Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Nimeona onyo la Msajili wa vyama akiwaonya CHADEMA kwa kitendo chao cha kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka mengine.

Mwanzo sikuchukulia serious, lakini kitendo cha kuona kuwa kumbe ni kweli CHADEMA wamebadili wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao ya uvyama vyama kwa kweli, hicho siyo kitendo cha busara na uungwana kwa Taifa.

Sote tunaisema CCM kuwa CCM ni Chama dola, kumbe kuna Chama kingine ambacho kinawaza na kuota kuwa chenyewe kiwe ndiyo Taifa Kabisaa!!. Absurd!!

Mistake kama hizi ndizo zinazoweza kuwafanya wananchi wawaone Wapinzani kama watu Fanatic, waleta vurugu, wasioheshimu alama na nembo za Taifa.

Na kwa kweli vitendo kama hivi vikionyeshwa kwa wananchi wengi, wanakuwa pissed off kwa kuwaona Wapinzani kama watu ambao ni immature!

Kuna sababu gani kwa mfano kubadili maneno ya Taifa na kuweka mengine ndani ya wimbo huo?. Kwa nini wasiimbe wimbo wa Taifa kama ulivyo ndani ya vikao vyao, kuna tatizo gani kuuchukua wimbo wa Taifa kama ulivyo?

Katika hili siwezi kuwatetea Chadema hata kidogo, Lazima waonyeshe maturity, wasiwe watu wa ushabikishabiki na bila sababu.

Hebu tazama hapa chini CHADEMA wakidistort wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao.

Mwenyekiti Mbowe Shame on you
Katibu Mkuu wa Chadema Shame on you
Tundu Lissu Shame on you

Mmetukosea wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama kwa kuleta mzaha kwenye wimbo unautuunganisha taifa zima kwa kuleta uvyamavyama(partsanship) kwenye suala hilo

Siku nyingine tumieni busara kwenye kufanya mambo, hakuna haja ya kutafuta unnecessary troubles!

Hebu tazama hapa wanavyoimba:

 
Hata mimi napinga, lakini siku ukianza kupinga magari ya Serikali kuwekewa private namba na kutumiwa na Chama, wafungwa kupandisha bendera za chama, wafanyakazi wa umma wanaomlinda rais kuvalishwa sare za chama, na mgombea wa chama kutokupewa ulinzi wa umma na kutambulika kama raisi mteule kabla ya kupigiwa kura tutakua tumefika pazuri pa kutengeneza mfumo utakao tulinda na yote haya. Na siku hiyo nitakuunga mkono asilimia 100
 
Makosa yanajirudia mara mbili ndan ya wiki uwanja wa taifa walikiuka itifaki

Mkutano wao wamenajisi wimbo wa taifa


Watetez wao wanakuambia eti sio msitali ya biblia au msaafu

Huu ni utetezi wa watu wasio jua nembo yao ya taifa ni pamoja na wimbo wa taifa

Siku mkipewa nchi si mtabadili na rangi ya bendera mnaweka yenu ndio iwe ya taifa

Tuwe makini na vitu tunavyo tetea
 
Hata mimi napinga ila ni vizuri kuwe na mizania sawa kwenye hayo makatazo.
View attachment 1527227

Hii video uliyoweka, hawa wanaoimba wana nafasi gani ndani ya CCM, Je kitendo chao kilikuwa endorsed na CCM, au ni rogue elements tu zimeamua kuimba?

Anyway,. makosa mawili hayafanyi kosa lisiwe kosa.

hebu linganisha kosa lifanywe na Baraza kuu zima la Chadema, Mwenyekiti akiwepo, katibu mkuu yupo na mgombea uraisi yupo nao wanashiriki kudistort wimbo wa Taifa.

Yaani Baraza kuu zima la Chadema, mbele ya mwenyekiti, na katibu mkuu wake pamoja na wajumbe wanashiriki kudistort wimbo wa Taifa

Hizi video mbili hazilingani aisee!
 
Back
Top Bottom