Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Status
Not open for further replies.

Kangambili K

Member
Jan 16, 2016
17
17
Nimekuwa nafuatilia mjadala hasa wa Rais Mtukufu bwana Magufuli kuhusu mishahara ya watumishi kuwa mikubwa.

KIMSINGI Nadhani rais ana nia njema ya kujenga moyo wa uzalendo kwa watu ili watangulize maslahi ya Taifa kwanza na yao binafsi yaje baadae.

Tatizo langu nikwamba watu wengi tumejikita zaidi kumshambulia Nehemia Mchechu CEO wa NHC. Eti tu kwa kiwango tunachokiita kikubwa cha mshahara wa M35. Wengi wetu hatuzungumzii Mchechu alikutoka alikuwa analipwa 26M.

Na alianza project ya kujenga nyumba akiwa kwenye taasisi yake ya zamani. So serikali iliona atafunika NHC zaidi kwasababu ni wazi shirika lilishakuwa kinapumulia mipira.

NHC kifupi ikishakaribia kufa Bwana Mchechu hakuomba kazi NHC serikali ilimfuata. Mchechu amefanya kazi kubwa sana NHC ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo. Mchechu anastahili kulipwa zaid ya hapoo.

NHC ni shirika la 3 now kwa Ubora wa mashirika ya Nyumba africa lakwanza NHS ya SA yapili Ethiopia na Tatu Tanzania. Sasa mnataka huyu kijana wa watu afanye nini? Watu wanaongea hoja ya nyumba za NHC kuwa za bei kali sio za watu wa hali ya Chini.

Thats true but we have to know kwamba Sera ya NHC haijawahi kuwa na sera hiyo ya nyumba za bei nafuu kwa watu wa Hali ya Chini. Hakuna mahala popote NHC iliwekwaa kwaajili ya kujenga makazi ya Wanyonge.

So kama kuna watu tunahitaji NHC iwe ya wanyonge ni kuwakumbusha watunga Sera wetu wakabadili sera ya NHC kuacha kujiendesha kibiashara. Mchechu hata kwa hako ka M30 anatuhurumia tuu.

Wenye vyeo kama chake huko kwenye taasisi aliyotoka sasa hivi wanakula mpaka M75. Ifike mahali tusisukumwe kwa wivu pekee juu ya Mchechu tuache wivu tumuache afanye kazi.
 
Kwani yeye tu ndio CEO ambaye shirika lake lina mchango mkubwa? Kwanza sijui NHC inachangia kiasi gani kwenye pato la taifa. Kwa hoja yako basi DG wa TANAPA ndo anatakiwa ale hela ndefu maana tourism ina mchango mkubwa kwenye GDP ya nchi.
 
DG wa TANAPA unajua analipwa shingapi?
 
Watu wana wivu tu na mchechu. Hata rais ana wivu na mchechu.

Watu kibao wanalipwa zaidi ya mchechu ila hawaongelewi. Mchechu yamemkuta hayo kisa tu alikua team lowassa.

Yule mama wa tanzania investment centre anakula 38+m, na wengine wa dawasco,tpdc,tcra,rea nk ila hawaguswi.

Ni wivu tu kwa mchechu. Sioni sababu ya kumuonea wivu mchechu.
 
Aliyeharibu ni Mkwere alichukua watu akawalete na mishahara yao ambayo iko nje ya scheme of service ya hizi taasisi ndio maana malalamiko hayataisha maana wasaidizi wake department directors amewaacha gap la hatari.
 
Sasa ikawaje akaomba serikali iruhusu wasio raia kumiliki nyumba?

Does it ring a bell? It does to me, sounds like he didn't do market analysis kujua uwezo wa watanzania.

Mwisho wa siku tunataka kujua anachangia shilingi ngapi kwenye mfuko wa serikali Halafu Ndio tulinganishe na mshahara wake, maana usione majengo meeengi anajenga ukadhani shirika linaingiza faida kumbe pengine ni mikopo
 
Woote wenye mishahara mikubwa inapaswa ifyekwe

Hapa hatuangalii alikuwa timu nini cha muhimu alipwe mshahara wa kawaida
 
"Serikali ikamfuata huko na kumuomba kuwa CEO...................."

Pambafu kabisa, yani yeye ni mkubwa luliko serikali? Hakuna mtanzania yeyote anayeweza kufanya kazi kama yake na kulipwa salary inayoendana na scheme za serikali?

Usikute katika hiyo 35m anachukua 25 iliyobali inaingia katka beneficiaries wa aliyemtoa huko alikokua!
 
Serious alitaka wageni waruhusiwe kumiliki nyumba??

Sasa ikawaje akaomba serikali iruhusu wasio raia kumiliki nyumba?

Does it ring a bell? It does to me, sounds like he didn't do market analysis kujua uwezo wa watanzania.

Mwisho wa siku tunataka kujua anachangia shilingi ngapi kwenye mfuko wa serikali Halafu Ndio tulinganishe na mshahara wake, maana usione majengo meeengi anajenga ukadhani shirika linaingiza faida kumbe pengine ni mikopo
 
Kwani yeye tu ndio CEO ambaye shirika lake lina mchango mkubwa? Kwanza sijui NHC inachangia kiasi gani kwenye pato la taifa. Kwa hoja yako basi DG wa TANAPA ndo anatakiwa ale hela ndefu maana tourism ina mchango mkubwa kwenye GDP ya nchi.
Mkuu huko unakosema hata akilipwa 1ml nisawa tu Hao jamaa sindio wanaendaga kufanya mikutano ya BODI ULAYA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom