TTCL yanasaini mkataba wa bilion 300 na Huawei

TTCL yanasaini mkataba wa bilion 300 na Huawei

Mkuu,
Makampuni tajwa hayna Miundombinu ya kupabambana na TTCL wakiamua.

Kufunga fibre hapo Dar sio sawa na kufunga fibre nchi nzima. TTCL wana mkongo wa taifa ambao unawawezesha
kusambaza fast broadband nchi nzima kw urahsi mno kitu ambacho Vodacom/Airte/TIGO hawawezi. Ndio maana ukiwa mikoani na hizo mobiles ni kazi hata kusoma magazeti online.

Hapa hatuongele kutembelea facebook au Jamiiforums. Tunaongea uwezo wa kuendesha shugulza kiuchum kupitia internet. Kuanzia ufundishaji mashulen, huduma za afya kwa njia ya remote, kuangalia mapicha, distance learning,TV nk. Vitu hivyo huwezi kufanya bila infrastructure ya maana. Leo hii vyuo vya maa kama Harvard wana kozi nyingi za maana online, tena bure. Lakini kwa internet ya Tanzania,vijana wasahau.

Ndio maana wakati mwingine nawaonea huruma TTCL, uchumi wanao ila wameukalia.

Ila TTCL wakilala, huko tunakoenda, technology inabadilika kiasi kwamba itakuwa rahisi kuachive yote hayo kwa investment ndogo sana. Zamani copper wire tulikuwa tunaongelea maximum 8mbps lakini leo kwenye copper pair hiyo hiyo unaweza pump data hata zaidi ya 100Mbps. Gharama ya invesment kwenye backbone ikipungua sana Hapo ndipo hizo kampuni za mobile zitaweza kupambana kirahisi na kuiacha TTCL mbali.

Ni kweli ndugu,
Ila kuhusu Mkongo wa Taifa TTCL ni muendeshaji tu hana mamlaka nao,na pia kila mtoa huduma za mawasiliano anahaki ya kununua "capacity" anayotaka na kupelekwa kokote pale Mkongo wa taifa ulipofika.Hivyo TTCl bado anakazi kubwa mno ya kupambana na hawa watu.
 
Jidu,
Mkongo kwasasa TTCL ni muendeshaji tu kwasababu serikali inakwepa kuuweka chini ya TTCL il hao Airtel wasifadike nao. Siku TTCL ikiwa asilimia100 mikononi mwa serikali, huo mkongo wa taifa utakuwa chini ya TTCL moja kwa moja.

Hiyo ya kila mtoa huduma kuwa na haki ya kununua kutoka kwao; kuwa na haki sawa na TTCL ni theoretically tu, practically haiwi hivyo hata siku moja. Hata nchi zilizoedelea na ambazo zina sharia nyingi za biashara zinazofuatwa, hili jambo ni gumu Mfano ni UK ambako BT mbali ya kuwa mto huduma sawa na makampuni mengine, pia inamiliki mkongo kwa kutumia jina lingine la Openreach. Lakini ukifuatilia sana unakuta BT wao wana advantages kibao ukilinganisa na watoa hudum wengine hata kam bei wanaazolipa zinafanana.

Ni kweli ndugu,
Ila kuhusu Mkongo wa Taifa TTCL ni muendeshaji tu hana mamlaka nao,na pia kila mtoa huduma za mawasiliano anahaki ya kununua "capacity" anayotaka na kupelekwa kokote pale Mkongo wa taifa ulipofika.Hivyo TTCl bado anakazi kubwa mno ya kupambana na hawa watu.
 
Back
Top Bottom