Tuelimishane: Sakata la Mafuta ya kula (TRA vs. TBS) - Hiki ndicho kinachobishaniwa

tatizo TRA wamemaliza kumkamua ng'ombe kila njia sasa waanza mchuna ngozi na hapo ndo tatizo linapoanzia kodi haitakiwi kumuumiza mlaji na hapo wasidhani kwa kuweka kodi kubwa kwe mafuta ghafi basi wanaoumia ni kina mohamed dewji hapana..hii kodi huwa inashuka kama kawaida kwa mlaji wa mwisho ambaye ni mwananchi wa kipato cha chini
hili ndilo jibu hakuna zaidi ya hilo, ni kweli kwamba kwenye kukadiria kodi rules of origin in apply ambapo inatakiwa 70-75% iwe imetengenezwa kwenye nchi husika hapo ndio bidhaa itahesabika kuwa inatoka nchi hiyo sasa sidhani kwenye haya mafuta yako processed kwa kiwango hicho huko yatokako.
 
Watanzania!!!!! Ni kweli mtoa mada unachosema kwamba kinachobishaniwa ni mafuta hayo ni ghafi au safi yaani crude or refined? Lkn ukweli kwenye jambo hili mafuta haya yakiwa refined yanatakiwa yatolewe kodi ya serikali 25% kwa sheria iliyopitishwa na bunge finance bill 2016/2017 na kama ni crude lazima kodi iwe 10% kwa mujibu wa viwango vya kodi zilizopitishwa na bunge. Je, sasa ukweli ni upi kwenye sakata hili? Sio kweli kwamba mafuta yanayoletwa ni crude kwa sababu ili mafuta yawe crude trans fat free (tff) lazima iwe 5% kundelea juu hapo kodi ya serikali inatakiwa iwe 10% lakini mafuta yanayoletwa na wafanyabiasha ile trans fat free ni 2% na kwa mujibu wa viwango mafuta hayo bado ni refined kwa maana yameindizwa crude kidogo tu ili kukimbia 25% ya kodi na walipe 10%

Naanza kuelewa huenda baada ya hii sheria ya mwaka 2017 shida imeanzia hapo labda udhaifu wa sheria watu waagizaji wanataka kupigia hapo.
swali je wakati sheria hii inatugwa hivi vyombo hawakujua hiyo crude ao refine itaegemea kweye vipimo vipi?

Kunashida somewhere.
 
mtoa mada hebu nieleweshe, miaka ya nyuma walikua wanakubaliana vipi? au hayo mafuta yameanza kuagizwa hivi karibuni tu?
Toka enzi mafuta haya yamekuwa yanaagizwa tu. Yalikuwa yanaingizwa kama "crude". Sasa swali linakkuja 'kwa nini sasa?'.

Hata mimi ninashangaa kama wengine ila naelewa shida ilipo.

Kiuhalisia sio TBS wala TRA anayetakiwa kuamua hili. Kwa sababu TBS ni watu wa viwango. TRA ni watu wa kodi. Wapo wataalam ambao wanaweza kupima na kuchambua kwa viwango kwamba kwa kiwango gani uzalishaji umefanyika ktk nchi A na B. Hivyo kuipa "uasili" hiyo bidhaa ktk nchi mojawapo. Na ni zoezi la kitaalam na "Certificate of Origin" inatolewa. Hapo TRA wanafuata tu walichoamua wataalam. Sasa ubishi huu ni kwa sababu hatuna hii mifumo. Leo akija huyu anasema hivi, kesho akija yule anakataa. Basi wanyonge wanabaki kuumia.
 
Ni swali la sheria ya kodi ni code ndio zinazoamua hii ni crude hii ni refined ni jambo la kitaalaum kidogo
 
tatizo TRA wamemaliza kumkamua ng'ombe kila njia sasa waanza mchuna ngozi na hapo ndo tatizo linapoanzia kodi haitakiwi kumuumiza mlaji na hapo wasidhani kwa kuweka kodi kubwa kwe mafuta ghafi basi wanaoumia ni kina mohamed dewji hapana..hii kodi huwa inashuka kama kawaida kwa mlaji wa mwisho ambaye ni mwananchi wa kipato cha chini
Ni kweli msingi wa ubishi huu ni bei kuja kupanda tu hamna namna. Naelewa hivo. Serikali iongeze maarifa ili iwasaidie wanyonge. WANAUMIA SANA. SUKARI sasa ni MAFUTA. Hatari sana
 
Watanzania!!!!! Ni kweli mtoa mada unachosema kwamba kinachobishaniwa ni mafuta hayo ni ghafi au safi yaani crude or refined? Lkn ukweli kwenye jambo hili mafuta haya yakiwa refined yanatakiwa yatolewe kodi ya serikali 25% kwa sheria iliyopitishwa na bunge finance bill 2016/2017 na kama ni crude lazima kodi iwe 10% kwa mujibu wa viwango vya kodi zilizopitishwa na bunge. Je, sasa ukweli ni upi kwenye sakata hili? Sio kweli kwamba mafuta yanayoletwa ni crude kwa sababu ili mafuta yawe crude trans fat free (tff) lazima iwe 5% kundelea juu hapo kodi ya serikali inatakiwa iwe 10% lakini mafuta yanayoletwa na wafanyabiasha ile trans fat free ni 2% na kwa mujibu wa viwango mafuta hayo bado ni refined kwa maana yameindizwa crude kidogo tu ili kukimbia 25% ya kodi na walipe 10%

Wakati unafocus kwenye percentage za FAT FREE, huku mtaani walalahoi wanazidi kuumia ndoo ya lita 10 imetoka elfu thelathini mpaka arobaini ya lita ishirini imejump kutoka elfu 55 mpaka sabini na tano hapa tunapotezeana muda bure tuseme tu ukweli mapato TRA yamepungua sana watu wengi waliokuwa wanadaiwa na TRA wamefunga biashara au wamelipa madeni yao TRA inahaha hakuna mahali pakukamua maziwa.....ng’ombe amechoka karibia anaaga dunia.
 
Toka enzi mafuta haya yamekuwa yanaagizwa tu. Yalikuwa yanaingizwa kama "crude". Sasa swali linakkuja 'kwa nini sasa?'.

Hata mimi ninashangaa kama wengine ila naelewa shida ilipo.

Kiuhalisia sio TBS wala TRA anayetakiwa kuamua hili. Kwa sababu TBS ni watu wa viwango. TRA ni watu wa kodi. Wapo wataalam ambao wanaweza kupima na kuchambua kwa viwango kwamba kwa kiwango gani uzalishaji umefanyika ktk nchi A na B. Hivyo kuipa "uasili" hiyo bidhaa ktk nchi mojawapo. Na ni zoezi la kitaalam na "Certificate of Origin" inatolewa. Hapo TRA wanafuata tu walichoamua wataalam. Sasa ubishi huu ni kwa sababu hatuna hii mifumo. Leo akija huyu anasema hivi, kesho akija yule anakataa. Basi wanyonge wanabaki kuumia.
unachemka, kiwango ndiyo kila kitu, TBS kuhusika haikuwa bahati mbaya. Kiwango ni lazima kiweke bayana ni bidhaa ya daraja gani
 
Sakata Hili Litaondoka Na Watu Suala Ni Muda Tu
Mbona Miaka Yote Haikuwepo Hii Kadhia?

Kurukaruka Kwa Maharage Ndiyo Kuiva Kwake
 
Miaka mingine walikuwa wanafanyaje? Mbona hatujawahi kusikia ubishani wa namna hii kabla ya sasa
Toka enzi mafuta haya yamekuwa yanaagizwa tu. Yalikuwa yanaingizwa kama "crude". Sasa swali linakkuja 'kwa nini sasa?'.

Hata mimi ninashangaa kama wengine ila naelewa shida ilipo.

Kiuhalisia sio TBS wala TRA anayetakiwa kuamua hili. Kwa sababu TBS ni watu wa viwango. TRA ni watu wa kodi. Wapo wataalam ambao wanaweza kupima na kuchambua kwa viwango kwamba kwa kiwango gani uzalishaji umefanyika ktk nchi A na B. Hivyo kuipa "uasili" hiyo bidhaa ktk nchi mojawapo. Na ni zoezi la kitaalam na "Certificate of Origin" inatolewa. Hapo TRA wanafuata tu walichoamua wataalam. Sasa ubishi huu ni kwa sababu hatuna hii mifumo. Leo akija huyu anasema hivi, kesho akija yule anakataa. Basi wanyonge wanabaki kuumia.
 
unachemka, kiwango ndiyo kila kitu, TBS kuhusika haikuwa bahati mbaya. Kiwango ni lazima kiweke bayana ni bidhaa ya daraja gani
Hujanielewa, na hili ni somo gumu. Na sishangai hata nisipoeleweka kwani najua ugumu wake. Ni elimu ambayo haijazoeleka.
NB: Viwango ni kwa ajili ya kulinda afya. Ktk uamuzi wa kodi ni tofauti kidogo. Hata hayo maneno ya 'crude' au 'refined' yana maana tofauti linapokuja swala la kodi. Haiwezi kuwa hii ya kwetu mtaani au ya TBS au 'general meaning'.

Nimesoma haya mambo ktk viwango vya juu sana naelewa. Na bado naendelea kuyasoma. Ni miongoni mwa masomo magumu sana.
 
CWR2016 Nafikiri mtoa hoja umejikita sana katika sheria za kanuni za uasili wa bidhaa.haya mafuta hayana uhusiano wowote na hiyo inshu ya uasili wa bidhaa kwa sababu sheria uliyofanya reference (eac custom management act)inatambua kuwa uagizaji wa mafuta ghafi/semi refined lazima yatozwe kodi pindi yanapoingia nchini.

Kodi ya 'ghafi/crude' ni asilimia 10 kwa 18.
Kodi ya 'safi/refined' ni asilimia 25 kwa 18

Kwa hiyo kodi ya refined ni kubwa. Ndo maana wanabishana.

Sasa EAC Customs Management Act lazima isomwe pamoja na EAC Rules of Origin, 2015 R.E 2017.
 
Kwani kabla ya mgogoro huu wa sasa baina ya TBS na TRA je mafuta yalikua yakitozwa Kodi kwa utaratibu gani na hatua zipi TBS na TRA walifuata mpaka wakakubaliana huko mwanzoni na sasa wanashidwa kuelewana
Hatua walizokuwa wanafuata ni kukaa kwenye kameza kadogo ambako kamepakwa rangiya R-U-S-H-W-A na kumaliza mambo!
 
Wakati unafocus kwenye percentage za FAT FREE, huku mtaani walalahoi wanazidi kuumia ndoo ya lita 10 imetoka elfu thelathini mpaka arobaini ya lita ishirini imejump kutoka elfu 55 mpaka sabini na tano hapa tunapotezeana muda bure tuseme tu ukweli mapato TRA yamepungua sana watu wengi waliokuwa wanadaiwa na TRA wamefunga biashara au wamelipa madeni yao TRA inahaha hakuna mahali pakukamua maziwa.....ng’ombe amechoka karibia anaaga dunia.
Ng'omba anakamuliwa nyama. Hahaaa
 
Hatua walizokuwa wanafuata ni kukaa kwenye kameza kadogo ambako kamepakwa rangiya R-U-S-H-W-A na kumaliza mambo!
Yapo mengi nyuma ya pazia. ila ukweli tunaumia kwa sababu Tz hakuna ukweli kwenye mambo ya kodi. Yani serikali na TRA watalaumiwa milele ktk hili.

Ni Tz pekee ambapo bidhaa moja yenye sifa zile zile utailipia kodi tofauti wewe na mwingine...

Hamna uwazi kabisa.
 
Malizeni na mtatue mgogoro mapema maana mafuta ya kupikia yanaweza pia kukosekana kila mahali mpaka kwa mjomba Kantalamba
 
Back
Top Bottom