Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Status
Not open for further replies.
Hivi Tanzania hii iliyojaa wananchi wakulima na wafanyakazi wanaoishi kwa mlo mmoja kwa siku wapo watu wanaofanya kazi kwenye ofisi za umma wanapokea mshahara wa milioni moja kwa siku?!! Miloni 30 kwa mwezi katika nchi maskini ambayo wananchi walio wengi hawapati matibabu, wanafunzi wanakaa sakafuni kwa kukosa madawati!! Aibu sana kudai mishahara ya aina hiyo hata kama MTU kasoma sana na ana CV kama ya Waziri Muhongo! Tufike mahali tuwafikirie Watanzania wenzetu wanaolala hoi.
 
Tshs 32 millions. ....inasemwa which is 400 mn a year
Huo mshahara ulioutaja si wa Waziri Mkuu!? Kauliza kuhusu Rais, kama hujuini vema ukasema hujui.
Na hata waziri Mkuu hakamati hiyo pesa, ni zaidi ya hiyo.
 
Huo mshahara ulioutaja si wa Waziri Mkuu!? Kauliza kuhusu Rais, kama hujuini vema ukasema hujui.
Na hata waziri Mkuu hakamati hiyo pesa, ni zaidi ya hiyo.
mimi nimesema na nimetaja ninachokijua...wewe unakuja hapa na Vapor...Taja hicho unachokijua wewe
 
Nimekuwa nafuatilia mjadala hasa wa Rais Mtukufu bwana Magufuli kuhusu mishahara ya watumishi kuwa mikubwa.

KIMSINGI Nadhani rais ana nia njema ya kujenga moyo wa uzalendo kwa watu ili watangulize maslahi ya Taifa kwanza na yao binafsi yaje baadae.

Tatizo langu nikwamba watu wengi tumejikita zaidi kumshambulia Nehemia Mchechu CEO wa NHC. Eti tu kwa kiwango tunachokiita kikubwa cha mshahara wa M35. Wengi wetu hatuzungumzii Mchechu alikutoka alikuwa analipwa 26M.

Na alianza project ya kujenga nyumba akiwa kwenye taasisi yake ya zamani. So serikali iliona atafunika NHC zaidi kwasababu ni wazi shirika lilishakuwa kinapumulia mipira.

NHC kifupi ikishakaribia kufa Bwana Mchechu hakuomba kazi NHC serikali ilimfuata. Mchechu amefanya kazi kubwa sana NHC ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo. Mchechu anastahili kulipwa zaid ya hapoo.

NHC ni shirika la 3 now kwa Ubora wa mashirika ya Nyumba africa lakwanza NHS ya SA yapili Ethiopia na Tatu Tanzania. Sasa mnataka huyu kijana wa watu afanye nini? Watu wanaongea hoja ya nyumba za NHC kuwa za bei kali sio za watu wa hali ya Chini.

Thats true but we have to know kwamba Sera ya NHC haijawahi kuwa na sera hiyo ya nyumba za bei nafuu kwa watu wa Hali ya Chini. Hakuna mahala popote NHC iliwekwaa kwaajili ya kujenga makazi ya Wanyonge.

So kama kuna watu tunahitaji NHC iwe ya wanyonge ni kuwakumbusha watunga Sera wetu wakabadili sera ya NHC kuacha kujiendesha kibiashara. Mchechu hata kwa hako ka M30 anatuhurumia tuu.

Wenye vyeo kama chake huko kwenye taasisi aliyotoka sasa hivi wanakula mpaka M75. Ifike mahali tusisukumwe kwa wivu pekee juu ya Mchechu tuache wivu tumuache afanye kazi.

Give us a break! Miradi yote ya mchechu ni white elephant; hata JK pamoja na udhaifu wake aliwahi kuwauliza hizo nyumba wanazojenga za gharama kubwa hivyo wanamjengea nani?!
 
Wanajiimarisha na familia zao binafsi. Wengi wa mameneja wa nhc wana magorofa ya apartment kkoo. Refer tu yule admin manager wao mwemye bar pale maji machafu mikocheni. Wana mashule ya international rfer Shule fulani huko mbezi makonde
 
Wewe ni jipu. Yaani nchi hii-hii yenye baraza la mitihani la taifa yaani NECTA linashindwa kulipa posho za walimu, asikari na mgambo walio simamia NECTA FORM IV 2015, mpaka leo na hizo posho zimekuwa deni la taifa. Harafu shirika lingine la umma la nchi hii - hii linamulipa mkurugenzi wake milioni 35 kwa mwezi harafu wewe unaona kama kawaida, aseee. Posho ile ilikuwa 40,000 kwa siku na kwa siku 8 tu, NECTA mpaka leo hawajalipa wanasubiri wahusika waandamane. Harafu wewe unaleta habari zako hapa. Kama anaona hatandewi haki aache kazi vijana wenye weledi kuliko hata huyo Mchechu ni wengi muno nchi hii, yeye arudi huko alikutoka akalipwe hiyo M75, na siyo aendelee kutuibia kwa habari zenu mbofu - mbofu. Watanzania acheni unafiki. Nitashangaa sana kuona mkurugenzi wa NIDA anatubuliwa harafu huyu Mchechu ambaye within 3 years anaingiza more than 1.2 billion kwa mshahara tu ukiaacha posho anazo jilipa. Ikifuatiliwa vizuri yawezekana posho zikazidi mshahara maana wakati wa Kikwete Tanzania ilikuwa imegeuzwa shamba la bibi. Nakuhakikishia huyu jamaa akibaki harafu Rais Magufuli akatumbuwa majipu mengine, 2020 atakuwa sehemu ya kampeni.
Unaonaje tukianza kupunguza Mishahara ya maRAIS wastaafu na maWAZIRI WAKUU wanaokausha HAZINA ya TAIFA badala ya huyo MCHECHU
 
Angaliwe upya! Hana haja ya mshahara wote huo, maana anachokifanya sio faida kwa Watanzania walio wengi!

Mtu kama Mkurugenzi wa Muhimbili Hosp alistahili kulipwa zaidi ya Mchechu, maana anaokoa maisha ya watu!
Mkurugenzi wa MUHIMBILI analipwa shilingi ngapi
 
Kama mshahara wake unalingana na anachokizalisha kwenye shirika kwa utendaji wake mzuri.....basi hapo hakuna tatizo ila kama mshahara wake mkubwa hauendani na utendaji wa kampuni kwa maana ya faida...basi hastahili kulipwa hicho kiwango......
Mkuu we we unaonaje kuna cha maana anachozalisha au Hakuna...nivipi Kabla ya kupewa huo uKURUGENZI hamkuwahi kulalamika kwanini iwe sasa...Ukiona wanakujadili ujue wamekukubali
 
NHC imeingiza hazina kiasi gani cha pesa kama faida tangu aishike. Yeye ni banker, investment alizozifanya kwa niaba ya watanzania zina tija? NHC ina madeni kiasi gani? Nyumba wanazopangisha zinafanyiwa matengenezo yoyote kama wanavyofanya wenye nyumba wengine. Naomba Lukuvi akague hizi properties Mchechu alizoziridhi. Zitakazo kutwa vizuri wapangaji wenyewe wamekarabati. Lakini ni hizi hizi nyumba zinazomuweka mjini na kumpa huo mshahara aliouona ni haki yake.

Huu ni ulafi wa aina gani? wakati anajua mwalimu anapata laki tano, daktari anayeokoa maisha anapata labda milioni mbili? Kodi ya nyumba halipi, gari linajazwa mafuta na bila shaka hela ya entertainment anapewa.

Shame on him.

I however respect your stand on this matter. So let's agree to disagree.
Ndugu yangu hebu nisaidie wewe umewahi kufanyabiashara yoyote hata ya kuuza mtumba tu....!! unazungumzia madeni...!! Kudaiwa kwenye biashara unaona ajabu?...umewahi kwenda kwenye Ofisi zao ukawauliza kama kuna faida gani wamepata....!! Tambueni jambo 1kwanza kwenye biashara kubwa kama zile kuadaiwa ndio sehemu ya Biashara...unategemea majengo wanayojenga Hela iwe Ruzuku kutoka Serikalini...acheni haya Mambo maneno mengi hayasasidii hii...NCH tungekuwa na ..uchungu kweli CCM wasingeendelea kuchaguliwa tangu tupate UHURU
 
inamaana katika watanzania wote hakuna anayeweza kufanya hiyo kazi,yeye ana kipi cha ziada??

Nimekuwa nafuatilia mjadala hasa wa Rais Mtukufu bwana Magufuli kuhusu mishahara ya watumishi kuwa mikubwa.

KIMSINGI Nadhani rais ana nia njema ya kujenga moyo wa uzalendo kwa watu ili watangulize maslahi ya Taifa kwanza na yao binafsi yaje baadae.

Tatizo langu nikwamba watu wengi tumejikita zaidi kumshambulia Nehemia Mchechu CEO wa NHC. Eti tu kwa kiwango tunachokiita kikubwa cha mshahara wa M35. Wengi wetu hatuzungumzii Mchechu alikutoka alikuwa analipwa 26M.

Na alianza project ya kujenga nyumba akiwa kwenye taasisi yake ya zamani. So serikali iliona atafunika NHC zaidi kwasababu ni wazi shirika lilishakuwa kinapumulia mipira.

NHC kifupi ikishakaribia kufa Bwana Mchechu hakuomba kazi NHC serikali ilimfuata. Mchechu amefanya kazi kubwa sana NHC ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo. Mchechu anastahili kulipwa zaid ya hapoo.

NHC ni shirika la 3 now kwa Ubora wa mashirika ya Nyumba africa lakwanza NHS ya SA yapili Ethiopia na Tatu Tanzania. Sasa mnataka huyu kijana wa watu afanye nini? Watu wanaongea hoja ya nyumba za NHC kuwa za bei kali sio za watu wa hali ya Chini.

Thats true but we have to know kwamba Sera ya NHC haijawahi kuwa na sera hiyo ya nyumba za bei nafuu kwa watu wa Hali ya Chini. Hakuna mahala popote NHC iliwekwaa kwaajili ya kujenga makazi ya Wanyonge.

So kama kuna watu tunahitaji NHC iwe ya wanyonge ni kuwakumbusha watunga Sera wetu wakabadili sera ya NHC kuacha kujiendesha kibiashara. Mchechu hata kwa hako ka M30 anatuhurumia tuu.

Wenye vyeo kama chake huko kwenye taasisi aliyotoka sasa hivi wanakula mpaka M75. Ifike mahali tusisukumwe kwa wivu pekee juu ya Mchechu tuache wivu tumuache afanye kazi.
 
Mkuu nakuhakikishia... laiti ungejua kuna watanzania wanalipwa zaidi ya mchechu usingeshangaa. Tena ni mabosi wa mashirika ya uma.... Mchechu anazungumzwa sana kwa kuwa mshahara wake umewekwa wazi afu ikajulikana ni team Edoboy.
Shida si team Lowasa shida ni wastaafu waliokuwa kwenye nyumba za NHC ambao waligeuza kuwa nyumba zao.
Sasa mchechu anawataka walipie pango. Pia viongozi wengi walikuwa wanamiliki nyumba za NHC hata zaidi ya tano.
 
Nena kweli ni muhimu kujua NHC imeingiza hazina kiasi gani hadi leo na mabiashara makubwa makubwa wanayofanya.

Queen Esther
Rafiki ukiulizia hapa sidhani kama utapata hizo taarifa maana utasubiri sana...NHC kwa kuwa nishirika la UMA naww nimmiliki so unaweza kwenda kwenye Ofisi zao naamini watakupatia majibu yote ya maswali yako
 
Hivi Tanzania hii iliyojaa wananchi wakulima na wafanyakazi wanaoishi kwa mlo mmoja kwa siku wapo watu wanaofanya kazi kwenye ofisi za umma wanapokea mshahara wa milioni moja kwa siku?!! Miloni 30 kwa mwezi katika nchi maskini ambayo wananchi walio wengi hawapati matibabu, wanafunzi wanakaa sakafuni kwa kukosa madawati!! Aibu sana kudai mishahara ya aina hiyo hata kama MTU kasoma sana na ana CV kama ya Waziri Muhongo! Tufike mahali tuwafikirie Watanzania wenzetu wanaolala hoi.
Sasa ndugu yangu unataka kusema Mchechu ndio kawapa umaskini watanzania?....kwanini tusianzie kwa wale jamaa wa ndiyooo.....ambao ndio watunga SERA
 
"Serikali ikamfuata huko na kumuomba kuwa CEO...................."

Pambafu kabisa, yani yeye ni mkubwa luliko serikali? Hakuna mtanzania yeyote anayeweza kufanya kazi kama yake na kulipwa salary inayoendana na scheme za serikali?

Usikute katika hiyo 35m anachukua 25 iliyobali inaingia katka beneficiaries wa aliyemtoa huko alikokua!
Labour and professionalism ni commodity, bei yake hutegemea ubora wake na mahitaji ya soko. Watanzania wengi wanadhani mshahara huamuliwa na akili na kiwango cha elimu. Kitu ambacho ni kosa kubwa.

Mshahara huamuliwa na performance. Nini output yako. Unaweza kuwa na akili kama shetani, unaweza kuwa na PhD lakini mshahara wako ukazidiwa na mwenye diploma. Unapokuwa performer, unatafutwa, hutafuti kazi. Kwa sababu umetafutwa una-dictate terms. Kama hutaki terms zake unaachana nae, ataendelea na wengine.

Na nina hakika Msechu kutoka kwa mwajiri wake wa awali, na kwa kuijua serikali ilivyo kigeugeu atakuwa alijiwekea ulinzi wa kutosha wa kiajira. Na mkitaka kumtoa hapo, unaweza kulazimika kumlipa mshahara wake wa sasa kwa mwaka mzima au miaka miwili. Halafu unamlipa leo, kesho utamsikia ameajiriwa Ethiopia, Nigeria au SA. Kwa kuifanya NHC kuwa katika nafasi ya ubora katika Afrika, huyo mkurugenzi ni wa kutafutwa tu, hatalazimika kutafuta kazi. Ndivyo biashara za kisasa zinavyotaka.

Kuna wakati nilikuwa nalipwa mshahara wa $8,000, nilipofanikiwa kuongoza timu yangu na kupata mradi uliokuwa na thamani zaidi ya $4 billion, ndani ya wiki moja nilitafutwa na makampuni manne tofauti, kila mmoja na offer yake. Mimi niliweka terms za ajira, pamoja na mambo mengine, mshahara niliweka $16,000, mwajiri akaamua kunilipa $19,700. Tukazanie performane ili tuwe na nguvu katika kupanga mishahara.

Kwenye biashara za kisasa kinachoangaliwa unazalisha kiasi gani nawe unachukua kiasi gani. Mkurugenzi wa kwanza alikuwa anazalisha negative TZS 3 billion halafu analipwa TZS 5 million. Huyu alikuwa aghali zaidi kibiashara kuliko Msechu.
"Serikali ikamfuata huko na kumuomba kuwa CEO...................."

Pambafu kabisa, yani yeye ni mkubwa luliko serikali? Hakuna mtanzania yeyote anayeweza kufanya kazi kama yake na kulipwa salary inayoendana na scheme za serikali?

Usikute katika hiyo 35m anachukua 25 iliyobali inaingia katka beneficiaries wa aliyemtoa huko alikokua!
 
Ndugu yangu hebu nisaidie wewe umewahi kufanyabiashara yoyote hata ya kuuza mtumba tu....!! unazungumzia madeni...!! Kudaiwa kwenye biashara unaona ajabu?...umewahi kwenda kwenye Ofisi zao ukawauliza kama kuna faida gani wamepata....!! Tambueni jambo 1kwanza kwenye biashara kubwa kama zile kuadaiwa ndio sehemu ya Biashara...unategemea majengo wanayojenga Hela iwe Ruzuku kutoka Serikalini...acheni haya Mambo maneno mengi hayasasidii hii...NCH tungekuwa na ..uchungu kweli CCM wasingeendelea kuchaguliwa tangu tupate UHURU
Asingeleta maringo (nadhani "nyodo" ina apply zaidi) wakati anacheza na pesa yetu. Akiingiza hasara tutakao umia ni sisi, maana kosa la namna hii mahakamani miaka 3 jela, halafu community service na ka-fine. Watoto wetu wataendelea kukaa chini na kodi tutakamuliwa zaidi kulipia hasara aliyotuingiza. Yeye ni msomi au sio? Hakujua kwamba sio kila mtu ana high tolerance ya ufisadi na madudu mengine?

Kuna vitu viwili vikuu tunavyotakiwa kumuomba Mungu kwa bidii zote, hekima na unyenyekevu.
 
inamaana katika watanzania wote hakuna anayeweza kufanya hiyo kazi,yeye ana kipi cha ziada??
Shirika ni lasiku nyingi Mchechu siamepewa miaka ya hivi karibuni tu.....Jaribu kufatilia kabla hajapewa huyo jamaa na aliekuwa kabla yake
 
Asingeleta maringo (nadhani "nyodo" ina apply zaidi) wakati anacheza na pesa yetu. Akiingiza hasara tutakao umia ni sisi, maana kosa la namna hii mahakamani miaka 3 jela, halafu community service na ka-fine. Watoto wetu wataendelea kukaa chini na kodi tutakamuliwa zaidi kulipia hasara aliyotuingiza. Yeye ni msomi au sio? Hakujua kwamba sio kila mtu ana high tolerance ya ufisadi na madudu mengine?

Kuna vitu viwili vikuu tunavyotakiwa kumuomba Mungu kwa bidii zote, hekima na unyenyekevu.
Inaweza ikawa nikweli hiki ulichoandika lkn kama ni Mchechu kupewa mshahara mkubwa Kwanini tusianze na Viongozi wastaafu?....maRAIS na maWAZIRI wakuu wastaafu....ambao wamefanyakazi kipindi chao kimekwisha lkn mpaka sasa wanaendelea kulipwa...Kwanini tumlalamikie MCHECHU peke yake ambae anaishi kwa kutumia ELIMU yake hapa ndio maana sisi wengine tunasema Mfumo wetu umeoza tunahitaji Katiba itakayotunyoshea Mambo kumwambia Mchechu apunguziwe mshahara bila kuwa na utaratibu unaoeleweka inakuwa CHUKI tu kwa mtu rejea issue ya ZITTO kukataa Posho bungeni nikweli hachukui lkn kuna Impact gani kwakutochukua posho so ili twende sawa tuache kuSupport upuuzi wa CCM wananchi wanataka Katiba wao wanatuletea ILANI yao then kuna mijitu inafurahia....
 
Shirika ni lasiku nyingi Mchechu siamepewa miaka ya hivi karibuni tu.....Jaribu kufatilia kabla hajapewa huyo jamaa na aliekuwa kabla yake
hicho sio kigezo,makosa yalianza pale serekali ilipomfuata na kumuangukia,kazi ingetangazwa then watu washindanishwe,ingekuwa ndo hivyo sasa kuna maana gani ya watu kusoma??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom