Tuache kujibagaza, tukitaka kuwa wazalendo wa kweli tutafute suluhu ya kudumu dhidi ya mkulima Steyn

Akafungua kesi mahakamani hapahapa nchini akidai fidia ya $36M. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi na kumgrant "tuzo" hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo. Ikaunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mali zilizotaifishwa. Kamati hiyo iliongozwa na Mzee Chenge na Mkulo, ikapendekeza alipwe $20M kinyume na "tuzo" aliyopewa na mahakama ya $36M.
Kama waliamini kuwa mkulima anastahili $20M, je walirudi mahakamani au walikubaliana na huyo mkulima kwa kiwango hicho? Vinginevyo basi nchi yangu pendwa bado itakuwa inadaiwa $16M + accrued interest. Na takuwa na haki kutumia mbinu zozote (za kisheria) kupata haki yake.
 
Wasaliti wa Nchi wajiandae kisaikolojia
Swali anatudai au hatudai. Mahakama iliamua alipwe $36M wewe ukalipa $20M, hizo $16 zimekwenda wapi? Kugoma kulipa kama mahakama ilivyoagiza ni uzalendo au usaliti (wa sheria na katiba).
 
Huyo mkulima anatumika na wasaliti wa nchi
Swali anatudai au hatudai. Mahakama iliamua alipwe $36M wewe ukalipa $20M, hizo $16 zimekwenda wapi? Kugoma kulipa kama mahakama ilivyoagiza ni uzalendo au usaliti (wa sheria na katiba).
 
Huyo mkulima anatumika na wasaliti wa nchi
Mkuu jibu swali. Kwa nini serikali iwape hao "wasaliti" nafasi? Unaweza usimpende huyo mkulima lakini hiyo haikupi ticket ya kumdhulumu. Mlipe yaishe au rudi mahakamani ukajitetee.
Hata humu ndani tunaopigika tuko wengi, serikali inakalia haki zetu bila sababu ya msingi na kutuambia tufunge mikanda, kwa unyonge wetu tunakubali.
 
Unapoleta madai nyeti kama haya inabidi ubalance pande zote. Tunajua mawakili wake huyu mzungu na wanaoleta ukimbelembele wa madai haya ni hawa wenye majina ya akina MALISA.
Kwanza tuambie huyo mzungu hayo malaki ya maekari aliyapataje? Ni mzawa? Alipora hiyo ardhi ya umma kwa unyonyaji wa kikoloni ndo maana Nyerere akaitaifisha. Hata hivyo kwavile baadhi ya ardhi alikuwa ameishaiendeleza na Mali zinazohamishika kama magari, ndege ndogo za tours, n.k. ndo maana Nyerere akamuachia kiasi fulani cha ekari (nyingi tu) kama fidia ya mali zinazohamishika na Huyo mzungu akutaka kuendelea na mgogoro na serikali ya Tanzania akakubali yaishe. Nyie akina Malisa wapiga deal kwavile mnajua mna 10% ndo mnalianzisha ili mpige hela. Sasa sikia, kwa serikali hii kama kulipa italipa lakini sio rahisi kihivyo. Tunajua mnakopa hela nyingi tena kwa riba kufungua kesi ugenini mkidhani mtalipwa kirahisi na kurejesha mkopo. Hiyo hela ina mawili kulipwa au kutolipwa: Kwanza huyo mzungu alishalipwa dola mil.20 na mwinyi ni zaidi ya miaka 35 hivi. Pili huyo mzungu aliachiwa hekari kibao na bado anazo anaendelea kuzimiliki. Sasa nyie mnataka cash kusudi mpate 10% lakini huyo mzungu anajua itakula kwake maana atanyanganywa ardhi ndo maana alikubali yaishe. Endelea kupima joto la serikali hii mkidhani mtapata hela ya bure. Why now? Kwani nchi haina mali nje ya nchi miaka hiyo yoote mbona hazijawahi kuzuiwa? ATCL haikuwa na International routes kabla ya kufilisika mbona hatukusikia hawamu ya Mkapa, na Kikwete ndege zetu zikikamatwa? Baadhi ya balozi zetu nje ya nchi hayo majengo tumejenga wenyewe ni mali zetu mbano hayajawahi kiwekewa kofuli kufidia? Nchi ina gold deposits kwenye benki ya dunia kureflect paper/coin money mbona hazijawahi kushikiliwa? Ukweli ni kwamba myanya yooote ya wizi wa mali za umma na utakatishaji wa hela chafu na madawa ya kulevya, huo mtandao JPM kausambaratisha! Endeleeni kukopa hela kuendesha kesi mtaangukia pua! Shwaini!
Mkuu we nae akili yako sio nzuri, huyu Mkulima alikuwa analipwa kidogo kidogo mpaka miaka kadhaa iliyopita walipo msitishia malipo, dhuruma sio nzuri kama alipata hizo mali zake kwa haki ni vyema tumlipe..
 
Mbona na sisi tulikamata Makenikia? na kuzuia shughuli za ACACIA?

Mara tukasuluhishana na BARRICK
tuwe wapole cha mtu chake apewe tusiweke double standard.

Kabla ya kukamatwa ndege

Mwaka 1983 kupitia Kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act, 1983 kampuni sita za Mzungu Hermanus Steyn ambazo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd, Lente Estate Ltd, Loldebbis Ltd, Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd zilitaifishwa na Serikali ya Tanzania.

Baadaye Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi (arbitration) akiomba haki zake zote katika kampuni zote zilizotaifishwa, jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za Marekani 36,375,672.81 (Dola milioni 36).

Muda ukapita, lakini baadaye Mei 2011 Mzungu huyo akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika Mahakama Kuu ya Biashara ili iwe hukumu ya mahakama, hivyo iweze kutekelezeka.

Julai 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na Mzungu huyo wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola za Marekani 30,000,000 ( Dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali.

Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama, hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.

Kufikia Machi 2016, serikali ikawa tayari imemlipa Mzungu huyo Dola za Marekani 20,099,155.12 (dola milioni 20).

Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo, serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 Mahakama Kuu ya Biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua Mzungu kulipwa Dola za Marekani 36,375,672.81, kwa hoja kuwa ilikuwa na upungufu wa kisheria.

Desemba 2018, Jaji B.K. Philip alitoa uamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo, kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na Mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani, hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.

Katika maombi hayo serikali iliwakilishwa na Wakili Jacqueline Kinyasi, wakati Steyn aliwakilishwa na Wakili Erick Ng’maryo.

Hoja kuu ya Wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba uamuzi wa taasisi ya usuluhishi (arbitration) ulishakufa na haupo, na kuwa uamuzi huo uliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali, ambapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, hivyo serikali kuiomba mahakama ifanye marejeo ya hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.

Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus Afrika Kusini.
 
Ha ha ha ha, hii Nchi ina vituko Sana eti jamaaa aliyesoma pale SAUT baada ya kukosa vyuo vingine anakuja hapa Kumukosoa Prof. wa sheria kwenye Mambo ya kisheria na watu wanakuja hapa kumshangilia.

Hivi hii Nchi nani ametuloga?! Hata Kama angekuwa Sahihi Malisa hana Credibility ya Kumkosoa Prof. Kabudi achilia mbali Credibility ya kuzungumza mambo ya kisheria na degree yake sijui ya Matango kutoka pale SAUT.

Hilo tu kwangu linatosha kupuuza alichoandika Malisa hata Kama angekuwa sahihi kiasi gani. Malisa hana credibility ya Kumkosoa Prof. Kabudi, lakini pia hana Credibility ya kuzungumzia legal issues, he is a layman (Ni Mpumbavu kwenye tasnia hii).

Pamoja na upumbavu wake, kwakuwa ameshaandika labda aje atueleze Kama hata hiyo Resjudicata anaijua maana yake, applicability yake je, at what point unaweza ku invoke hii principle. Je kuwa tu umeshashindwa kwenye Mahakama fulani inakufanya usiwe na uwezo wa kufungua kesi sehemu nyingine( Na hapa ieleweke Kuna tofauti ya kufungua kesi na kushinda kesi).

Nani anapaswa ku raise hiyo arguement ya Resjudicata na katika hatua gani. Ni hivi huyo mkulima kuwa ameshashindwa principle ya Resjudicata haimuzuii kufungua shauri sehemu nyingine, anaruhusiwa kufungua then upande wa pili ndo una jukumu la kwenda mbele ya Mahakama na kuraise hiyo issue ya Resjudicata na Mahakama ipitie Nyaraka na ijiridhishe then I rule out. Kwamba Stain alishindwa Africa Kusini haimanishi Mahakama za Canada zinajua hilo. Ni Mpaka pale upande wa pili utakapoijulisha kuwa swala hilo limeshaamriwa na Mahakama nyingine on Merit.

Narudia kama una akili, when It comes to legal issues utakuwa ni Mpumbavu wa mwisho Kama utachagua kumsikiliza na kuamini alichokisema Malisa badala ya Prof. Kabudi, narudia wewe utakuwa ni Mbumbumbu wa kutupwa, hata Kama Malisa angekuwa sahihi kiasi gani, hapa Kabudi anapaswa kusikilizwa.

The man has got credibility, acheni uzwazwa, Malisa aache uzwazwa, aache kuvamia vitu asivyovijua, Kama anapenda aende asome sheria apate credibility ya kuzungumza sheria, otherwise yeye ni Mpumbavu wa sheria hata angejitutumua kiasi gani.
 
Naona immma wanatafuta hela kinguvu, tumeshawalipa sana enzi ta Kikwete hizo fedha mlipeleka wapi? Au ndo hizo mnazitumua kijikimu Ulaya na familia zenu hadi dereva na familia yake?
 
Ha ha ha ha, hii Nchi ina vituko Sana eti jamaaa aliyesoma pale Sauti baada ya kukosa vyuo vingine anakuja hapa Kumukosoa Prof. wa sheria kwenye Mambo ya kisheria na watu wanakuja hapa kumshangilia. Hivi hii Nchi nani ametuloga?! Hata Kama angekuwa Sahihi Malisa hana Credibility ya Kumkosoa Prof. Kabudi achilia mbali Credibility ya kuzungumza mambo ya kisheria na degree yake sijui ya Matango kutoka pale SAUT. Hilo tu kwangu linatosha kupuuza alichoandika Malisa hata Kama angekuwa sahihi kiasi gani.
Malisa hana credibility ya Kumkosoa Prof . kabudi, lakini pia hana Credibility ya kuzungumzia legal issues, he is a layman(Ni Mpumbavu kwenye tasnia hii).
Pamoja na upumbavu wake, kwakuwa ameshaandika labda aje atueleze Kama hata hiyo Resjudicata anaijua maana yake, applicability yake je, at what point unaweza ku invoke hii principle. Je kuwa tu umeshashindwa kwenye Mahakama fulani inakufanya usiwe na uwezo wa kufungua kesi sehemu nyingine( Na hapa ieleweke Kuna tofauti ya kufungua kesi na kushinda kesi). Nani anapaswa ku raise hiyo arguement ya Resjudicata na katika hatua gani. Ni hivi huyo mkulima kuwa ameshashindwa principle ya Resjudicata haimuzuii kufungua shauri sehemu nyingine, anaruhusiwa kufungua then upande wa pili ndo una jukumu la kwenda mbele ya Mahakama na kuraise hiyo issue ya Resjudicata na Mahakama ipitie Nyaraka na ijiridhishe then I rule out. Kwamba Stain alishindwa Africa Kusini haimanishi Mahakama za Canada zinajua hilo. Ni Mpaka pale upande wa pili utakapoijulisha kuwa swala hilo limeshaamriwa na Mahakama nyingine on Merit.
Narudia kama una akili, when It comes to legal issues utakuwa ni Mpumbavu wa mwisho Kama utachagua kumsikiliza na kuamini alichokisema Malisa badala ya Prof. Kabudi, narudia wewe utakuwa ni Mbumbumbu wa kutupwa, hata Kama Malisa angekuwa sahihi kiasi gani, hapa Kabudi anapaswa kusikilizwa.The man has got credibility, acheni uzwazwa, Malisa aache uzwazwa, aache kuvamia vitu asivyovijua, Kama anapenda aende asome sheria apate credibility ya kuzungumza sheria, otherwise yeye ni Mpumbavu wa sheria hata angejitutumua kiasi gani.
Hujui hata ulichokiandika wewe
 
, member:utakuwa ni Mpumbavu wa mwisho Kama utachagua kumsikiliza na kuamini alichokisema Malisa badala ya Prof. Kabudi, narudia wewe utakuwa ni Mbumbumbu wa kutupwa, hata Kama Malisa angekuwa sahihi kiasi gani, hapa Kabudi anapaswa kusikilizwa.The man has got credibility, acheni uzwazwa, Malisa aache uzwazwa, aache kuvamia vitu asivyovijua, Kama anapenda aende asome sheria apate credibility ya kuzungumza sheria, otherwise yeye ni Mpumbavu wa sheria hata angejitutumua kiasi gani.

Ina maana hapa tupo katika Hadithi ya Malisa na Kabudi au tupo kwenye Reality
Ndege imekamatwa wewe weka Hoja zako hapa achana na Malisa au Post ya Mshana inaonesha wewe ni MPUMBAVU kabisa wa kutumwa eti watu wa upande huu wa Goli lililofungwa ni wapumbavu wanamuamini. Wewe leta Hoja huyo Steyn ASILIPWE basi gari zake 250 mashamba na mitambo aliiba au Dola 20M alizopewa awamu ya 3 zilimtosha.
 
Mm nmelewa kwann ulitaka wenye akili timamu tu!! "uncle nikiwa kiongoz wao nimekusoma vyema.
 
Back
Top Bottom