Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Status
Not open for further replies.
Nimekuwa nafuatilia mjadala hasa wa Rais Mtukufu bwana Magufuli kuhusu mishahara ya watumishi kuwa mikubwa.

KIMSINGI Nadhani rais ana nia njema ya kujenga moyo wa uzalendo kwa watu ili watangulize maslahi ya Taifa kwanza na yao binafsi yaje baadae.

Tatizo langu nikwamba watu wengi tumejikita zaidi kumshambulia Nehemia Mchechu CEO wa NHC. Eti tu kwa kiwango tunachokiita kikubwa cha mshahara wa M35. Wengi wetu hatuzungumzii Mchechu alikutoka alikuwa analipwa 26M.

Na alianza project ya kujenga nyumba akiwa kwenye taasisi yake ya zamani. So serikali iliona atafunika NHC zaidi kwasababu ni wazi shirika lilishakuwa kinapumulia mipira.

NHC kifupi ikishakaribia kufa Bwana Mchechu hakuomba kazi NHC serikali ilimfuata. Mchechu amefanya kazi kubwa sana NHC ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo. Mchechu anastahili kulipwa zaid ya hapoo.

NHC ni shirika la 3 now kwa Ubora wa mashirika ya Nyumba africa lakwanza NHS ya SA yapili Ethiopia na Tatu Tanzania. Sasa mnataka huyu kijana wa watu afanye nini? Watu wanaongea hoja ya nyumba za NHC kuwa za bei kali sio za watu wa hali ya Chini.

Thats true but we have to know kwamba Sera ya NHC haijawahi kuwa na sera hiyo ya nyumba za bei nafuu kwa watu wa Hali ya Chini. Hakuna mahala popote NHC iliwekwaa kwaajili ya kujenga makazi ya Wanyonge.

So kama kuna watu tunahitaji NHC iwe ya wanyonge ni kuwakumbusha watunga Sera wetu wakabadili sera ya NHC kuacha kujiendesha kibiashara. Mchechu hata kwa hako ka M30 anatuhurumia tuu.

Wenye vyeo kama chake huko kwenye taasisi aliyotoka sasa hivi wanakula mpaka M75. Ifike mahali tusisukumwe kwa wivu pekee juu ya Mchechu tuache wivu tumuache afanye kazi.
Wewe ni jipu. Yaani nchi hii-hii yenye baraza la mitihani la taifa yaani NECTA linashindwa kulipa posho za walimu, asikari na mgambo walio simamia NECTA FORM IV 2015, mpaka leo na hizo posho zimekuwa deni la taifa. Harafu shirika lingine la umma la nchi hii - hii linamulipa mkurugenzi wake milioni 35 kwa mwezi harafu wewe unaona kama kawaida, aseee. Posho ile ilikuwa 40,000 kwa siku na kwa siku 8 tu, NECTA mpaka leo hawajalipa wanasubiri wahusika waandamane. Harafu wewe unaleta habari zako hapa. Kama anaona hatandewi haki aache kazi vijana wenye weledi kuliko hata huyo Mchechu ni wengi muno nchi hii, yeye arudi huko alikutoka akalipwe hiyo M75, na siyo aendelee kutuibia kwa habari zenu mbofu - mbofu. Watanzania acheni unafiki. Nitashangaa sana kuona mkurugenzi wa NIDA anatubuliwa harafu huyu Mchechu ambaye within 3 years anaingiza more than 1.2 billion kwa mshahara tu ukiaacha posho anazo jilipa. Ikifuatiliwa vizuri yawezekana posho zikazidi mshahara maana wakati wa Kikwete Tanzania ilikuwa imegeuzwa shamba la bibi. Nakuhakikishia huyu jamaa akibaki harafu Rais Magufuli akatumbuwa majipu mengine, 2020 atakuwa sehemu ya kampeni.
 
Angaliwe upya! Hana haja ya mshahara wote huo, maana anachokifanya sio faida kwa Watanzania walio wengi!

Mtu kama Mkurugenzi wa Muhimbili Hosp alistahili kulipwa zaidi ya Mchechu, maana anaokoa maisha ya watu!
 
Basi sawa...mimi nikiwa miongoni mwa wananchi wa kawaida NILICHOKISHIKILIA AKILINI ni maneno ya Lukuvi: "NHC jengeni nyumba za bei nafuu za bei nafuu kweli"
 
M35 kwa mwezi hivi huyo si jui nani???anakazi ngumu kumshinda mwalimu wa chekechea..???????

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu kwanza sina ukaribu nae kwa namna yoyote ila namSupport kama Mtanzania mwenzangu anaeThubutu kufanyakazi ninachopinga humu wengi wanaendekeza uSWAHILI
Kama mshahara wake unalingana na anachokizalisha kwenye shirika kwa utendaji wake mzuri.....basi hapo hakuna tatizo ila kama mshahara wake mkubwa hauendani na utendaji wa kampuni kwa maana ya faida...basi hastahili kulipwa hicho kiwango......
 
Nimekuwa nafuatilia mjadala hasa wa Rais Mtukufu bwana Magufuli kuhusu mishahara ya watumishi kuwa mikubwa.

KIMSINGI Nadhani rais ana nia njema ya kujenga moyo wa uzalendo kwa watu ili watangulize maslahi ya Taifa kwanza na yao binafsi yaje baadae.

Tatizo langu nikwamba watu wengi tumejikita zaidi kumshambulia Nehemia Mchechu CEO wa NHC. Eti tu kwa kiwango tunachokiita kikubwa cha mshahara wa M35. Wengi wetu hatuzungumzii Mchechu alikutoka alikuwa analipwa 26M.

Na alianza project ya kujenga nyumba akiwa kwenye taasisi yake ya zamani. So serikali iliona atafunika NHC zaidi kwasababu ni wazi shirika lilishakuwa kinapumulia mipira.

NHC kifupi ikishakaribia kufa Bwana Mchechu hakuomba kazi NHC serikali ilimfuata. Mchechu amefanya kazi kubwa sana NHC ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo. Mchechu anastahili kulipwa zaid ya hapoo.

NHC ni shirika la 3 now kwa Ubora wa mashirika ya Nyumba africa lakwanza NHS ya SA yapili Ethiopia na Tatu Tanzania. Sasa mnataka huyu kijana wa watu afanye nini? Watu wanaongea hoja ya nyumba za NHC kuwa za bei kali sio za watu wa hali ya Chini.

Thats true but we have to know kwamba Sera ya NHC haijawahi kuwa na sera hiyo ya nyumba za bei nafuu kwa watu wa Hali ya Chini. Hakuna mahala popote NHC iliwekwaa kwaajili ya kujenga makazi ya Wanyonge.

So kama kuna watu tunahitaji NHC iwe ya wanyonge ni kuwakumbusha watunga Sera wetu wakabadili sera ya NHC kuacha kujiendesha kibiashara. Mchechu hata kwa hako ka M30 anatuhurumia tuu.

Wenye vyeo kama chake huko kwenye taasisi aliyotoka sasa hivi wanakula mpaka M75. Ifike mahali tusisukumwe kwa wivu pekee juu ya Mchechu tuache wivu tumuache afanye kazi.
Tena hawa wenye mishahara mikubwa kama hii ndio mchwa tunaowatafuta.........

Dawa yao inachemka, hebu watajeni mchwa wote tuwajue
 
Ndugu yangu acha kulialia tafuta HELA unamlalamikia NEHEMIA kwani yeye ndio kawasababishia uMASKINI watanzani? Tatizo ccm
NHC imeingiza hazina kiasi gani cha pesa kama faida tangu aishike. Yeye ni banker, investment alizozifanya kwa niaba ya watanzania zina tija? NHC ina madeni kiasi gani? Nyumba wanazopangisha zinafanyiwa matengenezo yoyote kama wanavyofanya wenye nyumba wengine. Naomba Lukuvi akague hizi properties Mchechu alizoziridhi. Zitakazo kutwa vizuri wapangaji wenyewe wamekarabati. Lakini ni hizi hizi nyumba zinazomuweka mjini na kumpa huo mshahara aliouona ni haki yake.

Huu ni ulafi wa aina gani? wakati anajua mwalimu anapata laki tano, daktari anayeokoa maisha anapata labda milioni mbili? Kodi ya nyumba halipi, gari linajazwa mafuta na bila shaka hela ya entertainment anapewa.

Shame on him.

I however respect your stand on this matter. So let's agree to disagree.
 
Acha kukariri... Kuna vijana wengi tu wananunua hizo nyumba...

Na wengine wananunua alafu wanawapangishia vijana wanalipa kodi za mwezi kidogo kidogo..
Hao vijana wako wamepata pesa wapi?
 
Mpendwa je kuna mahali Mhe. Rais ametaja jina la Msechu???

Queen Esther

Haya mwambieni mheshimiwa rais ampige chini Mchechu kwasababu ya milioni 35 tu kisha amtafute Mzungu azibe nafasi yake huku akilipwa milioni 70 kwa mwezi,maana hii ndiyo mentality ya Mbongo kuchukia mafanikio ya Mbongo mwenzie,lkn kwa wageni wala hatuna neno.
 
Nena kweli ni muhimu kujua NHC imeingiza hazina kiasi gani hadi leo na mabiashara makubwa makubwa wanayofanya.

Queen Esther

NHC imeingiza hazina kiasi gani cha pesa kama faida tangu aishike. Yeye ni banker, investment alizozifanya kwa niaba ya watanzania zina tija? NHC ina madeni kiasi gani? Nyumba wanazopangisha zinafanyiwa matengenezo yoyote kama wanavyofanya wenye nyumba wengine. Naomba Lukuvi akague hizi properties Mchechu alizoziridhi. Zitakazo kutwa vizuri wapangaji wenyewe wamekarabati. Lakini ni hizi hizi nyumba zinazomuweka mjini na kumpa huo mshahara aliouona ni haki yake.

Huu ni ulafi wa aina gani? wakati anajua mwalimu anapata laki tano, daktari anayeokoa maisha anapata labda milioni mbili? Kodi ya nyumba halipi, gari linajazwa mafuta na bila shaka hela ya entertainment anapewa.

Shame on him.

I however respect your stand on this matter. So let's agree to disagree.
 
Kwa hio shirika linajenga nyumba kwa watu "MATAJIRI"

Asilimia 95 ya watanzania ni MASIKINI

Hizo nyumba zina Umuhimu gani kwa wananchi?

Halafu...Mchechu aliomba jkazi NHC sema alibebwa na Luhanjo...sio kwamba alifuatwa

CBA Bank ndipo alipotoka....CBA bank haijawahi kuwa na mradi wa kujenga Nyumba

Come to Basics....Huwezi kulipa wakurugenzi mashahara zaidi ya Rais...Never.....Sio kwenye Public sector
Kwani raisi analipwa tsh.ngapi?
 
Naona umeamua kumchonganisha Mhe. Rais na Msechu kwa kusema Mhe. Rais anamuonea wivu???

Pili Mimi sikumsikia Mhe. Rais akitaja jina la Msechu. Kama kuna Ma CEO wengi wanalipwa hivi, ni kwanini kila mtu kamngangania Msechu??

Queen Esther
Hahitaji kutaja jina, hata kama hatuhui kusoma bado tuna macho tunaona.
 
Inaonekana naww ni muathilika wa uPUUZI wa CCM kwamba NCHI hii maskini bakini hapo hapo mkiwa na Fulana za kijani na njano
Kwenye Red ni wazi Lowassa hakukosea kusema Elimu, Elimu, Elimu.
Kwenye Bold nikufahamishe tu kwangu hakuna kitu chochote chenye rangi ya kijani na Njano, hata mswaki huwezi kukuta.
 
Aliyeharibu ni Mkwere alichukua watu akawalete na mishahara yao ambayo iko nje ya scheme of service ya hizi taasisi ndio maana malalamiko hayataisha maana wasaidizi wake department directors amewaacha gap la hatari.
Kikwete aliamua kusaka brain! Lkn ktk free labour market, lazima ufanye competition na taasisi nyingine lkn pia ukate jeuri ya mtu unayemtaka!
We unadhani ktk miaka 5 Sugu atatumia kiasi gani cha fedha za umma? Anaweza kuzalisha nini ktk kipindi chote hicho?
Kuna wabunge wangapi wa viti maalum? We unadhani wanaweza kuzalisha nini nchini?
Mi nadhani kuna saa tuangalie zaidi tunayemsajii kuliko kuropoka tu, juu ya mshahara ilhali huyo mtu anazalisha Mara 1,000,000 zaidi ya anachotumia!
 
Watu wana wivu tu na mchechu. Hata rais ana wivu na mchechu.

Watu kibao wanalipwa zaidi ya mchechu ila hawaongelewi. Mchechu yamemkuta hayo kisa tu alikua team lowassa.

Yule mama wa tanzania investment centre anakula 38+m, na wengine wa dawasco,tpdc,tcra,rea nk ila hawaguswi.

Ni wivu tu kwa mchechu. Sioni sababu ya kumuonea wivu mchechu.
Wakati nafanya kazi Barrick Gold Mine, chief wangu alikuwa analipwa 18m na mimi nalipwa laki 8. Nkaona huu ni upuuzi kabisa. mimi naamka asubuhi, naingia site naleta data, mtu kaka kusubiria kuprocess data zangu, afu mie ujira ananizidi mara kumi na kitu. Huo ndo tunasema ubinafsi. Mnaomtetea jamaa, hiyo hela ni kubwa mno. Sasa wa chini yake analipwaje? gap kubwa sana sema mna macho but hamuoni. Hata hizo Agency zingine, huo woote ni wizi tu kwa watanzania wengine. Isitoshe, hizo nafasi wawaachie wengine pia maana wameshatosheka nao. wameshakusanya sana, waachie wengine nao wakusanye.
 
Sasa hizo data unaenda wewe tu kujitafutia au unapewa mwongozo wa namna ya kuzipata hizo data?anyway kwa utaratibu wa makampuni na management zao ulivyo ni kwamba kadri unavyokwenda juu ktk ladder ya uongozi na ndivyo mzigo wa shughuli unavyopungua na malipo yanavyoongezeka,nyinyi huku chini mnafanya kazi nyingi malipo kidogo kwasababu mna maarifa kidogo.Hamjui hata kwanini kampuni husika inafanya vizuri kibiashara,kuna watu wanakesha wakiumiza vichwa wafanyaje kampuni yao iendelee kutawala soko husika au kuongeza wateja wapya au kuwalinda wateja waliopo.
Wakati nafanya kazi Barrick Gold Mine, chief wangu alikuwa analipwa 18m na mimi nalipwa laki 8. Nkaona huu ni upuuzi kabisa. mimi naamka asubuhi, naingia site naleta data, mtu kaka kusubiria kuprocess data zangu, afu mie ujira ananizidi mara kumi na kitu. Huo ndo tunasema ubinafsi. Mnaomtetea jamaa, hiyo hela ni kubwa mno. Sasa wa chini yake analipwaje? gap kubwa sana sema mna macho but hamuoni. Hata hizo Agency zingine, huo woote ni wizi tu kwa watanzania wengine. Isitoshe, hizo nafasi wawaachie wengine pia maana wameshatosheka nao. wameshakusanya sana, waachie wengine nao wakusanye.
 
Tena hiyo ndogo sana... Mchechu anastahili kulipa Million 70 kama wanavyolipwa DG wengine...
Mimi ndiye nilibainisha huo mshahara kwenye mitandao. Kwa nafasi niliyonayo, nina rekodi ya mishahara yote ya Ma-DG wa sekta ya umma. Kwa kukusaidia tu, hakuna DG wa sekta ya umma ambae anafikia kiwango cha Mchechu katika mshahara...achilia mbali marupurupu...By the way, wengi wenu hata hamjui Mchechu aliingia vipi NHC....Ngoja tuwape info kwa uchache tu.

Mchechu ana undugu na aliyewahi kuwa katibu mkuu kiongozi, bwana Luhanjo. Mchechu alipata kuwa CEO katika umri mdogo kabisa, akiwa na miaka 29 tu, katika sekta ya taasisi za kifedha (wakati huo alianza KBC, CBA).

Wakati aliyekuwa DG wa NHC anastaafu, serikali ilijidhatiti kumtafuta DG mpya....Luhanjo ndio akatumia hiyo fursa kumuunganisha Mchechu kwa waziri Chiligati wakati huo akiwa waziri mwenye dhamana ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi...(wote tunajua Mchechu hakustaili kuwa DG wa NHC kutokana na kukosa vigezo).....Rejea matangazo ya serikali kuhusu nafasi za kazi kwa ngazi za u-DG (hata hiyo ya NHC ilitangazwa mwaka 2010 kwenyw magazeti...na ilitaka minimum qualification iwe Masters).....mara zote minimum qualificafion ni Masters...Mchechu amekuwa DG wa NHC akiwa na undergraduate degree....Mambo ya Chiligati na Luhanjo hayo. Hivyo kijana pamoja na kukosa sifa, alichukuliwa hivyo hivyo na kufanywa DG wa NHC.....Na suala la mshahara pia likafanyiwa mabadiliko ili kukidhi matakwa ya kijana (kinyume kabisa na sheria ya NHC ya mwaka 1990)....Kwa maneno mengine, bodi ilishinikizwa na katibu mkuu kiongozi kupitia kwa waziri kuidhinisha malipo hayo ya mshahara wa milioni 35 kwa mwezi.

Sina muda wa kumaliza ishu zote kuhusu NKM....Nikipata nafasi nitaeleza kwa kirefu ili watu muelewe. Ila kwa kumalizia tu, uwepo wa Mchechu NHC ni suala la muda tu.
 
Wakati nafanya kazi Barrick Gold Mine, chief wangu alikuwa analipwa 18m na mimi nalipwa laki 8. Nkaona huu ni upuuzi kabisa. mimi naamka asubuhi, naingia site naleta data, mtu kaka kusubiria kuprocess data zangu, afu mie ujira ananizidi mara kumi na kitu. Huo ndo tunasema ubinafsi. Mnaomtetea jamaa, hiyo hela ni kubwa mno. Sasa wa chini yake analipwaje? gap kubwa sana sema mna macho but hamuoni. Hata hizo Agency zingine, huo woote ni wizi tu kwa watanzania wengine. Isitoshe, hizo nafasi wawaachie wengine pia maana wameshatosheka nao. wameshakusanya sana, waachie wengine nao wakusanye.
kipindi huyo Chief wako yeye anasota shuleni kupata maarifa nahisi wewe ulikua una unga unga life kitaani... asa hivi ana anza kula matunda ya elimu yake unaona kama mnastahili kua ktk level moja au kukaribiana....

ata Socrates alishasema katika jamii kuna matabaka... kuna watu wao ni chuma wengine ni Silva na wengine ni Dhahabu!!!

Acha kila mtu ale kwa ujanja na utashi wa "mchungaji" wake.... maana ukisema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake... unaweza ukafungwa kamba ndefu ila mchungaji wako akawa amekufunga katika eneo la jangwa sasa sijui utakula nini apo..??!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom