Mkuu nimekutajia na mwezi kabisa nikijua nini ninachoongea. Nakumbuka wewe ndio ulianzisha uzi wa kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kutomuangusha rais na dhamira yake ya viwanda. Katika uzi ule ulipiga mkwara kutaka kuonyesha rais na ccm hamtomvumlia mkuu yoyote wa mkoa au wilaya ambaya hatofikia lengo hili la rais. Katika uzi ule mimi na wewe tulijadiliana kwa kirefu na nikakuambia ahadi si kitu kigeni kwenye serekali nyingi za ccm. Ulikataa katu katu na kusema serekali hii ni ya hapa kazi tu. Baada ya mjadala kuwa mkali, nikakuambia ikifika mwishoni mwa mwezi wa tatu nitaomba unipe taarifa ya awali ya ujenzi wa hivyo viwanda au kufufua. Jukumu lile ulionekana kujivika kwani ulitaka kupata ushindi na kuonyesha kwamba safari hii chini ya awamu hii hakuna ubabaishaji.
halafu hata mwezi uliopita kama sio tarehe 29 basi ni 30 nilikuambia na kukumbusha kuhusu ahadi yangu itakapofika mwishoni mwa mwezi wa machi uniletee taarifa za awali za hivyo viwanda kila mkoa. Tena nilikuomba uandae jedwali zuri la kila mkoa, kiwanda na mahali kilipo. Ulidhani ni masihara kwani unadhani kila aliye hapa jukwaani hajui nini kinaendelea. Ulinijibu kwamba utaleta kwa ukali kidogo huku ukiniambia ninadhani viwanda havijengwi. Nikakuambia muda ndio utatoa jibu. Leo unataka kukwepa jambo tulilokubaliana kwani unajua utaumbuka. Kimsingi sitafuti ushindi wala lengo langu sio kukuumbua, bali nimejua wewe ni mbabaishaji na kibaya zaidi unajua hilo lililosemwa ni utapeli kama utapeli mwingine. Lakini haidhuru, hiyo ni kauli mbiu ya rais na itakuwa ahueni kwa vijana wetu kupata ajira. kwa kuwa ni ilani ya chama, na ni kipaombele cha mwenyekiti wenu, tumia nafasi yako huko chamani waambie kwamba Tindo wa jf anauliza jambo la msingi na linapaswa kujibiwa kwa usahihi ili kutudhihirishia kwamba mnachosema ndio kinachotendeka.
Kuna wenzako wengi wamenikimbia kwa sababu hizihizi, kila siku wanaleta propaganda hapa na nilipowabana na wakajua niko serious na ninajua ninachohoji sasa hivi wananikwepa. Kuna niliowauliza kuhusu gas na hapa tulipofikia, naona akakimbia baada ya maswali ya kina. Kuna mwingine nilimuuliza kuhusu klimo kwanza naye aliingia mitini. Sasa leo nimekubananisha wewe kwenye viwanda sijui utachomokaje. Jambo hili ndio litapandisha heshima yako au ya chama chako. Kinyume na hapo mtaendelea kukaa madarakani sio kwa ubora wa utekelezaji wa ilani, bali wizi wa kura, ubovu wa tume, mtaji wa ujinga na nguvu ya dola. Nakuhakikishia kwenye hili nitapata majibu ya kina. Ngoja niwaite wenzio
Naona unataka kujikweza kwa kujijenga juu ya hoja za kizushi kama ilivyo kawaida yenu...nitakukumbushia kuhusu uzushi mmoja maarufu mliowahi kuuleta ...yaani Magufuli kakataza vyama vya siasa kufanya siasa wakati Rais alisema wazi tuache siasa na tuwatumikie wananchi kwa ajili ya maendeleo yao...mlimanipulate maneno ya Rais na akawakomesha vilivyo.
Kwa hiyo usijaribu kumanipulate hoja zangu ili ujijenge kwani hutaweza...Im so goood in details nafanya follow up ya maswali na maswala ya msingi katika nchi na kama unanifuatilia utakuwa umegundua hilo.
Kuhusu viwanda nimekuwa ni mmoja wa watu ninaoleta updates muhimu sana kuhusu ujenzi na ufufuaji wa viwanda though wewe na vibaraka wengine mmekuwa mkidhihaki na kutukana.
Kiukweli kuna viwanda vingi sana vinaemerge kiasi hata kuupdate inakuwa ni kero kwenu !
Kama kweli unafuatilia utaweza kugundua haipiti wiki tatu vipo viwanda vinavyofufuliwa na kuanzishwa.suala la viwanda ni nyeti na linahitaji kupewa attention na wote yaani CCM na upinzani.sijawahi kusikia Chadema ambao ni wanafiki wakiuliza au kuongelea viwanda kwenye press zao ...kwa nini?hii ni kwa sababu wanajua CCM inasonga mbele kwenye eneo hili.
Kama uko makini nilishawahi kuleta idadi ya viwanda vilivyoanzishwa especially mkoa wa pwani na nikampa hongera mkuu wa mkoa wa pwani.
Hongera kwa mkoa wa Pwani katika uwekezaji wa viwanda
mada kama hizi nilizowahi kuzileta huwa mnazichukia sana.
Kama kweli unataka kufuatilia suala hili la viwanda ungekuja na thread inayohoji idadi au utekelezaji wa ujenzi wa viwanda ...ungeifanya hiyo kama ni hoja kuu halafu uone.
Kwa kufupisha ni kwamba CCM iliahidi viwanda kwenye ilani...na katika utekelezaji waziri aliwataka wakuu wa mikoa angalau waoneshe viwanda 100+ kwa kila mkoa...hii ni ahadi na inatekelezeka whether nikupe update ya kila mwezi au kila mwaka ...ila 2020 utanihukumu au kuihukumu CCM katika ahadi hii.
Hoja yako inataka kutuaminisha kuwa hakuna kiwanda kinachojengwa wakati hoja yangu ni kuwa vipo viwanda vingi vinavyojengwa ila hamtaki kuvisema.
Bado nakuahidi kuwa nitakupa update ya ujenzi wa viwanda nchini na ulinganisho nitakuletea idadi ya viwanda 2015 na 2020 ...Iam sure tutafikia double au treble the number of viwanda.
Kama kweli ni mfuatiliaji unaweza kujua idadi ya viwanda 2015 na idadi ya viwanda kwa sasa.
kama vimepungua au bado ni idadi ile ile nitaarifu na nitaacha kupost JF.
wewe kama mwanaJF mfuatiliaji wa ahadi ya viwanda nchini kwa nini hujaleta habari hii hapo chini kuhusu viwanda kama huna unafiki?
Unafiki wenu wa kutuletea drama ndio unaopumbaza wananchi wasiulizie kuhusu ahadi na utekelezaji wake...
Mwijage azindua kiwanda cha kwanza cha mita za luku Dar