Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Mbona na ccm wameubadili n kuweka maneno mengine ya kumsifia maguduli.. nyie vipi.. acheni utoto
Kwahyo mnaahindana kufanya utopolo sio, CDM ka upinzani na mubadala kwanini mfanye madudu tena
 
Nimeona onyo la Msajili wa vyama akiwaonya CHADEMA kwa kitendo chao cha kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka mengine.

Mwanzo sikuchukulia serious, lakini kitendo cha kuona kuwa kumbe ni kweli CHADEMA wamebadili wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao ya uvyama vyama kwa kweli, hicho siyo kitendo cha busara na uungwana kwa Taifa.

Sote tunaisema CCM kuwa CCM ni Chama dola, kumbe kuna Chama kingine ambacho kinawaza na kuota kuwa chenyewe kiwe ndiyo Taifa Kabisaa!!. Absurd!!

Mistake kama hizi ndizo zinazoweza kuwafanya wananchi wawaone Wapinzani kama watu Fanatic, waleta vurugu, wasioheshimu alama na nembo za Taifa.

Na kwa kweli vitendo kama hivi vikionyeshwa kwa wananchi wengi, wanakuwa pissed off kwa kuwaona Wapinzani kama watu ambao ni immature!

Kuna sababu gani kwa mfano kubadili maneno ya Taifa na kuweka mengine ndani ya wimbo huo?. Kwa nini wasiimbe wimbo wa Taifa kama ulivyo ndani ya vikao vyao, kuna tatizo gani kuuchukua wimbo wa Taifa kama ulivyo?

Katika hili siwezi kuwatetea Chadema hata kidogo, Lazima waonyeshe maturity, wasiwe watu wa ushabikishabiki na bila sababu.

Hebu tazama hapa chini CHADEMA wakidistort wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao.

Mwenyekiti Mbowe Shame on you
Katibu Mkuu wa Chadema Shame on you
Tundu Lissu Shame on you

Mmetukosea wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama kwa kuleta mzaha kwenye wimbo unautuunganisha taifa zima kwa kuleta uvyamavyama(partsanship) kwenye suala hilo

Siku nyingine tumieni busara kwenye kufanya mambo, hakuna haja ya kutafuta unnecessary troubles!

Hebu tazama hapa wanavyoimba:

View attachment 1527225
Wangefanya ccm asingetoa neno, unafiki tuu
 
Walichofanya Chadema, wameimba kwanza wimbo wa Taifa...... Then wakajiimbia wimbo wao kwa kutumia tune ya wimbo wa Taifa.

Original tune ya wimbo huu wa South Africa na ulitungwa mwaka 1897. Sisi tumeiga, Zambia pia wameiga na Chadema nao wameiga.
Sahihi kabisa, ccm mnasikitisha bora mm sina chama
 
Unaweza kuweka hapa tuone alivyopost?
Alafu utofauti wenu na ccm uko wapi sasa? Kama kila kitu mnasema mbona ccm vile mara hivi,! Acheni ujinga

CHADEMA hawajilinganishi na CCM hapa. Taabu ni mbili: sheria inasemaje? Na je, Msajili anapoikemea CHADEMA anao pia ubavu wa kuikemea CCM kwa tukio linalowiana - ili kuthibitisha kuwa hana double standards?

Halafu umenishangaza kama vile unakubali kuwa kilichofanywa na CCM / Magufuli nacho ni cha kijinga kisichofaa kuigwa na CHADEMA! Hii ni sawa na kuwa tayari kuzoa maji taka kwa mikono ili tu umchafue adui anayekukera sana! punguza obsession na CHADEMA.
 
Mkuu natamani kama ungeongeza zaidi maoni yako kuhusu hili tukio.
Mimi nipo njia panda nikosoe au niafikiane na CDM.

I'm standing at the crossroads indeed.
Have you read The National Flag and Coat of Arms Act of 1971 ????
 
Taifa la chadema ndani ya taifa la Tanzania.Mambo yanaanza taratibu hivi.Mi sisemi !!!
Pia kuna taifa la Zanzibar ndani ya taifa la Tanzania, wanasiasa nao kila mmoja ana taifa lake ndani ya taifa la Tanzania, hiyo ni kawaida sana kwa nchi hii. Ila tatizo hapa ni taifa la Tanganyika kujificha ndani ya taifa la Tanzania.
 
Kafungueni kesi mahakamani kama mmekereka tuje kuwagalagaza huko huko mahakamaccm.
Tuliwahi badili wimbo wa chuo kuna beti ikisema ualimu ni wito sote tumeitikia,watu tukawa tunaimba ualimu ni kazi wote tunaisomea
 
Mlolongo wa masuala na matatizo tuliyo nayo nchini ni mkubwa kiasi kwamba ni aibu watu wanaojinasibu kama GTs kupoteza muda na tukio hili. This is a non-issue.

Nasubiri sana kuona kampeni ya CHADEMA itakavyoweka msisitizo (focus) kwenye mabadiliko ya msingi ya katiba hasa kupunguza madaraka ya Rais; kuweka mgawanyo sahihi wa madaraka kitaasisi; kuainisha muundo wa serikali na taasisi za umma na taratibu zake (sio kila Rais anajipangia serikali anavyoitaka); kurejesha nguvu ya umma kuiwajibisha serikali kupitia Bunge makini, na taratibu sahihi za uongozi wa vyombo vya dola chini ya usimamizi wa kiraia - to mention just a few critical elements.

Baadaye ndipo tuhangaike na hivyo vipodozi (cosmetics) kama wimbo wa taifa, nembo, mavazi, nk.
 
Kubadili mifuko ya suti na kuweka bendera kama Kangi Lugora si sahihi

TL kauliza, sheria gani ya nembo za Taifa imevunjwa?

Jaji Mutungi ambaye ni Jaji alipaswa kujua hili.

Nina question sana utartibu unaotumika hasa kupata wateule, mabalozi, majaji n.k.

JokaKuu
 
Nimeona onyo la Msajili wa vyama akiwaonya CHADEMA kwa kitendo chao cha kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka mengine.

Mwanzo sikuchukulia serious, lakini kitendo cha kuona kuwa kumbe ni kweli CHADEMA wamebadili wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao ya uvyama vyama kwa kweli, hicho siyo kitendo cha busara na uungwana kwa Taifa.

Sote tunaisema CCM kuwa CCM ni Chama dola, kumbe kuna Chama kingine ambacho kinawaza na kuota kuwa chenyewe kiwe ndiyo Taifa Kabisaa!!. Absurd!!

Mistake kama hizi ndizo zinazoweza kuwafanya wananchi wawaone Wapinzani kama watu Fanatic, waleta vurugu, wasioheshimu alama na nembo za Taifa.

Na kwa kweli vitendo kama hivi vikionyeshwa kwa wananchi wengi, wanakuwa pissed off kwa kuwaona Wapinzani kama watu ambao ni immature!

Kuna sababu gani kwa mfano kubadili maneno ya Taifa na kuweka mengine ndani ya wimbo huo?. Kwa nini wasiimbe wimbo wa Taifa kama ulivyo ndani ya vikao vyao, kuna tatizo gani kuuchukua wimbo wa Taifa kama ulivyo?

Katika hili siwezi kuwatetea Chadema hata kidogo, Lazima waonyeshe maturity, wasiwe watu wa ushabikishabiki na bila sababu.

Hebu tazama hapa chini CHADEMA wakidistort wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao.

Mwenyekiti Mbowe Shame on you
Katibu Mkuu wa Chadema Shame on you
Tundu Lissu Shame on you

Mmetukosea wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama kwa kuleta mzaha kwenye wimbo unautuunganisha taifa zima kwa kuleta uvyamavyama(partsanship) kwenye suala hilo

Siku nyingine tumieni busara kwenye kufanya mambo, hakuna haja ya kutafuta unnecessary troubles!

Hebu tazama hapa wanavyoimba:

View attachment 1527225
Siku zote nimekua nikimkemea yule Pepo mkuu ndani ya Chadema.

Kosa kubwa walilofanya Chadema ni kushindwa kujenga Demokrasia ya kushindana kwa hoja ndani ya Chama na matokeo yake kukosa fursa ya kupata Mwenyekiti mwingine mpya zaidi ya Mlevi ,mhuni,mlaghai ,mwizi wa ruzuku ,Mh. Mbowe.
Kumrudisha Mbowe kundelea kuongoza Chadema lilikua kosa kubwa sana la koufundi mpaka sasa.
Mbowe na ulevi wake kwa sasa hana jipya zaidi ya kifanya siasa za kitoto na matukio tu ya kuokoteza bila mipango.

Ni kweli hakuna Kosa kisheria lakini ni jambo la kejeli na kuweka mbele mavyama badala ya taifa na utaifa.
Chini ya Mbowe Chadema kikishika dola litakuwa Chama cha hovyo kuliko CCM na chenye mambo ya kihuni na kimafya sana.
Mbowe sio mtu mzuri kabisa kwenye biashara yake ya siasa . Tunataka sera sio ngonjera na mambo ya kijinga kijinga kwa ajili ya kuleta mivutano na serikali.

Mh.Mbowe sasa umekua mtu mzima na Chama chako kina zaidi ya robo Mmktarne sasa..
 
Have you read The National Flag and Coat of Arms Act of 1971 ????
Yes, I did.
According to that law there is nothing wrong in what CHADEMA has done to our National Anthem.
My dilemma comes from my knowledge of unwritten laws (customs, Judicial decisions, Common Laws).

Mambo haya yamenifanya nifuatilie kisa cha vijana wa Mashahidi wa Jehova kugomea kuimba wimbo wa taifa shuleni huko Mbozi Mbeya na kukataa kuheshimu bendera ya Taifa, Vijana walishinda rufaa ya kesi yao.
 
Kubadili mifuko ya suti na kuweka bendera kama Kangi Lugora si sahihi

TL kauliza, sheria gani ya nembo za Taifa imevunjwa?

Jaji Mutungi ambaye ni Jaji alipaswa kujua hili.

Nina question sana utartibu unaotumika hasa kupata wateule, mabalozi, majaji n.k.

JokaKuu
Inawezekana ni kwa mazoea tu au Common-Law (unwritten law).
Nje ya utamaduni , desturi na maadili yetu hakuna uvunjifu wowote wa kisheria wamefanya.
Tena kwa hakika ile 'tune' au ala za ule wimbo serikali ya Tanzania hawana hati miliki yeyote na wala siyo waliobuni.

Ila naogopa sana tukianza kupuuzia desturi, tamaduni na mila zetu kwa sababu hakuna sheria iliyoandikwa rasmi na bunge ya kuzuwia jambo husika.
Mengi sana humu tunalaani huu siyo utamaduni wetu wanapotenda jambo flani viongozi wetu.
 
Hivi rais anaposema sitowapa huduma flani kwa sababu mlichagua upinzani ni sahihi? Jaji mtungi hana la kukemea hapo? wale wananchi waliochagua upinzani kodi zao zinaenda wapi? kama zinaenda upinzani hapo yuko sahihi.
 
Hahah yaani watu waache kusikitia mafao yao kucheleweshwa,ajira tangu 2015 hazitolewi kwa vijana wanaotoka mavyuoni,nyongeza za mishahara hakuna eti waje waonyeshwe clip ya wimbo wasikitike?

Hahah Nimecheka kifalaaa aisee.
Nadhani wanaokomalia hiyo kitu wanasababu zao, ila sio wimbo wa kwanza kupigwa marufuku.
 
Back
Top Bottom