• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Tuache kujibagaza, tukitaka kuwa wazalendo wa kweli tutafute suluhu ya kudumu dhidi ya mkulima Steyn

Sevenjr

Sevenjr

Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
26
Points
150
Sevenjr

Sevenjr

Member
Joined Aug 3, 2018
26 150
TAHADHARI: Kama huna akili timamu usisome!
_______________________________

Kuhusu kuzuiliwa kwa ndege yetu huko Canada, swali la msingi la kujiuliza ndege zetu zitaendelea kuzuiliwa mpaka lini? Hii ni ndege ya 3 tangu zimeanza kuzuiliwa.

Ya kwanza ilizuiwa Canada kufuatia kesi iliyofunguliwa na kampuni ya ukandarasi ya Sterling Construction and Engineering Ltd (SCEL), nyingine ilizuiliwa Afrika Kusini kufuatia kesi iliyofunguliwa na mkulima Hermanus Steyn, na huyohuyo ndiye amezuia tena ndege hii ya sasa.

Tukitaka kuwa WAZALENDO wa kweli tutafute suluhu ya kudumu ya tatizo hili. Nimemsikiliza Prof. Kabudi akiongea na Rais JPM kwa kujibagaza kama kawaida yake. Akijitutumua na kuongea kwa tashwishwi na tamathali nyingi za semi, lakini hajatoa suluhisho la kudumu, badala yake ameishia kumpotosha Rais.

Kabudi ameongea kana kwamba tatizo la msingi ni Canada, na amefanikiwa kushawishi Watanzania waamini hivyo. Akafika mbali na kusema alimuita Balozi wa Canada na kumwambia eti serikali imekasirika sana (hii kauli ya kifutuhi tuipuuze. Tuhesabu tu kwamba Kabudi alitaka kufurahisha umati kama kawaida yake).

Lakini je, tatizo ni Canada? Jibu ni HAPANA. Tatizo si Canada, si Afrika Kusini, wala si Chato. Tatizo la msingi ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya serikali na serikali kuangukia pua. Kwa hiyo badala ya kudeal na Canada tudeal na kesi hizo. Unless otherwise ndege zetu zinaweza kukamatiwa hata Burundi.

Kwa mfano kesi iliyoshikilia ndege kwa sasa ni ya mkulima Hermanus Steyn. Huyu alikua mlowezi aliyemiliki mashamba makubwa sana ya kilimo mkoani Arusha. Mwaka 1982 serikali ya Nyerere ikataifisha mashamba yake, magari yake 250, ndege ndogo 12, mifugo na majengo.

Akafungua kesi mahakamani hapahapa nchini akidai fidia ya $36M. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi na kumgrant "tuzo" hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo. Ikaunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mali zilizotaifishwa. Kamati hiyo iliongozwa na Mzee Chenge na Mkulo, ikapendekeza alipwe $20M kinyume na "tuzo" aliyopewa na mahakama ya $36M.

Serikali ya Rais Mwinyi ikamlipa $20M kama ilivyopendekezwa na kamati ya akina Chenge. Wakati huo sarafu yetu bado ilikua na nguvu. $20M zilikua kama TZS 44M hivi kwa wakati huo. Mkulima Steyn akapewa lakini hakuridhika. Akaendelea kudai kiasi kilichobakia. Na amekua akidai tangu wakati huo hadi sasa bila kulipwa. Kiasi kilichobakia kilikua $16M lakini kutokana na kukaa kwa muda mrefu pamoja na riba kimefika $33M, sawa na TZS 70 Bilioni kwa sasa.

Serikali ya Tanzania ilipoona anasumbua sana kudai fedha hizo ikampiga marufuku kukanyaga ardhi ya Tanzania. Steyn akaona atapoteza haki yake. Akachukua hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa ushindi na kwenda kusajili tuzo yake katika Mahakama ya Afrika kusini. The Arbitration Act, cap.15 inamruhusu kufanya hivyo.

Akaomba mali za serikali ya Tanzania zilizopo Afrika kusini zikamatwe ili kufidia deni lake. Kifungu cha 30 cha sheria hiyo kinatoa masharti ya kufanya hivyo (conditions for enforcement of foreign awards). Na ndipo ndege yetu aina ya Airbus A220-300 ilipozuiwa nchini humo.

Lakini ikaachiwa baada ya mahakama ya Guateng kujiridhisha kuwa Hermanus alikosea kusajili "tuzo" yake mahakamani hapo (procedural irregularities). Sasa mkulima huyo amesajili "tuzo" hiyo nchini Canada, na ndio maana ndege yetu nyingine imekamatwa.

Jambo ambalo Kabudi anapotosha kwa makusudi ni kusema kuwa tulimshinda mkulima Hermanus Steyn on merit. Uongo mtupu. Kama tulishinda on merit why the matter is not res judicata?

Hatukumshinda Steyn on merit. Yani hatukumshinda katika kesi ya msingi ya kutaka alipwe fedha anazotudai. Tulimshinda kwa "technicalities" za kisheria (procedural irregularities) baada ya yeye kukosea kusajili tuzo hiyo kwenye mahakama ya Guateng.

Kwa lugha rahisi ni kwamba Hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa Hermanus tuzo ya $36M bado haijabatilishwa. Na Hermanus anaweza kuisajili tuzo hiyo katika nchi yoyote ya Jumuiya ya Madola. Kwahiyo hata ndege ikiachiwa Canada, anaweza kusajili tuzo yake India, Kenya, Zambia, Australia, au nchi yoyote yenye mali za Tanzania zinazoweza kufikia thamani ya tuzo hiyo, na mali hizo kukamatwa.

Kwahiyo Kabudi anapoishangaa Canada, ni kukosa umakini tu. Ameongea kama "layman" ambaye hajui sheria kabisa. Vijana wa LLB1 pale UDSM, Mzumbe au SAUT wanamshangaa.

Mali zetu zimekamatwa zaidi Canada kwa sababu ndio nchi yenye mali nyingi za Tanzania kwa sasa (ndege zote za Bombadier zinatengenezwa huko). Hata Brazil ambapo Kabudi anashauri tukanunue ndege, zinaweza kukamatwa pia kama Steyn akiamua kwenda kusajili tuzo yake kwenye mahakama za huko.

Hivyo basi, tunahitaji kupata suluhisho la kudumu badala ya kupiga 'ngonjera' kwamba kuna Watanzania wanatumiwa na mabeberu kutuhujumu. Hakuna cha "beberu" wala "mbuzi jike" anayetuhujumu, ni makosa yetu wenyewe. Tutafute mbinu za kuyatatua badala ya kujificha kwenye visingizio vya mabeberu. Na tusimpotoshe Mheshimiwa Rais.

Nini kifanyike?

1. Serikali imuondolee mkulima Hermanus Steyn marufuku iliyompiga ya kuingia nchini. Ikumbukwe anahangaika huko nje kwa sababu amezuiwa kuja nchini. Kabla hajapigwa marufuku ya kuja Tanzania alikuwa anakuja kudai haki yake hapa. Alipozuiwa ndipo akaamua kuichukua "tuzo" yake mahakama kuu na kwenda kuisajili huko nje.

2. Kamati ya Chenge na Mkulo iitwe na kuulizwa msingi wa kupendekeza Steyn alipwe kiasi kidogo tofauti na "tuzo" aliyopewa na mahakama kuu. Kama sababu hizo zitakua na mashiko, zitumiwe kumshawishi Steyn akubali kiasi alicholipwa na kufuta shauri hilo mahakamani.

3. Kama serikali haikubaliani na option hizo mbili hapo juu, basi ikate rufaa au iombe "judicial review" kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya kumpa Steyn tuzo ya $36M. Na maamuzi yatakayotolewa kwenye rufaa hiyo yaheshimiwe na pande zote mbili.

Vinginevyo tutaishia kuwalaumu "mabeberu", kesho tutawalaumu "majogoo", keshokutwa tutawalaumu "mitetea" pasi na sababu zozote za msingi. Kama mkulima huyu kudai haki yake ni ubeberu basi Mahakama Kuu ya Tanzania ndio beberu kuu maana ndiyo iliyompa ushindi wa tuzo hiyo. Tuache porojo. Tudeal na msingi wa tatizo.

Tuanzie na sababu za Nyerere kutaifisha mali za Steyn, kisha twende kwenye hukumu iliyotolewa na mahakama kuu na kumpa ushindi. Then tumalizie na ripoti ya kamati ya akina Chenge. Halafu tumuite Steyn tukae nae mezani tuyamalize. Tuache kurukaruka kama maharage yaliyokosa maji.!

Imeandikwa na Malisa GJ
2220181_FB_IMG_1574570206690.jpeg
2220183_FB_IMG_1574570185632.jpeg
 
Wizzdude

Wizzdude

Senior Member
Joined
Apr 4, 2015
Messages
152
Points
250
Wizzdude

Wizzdude

Senior Member
Joined Apr 4, 2015
152 250
Ukweli mchungu. Najua kuna watu hawapendi kuusikia ila ndio uhalisia huo.
 
Kawe Alumni

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
5,788
Points
2,000
Kawe Alumni

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
5,788 2,000
Wasaliti wa Nchi wajiandae kisaikolojia
 
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Messages
4,158
Points
2,000
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2012
4,158 2,000
Hik serikali ya masifa na matapeli sana yaani ni mishen town flani wanaotembea mchana kuonekana nadhifu na wenye hela kumbe wanamkwepa mwenye nyumba kwa kudaiwa kodi.

Hawa mabwana walitudanganya kuwa mkulima hatudai na tumemshibda kwa hoja za wanasheria nguli zaidi ya 20

Tulivyoletewa hoja hizo kumbe walidai mkulima alishikilia ndege ya rais na inavyombo vya kiusalama na nyaraka za siri.

Kumbe ndege iliachiwa kwa kuwa ilionekana ni ya rais na inatumika na rais.

Na South hukumu ilitoka amri ya magogoni kwa madiba kuonewa huruma na ule ubaguz ikaachiwa na ikarudi empty bila hata kubeba raia kukimbia isije zuiwa tena.

Huko Canada wanakojua sheria wameikamata wanaitwa mabeberu kama ulushinda kesi na zaid ni prof wa sheria analialia nini? Si akajibu kisheria au dawa ya deni si kulipa?

Kama tuna hela si tulipe kama videni vidogo tuko ivi madeni makubwa je?
 
No retreat no surrender

No retreat no surrender

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Messages
1,790
Points
2,000
No retreat no surrender

No retreat no surrender

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2018
1,790 2,000
Unapoleta madai nyeti kama haya inabidi ubalance pande zote. Tunajua mawakili wake huyu mzungu na wanaoleta ukimbelembele wa madai haya ni hawa wenye majina ya akina MALISA.
Kwanza tuambie huyo mzungu hayo malaki ya maekari aliyapataje? Ni mzawa?

Alipora hiyo ardhi ya umma kwa unyonyaji wa kikoloni ndo maana Nyerere akaitaifisha. Hata hivyo kwavile baadhi ya ardhi alikuwa ameishaiendeleza na Mali zinazohamishika kama magari, ndege ndogo za tours, n.k. ndo maana Nyerere akamuachia kiasi fulani cha ekari (nyingi tu) kama fidia ya mali zinazohamishika na Huyo mzungu akutaka kuendelea na mgogoro na serikali ya Tanzania akakubali yaishe.

Nyie akina Malisa wapiga deal kwavile mnajua mna 10% ndo mnalianzisha ili mpige hela. Sasa sikia, kwa serikali hii kama kulipa italipa lakini sio rahisi kihivyo. Tunajua mnakopa hela nyingi tena kwa riba kufungua kesi ugenini mkidhani mtalipwa kirahisi na kurejesha mkopo.

Hiyo hela ina mawili kulipwa au kutolipwa: Kwanza huyo mzungu alishalipwa dola mil.20 na mwinyi ni zaidi ya miaka 35 hivi. Pili huyo mzungu aliachiwa hekari kibao na bado anazo anaendelea kuzimiliki. Sasa nyie mnataka cash kusudi mpate 10% lakini huyo mzungu anajua itakula kwake maana atanyanganywa ardhi ndo maana alikubali yaishe. Endelea kupima joto la serikali hii mkidhani mtapata hela ya bure. Why now?

Kwani nchi haina mali nje ya nchi miaka hiyo yoote mbona hazijawahi kuzuiwa? ATCL haikuwa na International routes kabla ya kufilisika mbona hatukusikia hawamu ya Mkapa, na Kikwete ndege zetu zikikamatwa?

Baadhi ya balozi zetu nje ya nchi hayo majengo tumejenga wenyewe ni mali zetu mbano hayajawahi kiwekewa kofuli kufidia? Nchi ina gold deposits kwenye benki ya dunia kureflect paper/coin money mbona hazijawahi kushikiliwa?

Ukweli ni kwamba myanya yooote ya wizi wa mali za umma na utakatishaji wa hela chafu na madawa ya kulevya, huo mtandao JPM kausambaratisha! Endeleeni kukopa hela kuendesha kesi mtaangukia pua! Shwaini!
 
Kawe Alumni

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
5,788
Points
2,000
Kawe Alumni

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
5,788 2,000
Mabeberu Wamemshindwa kwenye karatasi sasa wanavizia mali zetu

Vibaraka wa mabeberu wanaenda kuaibika vibaya
 
N

ngusillo

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2019
Messages
853
Points
1,000
N

ngusillo

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2019
853 1,000
Hii nchi tunadanganywa sana na wanasiasa. Sasa wamepata wasaa wa kutengeneza matokeo feki ya uchafuzi wa serikali za mitaa. Kesho tutaletewa picha za 2015 kuwa misururu ilikuwa mikubwa sana.
 
Mndali ndanyelakakomu

Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2016
Messages
12,709
Points
2,000
Mndali ndanyelakakomu

Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2016
12,709 2,000
Kuna kitu tunaita ukijua unacho kifanya huwezi kupata shida

Ila ukielekezwa cha kufanya lazima ujute tuingia kwenye mtego wa wanasiasa
 
akatanyukuile

akatanyukuile

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Messages
227
Points
250
akatanyukuile

akatanyukuile

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2019
227 250
No retreat no surrender, Ufikirie upya alichokiandika malisa ni ukweli mtupu usiopingika kwann mnatumia nguvu nyingi na akiki kidogo, unadhan dawa ya deni ni ngonjera kama za kabudi, mh yetu macho
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
45,166
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
45,166 2,000
No retreat no surrender, Masikini wa fikra kama wewe ndiyo mnasababisha hiyo midege inakamatwa kila siku.

Wakili awe malisa au Dotto inabaki palepale kuwa kuwa dawa ya deni kulipa.

Kuna maandishi/ushahidi wowote kuwa mkulima ametoa tamko kuwa aliamua kupotezea deni??

Kwa nini serikali ilianza kulipa sehemu ya deni husika kama mkulima ni tapeli????
 
stella1975

stella1975

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Messages
627
Points
1,000
stella1975

stella1975

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2018
627 1,000
Wao wanatumia nguvu, sio akiri ndio maana wanailaumu Canada pasipo Kujua kuwa nchi za wenzetu hawaingiiiliii sheria wao kwa kuwa wamezoea kuingilia mihimili ndio maaana wailaumu serikali Ya Canada wakisema kwa nini Serikali Ya kanada inaruhusu haya? Sasa serikali ifanyeje?

Hata huyu mkulima akienda tu hapa Kenye serikali Ya Kenyatta haiwezi ingilia Mahakama Ya Kenya, hilo linawezekana kwa Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda ndio Hakuna mihimili inayojitegemea Yote imeshikana Kama mayoga
 
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,924
Points
2,000
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,924 2,000
Angalau law firms naweza kuwaelewa kwani wanalipwa lkn wewe mnywa mbege hata tukilipa unafaidika nini? Siajabu hata ofisi ya immmma huwezi ingia, utafukuzwa getini, ...
 
stella1975

stella1975

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Messages
627
Points
1,000
stella1975

stella1975

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2018
627 1,000
No retreat no surrender, Huyu nae Hana akiri, yani ulimsikiliza vizuri kabudi? Kama ulimsikiliza vizur nikuwa anailaumu serikali Ya Canada yani kwa akiri ndogo Kabisa hata kwa mtu ambae hajaenda shule anajua kuwa huyu hajui sheria na unagundua kuwa kumbe Tanzania swala la serikali kuingilia mhimili wa Mahakama ni kitu cha kawaida, ebu jiulize swali wewe ukiwa unamdai mtu ukaenda mahakamani kudai haki Yule uliemfungulia mashtaka utailaumu serikali? Acha kutumia nguvu kuliko akiri wenzetu wana fuata haki za kisheria hawawez mwelekeza jaji hata Siku moja ndio maaana unakuta nchi zingne Mahakama inamwiita waziri Fulani ajieleze mahakamani kutokana na matamshi yake kwa umma hapa kwetu inawezekana hilo?
 
stella1975

stella1975

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Messages
627
Points
1,000
stella1975

stella1975

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2018
627 1,000
No retreat no surrender, Nimefurahi kwa kauli yako kuwa serikali hiii italipa Lakini sio Kwa urahis hivyo, hapa sasa ndio umeonekana kutumia nguvu pasipo akiri yani ukubali kuja kulipa bilioni hamsini badala Ya bilioni 20 Lakini pia kumbuka utapata aibu kila Wakati, utapata, hasara kubwa maaana ujue ikikamatwa mnawatafuta wazungu wawe mawakiri wenu, hivi unajua pesa wanazolipwa hao mawakiri ni kiasi gani? Tumia akiri ili upunguze hasara na mlolongo
 
Mshana Jr

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
134,012
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

Platinum Member
Joined Aug 19, 2012
134,012 2,000
Kuhusu kuzuiliwa kwa ndege yetu huko Canada, swali la msingi la kujiuliza ndege zetu zitaendelea kuzuiliwa hata lini? Hii ni ndege ya 3 tangu zimeanza kuzuiliwa.

Ya kwanza ilizuiwa Canada kufuatia kesi iliyofunguliwa na kampuni ya ukandarasi ya Sterling Construction and Engineering Ltd (SCEL), nyingine ilizuiliwa Afrika Kusini kufuatia kesi iliyofunguliwa na mkukima Hermanus Steyn, na huyohuyo ndiye amezuia tena ndege hii ya sasa.

Tukitaka kuwa WAZALENDO wa kweli tutafute suluhu ya kudumu ya tatizo hili. Nimemsikiliza Prof.Kabudi akiongea na Rais JPM kwa kujibagaza kama kawaida yake. Akijitutumua na kuongea kwa tashwishwi na tamathali nyingi za semi, lakini hajatoa suluhisho la kudumu, badala yake ameishia kumpotosha Rais.

Kabudi ameongea kana kwamba tatizo la msingi ni Canada, na amefanikiwa kushawishi watanzania waamini hivyo. Akafika mbali na kusema alimuita Balozi wa Canada na kumwambia eti serikali imekasirika sana (hii kauli ya kifutuhi tuipuuze. Tuhesabu tu kwamba Kabudi alitaka kufurahisha umati kama kawaida yake).

Lakini je tatizo ni Canada. Jibu ni HAPANA. Tatizo si Canada, si Afrika kusini, wala si Chato. Tatizo la msingi ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya serikali na serikali kuangukia pua. Kwa hiyo badala ya kudeal na Canada tudeal na kesi hizo. Unless otherwise ndege zetu zinaweza kukamatiwa hata Burundi.

Kwa mfano kesi iliyoshikilia ndege kwa sasa ni ya mkulima Hermanus Steyn. Huyu alikua mlowezi aliyemiliki mashamba makubwa sana ya kilimo mkoani Arusha. Mwaka 1982 serikali ya Nyerere ikataifisha mashamba yake, magari yake 250, ndege ndogo 12, mifugo na majengo.

Akafungua kesi mahakamani hapahapa nchini akidai fidia ya $36M. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi na kumgrant "tuzo" hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo. Ikaunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mali zilizotaifishwa. Kamati hiyo iliongozwa na Mzee Chenge na Mkulo, ikapendekeza alipwe $20M kinyume na "tuzo" aliyopewa na mahakama ya $36M.

Serikali ya Rais Mwinyi ikamlipa $20M kama ilivyopendekezwa na kamati ya akina Chenge. Wakati huo sarafu yetu bado ilikua na nguvu. $20M zilikua kama TZS 44M hivi kwa wakati huo. Mkulima Steyn akapewa lakini hakuridhika. Akaendelea kudai kiasi kilichobakia. Na amekua akidai tangu wakati huo hadi sasa bila kulipwa. Kiasi kilichobakia kilikua $16M lakini kutokana na kukaa kwa muda mrefu pamoja na riba kimefika $33M, sawa na TZS 70 Bilioni kwa sasa.

Serikali ya Tanzania ilipoona anasumbua sana kudai fedha hizo ikampiga marufuku kukanyaga ardhi ya Tanzania. Steyn akaona atapoteza haki yake. Akachukua hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa ushindi na kwenda kusajili tuzo yake katika Mahakama ya Afrika kusini. The Arbitration act, cap.15 inamruhusu kufanya hivyo.

Akaomba mali za serikali ya Tanzania zilizopo Afrika kusini zikamatwe ili kufidia deni lake. Kifungu cha 30 cha sheria hiyo kinatoa masharti ya kufanya hivyo (conditions for enforcement of foreign awards). Na ndipo ndege yetu aina ya Airbus A220-300 ilipozuiwa nchini humo.

Lakini ikaachiwa baada ya mahakama ya Guateng kujiridhisha kuwa Hermanus alikosea kusajili "tuzo" yake mahakamani hapo (procedural irregularities). Sasa mkulima huyo amesajili "tuzo" hiyo nchini Canada, na ndio maana ndege yetu nyingine imekamatwa.

Jambo ambalo Kabudi anapotosha kwa makusudi ni kusema kuwa tulimshinda mkulima Hermanus Steyn on merit. Uongo mtupu. Kama tulishinda on merit why the matter is not res judicata?

Hatukumshinda Steyn on merit. Yani hatukumshinda katika kesi ya msingi ya kutaka alipwe fedha anazotudai. Tulimshinda kwa "technicalities" za kisheria (procedural irregularities) baada ya yeye kukosea kusajili tuzo hiyo kwenye mahakama ya Guateng.

Kwa lugha rahisi ni kwamba Hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa Hermanus tuzo ya $36M bado haijabatilishwa. Na Hermanus anaweza kuisajili tuzo hiyo katika nchi yoyote ya Jumuiya ya madola. Kwahiyo hata ndege ikiachiwa Canada, anaweza kusajili tuzo yake India, Kenya, Zambia, Australia, au nchi yoyote yenye mali za Tanzania zinazoweza kufikia thamani ya tuzo hiyo, na mali hizo kukamatwa.

Kwahiyo Kabudi anapoishangaa Canada, ni kukosa umakini tu. Ameongea kama "layman" ambaye hajui sheria kabisa. Vijana wa LLB1 pale UDSM, Mzumbe au SAUT wanamshangaa.

Mali zetu zimekamatwa zaidi Canada kwa sababu ndio nchi yenye mali nyingi za Tanzania kwa sasa (ndege zote za Bombadier zinatengenezwa huko). Hata Brazil ambapo Kabudi anashauri tukanunue ndege, zinaweza kukamatwa pia kama Steyn akiamua kwenda kusajili tuzo yake kwenye mahakama za huko.

Hivyo basi tunahitaji kupata suluhisho la kudumu badala ya kupiga 'ngonjera' kwamba kuna watanzania wanatumiwa na mabeberu kutuhujumu. Hakuna cha "beberu" wala "mbuzi jike" anayetuhujumu, ni makosa yetu wenyewe. Tutafute mbinu za kuyatatua badala ya kujificha kwenye visingizio vya mabeberu. Na tusimpotoshe Mheshimiwa Rais.

Nini kifanyike?

1. Serikali imuondolee mkukima Hermanus Steyn marufuku iliyompiga ya kuingia nchini. Ikumbukwe anahangaika huko nje kwa sababu amezuiwa kuja nchini. Kabla hajapigwa marufuku ya kuja Tanzania alikua anakuja kudai haki yake hapa. Alipozuiwa ndipo akaamua kuichukua "tuzo" yake mahakama kuu na kwenda kuisajili huko nje.

2. Kamati ya Chenge na Mkulo iitwe na kuulizwa msingi wa kupendekeza Steyn alipwe kiasi kidogo tofauti na "tuzo" aliyopewa na mahakama kuu. Kama sababu hizo zitakua na mashiko, zitumiwe kumshawishi Steyn akubali kiasi alicholipwa na kufuta shauri hilo mahakamani.

3. Kama serikali haikubaliani na option hizo mbili hapo juu, basi ikate rufaa au iombe "judicial review" kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya kumpa Steyn tuzo ya $36M. Na maamuzi yatakayotolewa kwenye rufaa hiyo yaheshimiwe na pande zote mbili.

Vinginevyo tutaishia kuwalaumu "mabeberu", kesho tutawalaumu "majogoo", keshokutwa tutawalaumu "mitetea" pasi na sababu zozote za msingi. Kama mkulima huyu kudai haki yake ni ubeberu basi Mahakamu kuu ya Tanzania ndio beberu kuu maana ndiyo iliyompa ushindi wa tuzo hiyo. Tuache porojo. Tudeal na msingi wa tatizo.

Tuanzie na sababu za Nyerere kutaifisha mali za Steyn, kisha twende kwenye hukumu iliyotolewa na mahakama kuu na kumpa ushindi. Then tumalizie na ripoti ya kamati ya akina Chenge. Halafu tumuite Steyn tukae nae mezani tuyamalize. Tuache kurukaruka kama maharage yaliyokosa maji.!

Malisa GJ
2220277_IMG-20191124-WA0015.jpeg
 
barafuyamoto

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Messages
27,165
Points
2,000
barafuyamoto

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2014
27,165 2,000
Kwenye suala la picha, body language hutazamwa ktk mazunguzo laivu au ktk video ya wanaoongea.
Ingawa una hoja kiasi fulnk, ila kuna nguvu ya ziada unaitumia pia ktk kupotosha.
 

Forum statistics

Threads 1,402,619
Members 530,952
Posts 34,400,493
Top