Tuachieni Nyerere Wetu

Tuachieni Nyerere Wetu

JULIASI KAMBARAGE NYERERE.
Wewe ndio raisi wa kwanza wa taifa hili la Tanganyika na baadae Tanzania. Umeondoka duniani miaka kumi na nne iliyopita sikumbuki walisema kwa shinikizo la nini vile. Ninakukumbuka sana na ninayakumbuka maneno yako matamu uyatoayo ukiwa mbele za watu. Umekua ukikemea UDINI, UKABILA, UMASIKINI,RUSHWA, UFISADI N.K. Mheshimiwa ningependa sana kile ulichokuwa ukikizungumza majukwaani kingekuwa ndio matendo yako halisi ila hali ilikuwa tofauti. Nakupongeza kwakuwa ulikuwa sikiongozi unaependa kujilimbikizia mali lakini karibu mateso yote tupatayo watanzania baada ya miaka 51 ya uhuru wewe ndio chanzo cha matatizo hayo. Ngoja nikukumbushe mheshimiwa miaka ile ya sabini uliwalazimisha watanzania kwenda kuishi vijiji vya ujamaa na waliogoma kama babu yangu ulimchomea nyumba yake na kuifanya familia yake ikalala nje. Wewe ndie uliyekuwa ukilazimisha watanzania wanunue betri za NATIONAL zilizotengenezwa kwenye kiwanda chako binafsi pamoja na kwamba haukuwa ruhusu watanzania kuwa na radio, uliifikisha nchi sehemu mbaya mpaka watu wakafikia kula nyasi. Ulikuwa haudhamini ELIMU na uliwaruhusu wachache kusoma tena kwa maagizo ya kuja kuendeleza fikra zako. Wewe ndie uliyetaifisha mali za watu na taasisi na kuwarudishia wengine na kuwanyima wengine. Wewe ulikuwa dikteta mbaya sana uliyewaua kila uliowaona wanamawazo kinyume na yakwako. Ulikuwa unapenda kusikika wewe tu na kutajwa pekeyako na viongozi wengine waliokuwa nawe hukutamani wasikike. Tanzania mpaka leo inasheria kandamizi katika katiba uliyotengeneza wewe mwenyewe pasi kuwashirikisha watanzania. Leo magazeti yanafungiwa kwa sheria zilezile kandamizi ulizoziweka dikteta wewe. Najisikia uchungu kuendelea kuandika kwani sijui niandike lipi niache lipi.
 
th
th


Sote tunajua kwamba unapozungumzia historia ya TZ . huachi kuyataja majina ya watu wawili. Mwalimu nyerere na hayati Karume.Kila wakati nasikia Chadema wao wanakimbilia kwa mwalimu na sijabahatika kuwaona Viongozi wakuu wa Chadema kama DK SLAA na Mbowe wakihudhuria katika kaburi la Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania (hayati Karume)


th
 
nikuenzi na kusimamia msingi ilioachwa na waasisi hawa wawili tundio la msingi ....habari ya makuburi sion tija yake kama usimamii misingi...
 
Si hawataki muungano? Sasa Cdm ijihusishe na rais wa nchi za nje ili iweje?
 
Kwani kati ya karume na Nyerere ni nani baba wa taifa? Mtangazeni basi na karume kuwa makamu baba wa taifa!
 
Karume sio mwasisi wa taifa lolote lile duniani,

Mapinduzi hakuyafanya wala kuyaongoza yeye,

Siku ya mapindizi yeye alikuwa viunga vya Jiji la maraha la Daslamu.

Baba wa taifa la Zanzibar ni John Okello a.k.a Field Marshal
 
Miongoni mwa wana CCM ni Nyerere tu ambaye hakuwa na magamba!
 
mbona huko wanadhuru?

Misingi na maadili ya viongozi ndivyo vitu vya kuenzi sio kwenda makaburini. Lakini hata wakienda kuzuru makaburi ulitaka watangaze kuwa tunaenda ? Kama walienda kwa Mwalimu na wewe ukajua basi hiyo ni publicity ya vyombo vya habari na sio wao japo si tija sana. Kuna watu wengi wamezuru kaburi la Nyerere lakini matendo yao na kauli zao haviahakisi maudhui na maadili ya Mwalimu
 
Mambo ya ajabu haya karume ni mwasisi wa Taifa gani? ana tofauti gani na mkuu wa mkoa katika nchi ya Tanzania? mbona hata wazanzibar hawamwiti baba wa Taifa kwa taarifa yako Karume hata Uganda hajulikani acha siasa za kijinga halafu Nyerere anaenziwa kwa misingi aliyoisimamia Karume unaweza ukatueleza sisi vijana alifanya nini kwa watanzania?
 
Mambo ya ajabu haya karume ni mwasisi wa Taifa gani? ana tofauti gani na mkuu wa mkoa katika nchi ya Tanzania? mbona hata wazanzibar hawamwiti baba wa Taifa kwa taarifa yako Karume hata Uganda hajulikani acha siasa za kijinga halafu Nyerere anaenziwa kwa misingi aliyoisimamia Karume unaweza ukatueleza sisi vijana alifanya nini kwa watanzania?
labda dini yake haiwavutii chadema
 
Waende wakafanye nn zanzbr?nyerere mkristu karume muislam.
 
Dini ni tofauti hakuna cha kuficha.
 
Back
Top Bottom