Tuachieni Nyerere Wetu

Tuachieni Nyerere Wetu

Baba wa Taifa kwako na familia yako. Nachojivunia kwake ni kutuunganisha kuwa lugha moja ila ana UCHAFU mwingi kuliko Usafi.
Tulilukuwa tukiwasiliana kwa Kiswahili kabla ya nyerere!

Alikuja kukishadidia kiwe lugha ya taifa kwa ajili watanzania wapate kusoma kirahisi biblia ambayo ilishaandikwa kwa Kiswahili kwa wingi na wamishionari waliofuatana na mkoloni.
 
Baba wa Taifa kwako na familia yako. Nachojivunia kwake ni kutuunganisha kuwa lugha moja ila ana UCHAFU mwingi kuliko Usafi.

kila mtu ana mapungufu yake mkuu,swala la kuwa baba wa taifa kwangu na familia yangu haina akili,sababu ndogo tu mfano leo shughuli zimekwama si ajabu hata kwako,na hii huwezi kuibadilisha labda uhame nchi hii.
 
watu wenye akili fupi kama yako hamtakiwi kwenye jamii ya watu wastaarabu, kama nchi ni ya kikristu inakuwaje rais ni mwislamu ? acha kuiga mawazo mgando

Sasa sijui baina yangu mimi na wewe NI NANI MWENYE MAWAZO MGANDO??

WAPI.MIMI NIMESEMA TANZANIA NI NCHI YA KIKRISTO??

Basi Ndugu yangu unadandia treni kwa mbele! Si utakufa??
Narudia tena! Nyerere ndio muasisi wa MFUMO KRISTO! na ndio maana leo unaskia KANISA KATOLIKI LIMEMPA CHEO CHA HERI HERI!
NA WANATAKA KUMPA "UTAKATIFU"
We unadhani utakatifu anapewa kiongozi yyt wa nchi??
Sharti moja la kupewa UTAKATIFU NI KUWA" LZM UWE DEDICATED KTK MAISHA YAKO YOTE KWA AJILI YA KANISA!
Sasa kama huna elimu hio Nenda kapate elimu kwanza kabla ya kuingia kwenye thread usio iweza!
 
Last edited by a moderator:
You cant tell me what to do! I am Tanzanian born and bred!
I have all the rights to say what I believe to be right!
Wewe kama unataka kutukuza udhalimu basi endelea! Mimi nasema kilicho haki!
Nyerere alikuwa ni mdini mkubwa na mvujaji wa haki za binaadamu!
Alipanga sheria kwenye bunge lililoko chini yake za kunyanyasa watu na kufunga watu jela BILA KUPITIA MAHAKAMA!
Familia zilikosa wazazi kwa sababu yake!
Leo mnakusanyika kumtukuza muovu??
Hata aibu hamuoni? Au mnata kusema haya madai yangu ni ya uongo?

sina hakika sana na unachokisema kwenye red hapo mkuu,ila nachojua kumaintain peace katika jamii ni jambo gumu sana lazima kuna watu wataumia,kwa mfano nchi za iraq na misri viongozi waliondolewa kwa kigezo cha kukiuka haki za binadamu lakini kinachoendelea saivi huko bora walivyokuwepo
 
Sasa sijui baina yangu mimi na wewe NI NANI MWENYE MAWAZO MGANDO??

WAPI.MIMI NIMESEMA TANZANIA NI NCHI YA KIKRISTO??

Basi Ndugu yangu unadandia treni kwa mbele! Si utakufa??
Narudia tena! Nyerere ndio muasisi wa MFUMO KRISTO! na ndio maana leo unaskia KANISA KATOLIKI LIMEMPA CHEO CHA HERI HERI!
NA WANATAKA KUMPA "UTAKATIFU"
We unadhani utakatifu anapewa kiongozi yyt wa nchi??
Sharti moja la kupewa UTAKATIFU NI KUWA" LZM UWE DEDICATED KTK MAISHA YAKO YOTE KWA AJILI YA KANISA!
Sasa kama huna elimu hio Nenda kapate elimu kwanza kabla ya kuingia kwenye thread usio iweza!

utakatifu anapewa mtu yeyote aliyeishi maisha mazuri, hata kama ni wewe ukiwa mkristu na ukaishi maisha ya ukristu vizuri unaweza ukawa mtakatifu, niambie kitu gani alichokifanya nyerere kibaya hasa cha kubagua dini hasa uislam
 
Niko kwenye kongamano la kuazimisha miaka 14 tangu alipokufa baba yetu Nyerere hapa Segerea kwa bibi, mgeni rasmi ni mh Tundu Lissu Kiboko ya KIKWETE na CCM.


Mada ni miaka 14 ya kifo cha Mwalimu na Tanzania tuitakayo. Kama ningekuwa ni mmoja kati ya wahutubu, nisingesita kusema kuwa asilimia kubwa ya Watanzania hatuijui Tanzania tuitakayo na kwa hivyo mada imekosa mashiko, badala yake naona ni vema ingekuwa miaka 14 ya kifo cha Nyerere na umbumbu wa Watanzania.


Kitendo cha watanzania mil 20 kujiandikisha kupiga kura uchaguzi uliopita na kisha mil 8 tu ndio waliojitokeza kupiga kura ni kiashiria tosha kuwa Watanzania hawana ndoto njema yoyote kwa nchi yao. Ndoto ya mwananch hutekelezwa na serikali inayoongoza nchi kwa niaba ya umma, ndoto ni zile ahadi, ilani na sera za chama au mgombea katika majukwaa ya siasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi; hususani kipindi cha kampeni.


Sasa kama mwananch hashiriki katika kuweka na kutoa serikali madarakani tutasemaje kama yuko na ndoto na nchi yake? Je, mwanach wa namna hii kuna Tanzania ambayo anaitaka?


Nafikiri tunawajibu sisi tunao jielewa, sisi ambao tuko na ndoto njema kwa Tanzania yetu kufanya kila namna kwa nafasi yetu kuhakikisha kuwa, wale wasojitambua, wanajitambua na wale waliolala, wanaamka hata uchaguzi ujao washiriki katika kuibakisha CCM madarakani au kuiondoa CCM madarakani, kinyume chake tutaendelea kuwa taifa lisilo na ndoto bali ni taifa la kupangiwa nini cha kuota na wenye nguvu ya fedha kwa kutumia udhaifu wetu wa kutojitokeza kupiga kura.

Asanteni.

Njano5.
0784845394.
 
utakatifu anapewa mtu yeyote aliyeishi maisha mazuri, hata kama ni wewe ukiwa mkristu na ukaishi maisha ya ukristu vizuri unaweza ukawa mtakatifu, niambie kitu gani alichokifanya nyerere kibaya hasa cha kubagua dini hasa uislam

Ntajaribu kukupa muangaza kidogo tu!
Wa namna huyo baba yako wa taifa alivyo wabagua WAISLAMU!

Sidhani kama wewe binafsi umeshawahi kuudadavua vema HUU MFUMO KRISTO KAMA ULIVYO.

NAKUOMBA UFUATANE NA MIMI KTK TAKWIMU ZIFUATAZO:-

kwanza kabisa hebu turudi nyuma kidogo!

Katika mwaka wa 1981 kumenukuliwa ktk kitabu kiitwacho " DEVELOPMENT AND RELIGION IN TANZANIA" by R.Bagan UKURASA WA 335 MATAMSHI YA NYERERE KAMA IFUATAVYO;-

"..I AM LAYMAN BUT I TRY TO DO WHAT I CAN AND WILL NOT GO AGAINST MY OWN CHURCH, I WANT TO GIVE CHURCH A BETTER CHANCE HERE, TELL THE BISHOPS THAT I HAVE ESTABLISH IN TANU A DEPARTMENT IN POLITICAL AND EDUCATIONS AND I HAVE PUT A LUTHERAN MINISTER INCHARGE, HE WAS NOT A GREATER POLITITION BUT A CHOSE HIM BECAUSE OF HIS STRONG CHRISTIAN FAITH "


MAANA YAKE" MIMI SI MJUZI WA DINI LKN HUWA NAFANYA KILE NIWEZACHO NA KAMWE SIWEZI KWENDA KINYUME NA KANISA LANGU, NATAKA KULIPA KANISA NAFASI BORA HAPA, WAAMBIE WACHUNGWAJI NIMEANDISHA IDARA KTK TANU IITWAO SIASA NA ELIMU NA NIMEMTEUA WAZIRI WA DHEHEBU LA KILUTHERAN KUWA MSIMAMIZI, NA HAKUWA MWANA SIASA HODARI BALI NIMEMCHAGUA KWA UIMARA WA IMANI YAKE YA KIKRISTO."

Sasa hapa NDUGU YANGU unaona waziwazi kuwa RAIS WA NCHI anaanzisha wizara KWA AJILI YA KULIPA NAFASI BORA KANISA na kumkabidhi Mtu, si kwa uhodari wake KISIASA, LA HASHA BALI KWA UIMARA WA IMANI YAKE YA KIKRISTO.

Tukiendelea na takwimu sasa;-

takwimu hizi NI MPAKA 2011,


TAZAMA CHEO NA JUMLA YA NAFASI SERIKALINI

UKAMISHNA- 1
WAKRISTO 1 WAISLAMU 0

WAKURUGENZI 9
WAKRISTO 7 WAISLAMU 2

NAIBU WAKURUGENZI 8
WAKRISTO 7 WAISLAMU 1

WAKAGUZI WAKUU WA KANDA. 11
WAKRISTO 10 WAISLAMU 1

MAAFISA ELIMU WA MIKOA 21
WAKRISTO 16 WAISLAMU 5

MAAFISA ELIMU WA WILAYA 125
WAKRISTO 102 WAISLAMU 23

UONGOZI WA TAASISI VYUO VIKUU 25
WAKRISTO 23 WAISLAMU 2

WAKUU WA SHULE DARESALAAM 11
WAKRISTO 11 WAISLAMU 0

WAKUU SHULE ZA KATA 215
WAKRISTO 200 WAISLAMU 15


SASA Ndugu yangu
HEBU TUHAMIE KWENYE NGAZI ZA JUU SERIKALINI!.

Tuanze na NECTA (BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA} LILILOANZISHWA 21/11/1973.

NAFASI YA WENYEKITI WA BARAZA HILI TOKA LIMEANZISHWA NI KAMA IFUATAVYO;-

1973-1977 PIUS MSEKWA.

1977-1980 I.M.KADUMA

1980-1988 N.A KUHANGA.

1988-1992 PROFESA G.R.V MMARI.

1992-1999 M.L. LUHANGA

1999-2004 PROFESA G.R.V.MMARI.

2004-2007 E.MWAIKAMBO

2007-2011 R,A,MKANDALA.[/B]


Kwa kifupi toka baraza la mitihani la taifa mpaka leo HAKUNA MUISLAMU ALISHAWAHI KUWA MWENYEKITI WA BARAZA HILO!!


HIZI NI TAKWIMU NIMEMALIZIA MPAKA 2011. Na sidhani kama kuna haja ya kukuongezea DATA ZAIDI! ZA MANAIBU NA KUENDELEA MBELE! ALMOST WOOTE NI WAKRISTO.

Hapa nilitaka kukuonjesha kidogo tu UONE NAMNA MFUMO KRISTO ULIVYO WABANA WAISLAMU KWA MIAKA MINGI SANA HASSA KWENYE NYANJA YA ELIMU.

Watu wengi wasio na elimu hukimbilia kusema kuwa WAISLAMU HAWAJASOMA! KWA HIVYO HAWASTAHIKI NAFASI KAMA HIZI!!
Ukitizama hoja hii utakuwa kuwa SIO KWELI KABISA! Tunao MAPROFESA WENGI TU WA KIISLAMU TANZANIA AMBAO HAWAKUPEWA NAFASI HATA KIDOGO HASA KTK NYANJA HII MUHIMU YA ELIMU.

NA HILI NI MOJA YA SERA ZA MFUMO KRISTO,


Ukishaweza kubana watu kwenye elimu basi ni raisi sana kuwamiliki utakavyo.

sasa hapa nimekuonjesha tu kidogo namna ya HUYO MTAKATIFU WAKO AMBAE AMEISHI MAISHA MAZURI ALIVYO WAFANYA WAISLAMU KTK SEKTA MOJA TU!

HAPO BADO KUNA NYANJA ZINGINE KAMA 19 AMBAZO SINA MUDA WA KUDHIORODHESHA ZOTE HAPA!

Kama ulikuwa hufahamu ukweli! Basi usichukue maneno yangu tu! NENDA KAFANYE UTAFITI MWENYEWE! UONE KAMA DATA HIZI NI ZA UONGO!

I HOPE YOU WILL UNDERSTAND WHY THAT BABA OF YOURS DOESN'T DESERVE ANY PRAISES!

Wacha kumuita BABA WA TAIFA
HAIFAI HATA KUMUITA JIRANI WA TAIFA.
 
Last edited by a moderator:
IF A DOOR IS SHUT,
ATTEMPTS SHOULD BE MADE TO OPEN IT,
IF IT IS AJAR,
IT SHOULD BE PUSHED UNTIL IS WIDE OPEN.
IN NEITHER CASE SHOULD THE DOOR BE BLOWN UP AT THE EXPENSE OF THOSE INSIDE.by J.K NYERERE

#mwalimu alikuwa na mtazamo wa mbali sana na maamuz haya ndo tunayotakiwa kuyafanya ifikapo 2015.
 
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kweli tuna kuenzi kwa mambo mengi sana lakini binafsi nianze na haya lakini wana CCM wenzangu watanikumbusha mengine.
  1. -Baada ya wewe kufa tulipata nguvu mpya ya kuuza viwanda vyote
  2. -Tunauza wanyama nje ya nchi kisha pesa tuna gawana wajanja wanja.
  3. -Tofauti na wewe ulivyokufa masikini hivi sasa viogozi wetu wa CCM tunaficha Uswiss mabilioni tuliyoyakwapua kutoka wa watanzania
  4. -wahuni/malaya aliuwakataa mwaka 1995 ndiyo viongozi wetu mmoja tulimfukuza kwa ufisadi lakini tunajiandaa tumpigie kampeni awe raisi wa nchi yako.
  5. -Wajambazi tuna wasamehe lakini wanaoiba kuku tuna wachoma moto.
  6. -Rais wetu amekaa madarakani miaka saba lakini amesha safiri mara 358 hivyo ukifanya kwa wastani kila safari alikaa siku tatuinamaana 358 x3, hivyo miaka mitatu tumekuwa bila rais.
  7. -Nchi tunaitangaza kwa njia ya kipekee kabisa kwani kwasasa tunajulikana kwa kuuza sembe duniani
  8. -Katibu wa chama chako(Mwalimu) ndiyo jangili mkuu na ndiyo msafirishaji wa pembe za ndovu kwasasa tembo wana zidi kuteketea
  9. -Jeshi la tanzania wamegeuka wabakaji badala ya walinda amani
  10. -Jeshi la polisi kwa kushilikiana na viongozi wa juu wa CCM(chama cha Mwalimu) ndiyo wanao wauwa watanzania kwa kuwalipua kwa mabomu ya kichina
  11. -waandishi wa habari hawana uhakika na maisha yao kwani wakionekana kwenye mikutano ya chadema wanauliwa tu
  12. -chama chako mwalimu kimegeuka chama cha wangoa kucha, meno,na kunyofoa macho kama unabisha muulize kubenea, kubanda
  13. -Mwalimu chama chako kilitoa mabilioni ya sijui JK matokeo yake akapewa Riz1 na wauza unga wengine.
  14. -Raisi wa nchi anapiga deal za milion nane kwa kushirikiana na waziri...
  15. -Raisi ndiyo promotor wa Diamond, 50 Cents, Boyz II Men ndiyo kiongozi anaeongoza kwa kupiga picha na vidosho.
  16. -Ikulu imekuwa sebule ya wabwia unga (kama unabisha muulize Ray C)
  17. -Ndani ya nchi yako uliyoipenda kuna nchi nyingie inaitwa falme ya oman ni hapo Loliondo
  18. -Chama chako raisi kwasasa analipwa mil 32 na waziri mkuu mil 26..
  19. -Siku hizi Bungeni ukitaka kutoa hoja ni unapigwa tu...
  20. -Spika wa bunge anaendesha bunge kwa maelekezo kwa kutumiwa SMS.
Mwalimu naona nisikuchoshe ngoja wengine waje waongezee kama hawatagafilika wakaanza kupolomosha mimatusi kama wabunge wao...
 
Maneno mazito sana kiasi kwamba nimejihisi niko ulimwengu mwingine kabisa.

Mkuu Crashwise asante kwa uchambuzi makini.
 
Last edited by a moderator:
Ntajaribu kukupa muangaza kidogo tu!
Wa namna huyo baba yako wa taifa alivyo wabagua WAISLAMU!

Sidhani kama wewe binafsi umeshawahi kuudadavua vema HUU MFUMO KRISTO KAMA ULIVYO.

NAKUOMBA UFUATANE NA MIMI KTK TAKWIMU ZIFUATAZO:-

kwanza kabisa hebu turudi nyuma kidogo!

Katika mwaka wa 1981 kumenukuliwa ktk kitabu kiitwacho " DEVELOPMENT AND RELIGION IN TANZANIA" by R.Bagan UKURASA WA 335 MATAMSHI YA NYERERE KAMA IFUATAVYO;-

"..I AM LAYMAN BUT I TRY TO DO WHAT I CAN AND WILL NOT GO AGAINST MY OWN CHURCH, I WANT TO GIVE CHURCH A BETTER CHANCE HERE, TELL THE BISHOPS THAT I HAVE ESTABLISH IN TANU A DEPARTMENT IN POLITICAL AND EDUCATIONS AND I HAVE PUT A LUTHERAN MINISTER INCHARGE, HE WAS NOT A GREATER POLITITION BUT A CHOSE HIM BECAUSE OF HIS STRONG CHRISTIAN FAITH "


MAANA YAKE" MIMI SI MJUZI WA DINI LKN HUWA NAFANYA KILE NIWEZACHO NA KAMWE SIWEZI KWENDA KINYUME NA KANISA LANGU, NATAKA KULIPA KANISA NAFASI BORA HAPA, WAAMBIE WACHUNGWAJI NIMEANDISHA IDARA KTK TANU IITWAO SIASA NA ELIMU NA NIMEMTEUA WAZIRI WA DHEHEBU LA KILUTHERAN KUWA MSIMAMIZI, NA HAKUWA MWANA SIASA HODARI BALI NIMEMCHAGUA KWA UIMARA WA IMANI YAKE YA KIKRISTO."

Sasa hapa NDUGU YANGU unaona waziwazi kuwa RAIS WA NCHI anaanzisha wizara KWA AJILI YA KULIPA NAFASI BORA KANISA na kumkabidhi Mtu, si kwa uhodari wake KISIASA, LA HASHA BALI KWA UIMARA WA IMANI YAKE YA KIKRISTO.

Tukiendelea na takwimu sasa;-

takwimu hizi NI MPAKA 2011,


TAZAMA CHEO NA JUMLA YA NAFASI SERIKALINI

UKAMISHNA- 1
WAKRISTO 1 WAISLAMU 0

WAKURUGENZI 9
WAKRISTO 7 WAISLAMU 2

NAIBU WAKURUGENZI 8
WAKRISTO 7 WAISLAMU 1

WAKAGUZI WAKUU WA KANDA. 11
WAKRISTO 10 WAISLAMU 1

MAAFISA ELIMU WA MIKOA 21
WAKRISTO 16 WAISLAMU 5

MAAFISA ELIMU WA WILAYA 125
WAKRISTO 102 WAISLAMU 23

UONGOZI WA TAASISI VYUO VIKUU 25
WAKRISTO 23 WAISLAMU 2

WAKUU WA SHULE DARESALAAM 11
WAKRISTO 11 WAISLAMU 0

WAKUU SHULE ZA KATA 215
WAKRISTO 200 WAISLAMU 15


SASA Ndugu yangu
HEBU TUHAMIE KWENYE NGAZI ZA JUU SERIKALINI!.

Tuanze na NECTA (BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA} LILILOANZISHWA 21/11/1973.

NAFASI YA WENYEKITI WA BARAZA HILI TOKA LIMEANZISHWA NI KAMA IFUATAVYO;-

1973-1977 PIUS MSEKWA.

1977-1980 I.M.KADUMA

1980-1988 N.A KUHANGA.

1988-1992 PROFESA G.R.V MMARI.

1992-1999 M.L. LUHANGA

1999-2004 PROFESA G.R.V.MMARI.

2004-2007 E.MWAIKAMBO

2007-2011 R,A,MKANDALA.[/B]


Kwa kifupi toka baraza la mitihani la taifa mpaka leo HAKUNA MUISLAMU ALISHAWAHI KUWA MWENYEKITI WA BARAZA HILO!!


HIZI NI TAKWIMU NIMEMALIZIA MPAKA 2011. Na sidhani kama kuna haja ya kukuongezea DATA ZAIDI! ZA MANAIBU NA KUENDELEA MBELE! ALMOST WOOTE NI WAKRISTO.

Hapa nilitaka kukuonjesha kidogo tu UONE NAMNA MFUMO KRISTO ULIVYO WABANA WAISLAMU KWA MIAKA MINGI SANA HASSA KWENYE NYANJA YA ELIMU.

Watu wengi wasio na elimu hukimbilia kusema kuwa WAISLAMU HAWAJASOMA! KWA HIVYO HAWASTAHIKI NAFASI KAMA HIZI!!
Ukitizama hoja hii utakuwa kuwa SIO KWELI KABISA! Tunao MAPROFESA WENGI TU WA KIISLAMU TANZANIA AMBAO HAWAKUPEWA NAFASI HATA KIDOGO HASA KTK NYANJA HII MUHIMU YA ELIMU.

NA HILI NI MOJA YA SERA ZA MFUMO KRISTO,


Ukishaweza kubana watu kwenye elimu basi ni raisi sana kuwamiliki utakavyo.

sasa hapa nimekuonjesha tu kidogo namna ya HUYO MTAKATIFU WAKO AMBAE AMEISHI MAISHA MAZURI ALIVYO WAFANYA WAISLAMU KTK SEKTA MOJA TU!

HAPO BADO KUNA NYANJA ZINGINE KAMA 19 AMBAZO SINA MUDA WA KUDHIORODHESHA ZOTE HAPA!

Kama ulikuwa hufahamu ukweli! Basi usichukue maneno yangu tu! NENDA KAFANYE UTAFITI MWENYEWE! UONE KAMA DATA HIZI NI ZA UONGO!

I HOPE YOU WILL UNDERSTAND WHY THAT BABA OF YOURS DOESN'T DESERVE ANY PRAISES!
hapo kwenye red hujamtaja jina mtu wa kanisa aliyepewa kitengo na nyerere, vilevile nyerere ni mkatoliki kwa nini asingemuweka mkatolik maana luthereni siyo kanisa la nyerere. Pia unaposema sehemu nyingi wakristu wamejaa hapo nakubaliana kwa kuwa kwanza dini hizi mbili zililetwa na waarabu na wazungu. Tuangalie philosopy ya watu hawa katika suala la elimu. Wazungu (missionaries) walipokuwa wakijenga kanisa walijenga shule wakiamini kuwa mumini ili aelewe biblia lazima ajue kusoma lakini kwa waarabu walijenga misikiti na madrasa. Mh Kikwete mwenyewe kasomea misheni shule za kikristu, kwa hiyo uwingi wa wakristu enzi hizo katika idara mbalimbali tunaweza kutizama katika mtizamo huo na siyo kulikuwa na ubaguzi wa kidini
 
Pamoja na kuwa posti kama hizi ziningia ndani ya zile kampeni ya "delete futa kabisa" mimi ningeomba muwasilishaji adelete kwa hiyari yake ile namba 16 kwani kila mwenye matatizo anastahili msaada. Yaliyobaki naona yabaki tu.

Kama itakubalika naomba niongezee ujumbe kwa mwalimu.....

21-Siku hizi Chama chetu kimeshindwa kabisa siasa. Kimeamua kulazimisha watoto, hasa wanafunzi kufanya siasa kwa niaba ya chama. Hata shule ni za wasiwasi.

22-Najua uliamini twiga ni wanyama warefu, ila kunamabadiliko makubwa. Siku hizi wanakunjwa kwenye tenga na wanaenea. Huwa wanapandishwa hata kwenye ndege wanauzwa ulaya.

23-Ule ubinadamu na udugu uliotuachia umeondoka, siku hizi polisi ndiyo majambazi, wanajeshi wamekuwa CCM na wanatuua na kututesa bila sababu.

24-Ile katiba yetu mbovu uliyotuachia imekosa maana kabisa, siku hizi kila mtu anatumia sheria binafsi, wanaopigwa wanapigwa, wanaofungwa wanafungwa tu, hata kijana wetu Mwigulu haoni aibu kupoteza muda wa mahakama kwa kesi za kijingajinga.

25-Ile janja janja kati ya uongozi na maamuzi imekuwa worse. Hata kile chama chetu cha wakulima na wafanyakazi kimebadilishwa kihuni kuwa cha wahujumu, mafisadi na wafanyabiashara wakubwa. Kama huna hela hawana mpango na wewe. ukijipendekeza wanakutumia tu kama Nape na wakikukuona "loose canon" wanakutema tu!

26-Nakumbuka uliponda siasa ya ujamaa na kujitegemea kutelekezwa kihuni, ila siku hizi ujamaa umekwisha kabisa na pia kujitegemea tumeshindwa jumla. Hata Rais wetu amekazania kukopa na kuomba badala ya kuimarisha uchumi kwa kukazia kilimo na kusimamia mapato ya serikali. Madini na mbuga zetu hata sina hamu, wanagawana vitalu kama havina wenyewe. Tukiuliza tunapigwa.....
 
Hapa bavicha ameenda kufanya homework na kurudi na trash hii. Kweli BAVICHA ni hasara tupu.

Kuna Mzee mmoja ambaye alitaka kuwa Rais wa nchi yetu lakini wananchi walimkataa kwa sababu yaulaghai na pia hakuwahi hata kupitia pitio la ujana wakati wa ujana wake ambapo kwa sasa ndiyo anafanya mambo ya ujana. He's old but allover the place mpaka hata hajitambui kwenye maandishi yake.

Mtu anayejitambua hawezi kuandika kitu kama hiki kwenye jukwaa la siasa.
ZeMarcopolo,
Mawazo yako ni ya kipuuzi. Josephine ni mke wangu. Hata mkisema namna gani hakuna atakayebadilisha kwa kuwa ndoa ni kati ya watu wawili. Mungu tu ndiye atakayehukumu kwa kuwa ndiye anayejua nafsi na mioyonya wanaoingia kwenye Mkataba. Mnapoteza muda kuzungumzia ndoa ya Slaa na Josephine, wakati jamii ya watanzania wanamkubali na wamempokea Josephine Kama Mke wa Dr Slaa. Ni watu Kama wewe na CCM waliofanya kila jitihada kwenye magazeti na hata kusukuma watu kwenda mahakamani. Hayo yote hayabadilishi status ya Slaa na Josephine.


Pili, swala la Josephine kuingilia masuala ya Chadema, tafadhali kwa manufaa ya wasomaji wa JF na wanachadema kwa ujumla weka hadharani ni masuala gani ameingilia, na ni kifungu gani cha Katiba kimevunjwa. Kwa wengi msiofahamu, Josephine ni mwanaharakati tangu kabla hatujafahamiana. Matunda ya kazi zake yanaonekana kwenye mitaa ya Keko, Kinondoni, na Kimaria. Dr Slaa ni mwana demokrasia, na Siko tayari kuzuia vipaji na wito wa mtu. Shughuli hizo zinategemea moyo wa mtu na Mungu wake, ndio maana si kila mtu anaweza kufanya kazi hizo. Kama ambavyo ninawashawishi, ninawasukuma, ninawajenga uwezo watanzania mbalimbali kuwahudunia watanzania wenzao, kuwashirikisha watanzania katika ujumla wao katika kazi ya ukombozi wa Taifa letu. Kila mmoja wetu ni sawa na pingili ya Chain, na wote tunahitajiana. Asiyepingana na sisi yuko na sisi, alimradi kila mmoja wetu anatumia karama alizopewa na Mwenyezi Mungu. Wote tukiwa wanyenyekevu na kutambua Hilo kazi ya ukombozi itakuwa nyepesi.


Swala la Josephine kutumia ID ya Dr Slaa, is a none Issue. Rudi kwenye post ya Josephine. Alieleza kuwa Hana access ya Internet kwenye IPAD yake. Alikuwa mnyofu kuwa julisha wasomaji na japo ID ni ya Dr Slaa, akasaini Kama Josephine. Sasa hapo issue nini? Kama kuna agenda nyuma ya hapo si itamkwe wazi badala ya kuzunguka zunguka. Ni kukosa uadilifu kutunga mambo ya kipuuzi dhidi ya mtu mwingine. Ustaarabu nimkuwa Kama mtu hakuelewa alikuwa na haki ya kuuliza lakini siyo kuhukumu, navkueneza propaganda. Katika dini zetu umbea, majungu na kudanganya au kupotosha ni dhambi. Kama kweli kuna nia njema ni muhimu kuwa wakweli na wawazi katika yote tunayofanya. Ukweli na uwazi hutufanya kuwa na uhuru wa kweli vinginevyo mtaendelea kuishi katika unafiki na utumwa wa nafsi zenu wenyewe. Nimetumia lugha kali kwa kuwa hoja za kipuuzi zinapoteza muda bila sababu, muda ukipotea kwa umbeya na majungu tunapoteza fursa za kujenga Taifa letu ambalo kila Leo linazidi kutumbukia kwenye umaskini na kero mbalimbali. Tunahitaji kuweka nguvu pamoja, bila kujali itikadi kupambana na kero ili tujenge Taifa letu. Hakuna atakayejenga Tanzania isipokuwa Watanzania,lakini watanzania watakaojenga Taifa Lao siyo haw a ambao kila kukicha wanazungumza watu, tena kwa kuchanganya uwongo na propaganda. Kama kila anayechangia angetumia sehemu ndogo sana ya ubongo wake constructively, Tanzania ndani ya muda mfupi sana itajikomboa. Amerika iliendelea kiuchumi, kimaendeleo kwa kuwa hawana muda na majungu, umbeya wala upuuzi tunaosoma kila Leo kwenye Mitandao na hasa JF. Kila mmoja anatumia muda alionao kujiendeleza na kuendeleza Taifa lake. Mitaani hutaona ushabiki na propaganda za vyama, ndio hakuna ushabiki wa kushindania bender za vyama, badala karibu kila nyumba inapepea bendera ya Taifa Lao America. Watu wako proud na Taifa Lao na union wazi kwa jinsi wanavyosifia kila kitu cha kwao. Tujifunze hatujachelewa, tubadilike vinginevyo watoto na wajukuu watatulaani kwa kutokuwajengea mazingira mazuri Kama Mungu alivyokusudia.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...na-tuchore-mstari-tuseme-yatosha-sasa-10.html

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kweli tuna kuenzi kwa mambo mengi sana lakini binafsi nianze na haya lakini wana CCM wenzangu watanikumbusha mengine.

Mwalimu naona nisikuchoshe ngoja wengine waje waongezee kama hawatagafilika wakaanza kupolomosha mimatusi kama wabunge wao...
 
Mafanikio gani unayo yaongelea hapa!
Hebu tafadhali usichafue mazingira hapa!
Kupanga foleni ya unga wa njano ndio mafanikio hayo?
Kugawiwa sukari nusu kilo kwa mwenzi ndio mafanikioa hayo??
Kunyimwa uhuru wa kuikemea serikali na watu kutiwa mahabusu miaka chungu mzima ndio mafanikio hayo!?
Kutuletea MFUMO.KRISTO ndio mafanikio hayo??
Ustake kunchafua hapa! Baadhi ya Wenzetu wa Afrika wameanza kuona matunda ya uhuru mara baada tu ya wakoloni kuondoka!
Sisi badala ya kufurahi wakoloni kuondoka! Wazee wetu walinza kulaani namna serikali chini ya uongozi wa huyo mkatoliki ilivyo kuwa ina wanyanyasa!
Walitamani waingereza warudi kuendelea kuwatawala!
Sasa usiongee vitu kama huna kichwa!!

MFUMO.KRISTO the best dunia hii haijaona.Kama unataka alternative fuata AL SHABAB,TALEBAN,BOKO HARAM etc.
Fika Germany,Scandinavia etc uone matunda ya mfumo !naona Dau ameweka mfumo wenu pale NSSF,kwa hela zetu,najua na baraka toka juu
 
Maneno meeeengi lkn kwa mtanzania mwenye kuufahamu ukweli haya maana yoyote ! Na ni uongo mtupu!

We unamsifia MDINI? NA MBAGUZI?

Nyerere ktk umri wake toka baada tu ya kupata uhuru YYT ASIEKUWA.MKRISTO KWAKE ALIKUWA NI UCHAFU TU!

Kanisa aliliweka.mbele mpaka kwenye ruzuku za serikali.
We kaa ukijaribu kudanganya watu kuwa Nyerere alikuwa mwema!
Yule alikuwa ni nyoka anae kuuma huku anakupuliza! Anakuchekea hadharani akiingia ndani anakuwekea sumu kwenye chakula!
Ikiwa unampenda kiasi cha kutetea uovu wake hadharani namna hii! Basi mfate huko KUZIMU.

Wewe ni mwalimu wa kigalatia ambae usingefika kumsifia huyu muovu ispokuwa ule MFUMO KRISTO aliuacha umekufikisha hapo ulipo na kwa kuandika description zako na wapi unapatikana NI MOJA YA KUTAFUTA SIFA ZISIZO KUWA NA MAANA!

Ukitetea uovu basi iko siku utakudhuru wewe au kizazi chako! Watch out!!

Pumba za Misikitini hizi....
 
Ntajaribu kukupa muangaza kidogo tu!
Wa namna huyo baba yako wa taifa alivyo wabagua WAISLAMU!


[h=3]UDINI NA UTANZANIA:TULIPOTOKA,TULIPO,TUELEKEAPO
http://udadisi.blogspot.com/2012/06/udini-na-utanzaniatulipotokatulipotuele.html[/h]
























MCHANGO WA MOBHARE MATINYI KATIKA MJADALA WA UDINI



Naomba nichangie hapa kama Mtanzania - na si kama mwislamu au mkristo au mpagani.

1. Kwanza ni kweli kwamba kitabu cha yule padri mzungu kinaleta shida sana mawazoni mwa watu, Dkt. Sivalon. Lakini turejee kwenye ukweli wa kisomi, kwamba huwezi kuhitimisha jambo zito kwa kutumia chanzo kimoja. Hatuna maandiko mengine ya watu wasiokuwa na upande yanayothibitisha aliyosema bwana huyu. Hakuna utafiti wowote. Aidha, ni muhimu pia kuchunguza kujua alisema hivyo katika mazingira gani. Kuna Mkenya mmoja London aliwahi kuzuliwa na wenzake kwamba ni shoga na akatengwa kabisa. Aliyemzulia siku moja akamwambia Mkenya mwingine ninayemfahamu, kwamba anajua fika kuwa bwana yule si shoga lakini alifanya vile kumlipizia kisasi cha ugomvi wao. Uongo ulibadilishwa kuwa ukweli. Je, tuna hakika na maneno ya huyu mwandishi padri? Najua ukivutia upande mmoja itabidi useme uhakika upo kwa sababu kuna uthibitisho mwingine, lakini hali halisi inagoma. Nitaeleza.

2. Pili, ingawa Mwalimu Julius Nyerere analaumiwa sana na waislamu au watetezi wa waislamu, lakini kiukweli kama si yeye, hali ya kielimu ya waislamu nchini ingekuwa mbaya sana. Tusisahau kuwa, tulipopata uhuru serikali ya Mwingereza hakituachia shule za kutosha. Wakristo na dini za Waasia wakiwemo Wabohora, Waismailia na Wahindu walikuwa na shule lakini Waislamu hawakuwa na shule. Sasa ukumbuke pia kuwa, wakoloni wa Ulaya walikuja Afrika Mashariki kwenye karne ya 19 wakati wakoloni wa Uarabuni walikuwa tangu karne ya 13. Kwa miaka 600 Waarabu hawakujenga shule hata moja; bali walijenga madrasa kwa ajili ya masomo ya dini - jambo ambalo halikuwa dhambi.
Shule za kwanza zilijengwa Tanganyika na Mjerumani zikiwa ni za darasa la kwanza hadi la nne kwa kutumia Kiswahili. Zanzibar zilijengwa sana sana na Mwingereza. Tafuta maana na historia ya maneno haya: (i) Darasa/Madarasa (ii) Shule (iii) Skuli. Kimsingi, Nyerere ndiye aliyezitaifisha shule za wasiokuwa waislamu ili na watoto wa waislamu waende kusoma kwa sababu walikuwa wanakwepa kubadilishwa dini na kulishwa nguruwe ingawa wakristo wengine kama wasabato hawali nguruwe.

3. Nchi yetu ikapiga hatua zaidi na tukaanza kujenga shule za msingi. Nyerere akajenga shule kwa juhudi kubwa zaidi kwenye mikoa iliyokuwa nyuma, ambayo mingi ilikuwa ni ya pwani waliko waislamu wengi zaidi. Haikutosha, baada ya Nyerere kuibana mikoa mingine, ambayo wananchi wake waliamua kujijengea wenyewe, akaweka nafasi maalum kwa watu wa makabila ambayo hayakuwa na watoto wengi shuleni, yaani hayakuwa yanataka shule. Waliofaidika zaidi ni makabila ya pwani ambako shule ilikuwa kama kituo cha polisi kwao. Dini yao wengi wao tunaijua. Mwalimu akiwa anaongoza TANU na CCM akajenga shule za jumuiya ya wazazi kwenye mikoa ya pwani na hata alipopata msaada kutoka Kuba (Cuba), aliichagua mikoa ya pwani pia kujengewa shule, na ndipo tukapata shule kama Kibiti, Ruvu, n.k. Hata ile ya Waswidi ilijengwa Kibaha. Alifanya hivi kuwasaidia hao mnaowaita waislamu (mimi nawaita Watanzania). Kule kwingine kama Kilimanjaro, wakaamua kujenga shule za binafsi zao wenyewe na ndio maana hadi leo wanazo nyingi. Serikali ya Nyerere haikujenga shule za sekondari kule bali ilijenga hizo chache kwenye mikoa yenye waislamu wengi. Ndio ukweli huo ila watu hawataki kuutafuta. Rekodi zipo, tafuta shule zote uone.

4. Serikali ya Tanzania haikuishia hapo. Wakati wa Rais Mwinyi waislamu wakiongozwa na Waziri Kighoma Malima walilalamika sana. Zikafanyika juhudi nyingi ikiwemo kumweka Malima kwenye sehemu kama elimu ambapo alianzisha awamu mbili za kwenda shule, lengo likiwa kuongeza idadi ya watoto wa kiislamu wanaoingia sekondari ingawa na wakristo pia waliongezeka. Pia Tanzania ikapata nafasi za masomo kwenye mataifa ya Misri, Algeria, Iran, na Uturuki, maalum kwa ajili ya waislamu tu. Marafiki zangu walikwenda huko na walinithibitishia kwamba hii ilikuwa maalum kwa waislamu tu. Bado waislamu waliendelea kwenda nchi zingine zisizokuwa za kiislamu bila tatizo. Huu ulikuwa msaada mkubwa.

5. Ikaja serikali ya Ben Mkapa na yenyewe ikaweka rekodi ya kuipa dini moja majengo ya chuo kikuu. Leo hii kipo chuo kikuu cha waislamu Morogoro kwa kutumia majengo ya serikali. Serikali ya JK imejenga shule nyingi sana za sekondari nchi nzima na sijasikia ubaguzi kwa upande wa mikoa yenye waislamu wengi. JK pia amehakikisha waislamu wanaongoza wizara ya elimu ili kuondoa malalamiko, na si kweli kwamba eti asiyekuwa mwislamu akiwa waziri wa elimu, basi waislamu wanashindwa kusoma. Hakuna ukweli hapa.

6. Najua kuna malalamiko mengi kuhusu shule na hata hospitali za misheni, lakini tuzitendee haki. Hizi ni za kuhudumia Watanzania wote, na ndiko Kikwete na binti yake waliposoma, hata Mzee Makamba. Tuweni wakweli kwenye hili. Waislamu wanatibiwa kote huku, na ruzuku ndiyo mkombozi wa Mtanzania mnyonge.

WAISLAMU KWENYE VYEO NA ELIMU

7. Labda, tuje kwenye hili moja: KWA NINI HATUNA WAISLAMU WENGI KATIKA NAFASI ZA JUU SERIKALINI? Hili jambo ni la kweli lakini inabidi tujiulize swali jingine zaidi: KWA NINI KUNA MADAI KWAMBA WAISLAMU HAWAJASOMA?

8. Nianze na historia yetu. Waarabu walipokuja kwenye karne ya 13 walileta vitu kadhaa vikuu vikiwa ni dini nzuri ya Kiislamu na pili utamaduni wao wa kishenzi. Ndiyo, walileta utamaduni wa kishenzi. Utamaduni wa Kiarabu siyo dini ya Kiislamu na dini ya Kiislamu siyo utamaduni wa Kiarabu. Uislamu ndio ulioongoza elimu duniani kwenye karne ya saba na nane na hata vyuo vikuu vya kwanza duniani vilikuwa vya Waislamu, lakini si Waislamu wote hupenda elimu, kama ilivyo kwa dini zote zingine pia. Ukienda kwenye nchi za Maghrebu na baadhi ya Mashariki ya Kati, yaani Moroko, Algeria, Tunisia, Misri na zile za Uturuki, Siria, Iraki na Yodani, kuna waislamu wengi wenye elimu. Hapa Marekani wanaheshimika, mathalani, wahandisi mahiri hutoka Uturuki, Pakistan na India kwenye majimbo yenye waislamu.

9. Hali ni tofauti kabisa kule Ghuba kwenye nchi za Saudia Arabia, Yemeni, Kuwaiti, Omani, Katari, Imarata na Bahraini. Ghuba watu hawataki shule. Hawa wa Ghuba ndio walioletea ushenzi wao huu Afrika Mashariki kuanzia kule Somalia hadi Msumbiji kaskazini - kote huku kuna watu wenye utamaduni wa Ghuba wa kukataa shule. Hili liko wazi. Kwa kuwa Waarabu wa Ghuba ndio walioleta pia Uislamu, basi watu hujumuisha kwa pamoja tatizo la kukosa elimu kwa sababu za kuiga utamaduni wa Ghuba na dini nzuri ya kiislamu ambayo inajali elimu sana. Saudia watu ni vilaza watupu kiasi kwamba kuna Wamisri milioni moja na zaidi wanaofanya kazi za kisomi. Kote huko Ghuba kasoro Yemeni na Omani (kwa sababu ya umaskini wao) kuna wageni wengi ndani ya nchi kuliko wenyeji kwa sababu watu hawataki shule.

10. Waislamu wa pwani ya Tanzania, kama wenzao wote wa Somalia yote, Lamu, Malindi, Mombasa, Zanzibar, Mafia, Kilwa, Lindi na Pemba ya Msumbiji, wana utamaduni wa Waarabu wa Ghuba wa kugomea shule. Tofauti na wenzao, waislamu wa Tanzania walioko Machame na Usangi mkoani Kilimanjaro, au Bukoba, na hata wale wa kabila la Waganda (Baganda) kule Uganda, wao wanapenda shule. Maeneo yote waliyokaa Waarabu, kuanzia Bagamoyo nenda hadi Tabora/Nzega, na Ujiji, shule si mali kitu. TATIZO SI UISLAMU BALI UARABU WA GHUBA. Anayebisha hongera zake.

11. Tafiti mbili ninazozijua, nitazisaka baadaye, zinasema kwamba kwenye miaka ya nyuma kama ya 1990, pale UDSM waislamu walikuwa ni kati ya 14 - 15% ya wanafunzi wa shahada ya kwanza wote. Hiki ni kiasi kidogo mno lakini ni kidogo cha kiasi gani? Lazima tujue hili nalo, hata kwa makadirio tu.

12. Nyerere aliamua tuachane na sensa ya kupekua dini za watu kwa sababu nzuri kabisa - alitaka Watanzania tusitambuane kwa dini zetu (na makabila pia). Hivyo, ili kuweka usawa tukaanzisha msemo huu: Tanzania sisi nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo. Huu ni msemo tu na hauna usahihi. Pili, hata kama sensa ya zamani ilionesha kwamba waislamu ama wakristo au wapagani ndio wengi, haina maana yoyote leo wakati taifa letu lina watu milioni 45 hivi. Tulipata uhuru tukiwa milioni 12 na baadaye Zanzibar ikaongeza laki tatu. Watanzania hatukuwa na kelele za asilimia ngapi ni dini hii na ile. Leo zimerudi.

13. Kwa mujibu wa taarifa za kitafiti (siyo mimi), Waislamu nchini Tanzania ni theluthi moja ya watu wote. Naomba Nasser na Salim muende mkamuulize rais wetu, Jakaya Kikwete, kwamba kwa nini alipoteua mawaziri mwaka Novemba 2010 aliweka theluthi moja waislamu, na kisha manaibu akafanya hivyo hivyo? Pia, muulizeni, kwa nini alipoteua mawaziri hii juzi, aliweka 1/3 waislamu na kwenye manaibu akafanya hivyo hivyo? Kabla hamjaenda, chukueni rekodi zenu kwanza muone. Jiulizeni pia, kwa nini wajumbe wa Tume ya Kupitia Katiba ya Muungano, wale wa Bara, theluthi moja tena ni waislamu? Rais Kikwete, nijuavyo mimi, anajaribu sana kuliangalia hili suala la kelele za dini ili asiharibu nchi yetu. Anakuwa mwangalifu sana, hata kama kuna wakati anateleza. Je, mahesabu yake haya yana maana gani? Nina hakika anajua anachokifanya na kamwe hawezi kuwaonea waislamu wenzake ambao ni Watanzania kama yeye. Hawezi kufanya uonevu.

14. Zifuatazo ni taarifa zinaonesha idadi ya waumini wa kiislamu nchini Tanzania:

(i) 35% = Muslim Population in World Population Ranking.
(ii) 29 - 35% = Islam by country - Wikipedia, the free encyclopedia or The Future of the Global Muslim Population (Pew Research Center), http://pewforum.org/future-of-the-global muslim-population-preface.aspx.
(iii) 35% = Tanzania.

15. Hiyo taasisi ya kwanza ni ya kiislamu. Sijaweka za Wakristo kwa sababu sitafuti ushindani na siamini kama idadi ina maana yoyote, lakini kwa kuwa watu mnataka kupigia kelele, basi mzigo huo hapo. Mwaka jana mwanaharakati mmoja wa Tanga alikuja Marekani na akasema mkutanoni kwenye chuo kikuu kimoja kwamba waislamu ni 70% ya Watanzania wote, na pia kuna mwislamu mmoja mwenyeji wa Songea aliandika makala ya kitaaluma na akasema kwamba waislamu Tanzania ni 55% lakini akashindwa kueleza wanaishi wapi. Huyu wa 70% alishindwa pia kusema wanakaa wapi ambako hawaonekani. Pointi ni kwamba madai haya ni ya kijinga. Makala nyingine iliyoandikwa na msomi huyu Mtanzania ilisema kwamba Uganda wapo 45% na Kenya 33% na Msumbiji 40% (kama sijakosea). Hakuna popote duniani, hata kwenye mashirika ya kimataifa ya kiislamu zinapotajwa namba hizi za 55% kwa Tanzania na hao wengine wa Afrika Mashariki. Mashirika ya kiislamu yanasema kwamba Tanzania ina 30 - 35% tu. Ili kuleta amani, naomba tuseme kwamba Tanzania haina Wakristo kabisa, hata mmoja hayupo isipokuwa wale wenye madaraka serikalini. Tukumbuke pia, marais wetu wote watano wa sasa (kule Zenji na kwenye Muungano) ni waislamu.

16. Kwa nini idadi inakuwa muhimu hapa, achilia mbali kelele? Ni kwa sababu tunataka kuielewa ile 14-15% ya UDSM ambayo huenda hivi leo imeshabadilika kwa kuwa tuna vyuo vingi nchini. Tunahitaji maelezo, kwamba hao waislamu wengine wameishia wapi? Jibu lake linarudi kwenye ule UTAMADUNI WA WAARABU WA GHUBA. Hakuna mwislamu anayeonewa wala anayenyimwa shule. Mimi nimekulia na kusomea Dar es Salaam kwenye waislamu wa kutosha kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita, na JKT kabisa. Waislamu wote marafiki zangu waliokuwa wakali darasani waliendelea na elimu ya juu. Shule ya msingi tulikuwa watoto wanne machachari, mimi, Waziri, Salum na Izihaki, na wote tulifaulu. Vijana wa mwaka mmoja nyuma yetu pale Azania walikuwa na Mpemba aliyepata pointi SABA. Alikwenda tena Tambaza akawa nyuma yetu na akapata pointi TATU. Akaenda Ulaya. Hakunyimwa nafasi yoyote. Mwaka niliomaliza kidati cha sita kijana aliyeongoza Tanzania nzima alikuwa Karim, na yeye pia mwislamu. Hao wanaonyimwa wako wapi?

17. Kwa hiyo, kama 1/3 tu ndio waislamu (walau kinadharia), na pia wengi wao wako pwani kwenye utamaduni wa Ghuba usiotaka shule, tunashangaa nini wakienda wachache vyuo vikuu, tuseme 20%? Je, watakuwaje sawa serikalini na Wakristo ambao walianza utamaduni wa elimu tangu enzi hizo? Ni suala la historia tu lakini si kwamba ukiwa mwislamu huwezi kwenda shule.

OMBI

Tufanye juhudi kuwakomboa wale wote walio nyuma kielimu Tanzania. Wako wengi, kwa dini na makabila, lakini wote ni Watanzania. Walio nyuma wasiseme kuna uonevu, bali waondoe kilichowakwamisha. Hatuwezi kulinganisha utamaduni wa elimu wa watu wa Kilwa, Mafia, Rufiji na Pangani, na watu wa Moshi, Kyela, au mkoani Kagera. Tuwe wakweli. Mwenyezi Mungu hapendi waongo. Kwa nini shule za binafsi hazina pia waislamu wengi? Nani anawazuia waislamu kujenga shule Tanzania? Je, kama kweli unataka mtoto wako apate elimu safi, na amekosa nafasi ya shule ya serikali, utampeleka wapi? Pale Kinondoni Muslim? Tuseme ukweli.

Naamini tunao uwezo wa kuyatatua matatizo yetu ya kihistoria na kitamaduni na si kukaa chini kupanga vurugu kwa madai ya kuonewa. Waislamu wa Saudi Arabia hawajasoma licha ya utajiri wao. Je, hao nao waziri wao wa elimu na baraza la mitihani ni ya Tanzania? Kwani waislamu wa Uturuki, Tunisia, Misri, Senegal na Afrika Magharibi yote wana elimu?

Tutafute chanzo cha kweli cha tatizo, halafu wote tushirikiane kulitatua; wote kabisa.



[url]http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/message/15271[/URL]
 
Watu wengi wasio na elimu hukimbilia kusema kuwa WAISLAMU HAWAJASOMA!
Ukishaweza kubana watu kwenye elimu basi ni raisi sana kuwamiliki utakavyo.

Baada ya kuona idadi ya waislamu kuringanisha na wakristo inapungua kadri level ya elimu inavyoongezeka,mfano ni asilimia 15 tu ya wanafunzi wa elimu ya juu walikuwa waislamu,chuo kikuu cha UDSM kilifanya utafiti kubaini sababu ya mdororo huo. Iligundulika kuwa mfumu wa elimu wa sasa unawaathiri sana watoto wa kiislamu. Wakati mtoto hujenga uelewa wake awapo rika la shule ya msingi,miaka 6 mpaka 15 hivi,mtoto wa kiislamu hujikuta katika mifumo miwili ya Elimu inayokinzana,yaani SHULE NA MADRASA.Mwangalie mtoto wa darasa la kwanza;

  1. Shuleni anajifunza kuelewa,madrasa anafundishwa kukariri
  2. Shuleni anafundishwa kusoma Kiswahili,Madrasa anafundishwa kusoma kiarabu
  3. Shuleni anafundishwa kuandika herufi zilizoachana, Madrasa wanafundishwa maandishi yaliyoshikana
  4. Shuleni anaandika toka kushoto kwenda kulia,madrasa anatoka kulia kwenda kushoto
  5. Shuleni anajifunza elimu dunia, Madrasa anajifunza elimu akhera, n.k.

Kutokana na umri mdogo alionao, mzigo huu unamzidi uwezo,mtoto hulazimika kuelekeza nguvu zaidi upande ambao wazazi wake wanapendelea.Idadi kubwa ya wazazi hupendelea Madrasa,watoto wakifanya vyema kwenye elimu akhera husifiwa sana,lakini akifanya vyema shuleni na kuboronga madrasa huadhibiwa.Mazingira haya ni tofauti kwa mtoto wa kikristo,anachosoma sundayschool humsaidia darasani,maana husoma na kuandika kwa kiswahili.

wataalamu walipendekeza kuwa ikiwezekana,watoto waanze madrasa darasa la sita,na kama haiwezekani basi katika hatua za awali wasome na kuandika kwa kiswahili.Bahati mbaya pendekezo hilo lilikataliwa.Maamuzi mbadala yalifanyika wakati wa utawala wa Mwinyi ukiwepo uamuzi uliowanufaisha sana wakristo wa kuruhusu vyuo vikuu vya watu binafsi.

Utafiti uliofanyika hivi karibuni umeonyesha kuwa idadi ya wakristo wanaohitimu vyuo vikuu imeongezeka sana kulinganisha na waislamu. Vyuo vikuu vya serikali vimejaza wakristo,hata vyuo vya kidini wamejaa wakristo,seminari nzuri za kiislamu kama FEZA wamejaa wakristo,na hali huenda ikawa mbaya zaidi baada ya serikali kurudisha mitihani ya kuchuja ya darasa la 2, 4, na kidato cha pili. Amini usiamini kipindi pekee walichosoma sana waislamu kulinganisha na wakristo ni cha utawala wa Mwalimu Nyerere.

Haisaidii kutumia jazba kutatua tatizo hili,wakati mnamlaumu Nyerere,wakristo wanasonga mbele.Wakati mnatembea wenzenu wanakimbia. Adui mkubwa wa waislamu ni yule anayewaambia uongo kuwa sasa wanasoma wakati idadi yao inazidi kushuka.Ni vema wakatafakari upya pendekezo la wasomi wa UDSM. TAFAKARI
 
Back
Top Bottom