TTCL yanasaini mkataba wa bilion 300 na Huawei

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
Kampuni kongwe na yakizalendo TTCL leo imesaini mkataba wa ku supply na kujenga miundombinu mipya kutoa huduma bora ya mawasiliano ya GSM 3G NA LTE (4G).

Hii ni sehemu ya mpango mkakati wa kujijenga upya na kulivamia soko la mawasiliano kiushindani.

Tunampongeza CEO wa kampuni hii na timu yake kwa kupambana vilivyo hasa ikizingatiwa mnyonyaji wao kampuni ya simu ya moroko bado anang'ang'ania hataki kutoka.
===========================

Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakisaini mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani Milioni 182.

Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani Milioni 182.

Picha ya Pamoja.

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Kampuni ya MS Huawei Technologies ya China wameingia mkataba utakaolenga katika kujenga, kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo miradi hiyo itagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani Milioni 182.

Awamu ya kwanza ya mradi huu inategemea kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, 2015.

Miradi ambayo iko kwenye mkataba itahusisha ujenzi wa mtandao wa teknolojia ya kisasa ya 4G Long Term Evolution (LTE), 3G - UMTS pamoja na 2G- GSM, teknolojia hizi zitasaidia Kampuni kupanua na kuboresha huduma zake nchi nzima na katika ubora wa hali ya juu. Teknolojia hizi zitatoa huduma bora ya sauti na intaneti (data) yenye kasi zaidi.

Mkataba huu pia unahusisha ununuzi wa mitambo kwa ajili ya kupeleka mawasiliano vijijini chini ya mpango wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

TTCL imeshinda zabuni ya kupeleka mawasiliano katika kata 69 zinazojumuisha vijiji zaidi ya 400 vyenye wakaazi zaidi ya laki tano. Chini ya mradi huo UCSAF itaipatia TTCL Dola za Marekani milioni kumi kujenga miundo mbinu ya mawasiliano katika Kata hizo.

Mkataba wa TTCL na Huawei ni moja ya juhudi zinazofanywa na Kampuni katika kutekeleza mikakati endelevu ili kuboresha na kupanua upatikanaji wa huduma nafuu za mawasiliano ya simu na intaneti nchi nzima.

Aidha, mikakati hii inaunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha huduma za simu na intaneti zinawafikia watanzania waliopo vijijini na mjini.

Hivyo, TTCL inawahakikisha watanzania na wateja wake wote kuwa iko imara, na imejipanga kimkakati katika kuhakikisha inaendelea kutoa huduma endelevu, bora na nafuu kwa wateja wetu wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Chanzo: Michuzi
 
Kampuni kongwe na ya.kizalendo TTCL leo imesaini mkataba wa kusupply na kujenga miundombinu.mipya kutoa huduma bora ya mawasiliano ya GSM 3G NA LTE (4G). Hii ni sehemu ya mpango mkakati wa kujijenga upya na kulivamia soko la mawasiliano kiushindani.

Tunampongeza CEO wa kampuni hii na timu yake kwa kupambana vilivyo hasa ikizingatiwa mnyonyaji wao kampuni ya simu ya moroko bado anang'ang'ania hataki kutoka.
 
Hii Nchi ni shamba la bibi. Kabla ya kumpongeza huyo CEO tujiulize kachukua hatua gani dhidi ya mwizi wa pale moroko? Kama kakiuka mkataba atuambie hatua gani zilichukuliwa kabla ya kukimbilia kutafuta mwekezaji mwingine
 
Ni dela kubwa tutegemee mabadiliko makubwa kwene sekta ya mawasiloano kwene kampuni hii ya uma
Soon arsenal wataingia mkataba pia na ttcl
 
mkuu timpe muda aliingia ttcl kakuta hakuna maboresho yoyote upande wa network ttcl haikopesheki na bank yoyote ingekua ngumu kuweza kujiendeleza hii mikataba na hao wezi nafkiri ni wakati sasa serikali kupitia na kuangalia makosa yaikua wapi na wahusika wachukuliwe hatua
 
Ni dela kubwa tutegemee mabadiliko makubwa kwene sekta ya mawasiloano kwene kampuni hii ya uma
Soon arsenal wataingia mkataba pia na ttcl

Lugha yako utata mtupu.

Any way, hongera TTCL kwa hatua hiyo. Maana mhhhh! Mnasuasua mno.
 
Kampuni kongwe na ya kizalendo TTCL leo imesaini mkataba wa kusupply na kujenga miundombinu mipya kutoa huduma bora ya mawasiliano ya GSM 3G NA LTE (4G).

Hii ni sehemu ya mpango mkakati wa kujijenga upya na kulivamia soko la mawasiliano kiushindani.

Tunampongeza CEO wa kampuni hii na timu yake kwa kupambana vilivyo hasa ikizingatiwa mnyonyaji wao kampuni ya simu ya moroko bado anang'ang'ania hataki kutoka...

Si juzi juzi tu tumeambiwa kampuni inasua sua na madeni na ina hali mbaya, huyu mwekezajia mekuja na masharti gani maana tunajua hakuna lunch ya bure duniani!!!

Otherwise kuna kitu hakisemwi wazi wazi...
 
Kuna kiza kinene kimetanda hapo TTCL. Yaelekea kuna vibosile wameweka mirija yao hapo; na hawataki kuachia mpaka huyu ng'ombe abakie mifupa mitupu. So sad!
 
Kampuni kongwe na yakizalendo TTCL leo imesaini mkataba wa ku supply na kujenga miundombinu mipya kutoa huduma bora ya mawasiliano ya GSM 3G NA LTE (4G).

Hii ni sehemu ya mpango mkakati wa kujijenga upya na kulivamia soko la mawasiliano kiushindani.

Tunampongeza CEO wa kampuni hii na timu yake kwa kupambana vilivyo hasa ikizingatiwa mnyonyaji wao kampuni ya simu ya moroko bado anang'ang'ania hataki kutoka.

Too late!! utafanyaje kumshawishi mtu aachane na VODA,TIGO,AIRTEL,ZANTEL! na badala yake ajiunge na network ya TTCL?? What's so special in that teqnology of HUWAEI?? Ambacho haya makampuni mengine hayawezi fanya/boresha??
 
Kuna kiza kinene kimetanda hapo TTCL. Yaelekea kuna vibosile wameweka mirija yao hapo; na hawataki kuachia mpaka huyu ng'ombe abakie mifupa mitupu. So sad!

Mkuu haiwezekani kampuni iliyo mufilisi, atokee muwekezaji fasta fasta hivi, ina maana yale mabilioni yanayodaiwa TTCL amekubali kuyanunua, tunajua biashara TTCL ni mbaya sana tu, iko hoi bin taabani, halafu hata mwezi haujapita ati katokea muwekezaji, tena mchina...

Siku administartion ikibadilika tuntaonamengi sana, Mungu atupe uzima tu...
 
Hiyo ni sawa na kujaribu KUFUFUA maiti kama afanyavyo GWAJIMA na misukule yake!
 
Too late!! utafanyaje kumshawishi mtu aachane na VODA,TIGO,AIRTEL,ZANTEL! na badala yake ajiunge na network ya TTCL?? What's so special in that teqnology of HUWAEI?? Ambacho haya makampuni mengine hayawezi fanya/boresha??
Simu zao hazikatikikatiki. Hujawahi kusikia "mbona unakatikakatika, sikusikii vizuri, hebu kata nikupigie tena".
 
Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakisaini mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani Milioni 182.

Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekaniMilioni 182.

Picha ya Pamoja.

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Kampuni ya MS Huawei Technologies ya China wameingia mkataba utakaolenga katika kujenga, kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo miradi hiyo itagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani Milioni 182. Awamu ya kwanza ya mradi huu inategemea kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, 2015.

Miradi ambayo iko kwenye mkataba itahusisha ujenzi wa mtandao wa teknolojia ya kisasa ya 4G Long Term Evolution (LTE), 3G - UMTS pamoja na 2G- GSM, teknolojia hizi zitasaidia Kampuni kupanua na kuboresha huduma zake nchi nzima na katika ubora wa hali ya juu. Teknolojia hizi zitatoa huduma bora ya sauti na intaneti (data) yenye kasi zaidi.

Mkataba huu pia unahusisha ununuzi wa mitambo kwa ajili ya kupeleka mawasiliano vijijini chini ya mpango wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). TTCL imeshinda zabuni ya kupeleka mawasiliano katika kata 69 zinazojumuisha vijiji zaidi ya 400 vyenye wakaazi zaidi ya laki tano. Chini ya mradi huo UCSAF itaipatia TTCL Dola za Marekani milioni kumi kujenga miundo mbinu ya mawasiliano katika Kata hizo.

Mkataba wa TTCL na Huawei ni moja ya juhudi zinazofanywa na Kampuni katika kutekeleza mikakati endelevu ili kuboresha na kupanua upatikanaji wa huduma nafuu za mawasiliano ya simu na intaneti nchi nzima.

Aidha, mikakati hii inaunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha huduma za simu na intaneti zinawafikia watanzania waliopo vijijini na mjini.
Hivyo, TTCL inawahakikisha watanzania na wateja wake wote kuwa iko imara, na imejipanga kimkakati katika kuhakikisha inaendelea kutoa huduma endelevu, bora na nafuu kwa wateja wetu wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

TTCL na Huawei waingia Mkataba wa Kuboresha mawasiliano Nchini
Mkataba unagharimu $182 Millions

Labda TTCL itafufuka.

Pia huu mkataba ungepelekwa bungeni ujadiliwe kwanza yasije kutokea kama mkataba wa Awali na Celtel (Airtel)
 
Back
Top Bottom