Tuambiane ukweli kwa Mpira mbovu uliochezwa na Simba SC Kipindi cha Pili dhidi ya Mbeya City ikicheza na Azam na Yanga itafungwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,069
107,561
Kwanza nianze kwa Kupongeza Ushindi mzuri wa Goli 4 kwa 1 ambayo Simba SC imeshinda leo ( Usiku huu ) dhidi ya Mbeya City.

Pia nikiri kuwa Klabu ya Simba si tu kwamba inaishia kuwa na Kikosi kizuri (Timu nzuri) ila pia ina Wachezaji wenye Vipaji Asilia Binafsi kuliko wa Timu nyinginezo nchini Tanzania.

Hata hivyo pamoja na Kongole (Pongezi) zote hizi kuna baadhi ya Mapungufu ya Kimsingi niliyoyaona na kama Benchi la Ufundi pamoja na Wachezaji wenyewe wasipoyafanyia Kazi kuna uwezekano mkubwa mno Azam FC wakatufunga katika ASFC tarehe 26 June, 2021 na Yanga SC nao wakatufunga tarehe 3 June, 2021.

1. UKABAJI MBOVU
Bado Simba SC ina tatizo katika Ukabaji japo kidogo kidogo wanalifanyia Kazi, ila bado naliona hivyo lisipofanyiwa Kazi Mechi zote za Smba SC ilizobakiza dhidi ya Yanga SC, KMC FC, Coastal Union FC, Azam FC na Namungo FC.

2. WACHEZAJI WANAJIAMINI KUNAKOPITILIZA
Sema tu Mbeya City walishindwa kuja na Plan B ambayo wangekuwanayo na wangeshinda ( wangetufunga ) sana tu na Simba SC Kuumbuka.

3. MIPIRA YA JUU (VICHWA )
Bado tatizo la Wachezaji wa Simba SC hasa Mabeki kutokujua Kuruka Miipira huku 'Wakitegeana' lipo na Benchi la Ufundi wasipolifanyia Kazi mechi zetu Muhimu za Azam FC na Yanga SC 'tutafungwa' Goli nyingi na kuanza Kutafutana kwa Mkapa Temeke.

4. PUMZI KUKATA MAPEMA
Timu inaanza Kucheza vyema Kipindi cha Kwanza ila cha Pili Wacheza wanapoteana sana huku wakionyesha dhahiri kuwa hawana 'Match Fitness' na huenda pia huko kukaa Wiki Mbili Ligi Kuu ya VPL Kusimama Kumechangia Mpira mbovu walionao Simba SC sasa na ule walioucheza leo Kipindi cha Pili.

5. MTIBIENI VYEMA MUGALU NA MMWAMBIE LWANGA KADI ZA NJANO ZISIMZOEE
Leo tumeona kabisa Pengo la Chris Mugalu katika Ushambuliaji akiwa kama Pacha wa John Boko Magoli na la Thadeo Lwanga katika Kiungo cha Ukabaji kiasi kwamba ilimlazimu Kocha abadili Mfumo na Kucheza na 'Double Pivot' katika Nafasi ya Kiungo cha Kukaba.

Tafadhali Chris Mugalu atibiwe upesi Majeraha yake ili kstika Mechi na Azam FC katika ASFC awepo lakini pia Thadeo Lwanga nae aambiwe aepuke mno hizi Kadi xa Njano na Nyekundu anazozipata mara kwa mara kwani huwa zinaigharimu Timu katika sehemu hiyo Muhimu ya Kiungo cha Ukabaji.

6. KIPA BENO KAKOLANYA KAPOTEZA KABISA KUJIAMINI NASHAURI ATAFUTWE KIPA MKUBWA WA KUMPA CHANGAMOTO KIPA AISHI MANULA
Kama isingekuwa Bahati tu leo Kipa Beno Kakolanya 'angeigharimu' Simba SC kutokana na Udakaji wake mbovu, usio wa Kimakini huku akiwa amepoteza Kabisa 'Kujiamini' ili atufungishe 'Kizembe' Magoli karibu matatu.

Sijui ni kwanini Kocha Mkuu Gomez hataki kumpa nae ( Kipa Kakolanya ) game time ili 'Kujiamini' Kwake kurejee kwani 'technically' imeonyesha kuwa Matukio ya Kizembe aliyoyafanya leo ni kwakuwa amelizoea mno Benchi.

Nashauri kama Kocha Gomez hamuamini Kipa Kakolanya basi auombe Uongozi wa Simba SC utafute Kipa bora kumzidi Aishi Manula (tena awe ni wa Kigeni) ili Simba SC iwe na hazina ya Uhakika ya Makipa Wawili au Watatu ambao watakuwa na Msaada mkubwa kwa Timu katika Michuano ya ndani na ile ya nje (Kimataifa)

7. WACHEZAJI WAPUNGUZE SANA ANAO ANAO ( SHOW GAME ) KWANI WANAKARIBISHA KUCHEZEWA RAFU ZA KUWAWEKA NJE KWA MAUMIVU
Haoa nieleweke vyema tafadhali sisemi kuwa Simba SC iachane na 'Culture' yake ya 'passing and flowing game' wenyewe mnaita Pira Biriani, Pira Sambusa na Pira Sharma bali ichezwe kwa uangalifu mkubwa ili Wachezaji wetu wasiwe wanaumizwa 'Kimakusudi' na Wachezaji wa Timu Pinzani na wasije 'Kuigharimu' Timu kwa Kutokuwepo ( Kutokucheza ) Kwao.

Tafadhali namalizia kwa Kusisitiza kuwa Simba SC isirudie tena Kucheza Mpira mbovu ilioucheza leo Kipindi cha Pill dhidi ya Mbeya City pale ikicheza na Azam FC Kombe la (ASFC) tarehe 26 June, 2021 na ikicheza na Yanga SC (VPL) tarehe 3 July, 2021 kwani kuna hatari Simba SC ikafungwa na Azam FC na 'Kulitema' Kombe la ASFC na pia ikafungwa na Yanga SC katika VPL na tukachukua Ubingwa ila tukiwa na Jeraha Kubwa la Kufungwa nao.

Huu ni Uchambuzi wangu tu wa Kimtazamo Mimi GENTAMYCINE na sikulazimishi uukubali japo umalazimika Kuuheshimu kama ambavyo nami pia nitaenda Kuiheshimu yenu.
 
Mie niliona ttz ni nyoni ukweli huyu astaafu kwa heshima na pili ni kitendo cha kenedy kucheza namba siyo yake hivyo Kati paka pwaya Sana
Ila kuna ttz kimejionyesha kwenye mechi mbili za mwisho leo limekuwa dhahiri

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
Mfumo leo ulikuwa mpya na kama ulivyosema watu kucheza namba ambazo siyo zao. Yote kwa yote wamejitahidi kadri ya uwezo wao kuadapt.
 
Umeongea ukweli mchungu hapo tu ndio ninapoipendea Simba ina Mashabik wasio wanafki ukizingua unaambiwa ukweli sio km akina mwafulan wao lawama kwa tff badala ya kuwalaum wachezaj kwa show mbovu wanayotoa.

Na mm niongezee Jambo kwenye kucheza Sana na majukwaa na kujiamini kupituliza ,hii kuna siku itakuja kututokea puani ,ifike mahali userious kwa wachezaj uwe wa juu wapunguze kucheza na majukwaa.

Pia ubovu wa beki hasa mipira ya juu hili ni tatizo kubwa Sana kwa Simba yaan hawakabi kabisa ,mtu anapiga free header wao wanatoa macho tu.

Lile goli moja tumefungwa kwa uzembe wa bwalya ingawa simlaumu ni bahat mbaya ila siku nyingine mtu ukishajijua huna nguvu usikae Sana na mpira ,ule mpira alitakiwa autoe mapema Sana lakin yeye kachelewa wakamshinda nguvu na kumpokonya kizembe Sana ,siku nyingine asirudie.

Nadhan mengine yote umemaliza kiongoz.
 
Hao jamaa jana sijui walikula maharage ya wapi?! Kuna muda hadi matola alisimama na kusema mambo gani hayo mnafanya ilikuwa kati ya Kennedy na Nyoni hapa na hapa walipeana pasi za hovyo kabisaa! Kuhusu kakolanya alichagizwa pia na ubovu wa safu ya ulinzi mbeya city walifika sana kwenye box la simba hii ni hatari sana kwa timu zenye washambuliaji hatari!
 
Sina neno na nyie wachezaji wetu binafsi siwadai mapungufu ni ya kawaida hasa ikizingatiwa hatua ya ligi ilipofikia.
 
Umeongea ukweli mchungu hapo tu ndio ninapoipendea Simba ina Mashabik wasio wanafki ukizingua unaambiwa ukweli sio km akina mwafulan wao lawama kwa tff badala ya kuwalaum wachezaj kwa show mbovu wanayotoa...
Heko Mkuu nimependa nawe Uchambuzi wako kwani kuna Vitu vya maana umeviongezea ambavyo ni Ukweli mtupu.
 
Hao jamaa jana sijui walikula maharage ya wapi?! Kuna muda hadi matola alisimama na kusema mambo gani hayo mnafanya ilikuwa kati ya Kennedy na Nyoni hapa na hapa walipeana pasi za hovyo kabisaa! Kuhusu kakolanya alichagizwa pia na ubovu wa safu ya ulinzi mbeya city walifika sana kwenye box la simba hii ni hatari sana kwa timu zenye washambuliaji hatari!
Mkuu niamini maneno yangu kama Wachezaji wa Simba SC watacheza 'Kipuuzi' kama walivyocheza Kipindi cha Pili jana pale tukicheza na Azam FC Kombe la ASFC Jumamosi ile 'Derby' yetu na Yanga SC tarehe 3 July, 2021 tunaenda Kufungwa Mechi zote hizo Mbili ambazo ni Muhimu mno Kwetu.

Benchi la Ufundi liwaambie na Wachezaji wa Simba SC wabadilike kwani Azam FC na Yanga SC nao wana Wachezaji wakubwa na wazuri hivyo 'Kutuadhibu' kwa 'Uzembe' wetu kama ule wa Jana ni Jambo jepesi ( rahisi ) sana Kwao.

Binafsi naanza 'Kuogopa' kuwa huenda Simba SC tukafungwa na Azam FC na hata na Yanga SC kama tu 'Umakini' wa Kukiandaa vyema Kikosi chetu mahiri na kizuri hautafanyika 'Kiufundi' zaidi.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom