Tuambiane ukweli kwa Mpira mbovu uliochezwa na Simba SC Kipindi cha Pili dhidi ya Mbeya City ikicheza na Azam na Yanga itafungwa

Wachezaji wengi wa Simba umri ni mkubwa, sio vijana tena hivyo hawawezi kucheza kwa kasi ile ile mechi zote 34 za msimu mzima.

Zipo mechi inabidi watunze nguvu zao wakicheza mpira wa kasi ndogo. Kama Simba inataka msimu ujao ligi ya mabingwa afrika wavuke robo fainali basi kikosi cha kwanza kiwe na wachezaji kama watano au sita wenye damu changa.
Na uto watafika wapi? Tuanzie hapo kwanza!
 
Kwanza,Ni lini Lwanga aliwahi kupewa kadi nyekundu iwe kwenye VPL au international tournament?

Pili,wakati unawaza kuwa Simba inaweza kufungwa na Azam kwa uzembe kama wa jana ukumbuke kuwa na wao Azam kama wakiingia kichwa kichwa kama walivyocheza na Namungo hawatapona kwa Simba.

Tatu,Kuchoka kwa Simba kipindi cha pili ni kutokana na aina ya mpinzani aliyekutana nae,mbona hawakuchoka kipindi cha pili walipokutana na Polisi, Kaizer,Yanga, Gwambina,AS vita nk.... mpinzani unayekutana nae ndio atakufanya ucheze vipi.

Nne, kuhusu swala la Kakolanya.Kusajili kipa wa nje eti ili aje kumpa changamoto manula kwanza kimkakati hii sio sawa,kumbuka kwamba NAFASI za kusajili wachezaji wa kigeni ni KUMI tu.Hizi nafasi kumi unapaswa kuzitumia kwenye maeneo ambayo wachezaji wa ndani wameshindwa kuzipambania mfano beki wa kati, kiungo mshambuliaji (hili tatizo lipo hadi national team), mshambuliaji hatari (hapa Tz yupo Bocco tu) ukienda Yanga hata Azam wageni ndio wanaongoza kwa ku score.

Hivyo basi nafasi ya goli kipa kwa simba tayari tumeshapa mchezaji mzawa tena wa daraja la juu kabisaaa,na ikumbukwe kuwa nafasi za kipa huwa ni nafasi ambazo mara nyingi huwa hazifanyiwi rotation,sasa kusajili kipa wa kigeni halafu aje akae benchi huko ni matumizi mabaya ya fedha pia kimbuni unajifunga mwenyewe kwenye zile nafasi kumi za kusajili wachezaji wa kigeni.

Kinachotakiwa kufanywa ni kocha achague mechi ambazo atacheza kakolanya mfano za FA, halafu za kirafiki na mapinduzi acheze Ally Salim na kwenye ligi kuu na Kimataifa acheze Manula.At least hapo atakuwa amewasaidia sana.

Kitu ambacho nakuunga mkono hapo ni swala la wachezaji kujiamini sana mpaka wakapitiliza.Nadhani hapo benchi la ufundi linapaswa kulitazama kwa jicho la pili.

Pia,swala la mipira ya header bado ni Tatizo sana kwenye beki line ya simba,ni Onyango pekee mwenye uwezo wa kuruka vichwa na Kennedy kwa mbali hawa wengine kina Kapombe, zimbwe,Ame,duchu na gadiel bado ni Tatizo sana.
 
Kwanza nianze kwa Kupongeza Ushindi mzuri wa Goli 4 kwa 1 ambayo Simba SC imeshinda leo ( Usiku huu ) dhidi ya Mbeya City.

Pia nikiri kuwa Klabu ya Simba si tu kwamba inaishia kuwa na Kikosi kizuri (Timu nzuri) ila pia ina Wachezaji wenye Vipaji Asilia Binafsi kuliko wa Timu nyinginezo nchini Tanzania.

Hata hivyo pamoja na Kongole (Pongezi) zote hizi kuna baadhi ya Mapungufu ya Kimsingi niliyoyaona na kama Benchi la Ufundi pamoja na Wachezaji wenyewe wasipoyafanyia Kazi kuna uwezekano mkubwa mno Azam FC wakatufunga katika ASFC tarehe 26 June, 2021 na Yanga SC nao wakatufunga tarehe 3 June, 2021.

1. UKABAJI MBOVU
Bado Simba SC ina tatizo katika Ukabaji japo kidogo kidogo wanalifanyia Kazi, ila bado naliona hivyo lisipofanyiwa Kazi Mechi zote za Smba SC ilizobakiza dhidi ya Yanga SC, KMC FC, Coastal Union FC, Azam FC na Namungo FC.

2. WACHEZAJI WANAJIAMINI KUNAKOPITILIZA
Sema tu Mbeya City walishindwa kuja na Plan B ambayo wangekuwanayo na wangeshinda ( wangetufunga ) sana tu na Simba SC Kuumbuka.

3. MIPIRA YA JUU (VICHWA )
Bado tatizo la Wachezaji wa Simba SC hasa Mabeki kutokujua Kuruka Miipira huku 'Wakitegeana' lipo na Benchi la Ufundi wasipolifanyia Kazi mechi zetu Muhimu za Azam FC na Yanga SC 'tutafungwa' Goli nyingi na kuanza Kutafutana kwa Mkapa Temeke.

4. PUMZI KUKATA MAPEMA
Timu inaanza Kucheza vyema Kipindi cha Kwanza ila cha Pili Wacheza wanapoteana sana huku wakionyesha dhahiri kuwa hawana 'Match Fitness' na huenda pia huko kukaa Wiki Mbili Ligi Kuu ya VPL Kusimama Kumechangia Mpira mbovu walionao Simba SC sasa na ule walioucheza leo Kipindi cha Pili.

5. MTIBIENI VYEMA MUGALU NA MMWAMBIE LWANGA KADI ZA NJANO ZISIMZOEE
Leo tumeona kabisa Pengo la Chris Mugalu katika Ushambuliaji akiwa kama Pacha wa John Boko Magoli na la Thadeo Lwanga katika Kiungo cha Ukabaji kiasi kwamba ilimlazimu Kocha abadili Mfumo na Kucheza na 'Double Pivot' katika Nafasi ya Kiungo cha Kukaba.

Tafadhali Chris Mugalu atibiwe upesi Majeraha yake ili kstika Mechi na Azam FC katika ASFC awepo lakini pia Thadeo Lwanga nae aambiwe aepuke mno hizi Kadi xa Njano na Nyekundu anazozipata mara kwa mara kwani huwa zinaigharimu Timu katika sehemu hiyo Muhimu ya Kiungo cha Ukabaji.

6. KIPA BENO KAKOLANYA KAPOTEZA KABISA KUJIAMINI NASHAURI ATAFUTWE KIPA MKUBWA WA KUMPA CHANGAMOTO KIPA AISHI MANULA
Kama isingekuwa Bahati tu leo Kipa Beno Kakolanya 'angeigharimu' Simba SC kutokana na Udakaji wake mbovu, usio wa Kimakini huku akiwa amepoteza Kabisa 'Kujiamini' ili atufungishe 'Kizembe' Magoli karibu matatu.

Sijui ni kwanini Kocha Mkuu Gomez hataki kumpa nae ( Kipa Kakolanya ) game time ili 'Kujiamini' Kwake kurejee kwani 'technically' imeonyesha kuwa Matukio ya Kizembe aliyoyafanya leo ni kwakuwa amelizoea mno Benchi.

Nashauri kama Kocha Gomez hamuamini Kipa Kakolanya basi auombe Uongozi wa Simba SC utafute Kipa bora kumzidi Aishi Manula (tena awe ni wa Kigeni) ili Simba SC iwe na hazina ya Uhakika ya Makipa Wawili au Watatu ambao watakuwa na Msaada mkubwa kwa Timu katika Michuano ya ndani na ile ya nje (Kimataifa)

7. WACHEZAJI WAPUNGUZE SANA ANAO ANAO ( SHOW GAME ) KWANI WANAKARIBISHA KUCHEZEWA RAFU ZA KUWAWEKA NJE KWA MAUMIVU
Haoa nieleweke vyema tafadhali sisemi kuwa Simba SC iachane na 'Culture' yake ya 'passing and flowing game' wenyewe mnaita Pira Biriani, Pira Sambusa na Pira Sharma bali ichezwe kwa uangalifu mkubwa ili Wachezaji wetu wasiwe wanaumizwa 'Kimakusudi' na Wachezaji wa Timu Pinzani na wasije 'Kuigharimu' Timu kwa Kutokuwepo ( Kutokucheza ) Kwao.

Tafadhali namalizia kwa Kusisitiza kuwa Simba SC isirudie tena Kucheza Mpira mbovu ilioucheza leo Kipindi cha Pill dhidi ya Mbeya City pale ikicheza na Azam FC Kombe la (ASFC) tarehe 26 June, 2021 na ikicheza na Yanga SC (VPL) tarehe 3 July, 2021 kwani kuna hatari Simba SC ikafungwa na Azam FC na 'Kulitema' Kombe la ASFC na pia ikafungwa na Yanga SC katika VPL na tukachukua Ubingwa ila tukiwa na Jeraha Kubwa la Kufungwa nao.

Huu ni Uchambuzi wangu tu wa Kimtazamo Mimi GENTAMYCINE na sikulazimishi uukubali japo umalazimika Kuuheshimu kama ambavyo nami pia nitaenda Kuiheshimu yenu.
Well said broda. Japo tumeshinda, lakin sijafurahia mchezo kabisa. Simba wamebweteka sana
 
Binafsi Jana niliona tunashinda kwa goli zaidi ya 2, yes kipindi cha pili wachezaji Wali relax na kukosa lile pira biriani!

Benchi la ufundi lifanyie kazi mapungufu na mechi zilizobaki naamini ushindi wa above 1 goal upo pale pale.

Go, go our boys, we trust you and we need wins za kutosha!

Sometimes show them mpo weak, Waje kichwa kichwa then give them hell! Pathetic Uto n the like.
 
Naomba nitoe maoni yangu.
Kadri Simba inavyozidi kupata mafanikio ya ndani na nje ya nchi kwa miaka ya karibuni, ndivyo timu inapoangaliwa na kuchambuliwa zaidi na wachambuzi na wapenzi wa kandanda kwa ujumla. Timu inaweza kufanya makosa ambayo timu zingine yanafanya karibu kila mechi, lakini kwa timu kubwa kama Simba makosa yataonekana zaidi. Ndio faida na hasara za kuchezea timu kubwa popote duniani.
Naomba nitoe mfano. Nilikuwa mchezaji mwandamizi katika timu ya kikapu ya Vijana (Vijana City Bulls) kwenye miaka ya mwanzo ya 90. Umakini/ukali/matayarisho/msukumo (intensity,pressure, preparation,focus) ya mnapocheza na timu kubwa, hususani dhidi ya wapinzani wetu wa jadi Pazi ni tofauti sana na unapocheza na timu zingine. Mnaelewa msipocheza katika kiwango cha hali ya juu, mtafungwa. Si kwamba tulikuwa tunazidharau timu nyingine. Hapana. Tulikuwa tunajua uwezo wa timu zote na vipi tucheze ili tupate ushindi. Kwa Timu kama Pazi, ilihitaji utimamu wa asilimia 100%.
Tukirudi kwa Simba, huwezi kufananisha Simba ilivyocheza na Al Ahly, AS Vita, El Mereikh, FC Platinum,nk na itakapocheza na timu tunazoziita ndogo kama Mbeya City. Utimamu wa mchezo utakuwa mkubwa sana kwenye mechi kubwa. Tungependa wacheze sawasawa kama walivyocheza CAF CL, lakini kiuhalisia haiwezekani. Hata tukiangalia timu kubwa duniani kama Barcelona ya miaka ya nyuma. Inaweza kumfunga mpinzani wake wa jadi Real Madrid 5 - 0, lakini akafungwa au akapata ushindi wa tabu dhidi ya Valencia.
Sina nia ya kuwatetea Simba, lakini ndio timu iliyofungwa magoli machache, iliyofunga magoli mengi, na iliyocheza michezo michache. Hii itakupa picha zaidi ya vipi ilivyo imara. Makosa hayatakwepeka na kuna nafasi kubwa ya Simba kujiimarisha.
Nawasilisha.
 
Timu ipi ina washambulizi wazuri? Nitajie pia timu nzuri duniani ambayo huwa haifungwi! Kufungwa kwa simba jana ni matokeo ya kawaida ya mpira wa miguu. Huwezi ukahukumu uzuri au ubovu wa timu kwa kigezo cha mechi moja au mbili. Kitaalam hutumika mechi tano mfululizo kuamua form ya timu kwa wakati husika.
Portugal kafungwa 4 juzi na Ujerumani, na mabeki kisiki walijifunga magoli 2!! Je Portugal ni timu mbovu? Hao ndik mabi gwa watetezi!! Bale juzi kakosa penati!! Je Bale ni mchezaji mbovu? Ndio maana makocha makini hawamnyimi mchezaji kupiga penati eti kwa sababu penati iliyopita alishindwa kufunga!! Ni kweli jana Simba walijichanganya kipindi fulani cha pili, wakasababisha goli! Lakini walijirekebisha na mambo yakamalizika vizuri! Ronaldo ni mpigaji mzuri sanà wa penati lakini kuna penati zingine hushindwa kufunga! Huo ndio utamu wa mpira!!

Ukipunguza mihemko na ukasoma vema alicho kiandika mtoa mada na nilichokiandika utaweza elewa na kupata kitu!
 
Kwanza,Ni lini Lwanga aliwahi kupewa kadi nyekundu iwe kwenye VPL au international tournament?

Pili,wakati unawaza kuwa Simba inaweza kufungwa na Azam kwa uzembe kama wa jana ukumbuke kuwa na wao Azam kama wakiingia kichwa kichwa kama walivyocheza na Namungo hawatapona kwa Simba.

Tatu,Kuchoka kwa Simba kipindi cha pili ni kutokana na aina ya mpinzani aliyekutana nae,mbona hawakuchoka kipindi cha pili walipokutana na Polisi, Kaizer,Yanga, Gwambina,AS vita nk.... mpinzani unayekutana nae ndio atakufanya ucheze vipi.

Nne, kuhusu swala la Kakolanya.Kusajili kipa wa nje eti ili aje kumpa changamoto manula kwanza kimkakati hii sio sawa,kumbuka kwamba NAFASI za kusajili wachezaji wa kigeni ni KUMI tu.Hizi nafasi kumi unapaswa kuzitumia kwenye maeneo ambayo wachezaji wa ndani wameshindwa kuzipambania mfano beki wa kati, kiungo mshambuliaji (hili tatizo lipo hadi national team), mshambuliaji hatari (hapa Tz yupo Bocco tu) ukienda Yanga hata Azam wageni ndio wanaongoza kwa ku score.

Hivyo basi nafasi ya goli kipa kwa simba tayari tumeshapa mchezaji mzawa tena wa daraja la juu kabisaaa,na ikumbukwe kuwa nafasi za kipa huwa ni nafasi ambazo mara nyingi huwa hazifanyiwi rotation,sasa kusajili kipa wa kigeni halafu aje akae benchi huko ni matumizi mabaya ya fedha pia kimbuni unajifunga mwenyewe kwenye zile nafasi kumi za kusajili wachezaji wa kigeni.

Kinachotakiwa kufanywa ni kocha achague mechi ambazo atacheza kakolanya mfano za FA, halafu za kirafiki na mapinduzi acheze Ally Salim na kwenye ligi kuu na Kimataifa acheze Manula.At least hapo atakuwa amewasaidia sana.

Kitu ambacho nakuunga mkono hapo ni swala la wachezaji kujiamini sana mpaka wakapitiliza.Nadhani hapo benchi la ufundi linapaswa kulitazama kwa jicho la pili.

Pia,swala la mipira ya header bado ni Tatizo sana kwenye beki line ya simba,ni Onyango pekee mwenye uwezo wa kuruka vichwa na Kennedy kwa mbali hawa wengine kina Kapombe, zimbwe,Ame,duchu na gadiel bado ni Tatizo sana.
Je, hapa sasa Umechambua au Umenichamba au Umeleta ujuaji wako wa Kipumbavu na Kishamba?
 
Naunga mkono hoja - kuna tatizo katika back line hassa Kennrdy Juma allipoteza pasi nyingi na alickoka kipindi cha pili.
Kakolanya ni kipa wa kawaida kwa sasa hafai kwa mechi kubwa.
Erasto Nyoni alicheza eneo ambalo linahitaji pumzi na stamina na kwa umri wake alipwaya jana.
Kwa ujumla nilichoona jana ni uchovu wa wachezaji na kujiamini kupitiliza inaonyesha hawakuwa vizuri kambini ( kimaadili baadhi yao).
Illa tujue tu kocha kayaona na sidhani kabisa - Simba kwa level waliofikia watadharau mechi kubwa au zenye ubabe na kupania watacheza kama jana?
Tukumbuke tu mechi na Azam, Songea na changamoto ya uwanja haitabiriki.
Wachezaji wa Simba wakiamua hassa wanashinda mechi zote ni suala match fitness, stamina na maamuzi tu.
Umegusia la uwanja,uwanja wa majimaji muusikie,wenyewe huko songea wanauita TANGAWIZI,kwa maana ya ile pitch,Sasa sijui Kama Hilo nalo liliwekwa sawa,ukicheza pasi Sana ni shida.
 
Kwanza,Ni lini Lwanga aliwahi kupewa kadi nyekundu iwe kwenye VPL au international tournament?

Pili,wakati unawaza kuwa Simba inaweza kufungwa na Azam kwa uzembe kama wa jana ukumbuke kuwa na wao Azam kama wakiingia kichwa kichwa kama walivyocheza na Namungo hawatapona kwa Simba.

Tatu,Kuchoka kwa Simba kipindi cha pili ni kutokana na aina ya mpinzani aliyekutana nae,mbona hawakuchoka kipindi cha pili walipokutana na Polisi, Kaizer,Yanga, Gwambina,AS vita nk.... mpinzani unayekutana nae ndio atakufanya ucheze vipi.

Nne, kuhusu swala la Kakolanya.Kusajili kipa wa nje eti ili aje kumpa changamoto manula kwanza kimkakati hii sio sawa,kumbuka kwamba NAFASI za kusajili wachezaji wa kigeni ni KUMI tu.Hizi nafasi kumi unapaswa kuzitumia kwenye maeneo ambayo wachezaji wa ndani wameshindwa kuzipambania mfano beki wa kati, kiungo mshambuliaji (hili tatizo lipo hadi national team), mshambuliaji hatari (hapa Tz yupo Bocco tu) ukienda Yanga hata Azam wageni ndio wanaongoza kwa ku score.

Hivyo basi nafasi ya goli kipa kwa simba tayari tumeshapa mchezaji mzawa tena wa daraja la juu kabisaaa,na ikumbukwe kuwa nafasi za kipa huwa ni nafasi ambazo mara nyingi huwa hazifanyiwi rotation,sasa kusajili kipa wa kigeni halafu aje akae benchi huko ni matumizi mabaya ya fedha pia kimbuni unajifunga mwenyewe kwenye zile nafasi kumi za kusajili wachezaji wa kigeni.

Kinachotakiwa kufanywa ni kocha achague mechi ambazo atacheza kakolanya mfano za FA, halafu za kirafiki na mapinduzi acheze Ally Salim na kwenye ligi kuu na Kimataifa acheze Manula.At least hapo atakuwa amewasaidia sana.

Kitu ambacho nakuunga mkono hapo ni swala la wachezaji kujiamini sana mpaka wakapitiliza.Nadhani hapo benchi la ufundi linapaswa kulitazama kwa jicho la pili.

Pia,swala la mipira ya header bado ni Tatizo sana kwenye beki line ya simba,ni Onyango pekee mwenye uwezo wa kuruka vichwa na Kennedy kwa mbali hawa wengine kina Kapombe, zimbwe,Ame,duchu na gadiel bado ni Tatizo sana.

Umechambua vizuri sana.
Ila naomba kuuliza, kujiamini kupitiliza ndio kukoje ?
Ni UPI MPAKA WA KUJIAMINI hasa katika mechi ya Simba dhidi ya Mbeya City ?
 
Wenzako wanajadili mechi iliyochezwa tayari,wewe unaleta utabiri wa hali ya hewa!
Utopolo ndio walivyo
FB_IMG_16217694080943737.jpg
 
Back
Top Bottom