukusudia tutamke chochote kuhusiana na tukio hilo kwa sababu tukio limechukua utaratibu wa kawaida wa Chama.
Kikao kilichomvua madaraka Zitto Kabwe ni kikao halali cha chama, Kamati Kuu ina mamlaka na uwezo huo na sisi kama viongozi wa chini hatupaswi kuhoji kwa mujibu wa taratibu za chama chetu."

Imeandikwa na Emmanuel Lengwa, Mbeya; Ashton Balaigwa, Morogoro na Joctan Ngelly, Kigoma.

Home

CHASO IRINGA

WEDNESDAY, DECEMBER 11, 2013

December 7 / 2013.

Chadema Students' Organization (CHASO) ni umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo iliyo chini ya Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) taifa iliyoanzishwa chini ya kanuni ya Mabaraza ya chama katika kipengele 7.8.2(a) cha katiba ya chadema


Msimamo:
Umoja wa wanafunzi wa vyuo (vikuu) wanachadema / Chadema Students Organisation(CHASO) IRINGA, unatamka rasmi wazi kwamba tunaunga mkono kwa asilimia zote maamuzi yaliyotolewa na kamati kuu ya chama Makao makuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuhusiana na kuvuliwa nyadhifa za uongozi kwa baadhi ya viongozi ndani ya chama.

Tukiwa ni taasisi ya Chama inayoundwa na wanafunzi wa elimu ya juu Mkoani Iringa, tunakubaliana moja kwa moja na maamuzi ya chama, pia tunaungana na wenzetu wa CHASO Kanda ya Dar-es-salaam kulaani vikali vikundi vya kihuni vinavyotumia vibaya jina la CHASO
kutoa matamko yanayopingana na maamuzi ya kamati kuu ya chama; kwani kama weledi ni wazi kwamba wanaelewa taratibu kamili zinazopasika kufikia hatima mahususi.


Maamuzi ya kamati kuu ya chama yanaonesha wazi na dhahiri kwamba Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ni chama kipevu yaani kilichokomaa na chenye misimamo yake: kisichoogopa Umaarfu wa Mtu bali ni chama kinachosimamia na kufuata misingi ya kikanuni na taratibu (katiba) iliyojiwekea.

Tunawaomba Watanzania kutoamini katika ushabiki wa kisiasa unaoendelea ama kutokuwa washabiki wa umaarufu wa mtu fulani ama kikundi fulani cha watu, katika kufikia maamuzi juu ya suala lolote katika jamii; pia tuwe wafuatiliaji na waelewa kwa kina juu ya mambo yanayohusika ili tuweze kufikia maamuzi sahihi bila upotofu (kupotoshwa).


Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesimamia dhana ya uwajibikaji katika ngazi zote bila kuangalia ama kuogopa nyadhifa au nafasi ya mtu, bali kuhakikisha utaratibu unafuatwa katika kufikia maamuzi bila woga, pasipo kuathiri matakwa ya kikatiba.


Watanzania wote kwa ujumla: wasomi kama dira ya jamii huu ni wakati ambao tunatakiwa kutumia uledi na busara katika kuangalia mambo(uchambuzi) kwa upeo mpevu. Ni rai kwetu kwamba si vema kutoa shutuma dhidi ya chama bila kufuatilia ama kuelewa taratibu na kanuni (katiba) zinazopasika katika kufikia maamuzi sahihi. Maamuzi sahihi sio lazima yamfurahishe kila mtu bali kulinda maslahi ya Chama na Umma kwa ujumla wake.


Watanzania hatupaswi kukurupuka kiushabiki na hurka binafsi/mihemko ama jazba na gadhabu kwani kwa kufanya hivyo tutawapa nafasi watu wenye hinda katika gurudumu la mabadiliko tunayoyaelekea hivyo tunapaswa kuwa makini.


Kimsingi tunatakiwa kuwa watu wenye Mantiki na upembuzi yakinifu katika kufikia maamuzi kwa kuzingatia uhalisia wa dhana ya uwajibikaji; hivyo basi, katika kuyaelewa mambo na tufanye tafiti za kina ili kuweza kufikia maamuzi ya kuamini watu wengine katika usahihi wake, hivyo kutozipa nafasi hisia za propaganda za mamluki.


Tunawaomba Watanzania wote katika makundi mbalimbali, kuondokana na dhana ya ushabiki katika mambo ya msingi kwani mpango wa Chadema ni kuangalia na kulinda maslahi ya Umma
na siyo kujenga jina ama umaarufu wa mtu mmoja mmoja, pia chama siyo sehemu ya malumbano; hivyo shauku yetu ni kujenga wanachama Imara na siyo kupata mashabiki kabambe.

Chadema itaendelea kuwa chemchemi ya Ukombozi wa Taifa na ujenzi wa viongozi wenye nidhamu, haki na uwajibikaji.


Pia tutumie fursa hii kuwaonya watu wanaotumiwa kusambaza propaganda zenye lengo la kuendeleza marumbano yasiyo na msingi.


Mwitikio wa vyama vya siasa nchini umekuwa ni watofauti kwa kuwa vinara wa kuleta mkanganyiko baina ya watanzania na uvumi wa propaganda; swali rahisi la kujiuliza wana maslahi gani juu ya maamuzi ya CHADEMA ama mtu yeyote ndani ya CHADEMA?, pia tunawataka watanzania waelewe kwamba malengo ya timu (wachezaji katika timu ni kuhakikisha wanafunga goli ili kupata ushindi mchezaji anayepiga chenga nyingi na kukimbia na mpira mpaka nje ya uwanja anakuwa hafai anapaswa kukaa benchi).


Tunawaomba watanzania tushikamane katika kipindi hiki cha mpito, tukielewa ya kwamba tunapaswa kuwa makini na propaganda zinazofanywa na makundi ya watu wenye lengo baya la kurudisha nguvu ya harakati dhidi ya mabadiliko tunayoyakusudia, kwani kila mapinduzi au mageuzi yanakwenda na usaliti. Chadema kitaenzi mawazo na mchango mzuri wa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na chama kwa maslahi ya Umma.




MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA.



TIMOTHEO J. MKANYIA..............MWENYEKITIKITI CHASO IRINGA 0713739683
ANDEMBWISYE ISRAEL…………………….KATIBU CHASO IRINGA 0764969838
MICHAEL NOEL…………………KATIBU MWENEZI CHASO IRINGA 0716746442

MWENYEKITI CHASO


posted by Chadema Blogtz at 2:23 AM
 
Kamati kuu ilichelewa sana kumvua zzk uongozi ndo madhara haya tunayoona. Mwadela iiza?.. ifweero!
 
Last edited by a moderator:
Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa chadema wametoa tamko kali la kulaani hali mbaya kisiasa na mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya chama hicho huku kamti kuu ikiwavua uongozi naibu katibu mkuu zitto kabwe na mjumbe wa kamati kuu kitila mkumbo. Wamesema kuwa chadema taifa imejipambanua kama kikundi cha wachache wasiotaka kukosolewa wala kuona watu wanaotofautiana nao kimawazo. Wameweka msimamo kuwa wao wanamuunga mkono zitto kabwe na wanakitaka chama hicho kitumie busara kumaliza mgogoro huo kabla haujakiathiri chama.. Chanzo cluods radio habari.
umeona urudie tena uongo !? F.Y
 
Wanaacha kulaani kupanda kwa Umeme kwa asilimia 68 wanakuja na ujinga wa kulaani kwa kufukuzwa msaliti wa maendeleo? Hao ni njaa inawasumbua
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa chadema wametoa tamko kali la kulaani hali mbaya kisiasa na mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya chama hicho huku kamti kuu ikiwavua uongozi naibu katibu mkuu zitto kabwe na mjumbe wa kamati kuu kitila mkumbo. Wamesema kuwa chadema taifa imejipambanua kama kikundi cha wachache wasiotaka kukosolewa wala kuona watu wanaotofautiana nao kimawazo. Wameweka msimamo kuwa wao wanamuunga mkono zitto kabwe na wanakitaka chama hicho kitumie busara kumaliza mgogoro huo kabla haujakiathiri chama.. Chanzo cluods radio habari.

Wanafunzi wa chuo Chako labda
 
Wanaacha kulaani
kupanda kwa Umeme kwa asilimia 68 wanakuja na ujinga wa kulaani kwa
kufukuzwa msaliti wa maendeleo? Hao ni njaa inawasumbua

wewe kwa kuwa unalishwa na akina mbowe hapo Kinondoni kama broiller ndo uwanange wenzako? soon na wewe utakiona cha mtema kuni pindi nguvu ya umma itakaposhika hatamu
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa chadema wametoa tamko kali la kulaani hali mbaya kisiasa na mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya chama hicho huku kamti kuu ikiwavua uongozi naibu katibu mkuu zitto kabwe na mjumbe wa kamati kuu kitila mkumbo. Wamesema kuwa chadema taifa imejipambanua kama kikundi cha wachache wasiotaka kukosolewa wala kuona watu wanaotofautiana nao kimawazo. Wameweka msimamo kuwa wao wanamuunga mkono zitto kabwe na wanakitaka chama hicho kitumie busara kumaliza mgogoro huo kabla haujakiathiri chama.. Chanzo cluods radio habari.

Chadema vyuo vikuu ipo chini ya CHASO

Hao ni mamaluki wale waliomtangaza January kama Mgombea urais Mtarajiwa

Chadema vyuo vikuu chini ya CHASO watatoa tamko halali

Haya mazingaombwe yanafanyika kishamba sana.Watavuliwa nguo
 
Chadema vyuo vikuu ipo chini ya CHASO

Hao ni mamaluki wale waliomtangaza January kama Mgombea urais Mtarajiwa

Chadema vyuo vikuu chini ya CHASO watatoa tamko halali

Haya mazingaombwe yanafanyika kishamba sana.Watavuliwa nguo

"MIDA EIGHT anatumiwa na Dr. Slaa kugombanisha viongozi" - waraka
 
Back
Top Bottom