Tuelimishane: Uzalendo na Ucha Mungu wa Rais Magufuli ni upi?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,652
2,000
Ninalalizimka kuandika uzi huu kulingana na mwendelezo wa tafakuri zitokanazo na hotuba pendwa ya mheshimiwa huyu hasa ya hivi karibuni tokea pande za kule Chatto.

Katika hotuba yake Chatto mheshimiwa hakuwa na maneno mazuri sana kwa yeyote mwenye mtizamo wa kuwatenga watu katika kupambana na Corona.

Kwa nini Magufuli anadhani yeyote anayependekeza kuwatenga watu ili kudhibiti maambukizi ya Corona siyo Mzalendo na kuwa anatumiwa na mabeberu?

Kwa nini mheshimiwa anaona hata viongozi wa dini walioona ni busara kwa waumini wao kuepuka mikusanyiko japo kwa kutojumuika pamoja kwenye nyumba za Ibada, kuwa nao siyo wazalendo na wenye kutumiwa hata na ibilisi?

Kwa nini anadhani viongozi wa dini kama hao wamepotoka kwa kudhani kuwa wapo kwenye kuwahami waumini wao kwa njia hii? Kwa nini anadhani si yeye anayeweza kuwa ndiye aliyepotoka angalau kwenye hili?

Kwa nini mheshimiwa anadhani kila anayemsifia akiwamo mheshimiwa Mbatia na SMS zake za usiku usiku, kuwa ndiyo wazalendo peke yao na kuwa hao tu ndiyo pekee walioyaweka maslahi ya taifa hili mbele?

Kwenye hotuba yake rais alisisitiza sana pia kuwa, ataendelea kulipa mishahara ya wafanyakazi.

Kwa nini Magufuli anadhani watanzania wanahitaji mishahara tu bila ya kujali uhakika wa usalama wa maisha yao kwanza?

Zaidi pia alijitahidi sana kuonyesha tumeshashinda vita vya Corona bila ya kutoa takwimu zozote kuhusiana na ugonjwa huu hapa nchini tokea Apr 29.

Hii vita tumeishinda vipi bila ya kuwa na takwimu zozote?

Alisema pia kuwa, baba yake alifariki kwa kansa bila kusema alifariki lini. Covid-19 imekuja March 2020 nchini. Haina hakika alikuwa na maana gani.

Kuwa nani alikuwa na kansa hakumaanishi kuwa, hatimaye mwisho kafariki kwa kansa. Unaweza kuwa na kansa ukaja kufa kwa ajali ya gari, malaria, TB, ukimwi, au hata Covid-19, nk.

Kwa nini mheshimiwa anakereka anapoona vifo kuhusishwa na Corona?

Ikumbukwe kuwa nchi kama UK zimekuja kugundua baadaye kuwa vifo vingi vilivyotokea kwenye mlipuko wa Corona kwa makosa hawakuwa wamefahamu kuwa vilisababishwa na Corona na si kwa magonjwa mengine kama ilivyokuwa imedhaniwa. Ndiyo maana UK wame review takwimu zao na sasa wana vifo vingi vya covid-19 kuliko hata Italy.

Ni wazi kuna mkanganyiko baina ya uzalendo na ucha Mungu.

Vipi mtu mmoja anaweza jipima mwenyewe na kuona yeye ni mzalendo kuliko fulani au kuwa yeye ni mcha Mungu kuliko fulani inafikirisha.
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
27,839
2,000
Ila kwa suala la Mbatia kumtxt msg sijui asikate tamaa inadhihirisha njaa aliyonayo! Mwanaume mzima unamtext mwanaume mwenzako kumpamba ujinga kweli??
Wanaume wa sasa hivi ni wanafki kuliko wanawake...hakuna mwanamke mbunge wa upinzani mwenye muda mbovu kama wa Mbatia...ndo maana anazeeka daily!
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,641
2,000
Magufuli aliambiwa na Kakobe Atubu akagoma,

Haiwezekani serikali ya kishetani ikaongoza maombi ya Mungu kwa watu walio safi ikafanikiwa watanzania ni wasafi ila tunaongozwa na watu wanaonuka damu hata siku moja hatutafanikiwa mpaka tutubu kama Mkapa.

Nchi inanuka damu, watu wenye manung'uniko, kupotea kwa haki, kufungwa, kupotea halafu kiongozi mkuu aongoze maombi ya taifa la mamna hii?

Hatutakuja kufanikisha chochote kwenye corona hata kwa mengine bila kuchagua tupite njia gani either ya kishetani au ya Mungu lakini tukiendelea kuwa wanafiki never hatutatoboa. Mungu hataki unafiki.
 
ludist

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
383
500
Mbatia angekuwa wa kike angeshaliwa tyari, yaan mzee angeteleza tu
Ila kwa suala la Mbatia kumtxt msg sijui asikate tamaa inadhihirisha njaa aliyonayo! Mwanaume mzima unamtext mwanaume mwenzako kumpamba ujinga kweli??
Wanaume wa sasa hivi ni wanafki kuliko wanawake...hakuna mwanamke mbunge wa upinzani mwenye muda mbovu kama wa Mbatia...ndo maana anazeeka daily!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,652
2,000
Magufuli aliambiwa na Kakobe Atubu akagoma,

Haiwezekani serikali ya kishetani ikaongoza maombi ya Mungu kwa watu walio safi ikafanikiwa watanzania ni wasafi ila tunaongozwa na watu wanaonuka damu hata siku moja hatutafanikiwa mpaka tutubu kama Mkapa.

Nchi inanuka damu, watu wenye manung'uniko, kupotea kwa haki, kufungwa, kupotea halafu kiongozi mkuu aongoze maombi ya taifa la mamna hii?

Hatutakuja kufanikisha chochote kwenye corona hata kwa mengine bila kuchagua tupite njia gani either ya kishetani au ya Mungu lakini tukiendelea kuwa wanafiki never hatutatoboa. Mungu hataki unafiki.
Mkuu kwa maoni yangu umeandika kwa uchungu mkubwa.

Mawazo kamili ya uzalendo uliotukuka.

Tuko pamoja mkuu.
 
Mr Devil

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
2,672
2,000
Nilipita karbu na kanisa flani nka sikia wanataka kumtangaza kama mtukufu
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
12,806
2,000
Nilishangaa sana anapowatuhumu vibaya viongozi wa dini kwa kuzuia mikusanyiko makanisani!Haoni kuwa viongozi hao wamefanya jambo la maana?Sijamwelewa kabisa JPM ana nia gani na watanzania!
 
Tunasimama nao viongozi wa dini wale. Wala wasivunjuke moyo.

Watu waadilifu kabisa wasioangalia maslahi yao binafsi, bali wenye kuangalia usalama wa kondoo wao katika mazingira magumu na ya hatari yaliyojaa mbweha na mbwa mwitu!

Kwa hakika wanafuzu kuwemo katika ile orodha ya makandideti wa Nobel prize.

Hawa ikiwa mahsusi kabisa kwa jitihada zao binafsi za kuokoa naisha ya maelfu kutokuangamia kwa Corona.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,652
2,000
Swali la msingi:

Kama serikali ilifunga shule kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu,iweje Rais JPM awashambulie viongozi wa dini kufunga makanisa kuepusha misongamano?
Ni mambo ya kufikirisha. Ingependeza makanisa na misikiti zaidi ingefungwa ili kuendelea kunusuru watu.

Ikumbukwe wanaonusuriwa kwenye jitihada kama hizi ni waliomo na wasiokuwamo. Kama ulivyo mtego wa panya wanaambukizwa waumini na wasio waumini kwa kutotumia busara tu.
 
Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,443
2,000
Ila kwa suala la Mbatia kumtxt msg sijui asikate tamaa inadhihirisha njaa aliyonayo! Mwanaume mzima unamtext mwanaume mwenzako kumpamba ujinga kweli??
Wanaume wa sasa hivi ni wanafki kuliko wanawake...hakuna mwanamke mbunge wa upinzani mwenye muda mbovu kama wa Mbatia...ndo maana anazeeka daily!
Mbatia anatafuta nafasi ya kurudi 2020 na anajua pigo yakurudi nikumsifu kiongozi wa malaika.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,652
2,000
Bado mnamtegemea Magufuli?
Mkuu ninakusoma. Yote hii ni katika kudhani kuwa anaweza kubadilika. Walikuwapo wagumu kama kina Farao lakini kiliponuka sawa sawa walikubali kuwaachia mayahudi waondoke.

Tunadhani hawa waliosifiwa, hawa kina Mbatia, yule askofu na bwana mufti wanaweza kuwa wa msaada kumshauri huyu bwana abadilike au japo akutane na hawa wenye mawazo mengine.

Sote tunajenga nyumba moja.

Uzalendo au ucha Mungu siyo monopoly na hayupo mwenye hati miliki navyo.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,652
2,000
Nilipita karbu na kanisa flani nka sikia wanataka kumtangaza kama mtukufu
Kazi kweli kweli ...

Huyu bwana alisema Daniel alinusurika kwenye tumbo la samaki.

Hao watakuwa wachumia tumbo. Labda na Mbatia anasali hapo.
 
Alkene

Member
Aug 10, 2017
21
45
Ninalalizimka kuandika uzi huu kulingana na mwendelezo wa tafakuri zitokanazo na hotuba pendwa ya mheshimiwa huyu hasa ya hivi karibuni tokea pande za kule Chatto.

Katika hotuba yake Chatto mheshimiwa hakuwa na maneno mazuri sana kwa yeyote mwenye mtizamo wa kuwatenga watu katika kupambana na Corona.

Kwa nini Magufuli anadhani yeyote anayependekeza kuwatenga watu ili kudhibiti maambukizi ya Corona siyo Mzalendo na kuwa anatumiwa na mabeberu?

Kwa nini mheshimiwa anaona hata viongozi wa dini walioona ni busara kwa waumini wao kuepuka mikusanyiko japo kwa kutojumuika pamoja kwenye nyumba za Ibada, kuwa nao siyo wazalendo na wenye kutumiwa hata na ibilisi?

Kwa nini anadhani viongozi wa dini kama hao wamepotoka kwa kudhani kuwa wapo kwenye kuwahami waumini wao kwa njia hii? Kwa nini anadhani si yeye anayeweza kuwa ndiye aliyepotoka angalau kwenye hili?

Kwa nini mheshimiwa anadhani kila anayemsifia akiwamo mheshimiwa Mbatia na SMS zake za usiku usiku, kuwa ndiyo wazalendo peke yao na kuwa hao tu ndiyo pekee walioyaweka maslahi ya taifa hili mbele?

Kwenye hotuba yake rais alisisitiza sana pia kuwa, ataendelea kulipa mishahara ya wafanyakazi.

Kwa nini Magufuli anadhani watanzania wanahitaji mishahara tu bila ya kujali uhakika wa usalama wa maisha yao kwanza?

Zaidi pia alijitahidi sana kuonyesha tumeshashinda vita vya Corona bila ya kutoa takwimu zozote kuhusiana na ugonjwa huu hapa nchini tokea Apr 29.

Hii vita tumeishinda vipi bila ya kuwa na takwimu zozote?

Alisema pia kuwa, baba yake alifariki kwa kansa bila kusema alifariki lini. Covid-19 imekuja March 2019 nchini. Haina hakika alikuwa na maana gani.

Kuwa nani alikuwa na kansa hakumaanishi kuwa, hatimaye mwisho kafariki kwa kansa. Unaweza kuwa na kansa ukaja kufa kwa ajali ya gari, malaria, TB, ukimwi, au hata Covid-19, nk.

Kwa nini mheshimiwa anakereka anapoona vifo kuhusishwa na Corona?

Ikumbukwe kuwa nchi kama UK zimekuja kugumdua baadaye kuwa vifo vingi vilivyotokea kwenye mlipuko wa Corona kwa makosa hawakuwa wamefahamu kuwa vilisababishwa na Corona na si kwa magonjwa mengine kama ilivyokuwa imedhaniwa. Ndiyo maana UK wame review takwimu zao na sasa wana vifo vingi vya covid-19 kuliko hata Italy.

Ni wazi kuna mkanganyiko baina ya uzalendo na ucha Mungu.

Vipi mtu mmoja anaweza jipima mwenyewe na kuona yeye ni mzalendo kuliko fulani au kuwa yeye ni mcha Mungu kuliko fulani inafikirisha.
achana na hiyo hotuba, fanya kazi huku ukijilinda na kuwalinda wengine dhidi ya corona
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom