Wafanyabiashara Watakiwa Kuhakikisha Bidhaa Zinakaguliwa na TBS Kabla ya Matumizi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kuhakikisha bidhaa hizo zinakaguliwa ili kulinda afya za Watanzania, na wenye Viwanda vya ndani kuhakikisha bidhaa zinakaguliwa na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kabla ya matumizi.

Ametoa wito huo Septemba 18/09/2023 alipotembelea TBS kuona jinsi maabara za TBS 4 kati ya 9, ikiwemo maabara ya chakula, ngozi, nguo na kemia zinazovofanya kazi na kusikiliza changamoto zilizopo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Taasisi zote zilizopo chini ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023-2024 .

Aidha, Dkt. Kijaji ameridhishwa na utendaji kazi wa TBS na kuitaka ifanye kazi kwa kushirikiana na Taasisi zingine ili kurahisisha utendaji kazi kwa kuhakikisha Watanzania wanatumia bidhaa bora na salama kwa afya zao.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Lazaro Msasalaga amesema TBS ina maabara tisa zenye vifaa vya kisasa, wataalamu wa kutosha na zina ithibati kimataifa inazozitumia kupima ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoingia kutoka nje ya nchi.

Akitaja maabara hizo, Bw. Msasalaga amesema Maabara hizo ni Maabara ya Kemia, Maabara ya Uhandisi Ujenzi, Maabara ya Uhandisi Mitambo, Maabara ya Uhandisi Umeme, Maabara ya Kemia ya Chakula, Maabara ya Mikrobiolojia, Maabara ya Pamba, Nguo na Ngozi, Maabara ya Ugezi na Kituo cha Teknolojia ya Ufungashaji.

WhatsApp Image 2023-09-19 at 00.36.31.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 00.36.32.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 00.36.33.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 00.36.33(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 00.36.35.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-19 at 00.36.34(1).jpeg
 
Back
Top Bottom