Tudai uchaguzi wa haki badala ya kudai kuibiwa baada ya chaguzi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,899
Zimbabwe tayari wapinzani wanadai kuibiwa uchaguzi.

Gabon uchaguzi wao ni leo:

"Huko kwenye mtandao wa internet, TCRA ya huko tayari imeshafanya yake."

Zaidi mno Serikali ya huko imepiga marufuku uwepo wa waangalizi na wanabari wa kimataifa.

1. Twendeni mahakamani,
2. Kampeni zetu ziwe na mwelekeo thabiti - uchaguzi wa haki,
3. Tuunganishe nguvu na wengine wengi, letu kuwa moja:

Ikapate kueleweka waziwazi sasa, kuwa:

"Hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi mkuu (2024 wala 2025)."

Chaguzi za wizi za nini?
_________
Internet cut in Gabon on election day - NetBlocks
 
Haya madai ya Katiba Mpya naona ni Chadema ndio wako serious kuipigania kwa sasa, vyama vingine hata sivisikii kabisa, hawa ni either wanajua hawana cha kupoteza muda ukifika, au tayari wameshajiweka rehani waje kutumiwa na mtawala wa CCM kwa manufaa yake, endapo Katiba Mpya haitapatikana.

Lakini pia, hata nikiwasikiliza viongozi mmoja mmoja wa Chadema, hususan waliokuwa wabunge, wanaonekana nao wameshaanza kuutolea macho uchaguzi mkuu 2025 kwa kauli zao za kuwa tayari kugombea ili kuwaondoa CCM majimboni mwao, sasa hawa wanaonekana wana dhamira tofauti na msimamo wa chama chao, hapo kazi ipo.
 
Wanaoukodolea macho ubunge ni mzigo:

Haisaidii kuacha kuwaambia watu hawa hivyo wazi wazi.
 
Zimbabwe tayari wapinzani wanadai kuibiwa uchaguzi.

Gabon uchaguzi wao ni leo:

"Huko kwenye mtandao wa internet, TCRA ya huko tayari imeshafanya yake."

Zaidi mno Serikali ya huko imepiga marufuku uwepo wa waangalizi na wanabari wa kimataifa.

1. Twendeni mahakamani,
2. Kampeni zetu ziwe na mwelekeo thabiti - uchaguzi wa haki,
3. Tuunganishe nguvu na wengine letu wengi kuwa moja:

Ikapate kueleweka waziwazi sasa, kuwa:

"Hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi mkuu (2024 wala 2025)."

Chaguzi za wizi za nini?
_________
Internet cut in Gabon on election day - NetBlocks
Naunga mkono HOJA 🙏 🙏

Bila Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi,

Hapatokuwa na uchaguzi wowote.
 
Kupanga kusimamisha chaguzi zisizokuwa za haki hakuwezi kuitwa uhaini au kuwa ni jinai.
 
Tunakwenda kupendekeza chaguzi wa MITAA 2024 usogezwe mbele Ili tupate tume HURU na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Tutashinda, maana Mungu Yu upande wa HAKI!!

Amen
 
Tusiishie kupendekeza. Kama la bandari hili nalo si la kuliangalia tu, bali kulipigania kwa nguvu zetu zote.
 
Enyi akina Erythrocyte, kulikoni ndugu zetu kuutamani ubunge hivyo hata kama uchaguzi wote utaibiwa?

Kulikoni kuachana na dhana yetu asilia, kwamba hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi?

Nini kimewapata enyi ndugu zetu? Kwa maana hata kwenye magoma siku hIzi kama Vicky tu, hamtaki kufika?

Au nia yenu ni kusubiria ki Chamisa Chamisa kudai mmeibiwa kulikozoeleka, kusikokuwa na tija?
 
Zimbabwe tayari wapinzani wanadai kuibiwa uchaguzi.

Gabon uchaguzi wao ni leo:

"Huko kwenye mtandao wa internet, TCRA ya huko tayari imeshafanya yake."

Zaidi mno Serikali ya huko imepiga marufuku uwepo wa waangalizi na wanabari wa kimataifa.

1. Twendeni mahakamani,
2. Kampeni zetu ziwe na mwelekeo thabiti - uchaguzi wa haki,
3. Tuunganishe nguvu na wengine letu wengi kuwa moja:

Ikapate kueleweka waziwazi sasa, kuwa:

"Hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi mkuu (2024 wala 2025)."

Chaguzi za wizi za nini?
_________
Internet cut in Gabon on election day - NetBlocks
Hawatakubali hili litokee akiwemo huyu

1693222149295.png
 
naunga mkono hoja, prevention is better than cure!.
P
 
Mkuu 'Brazaj', naona mada hii imelala huku chini kabisa hapa jukwaani; lakini matumaini yangu ni kwamba huko ndani ya CHADEMA, ndiyo mada kuu iliyoshika chati ya juu kabisa kuliko jambo jingine lolote, hata pengine zaidi ya hizo "255" zinazoendelea sasa huko kwenye kanda, ambazo pamoja na umuhimu wake lakini siyo zaidi ya hii uliyoibandika hapa.

Kwa hiyo, mategemeo ni kwamba CHADEMA wanayaona yanayotokea huko kwingine kote na kujua kwamba ni hayo hayo yatakayofanyika hapa.
Kama watambua hivyo, litakuwa ni jambo la kusikitisha iwapo hawatakuwa tayari na kujiandaa kupambana na hali hiyo.
 
Comment #2, seat ya mbele ya bwana denooJ imejielekeza.

Huu uzi uko hapa tangu jana 17:02 angalia una comments ngapi.

Siyo kuwa jamii ya akina Erythrocyte Chadema nguli, wameufyata?

Si kuwa kina Heche Tarime, Jongwe Mbeya, Bonnie Yai Ubungo na wengine Tunduma huko, tamaa kali ya aina za kina Bulaya imewaingia hawaoni Wala hawasikii?

Hawa wenye maridhiano yao nao je?

Tuliwahi kugusia siku nyingi huko nyuma:

Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Hatutamwelewa yeyote mwenye kutaka uchaguzi kwenye mazingira yaliyopo sasa.

"Hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi."
 
"Hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi mkuu (2024 wala 2025)."
Hata hii katiba mbovu iliyopo haiwezi kuwasaidia chochote CCM, iwapo CHADEMA watakuwa wamejipanga vizuri kuwakabili hawa majambazi wa CCM.
Hakuna mahala popote ndani ya katiba hiyo panapoelezwa kwamba kupora uchaguzi na chama chochote kile ni halali.
Kwa hiyo, hii isiwe sababu ya CHADEMA kutoendelea na mipango yao (kama wanayo), ya kuhakikisha kwamba kura zitakazopigwa kwao hazivurugwi kwa njia yoyote ile ya kihalifu toka kwa CCM.

Hofu yangu tu, ni kuwa CHADEMA hawaonekani kujipanga vizuri kukabiliana na hali hiyo.

Hakuna sababu yoyote ya CHADEMA kuungana na vyama mawakala wa CCM.
 
Hata Nelson Chamisa na CCC Zimbabwe waliamini na kusema kama ulivyoandika.

Usisahau:

1. Mahakama ni zao
2. Polisi, tume na wale wengine wote ni wao.

Kwani Jecha ilikuwa je?

"Atakayekwenda kwenye uchaguzi hivi, asitwambie baadaye kaibiwa."

Tukubaliane hili sasa.
 
Back
Top Bottom