TTCL yanasaini mkataba wa bilion 300 na Huawei

TTCL yanasaini mkataba wa bilion 300 na Huawei

Hii Nchi ni shamba la bibi. Kabla ya kumpongeza huyo CEO tujiulize kachukua hatua gani dhidi ya mwizi wa pale moroko? Kama kakiuka mkataba atuambie hatua gani zilichukuliwa kabla ya kukimbilia kutafuta mwekezaji mwingine

Tanzania hii ina wasomi wengi tu wa mambo ya mawasiliano, kama nakumbuka vizuri CEO ni mmoja wa wasomi wa mambo haya, kinacho nishangaza mimi kwa nini yeye na timu yake wasikae chini wakafanya tathimini ni vifa gani vya mawasiliano vinavyo hitajika kusambaza mfumo wanao hitaji (3G, 4G (LTE au WiMax and what have you!) radio hizi na vifaa vyake vyote vinapatikana kwenye open market - Sweden, Ujerumani, China, Korea - cha muhimu hapa ni kujua unachotaka kufanya basi! Nataka nieleweke vizuri kwamba nalisema hili kwa nia njema tu na wala sina tatizo na CEO wa sasa hivi wa TTCL, mimi nampa changa moto tu - yeye kama Injinia ambaye alipata bahati ya kusomea kwenye Dunia ya kwanza ana uwezo mkubwa wa-kudesign network ya kusambaza mawasiliano nchi nzima yeye na Watanzania wenzake baada ya hapo ndio wakijike kununua vifaa vya mawasiliano kutoka kwa manufucturers ambao kusema kweli ni wengi tu, kwani Vodacom, AirTel nk nani kasema wanahunda hata kifaa kimoja cha mawasiliano - si wananunua tu kutoka kwa wahundaji wa vifaa hivyo, wana-install wenyewe na ku-configer SERVERS zao accordingly - sisi tunashindwa nini??

Ni lini Watanzania tutaondokana na kasumba ya kutojiamini, kwani hao Wachina wanatafanya kitu gani cha hajabu zaidi ya kufunga maredio na ma-antenna kwenye minanara na kuweka ma-servers ya kuratibu traffic ya mawasiliano nk, wapo Watanzania wenye weledi wa kuvifunga vifaa hivi vya mawasiliano na Taifa likapata mawasiliano kwa bei nafuu, nina uhakika CEO wa TTCL wa hivi sasa weledi huo anao, kwa nini a form team yake wakaenda kununua vifaa hivyo Huawei, ZTE,Philips,Siemens,Motorola, Ericsson etc. na kuvifunga?? Binafsi ningependa sana kuona CEO mwenye background ya kiufundi anakuwa mstari wa mbele kuwa mbunifu na kuhokoa fedha zetu za kigeni kwa kuwashirikisha Watanzania wenzake wenye ujuzi/weledi wa masula ya mawasiliano ili Taifa letu lifaidike kwa kutumia wezalendo wenzao, haipendezi kuona CEO mwenye ujuzi wa Mawasiliano anataka kufanana ni wana Sheria au wengine ambao hawana uweledi wowote katika mambo ya ufundi. Taifa letu bwana! Mpaka tunakwenda kuwafuta Wa-Vietnam waje kutufungia vifaa vya mawasiliano, tunawatafuta watu waliokuwa Vitani mpaka late 1970s - wao wanacho fanya ni kununua vifaa vya mawasiliano kutoka Nchi nilizo taja hapo juu - Vietnam kama ilivyo Tanzania it does not manufucture telecom equipment/system yoyote - wanatunia weledi wao kujua wapi waweke nini na vipatapitana wapi basi - sisi tunashindwa NINI? NIMALIZIE KWA KUSEMA HAYA NAYASEMA KWA NIA NZURI TU-WATANZANIA TUBADIRIKE mind set ZETU.
 
Hongera TTCL mungu awasaidie ila angalieni viongozi mnaowaweka kwenya customer service centers zenu wengine ni majanga tu, na huko ndiko wateja wanapoanzia.
 
Kampuni kongwe na yakizalendo TTCL leo imesaini mkataba wa ku supply na kujenga miundombinu mipya kutoa huduma bora ya mawasiliano ya GSM 3G NA LTE (4G).

Hii ni sehemu ya mpango mkakati wa kujijenga upya na kulivamia soko la mawasiliano kiushindani.

Tunampongeza CEO wa kampuni hii na timu yake kwa kupambana vilivyo hasa ikizingatiwa mnyonyaji wao kampuni ya simu ya moroko bado anang'ang'ania hataki kutoka.
===========================

Chanzo: Michuzi

Hivi si kulikuwa na mkataba kabla? nakumbuka mwak 2007 hadi simu za huwawei tulinunua toka ttcl, na zilikuwa na line ya ttcl tu, na huduma ilikuwa nzuri ila ilikuwa baadhi ya maeneo, je ile iliishia wapi? na nini kilifanya ule mpango ukafeli? Je suluhisho gani la muda mrefu limechukuliwa baada ya ile? Je mkataba huu mpya wanatuhakikishia vipi wateja na wananchi kuwa utaleta tija na si kutunyonya?

Wajibu kwanza maswali hayo, ndio tuende stage nyingine!
 
Tukae mkao wa kula tutasikia ufisadi mwingine
 
mkuu utaya upo kwani hukuoma juzi kwenw michuzi wakiwa na uongozi wa arsenal pitia michuzi usome au huitakoo mema kampini yako mama ya mawasiliano

Huawei | Our Partners | The Club | Arsenal.com

THE PARTNERSHIP

Arsenal and Huawei

gun__1408089757_huaweiv3.jpg

THE HUAWEI ASCEND P7

Huawei's new 4G Arsenal Edition smartphone, now on sale at Arsenal Direct, offers supporters stand-out design, an unparalleled camera experience and exclusive Arsenal Football Club features

Mheshiwa CEO wa TTCL Kamugisha!! We want this smartphone as soon as possible!!!

Huku arsenal na kule Huawei katikati TTCL na HUAWEI ASCEND P7!!!!- The sound of touch screen!!
 
Tujuze zaidi kuhusu hii issue ya Kamu kuonekana na wazungu wa Arsenal

Huawei ni official partner wa Arsenal,Huawei ni main supplier/sponsor wa TTCL upo!!!

Watanzania wategemee vitu vizuri kutoka Arsenal na Huawei!!!!
 
mkataba huu upelekwe BUNGENI jumatatu ijayo ili bunge liupitie na kuutathini kwa kina kama endapo utakuwa na tija kwa taifa letu/CCM NI LAZIMA WALIPIGANIE HILO ILI ATLEAST WATZ WAANZE KUJENGA MATUMAINI MAPYA!/NA YOTE YA KITAMBO NI LAZIMA IWE VERIFIED NA BUNGE LA JAMHURI
 
Sitaki kuamini haraka haraka habari ya mafanikio ya TTCL. TTCL imefikaje hapo ilihali yenyewe ilikuwa ndiyo kinara wa mawasiliano, ina rasli mali za kutosha ilishidwaje kikamata soko wakati yenyewe ilikuwa ikiungwa mkono na serikali. Wameng'ang'ania simu zao za kizamani wakati wenzao wako kwenye wireless, tuliambiwa wameingia ubia na Airtel ya wakati ule, ubia ulikufaje. TTCL walizoea kufanya kazi kwa mtindo wa nibebe nibebee wakasahau kwamba tupo kwenye ulimwengu wa utandawazi, serikali ilipofungua tu mbeleko wakaporomoka jumla. TTCL waache kudeka wafanye kazi za kiushindani, kama hawana mtaji wakakope kwa sababu wana raslimali nyingi. TTCL ya akina Kasambala na Mapunda ilikuwa na nguvu sana lakini kwa sababu ya kubebwa na serikali. Sasa ije kivingine, isimame kwa miguu yake. Dora milioni 180 ni sawa na Tsh zaidi ya bilioni 300, ni nyingi fanyeni kazi kwa weredi.
 
Mkakati wanaotumia TTCL itakuwa ngumu sana kufanikiwa.

Kwa mazingira ya biashara ya sasa itakuwa ngumu sana kuwashinda Vodacom,TIGO, Airtel na wengine kwa kutumia mobile. Itawachukua muda mrefu sana kuvuta wateja.

Kama ambavyo wengine tumewa tukiwashauri kila siku, wao wanze na upande wa broadband kwa kuingiza super fast broadband. Vodacom/TIGO/Airtel hawana infrastructure ya kupambana upande huu. Hao wateja wa broadband, ndio baadaye wanawea hata kutumia services za TTCL zingine baada ya kuonjeshwa broadband ya uhakika n kwa be nafuu.

Kikubwa zaidi wasijifungie wenyewe na kufikiri watafanikiwa kirahisi. Kuna Watanzania wengine ambao tayari wana mafanikio kwenye Nyanja hii ndani na nje nchi, washirikiane nao.

Itakuwa vizuri sana TTCL wakifnkiwa ila waache utani na wachape kazi na kuajiri watu wenye uwezo.
 
Mkuu,
Ha haaaa, Huawei pia ndio main supplier wa makampuni yote ya simu UK, kuanzia mobile companies mpaka BT.

Wana uwezo kabisa wa kuibadili TTCL Tatizo hapo ni TTCL wenyewe.
Huawei ni official partner wa Arsenal,Huawei ni main supplier/sponsor wa TTCL upo!!!

Watanzania wategemee vitu vizuri kutoka Arsenal na Huawei!!!!
 
Jamani si juzi nilisikia ttcl imefilisika au zile habari zilikua za uongo?
mwekezaji huyu amekubalije kuwekeza kwenye kampuni iliyofilisika?
 
Huyo sio kuwekezaji ni supplier. Inamaanisha kuwa TTCL imenunua service na equiments za hao wachina
 
Hivi si kulikuwa na mkataba kabla? nakumbuka mwak 2007 hadi simu za huwawei tulinunua toka ttcl, na zilikuwa na line ya ttcl tu, na huduma ilikuwa nzuri ila ilikuwa baadhi ya maeneo, je ile iliishia wapi? na nini kilifanya ule mpango ukafeli? Je suluhisho gani la muda mrefu limechukuliwa baada ya ile? Je mkataba huu mpya wanatuhakikishia vipi wateja na wananchi kuwa utaleta tija na si kutunyonya?

Wajibu kwanza maswali hayo, ndio tuende stage nyingine!

Ndugu Ttcl inatumia technolojia ya CDMA ambayo kwa hakika haijafanya vyema sokoni ...kwa sasa wakuja na mfumo wa GSM ambao unatumiwa na karibia makampuni mengi ya mawasiliano hapa nchini ila pia watakuja na LTE ambayo itawezesha watumiaji wake kupata internet ya kasi.hivyo basi technolojia ile ya GSM,CDMA na LTE zitakuwa zinafanya kazi pamoja bila hii ya cdma kuondolewa
 
Mkakati wanaotumia TTCL itakuwa ngumu sana kufanikiwa.

Kwa mazingira ya biashara ya sasa itakuwa ngumu sana kuwashinda Vodacom,TIGO, Airtel na wengine kwa kutumia mobile. Itawachukua muda mrefu sana kuvuta wateja.

Kama ambavyo wengine tumewa tukiwashauri kila siku, wao wanze na upande wa broadband kwa kuingiza super fast broadband. Vodacom/TIGO/Airtel hawana infrastructure ya kupambana upande huu. Hao wateja wa broadband, ndio baadaye wanawea hata kutumia services za TTCL zingine baada ya kuonjeshwa broadband ya uhakika n kwa be nafuu.

Kikubwa zaidi wasijifungie wenyewe na kufikiri watafanikiwa kirahisi. Kuna Watanzania wengine ambao tayari wana mafanikio kwenye Nyanja hii ndani na nje nchi, washirikiane nao.

Itakuwa vizuri sana TTCL wakifnkiwa ila waache utani na wachape kazi na kuajiri watu wenye uwezo.

Ndugu suala la miundo mbinu ilikuwa zamani hayo makampuni tajwa yana miundo mbinu iliyokuwa mikubwa nafikiri unaona mtaani jinsi wanavyolaza fiber cable kwa ushirikiano hivi punde tutarajie Data yenye kasi zaidi.
 
Mkuu,
Makampuni tajwa hayna Miundombinu ya kupabambana na TTCL wakiamua.

Kufunga fibre hapo Dar sio sawa na kufunga fibre nchi nzima. TTCL wana mkongo wa taifa ambao unawawezesha
kusambaza fast broadband nchi nzima kw urahsi mno kitu ambacho Vodacom/Airte/TIGO hawawezi. Ndio maana ukiwa mikoani na hizo mobiles ni kazi hata kusoma magazeti online.

Hapa hatuongele kutembelea facebook au Jamiiforums. Tunaongea uwezo wa kuendesha shugulza kiuchum kupitia internet. Kuanzia ufundishaji mashulen, huduma za afya kwa njia ya remote, kuangalia mapicha, distance learning,TV nk. Vitu hivyo huwezi kufanya bila infrastructure ya maana. Leo hii vyuo vya maa kama Harvard wana kozi nyingi za maana online, tena bure. Lakini kwa internet ya Tanzania,vijana wasahau.

Ndio maana wakati mwingine nawaonea huruma TTCL, uchumi wanao ila wameukalia.

Ila TTCL wakilala, huko tunakoenda, technology inabadilika kiasi kwamba itakuwa rahisi kuachive yote hayo kwa investment ndogo sana. Zamani copper wire tulikuwa tunaongelea maximum 8mbps lakini leo kwenye copper pair hiyo hiyo unaweza pump data hata zaidi ya 100Mbps. Gharama ya invesment kwenye backbone ikipungua sana Hapo ndipo hizo kampuni za mobile zitaweza kupambana kirahisi na kuiacha TTCL mbali.
Ndugu suala la miundo mbinu ilikuwa zamani hayo makampuni tajwa yana miundo mbinu iliyokuwa mikubwa nafikiri unaona mtaani jinsi wanavyolaza fiber cable kwa ushirikiano hivi punde tutarajie Data yenye kasi zaidi.
 
Hivi si kulikuwa na mkataba kabla? nakumbuka mwak 2007 hadi simu za huwawei tulinunua toka ttcl, na zilikuwa na line ya ttcl tu, na huduma ilikuwa nzuri ila ilikuwa baadhi ya maeneo, je ile iliishia wapi? na nini kilifanya ule mpango ukafeli? Je suluhisho gani la muda mrefu limechukuliwa baada ya ile? Je mkataba huu mpya wanatuhakikishia vipi wateja na wananchi kuwa utaleta tija na si kutunyonya?

Wajibu kwanza maswali hayo, ndio tuende stage nyingine!

Mkuu kilicho tokea ni kwamba kuna Wachina wajanja wachache waliwahi kuwarubuni TTCL waigie kwenye mfumo wa mawasiliano ambao unatumiwa ni nchi chache Duniani kusema kweli, Wachina walikuwa na nia ya kuweka shinikizo la kuhuza vifaa vyao vya mawasiliano ya mfumo wa CDMA badala ya mfumo wa GSM ambao unatumika katika Mataifa mengi, labda niongeza hapa kwamba CDMA ni superior kitekinolojia kuliko mfumo wa GSM, tatizo ni kwamba CDMA sio popular.

Swali ni je, kwa nini TTCL ilishindwa kustahimili ushindani katika sekta ya mawasiliano ya kutumia mobile phones? Jibu ni kwamba:TTCL ilikosea tangu mwanzo kwa kijihingiza kichwa kichwa kwenye mfumo ambao mteja analazimika kutumia SIM cards na simu za mfumo wa CDMA ambazo haziko portable i.e uwezi kutumia SIM Cards za CDMA kwenye simu za GSM, kumbuka GSM ni mfumo ambao unatumika katika nchi nyingi Duniani katika Voice communication kuliko CDMA; tatizo hilo ndilo liliwafanya wateja wasikimbilie sana kununua simu za TTCL - their sound quality notwithstanding.

Namkumbuka sana Mchina Salesman wa Kampuni ya ZTE, aliwahi kuja kwenye kampuni yetu kujaribu kutuhuzia vifaa vya mawasiliano vya mfumo wa CDMA, alikuwa na karama ya kujieleza na ushawishi mkubwa, akikukuta ujajipanga vizuri anaweza kukuhuzia mbuzi kwenye gunia, tulipo mbana kwa maswali alisema angerudi tena siku inayo fuata, tulisumbiri kwa hamu kumbana kwa maswali zaidi lakini alihamua kuingia mitini i.e hatukumuona TENA!!
 
Back
Top Bottom