Sevenjr
Member
- Aug 3, 2018
- 32
- 127
TAHADHARI: Kama huna akili timamu usisome!
_______________________________
Kuhusu kuzuiliwa kwa ndege yetu huko Canada, swali la msingi la kujiuliza ndege zetu zitaendelea kuzuiliwa mpaka lini? Hii ni ndege ya 3 tangu zimeanza kuzuiliwa.
Ya kwanza ilizuiwa Canada kufuatia kesi iliyofunguliwa na kampuni ya ukandarasi ya Sterling Construction and Engineering Ltd (SCEL), nyingine ilizuiliwa Afrika Kusini kufuatia kesi iliyofunguliwa na mkulima Hermanus Steyn, na huyohuyo ndiye amezuia tena ndege hii ya sasa.
Tukitaka kuwa WAZALENDO wa kweli tutafute suluhu ya kudumu ya tatizo hili. Nimemsikiliza Prof. Kabudi akiongea na Rais JPM kwa kujibagaza kama kawaida yake. Akijitutumua na kuongea kwa tashwishwi na tamathali nyingi za semi, lakini hajatoa suluhisho la kudumu, badala yake ameishia kumpotosha Rais.
Kabudi ameongea kana kwamba tatizo la msingi ni Canada, na amefanikiwa kushawishi Watanzania waamini hivyo. Akafika mbali na kusema alimuita Balozi wa Canada na kumwambia eti serikali imekasirika sana (hii kauli ya kifutuhi tuipuuze. Tuhesabu tu kwamba Kabudi alitaka kufurahisha umati kama kawaida yake).
Lakini je, tatizo ni Canada? Jibu ni HAPANA. Tatizo si Canada, si Afrika Kusini, wala si Chato. Tatizo la msingi ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya serikali na serikali kuangukia pua. Kwa hiyo badala ya kudeal na Canada tudeal na kesi hizo. Unless otherwise ndege zetu zinaweza kukamatiwa hata Burundi.
Kwa mfano kesi iliyoshikilia ndege kwa sasa ni ya mkulima Hermanus Steyn. Huyu alikua mlowezi aliyemiliki mashamba makubwa sana ya kilimo mkoani Arusha. Mwaka 1982 serikali ya Nyerere ikataifisha mashamba yake, magari yake 250, ndege ndogo 12, mifugo na majengo.
Akafungua kesi mahakamani hapahapa nchini akidai fidia ya $36M. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi na kumgrant "tuzo" hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo. Ikaunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mali zilizotaifishwa. Kamati hiyo iliongozwa na Mzee Chenge na Mkulo, ikapendekeza alipwe $20M kinyume na "tuzo" aliyopewa na mahakama ya $36M.
Serikali ya Rais Mwinyi ikamlipa $20M kama ilivyopendekezwa na kamati ya akina Chenge. Wakati huo sarafu yetu bado ilikua na nguvu. $20M zilikua kama TZS 44M hivi kwa wakati huo. Mkulima Steyn akapewa lakini hakuridhika. Akaendelea kudai kiasi kilichobakia. Na amekua akidai tangu wakati huo hadi sasa bila kulipwa. Kiasi kilichobakia kilikua $16M lakini kutokana na kukaa kwa muda mrefu pamoja na riba kimefika $33M, sawa na TZS 70 Bilioni kwa sasa.
Serikali ya Tanzania ilipoona anasumbua sana kudai fedha hizo ikampiga marufuku kukanyaga ardhi ya Tanzania. Steyn akaona atapoteza haki yake. Akachukua hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa ushindi na kwenda kusajili tuzo yake katika Mahakama ya Afrika kusini. The Arbitration Act, cap.15 inamruhusu kufanya hivyo.
Akaomba mali za serikali ya Tanzania zilizopo Afrika kusini zikamatwe ili kufidia deni lake. Kifungu cha 30 cha sheria hiyo kinatoa masharti ya kufanya hivyo (conditions for enforcement of foreign awards). Na ndipo ndege yetu aina ya Airbus A220-300 ilipozuiwa nchini humo.
Lakini ikaachiwa baada ya mahakama ya Guateng kujiridhisha kuwa Hermanus alikosea kusajili "tuzo" yake mahakamani hapo (procedural irregularities). Sasa mkulima huyo amesajili "tuzo" hiyo nchini Canada, na ndio maana ndege yetu nyingine imekamatwa.
Jambo ambalo Kabudi anapotosha kwa makusudi ni kusema kuwa tulimshinda mkulima Hermanus Steyn on merit. Uongo mtupu. Kama tulishinda on merit why the matter is not res judicata?
Hatukumshinda Steyn on merit. Yani hatukumshinda katika kesi ya msingi ya kutaka alipwe fedha anazotudai. Tulimshinda kwa "technicalities" za kisheria (procedural irregularities) baada ya yeye kukosea kusajili tuzo hiyo kwenye mahakama ya Guateng.
Kwa lugha rahisi ni kwamba Hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa Hermanus tuzo ya $36M bado haijabatilishwa. Na Hermanus anaweza kuisajili tuzo hiyo katika nchi yoyote ya Jumuiya ya Madola. Kwahiyo hata ndege ikiachiwa Canada, anaweza kusajili tuzo yake India, Kenya, Zambia, Australia, au nchi yoyote yenye mali za Tanzania zinazoweza kufikia thamani ya tuzo hiyo, na mali hizo kukamatwa.
Kwahiyo Kabudi anapoishangaa Canada, ni kukosa umakini tu. Ameongea kama "layman" ambaye hajui sheria kabisa. Vijana wa LLB1 pale UDSM, Mzumbe au SAUT wanamshangaa.
Mali zetu zimekamatwa zaidi Canada kwa sababu ndio nchi yenye mali nyingi za Tanzania kwa sasa (ndege zote za Bombadier zinatengenezwa huko). Hata Brazil ambapo Kabudi anashauri tukanunue ndege, zinaweza kukamatwa pia kama Steyn akiamua kwenda kusajili tuzo yake kwenye mahakama za huko.
Hivyo basi, tunahitaji kupata suluhisho la kudumu badala ya kupiga 'ngonjera' kwamba kuna Watanzania wanatumiwa na mabeberu kutuhujumu. Hakuna cha "beberu" wala "mbuzi jike" anayetuhujumu, ni makosa yetu wenyewe. Tutafute mbinu za kuyatatua badala ya kujificha kwenye visingizio vya mabeberu. Na tusimpotoshe Mheshimiwa Rais.
Nini kifanyike?
1. Serikali imuondolee mkulima Hermanus Steyn marufuku iliyompiga ya kuingia nchini. Ikumbukwe anahangaika huko nje kwa sababu amezuiwa kuja nchini. Kabla hajapigwa marufuku ya kuja Tanzania alikuwa anakuja kudai haki yake hapa. Alipozuiwa ndipo akaamua kuichukua "tuzo" yake mahakama kuu na kwenda kuisajili huko nje.
2. Kamati ya Chenge na Mkulo iitwe na kuulizwa msingi wa kupendekeza Steyn alipwe kiasi kidogo tofauti na "tuzo" aliyopewa na mahakama kuu. Kama sababu hizo zitakua na mashiko, zitumiwe kumshawishi Steyn akubali kiasi alicholipwa na kufuta shauri hilo mahakamani.
3. Kama serikali haikubaliani na option hizo mbili hapo juu, basi ikate rufaa au iombe "judicial review" kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya kumpa Steyn tuzo ya $36M. Na maamuzi yatakayotolewa kwenye rufaa hiyo yaheshimiwe na pande zote mbili.
Vinginevyo tutaishia kuwalaumu "mabeberu", kesho tutawalaumu "majogoo", keshokutwa tutawalaumu "mitetea" pasi na sababu zozote za msingi. Kama mkulima huyu kudai haki yake ni ubeberu basi Mahakama Kuu ya Tanzania ndio beberu kuu maana ndiyo iliyompa ushindi wa tuzo hiyo. Tuache porojo. Tudeal na msingi wa tatizo.
Tuanzie na sababu za Nyerere kutaifisha mali za Steyn, kisha twende kwenye hukumu iliyotolewa na mahakama kuu na kumpa ushindi. Then tumalizie na ripoti ya kamati ya akina Chenge. Halafu tumuite Steyn tukae nae mezani tuyamalize. Tuache kurukaruka kama maharage yaliyokosa maji.!
Imeandikwa na Malisa GJ