Ninalalizimka kuandika uzi huu kulingana na mwendelezo wa tafakuri zitokanazo na hotuba pendwa ya mheshimiwa huyu hasa ya hivi karibuni tokea pande za kule Chatto.
Katika hotuba yake Chatto mheshimiwa hakuwa na maneno mazuri sana kwa yeyote mwenye mtizamo wa kuwatenga watu katika kupambana na Corona.
Kwa nini Magufuli anadhani yeyote anayependekeza kuwatenga watu ili kudhibiti maambukizi ya Corona siyo Mzalendo na kuwa anatumiwa na mabeberu?
Kwa nini mheshimiwa anaona hata viongozi wa dini walioona ni busara kwa waumini wao kuepuka mikusanyiko japo kwa kutojumuika pamoja kwenye nyumba za Ibada, kuwa nao siyo wazalendo na wenye kutumiwa hata na ibilisi?
Kwa nini anadhani viongozi wa dini kama hao wamepotoka kwa kudhani kuwa wapo kwenye kuwahami waumini wao kwa njia hii? Kwa nini anadhani si yeye anayeweza kuwa ndiye aliyepotoka angalau kwenye hili?
Kwa nini mheshimiwa anadhani kila anayemsifia akiwamo mheshimiwa Mbatia na SMS zake za usiku usiku, kuwa ndiyo wazalendo peke yao na kuwa hao tu ndiyo pekee walioyaweka maslahi ya taifa hili mbele?
Kwenye hotuba yake rais alisisitiza sana pia kuwa, ataendelea kulipa mishahara ya wafanyakazi.
Kwa nini Magufuli anadhani watanzania wanahitaji mishahara tu bila ya kujali uhakika wa usalama wa maisha yao kwanza?
Zaidi pia alijitahidi sana kuonyesha tumeshashinda vita vya Corona bila ya kutoa takwimu zozote kuhusiana na ugonjwa huu hapa nchini tokea Apr 29.
Hii vita tumeishinda vipi bila ya kuwa na takwimu zozote?
Alisema pia kuwa, baba yake alifariki kwa kansa bila kusema alifariki lini. Covid-19 imekuja March 2020 nchini. Haina hakika alikuwa na maana gani.
Kuwa nani alikuwa na kansa hakumaanishi kuwa, hatimaye mwisho kafariki kwa kansa. Unaweza kuwa na kansa ukaja kufa kwa ajali ya gari, malaria, TB, ukimwi, au hata Covid-19, nk.
Kwa nini mheshimiwa anakereka anapoona vifo kuhusishwa na Corona?
Ikumbukwe kuwa nchi kama UK zimekuja kugundua baadaye kuwa vifo vingi vilivyotokea kwenye mlipuko wa Corona kwa makosa hawakuwa wamefahamu kuwa vilisababishwa na Corona na si kwa magonjwa mengine kama ilivyokuwa imedhaniwa. Ndiyo maana UK wame review takwimu zao na sasa wana vifo vingi vya covid-19 kuliko hata Italy.
Ni wazi kuna mkanganyiko baina ya uzalendo na ucha Mungu.
Vipi mtu mmoja anaweza jipima mwenyewe na kuona yeye ni mzalendo kuliko fulani au kuwa yeye ni mcha Mungu kuliko fulani inafikirisha.