RASILIMALI NA UZALENDO

o_2

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
348
287
Tanzania ni moja kati ya nchi chache zilizobarikiwa kuwa na rasilimali za kila aina. Mabwawa, maziwa, bahari na mito. Madini, misitu na milima.

Wote tunafahamu kwenye maji tunapata nini, aina zote za samaki, dagaa mashuhuri zinapatikana kuanzia migebuka, Sato n.k.

Ukija kwenye madini, Tanzanite, dhahabu, Almas, chuma, gesi...taja. Ya kila aina yanapatikana. Misitu... inatupa vivutio vingi vingi mno. Kila mkoa sasa hivi kuna mahali kuna kivutio cha utalii. Mbuga za wanyama. Nenda iringa, Mbeya, Njombe, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Geita, Kigoma....Dar es Salaam inatupa bandari.

Hizi rasilimali zote tajwa hapo juu zinashindwa kutumiwa ipasavyo au zinatumika ipasavyo..lakini matokeo yake ni ya kushangaza.

Uzalendo ni ile hali ya mtu kuipenda nchi yake......kuilinda na kuitetea. Hapo ndio tulipokwamia. Sasa hivi kila unayemuuliza tulijikwaa wapi? Lawama zote kwa CCM. CCM inatumika kama dhana. Kama kivuli cha watu kukwepa majukumu yao ya kizalendo katika kuilinda na kutetea rasilimali za nchi hii.

Asilimia kubwa ya WaTz sisi tumekuwa walafi wa kila kitu. Sasa hivi kila mwenye upenyo wa kuiba anaiba. Kubebana kwenye madaraka, ngazi za taasisi na uongozi. Rushwa kila mahali. Na kila mtu anajua rushwa ni adui wa haki. Rushwa ya ngono ndio kabisaaa karibia kila taasisi ukiichunguza mambo ni hayo.

Waliopo kwenye nyazifa, wanaweka ndugu zao bila kujali utendaji wa kazi. Vijana wanamaliza vyuo wanategemea ajira kutoka kwa serikali. Zikikosekana basi ni sonona. Zipo nyanja mbalimbali ambazo kijana yeyote anaweza kuziangalia kujiajiri pasipo kutegemea ajira kutoka serikalini. Wapo ambao wamejiajiri kwenye kilimo, biashara na ufundi. Ni maisha.


Utunzaji wa rasilimali unaendana na kuwa mzalendo. Bila ya kuwa na UZALENDO ndani yetu, hii nchi hakuna kitakacho badilika. Tuipende nchi yetu kwanza na tuifanyie mema kwanza na yenyewe itatulipa. Kila mtu atimize wajibu wake.

Kabla haujawaza hii nchi imekufanyia nini, jiulize kwanza wewe umeifanyia nini nchi yako? Timiza wajibu.
 
Back
Top Bottom