TTCL kusambaza huduma ya internet majumbani

Wasije kutupita na wananchi wa Hungumalwa na Ilelamhina watupitishie hyo intanet ila sio kwa bei ya mikocheni na mbez beach.
Hiyo laki moja ni mbuzi watatu na nusu au gunia mbili za mpunga, huko ni kutiana umasikini
 
It's a good step...

Nchi za wenzetu FTTH ndio mpango mzima, hapo utapata TV, voice na data receptions...
 
Hivi lini mtaacha ulafi? TTCL mnatumikia nani?
Unasema unaanza na nyumba 500 za uzitoni Dar na Dodoma kwanini msianzie pahala pengine kwa watu wa kawaida wanaohitaji huduma ya mtandao rahisi?Tukajua kweli mko serious kutumikia wananchi,nani kakwambia uzitoni wana shida ya mtandao wa gharama nafuu?Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka,biashara hamjui mmebakia kuchota pesa za walipa kodi mnaendea ruzuku ya serikali kazi kulembua macho na kuhaidi uongo shame on you.
 
tindo
Na wewe umejituliza pale ninapopataka siku zote!yaani kujadili hoja bila tusi na pia kuijadili serikali ya CCM kwa muktadha wa Ilani na ahadi zake.hili ni jambo kubwa lililokosekana kwa muda mrefu JF ,kwenye mitandao mingine ya kijamii,bungeni na kwenye press za kila wiki za chama unachoshabikia.

Hujakosea kuwa nipo serious katika suala la viwanda japo unatakiwa ujiongeze kwa kutambua kuwa nipo serious sana na mambo yote ninayopost au kuyajadili humu kwenye jamvi.Siwezi kukutaka radhi hadi pale utakapoacha rasmi na ushabiki wa chama chako ambacho kimekosa uelekeo na kuset agenda za kizushi na kipuuzi ambazo haziwasaidii wananchi na mustakabali wao.

siwezi kukutaka radhi hado pale utakapowaambia viongozi na wanachama wa chama unachokishabikia kuwa waache ulaghai na badala yake walete hoja nzito dhidi ya serikali kwa manufaa ya Taifa.ni muhimu kwako na kwa Taufa kuwafunza adabu hiyo!ninakuona kama unataka kujikweza kupitia mimi kwa sababu moja muhimu...

yaani kuleta hoja za kubabatiza ambazo zinajaribu kuelezea niliahidi hiki kumbe sikuwahi kufanya hivyo na yalikuwa ni matakwa na matarajio yako na mimi nitakuweka kwenye kundi la vibaraka na makarai ya Chadema kwa kuwa unaonesha the similar character ya viongozi na wanachama wa Chadema. Sielewi kwa nini na wewe unaingia kwenye mtego uleule kuwa mimi ninaleta hoja zangu kwa kuwa ni mwanaccm na sio mwanaJF...

Kuhusu Rais kukataza Siasa bado unaendelea kupitosha na ninafurahi Rais akisimama katika huo huo upotoshaji wenu kuwanyoosha.
Rais alisema wazi na clips ziko clear kuwa hataki siasa katika kutekeleza ahadi za wananchi na akawaasa wanasiasa wote iwe Chadema au CCM kuwa waache siasa na watekeleze ahadi zao kwa wananchi lakini walaghai wa chama unachoshabikia wakainteprate kuwa siasa ni marufuku. nikikuuliza kama una nukuu ya Rais kukataza siasa za vyama hutakuwa nayo na of course unaweza kuhukumiwa kwenda jela kwa uongo.Na Rais ana haki ya kisiasa ya kuwakomesha na misinterpretation yenu ya neno lake.

Ninakushangaa sana unaposema sileti updates za mara kwa mara humu jamvini halafu hapo hapi unakiri kuwa december 2017 na january 2018 nimekuletea upadates!!!!

bado nitakuita kibaraka wa CDM kwa kuwa unataka kuupotosha umma kuhusu mambo mengi pengine kwa ukinyonga wako wa uandishi dhidi ya Serikali kwa manufaa ya CDM ...yaani unaandika bila lile jazba la makarai ya CDM but kwa sisi tunaokusoma between lines tunakuelewa kuwa wewe ni walewale tu!

Kuhusu idadi ya viwanda inabidi uwe honest na ukubali pindi unapoambiwa kuwa viwanda kadhaa vimejengwa unless unataka kuendelea kuwa mpingaji usiye na data.

Kama una data kuwa viwanda vinapungua ilete jamvini.

Hapo kwenye nyekundu nionyeshe post yako nyingine yenye updates ya viwanda zaidi ya hiyo ya january nayo haikuwa ya updates ya viwanda bali kusisitiza idadi ya viwanda mpaka kufika december 2018. Nilkupa kipindi cha miezi mitatu mitatu kutoa taarifa za awali za maendeleo ya hivyo viwanda 100 kila mkoa.

Nikushauri jikite kwenye hili jambo, acha kuleta jazba na kuitaja cdm mara kwa mara na maneno mengi wakati kuna jukumu la msingi nimekupa. Hapa ndio nitaona umakini wako. Tarehe 30 march natarajia kupata taarifa ya awali ya hili ombi langu la maendeleo ya viwanda 100 kila mkoa.

Ili usiendelee kuleta jazba zisizo na msingi, link iko hapo chini wapi ulikuwa mjadala wetu na hili ninaloshikia bango.

Waziri wa Tamisemi aagiza ujenzi wa viwanda 100 kila mkoa!
 
TTCL kutumia Sh44 bilioni kusambaza intaneti
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linatarajia kutumia Sh44.7 bilioni kusambaza intaneti ya kasi kubwa hadi majumbani kupitia huduma mpya iitwayo Fiber Connect Bundle.
IN SUMMARY

  • Kupitia huduma hiyo mteja atapata intaneti ya kasi isiyo na ukomo kwa gharama ya kuanzia Sh100,000 hadi Sh200,000 kwa mwezi.

Hayo yamebainishwa leo, Jumanne Februari 27, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Waziri Kindamba aliyebainisha kuwa kupitia huduma hiyo mteja atapata intaneti ya kasi isiyo na ukomo kwa gharama ya kuanzia Sh100,000 hadi Sh200,000 kwa mwezi.

“Pia, atapata simu ya mezani bure yenye huduma ya wifi pamoja na muda wa maongezi bure na kadi ya simu,” amesema Kindamba.

“Kwa kuanzia mradi huu, tunatarajia kufikisha huduma katika nyumba 500 zilizopo Mikocheni na nyingine 500 za Mbezi Beach jijini hapa. Zaidi ya nyumba 200 zilizopo eneo la Medeli mkoani Dodoma nazo zimo kwenye mpango, baadaye huduma hii itaendelea kusambazwa nchi nzima.”

Amebainisha kuwa uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ni wa gharama kubwa, lakini shirikia hilo litaendelea kufanya kila liwezalo kuwafikia Watanzania wote kwa kuboresha mtandao wa simu na intaneti kwa gharama nafuu.

Mkuu wa Ufundi wa shirika hilo, Cecil Francis amesema muda wa majaribio ya mradi huo ni miezi mitatu kisha huduma hiyo itaanza kutolewa katika majiji yote ya Tanzania Bara pamoja na Unguja katika awamu ya kwanza.

“Awamu ya kwanza inatarajia kugharimu kati ya Dola 15 milioni za Marekani (zaidi ya Sh33 bilioni) hadi Dola 20 milioni (zaidi ya Sh44 bilioni). Utekelezaji wake tayari umeanza tangu Februari Mosi na baada ya siku 90 tutaendelea na maeneo mengine tulivyoyapa kipaumbele,” amesema Francis.

CHANZO:MWANANCHI

My Take:
CCM katika ilani yake ya uchaguzi 2015-2020 ilahidi kuongeza idadi ya watumiaji wa internet. Suala hili limetajwa katika ilani ya Ccm ukurasa wa 80 kipengele J.

(j) Kuongeza idadi ya watumiaji mitandao (internet)
kutoka milioni 9.0 mwaka 2015 hadi kufikia milioni
20.0 mwaka 2020.[B\]
Kumbe bado wapo? Watapata hasara sana kwa biashara hii yao mpya
 
Akutukanaye hakuchagulii tusi! Vyuma hivi na kulipia laki kwa mwezi wapi na wapi?
 
Safi sana. TTCL ndiyo sherika pekee la umma lilikua lina mipango ya kizalendo huku likiwa na wafanyakazi wenye mioyo ya kizalendo lakini liliminywa pumzi na wale waliopaswa kulisaidia.
Umesahau, ndio shirika lenye wazee wengi ambao hawatumiii internet katika maisha yao. Apo sioni maendeleo ya huo mpango. Wangeachana na hiyo laki na laki 2. Wangeanzia 500 kwa 300 Megabytes. Hawa jamaaa bwana makampuni kama Tigo na Voda wanacheka tuuu walivyosikia ivyo. Wao wangeboresha kwanza maeneo ya vyuoni na sehemu zote za apa Dar es salaam. Wao wanafikiri izo laki watawapata watu
 
Bei mbaya sana kwa mtanzania wa kawaida au hii huduma kwa ajili ya wale wanaojiweza tu,wenye kipato kikubwa..
Kutakuwa na bundle lenu linaitwa NOGESHA, litakuwa linaanza saa Tisa na nusu usiku mpaka saa 12 alfajiri. Gharama zake itakuwa jero kwa wiki, yaani buku 2 kwa mwezi.
 
TTCL kutumia Sh44 bilioni kusambaza intaneti
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linatarajia kutumia Sh44.7 bilioni kusambaza intaneti ya kasi kubwa hadi majumbani kupitia huduma mpya iitwayo Fiber Connect Bundle.
IN SUMMARY

  • Kupitia huduma hiyo mteja atapata intaneti ya kasi isiyo na ukomo kwa gharama ya kuanzia Sh100,000 hadi Sh200,000 kwa mwezi.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linatarajia kutumia Sh44.7 bilioni kusambaza intaneti ya kasi kubwa hadi majumbani kupitia huduma mpya iitwayo Fiber Connect Bundle.

Hayo yamebainishwa leo, Jumanne Februari 27, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Waziri Kindamba aliyebainisha kuwa kupitia huduma hiyo mteja atapata intaneti ya kasi isiyo na ukomo kwa gharama ya kuanzia Sh100,000 hadi Sh200,000 kwa mwezi.

“Pia, atapata simu ya mezani bure yenye huduma ya wifi pamoja na muda wa maongezi bure na kadi ya simu,” amesema Kindamba.

“Kwa kuanzia mradi huu, tunatarajia kufikisha huduma katika nyumba 500 zilizopo Mikocheni na nyingine 500 za Mbezi Beach jijini hapa. Zaidi ya nyumba 200 zilizopo eneo la Medeli mkoani Dodoma nazo zimo kwenye mpango, baadaye huduma hii itaendelea kusambazwa nchi nzima.”

Amebainisha kuwa uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ni wa gharama kubwa, lakini shirikia hilo litaendelea kufanya kila liwezalo kuwafikia Watanzania wote kwa kuboresha mtandao wa simu na intaneti kwa gharama nafuu.

Mkuu wa Ufundi wa shirika hilo, Cecil Francis amesema muda wa majaribio ya mradi huo ni miezi mitatu kisha huduma hiyo itaanza kutolewa katika majiji yote ya Tanzania Bara pamoja na Unguja katika awamu ya kwanza.

“Awamu ya kwanza inatarajia kugharimu kati ya Dola 15 milioni za Marekani (zaidi ya Sh33 bilioni) hadi Dola 20 milioni (zaidi ya Sh44 bilioni). Utekelezaji wake tayari umeanza tangu Februari Mosi na baada ya siku 90 tutaendelea na maeneo mengine tulivyoyapa kipaumbele,” amesema Francis.

CHANZO:MWANANCHI

My Take:
CCM katika ilani yake ya uchaguzi 2015-2020 ilahidi kuongeza idadi ya watumiaji wa internet. Suala hili limetajwa katika ilani ya Ccm ukurasa wa 80 kipengele J.

(j) Kuongeza idadi ya watumiaji mitandao (internet)
kutoka milioni 9.0 mwaka 2015 hadi kufikia milioni
20.0 mwaka 2020.[B\]
Wakati wenzao wameshafikia majumba ya watu wirelessly.
Hao jamaa sijui nani anawashauri
 
ADSL imewashinda ndio fiber wataweza poor services wafanyakazi mamwinyi ukipata fault wanasolve baada ya wiki 5
 
Kutakuwa na bundle lenu linaitwa NOGESHA, litakuwa linaanza saa Tisa na nusu usiku mpaka saa 12 alfajiri. Gharama zake itakuwa jero kwa wiki, yaani buku 2 kwa mwezi.
😀😀😀
 
Hivi wangeweka kwenye minara tu

Hayo mengine sijui itakuwaje
Fibre kwa bei hiyo hatari sana
 
TTCL kutumia Sh44 bilioni kusambaza intaneti
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linatarajia kutumia Sh44.7 bilioni kusambaza intaneti ya kasi kubwa hadi majumbani kupitia huduma mpya iitwayo Fiber Connect Bundle.
IN SUMMARY

  • Kupitia huduma hiyo mteja atapata intaneti ya kasi isiyo na ukomo kwa gharama ya kuanzia Sh100,000 hadi Sh200,000 kwa mwezi.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linatarajia kutumia Sh44.7 bilioni kusambaza intaneti ya kasi kubwa hadi majumbani kupitia huduma mpya iitwayo Fiber Connect Bundle.

Hayo yamebainishwa leo, Jumanne Februari 27, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Waziri Kindamba aliyebainisha kuwa kupitia huduma hiyo mteja atapata intaneti ya kasi isiyo na ukomo kwa gharama ya kuanzia Sh100,000 hadi Sh200,000 kwa mwezi.

“Pia, atapata simu ya mezani bure yenye huduma ya wifi pamoja na muda wa maongezi bure na kadi ya simu,” amesema Kindamba.

“Kwa kuanzia mradi huu, tunatarajia kufikisha huduma katika nyumba 500 zilizopo Mikocheni na nyingine 500 za Mbezi Beach jijini hapa. Zaidi ya nyumba 200 zilizopo eneo la Medeli mkoani Dodoma nazo zimo kwenye mpango, baadaye huduma hii itaendelea kusambazwa nchi nzima.”

Amebainisha kuwa uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ni wa gharama kubwa, lakini shirikia hilo litaendelea kufanya kila liwezalo kuwafikia Watanzania wote kwa kuboresha mtandao wa simu na intaneti kwa gharama nafuu.

Mkuu wa Ufundi wa shirika hilo, Cecil Francis amesema muda wa majaribio ya mradi huo ni miezi mitatu kisha huduma hiyo itaanza kutolewa katika majiji yote ya Tanzania Bara pamoja na Unguja katika awamu ya kwanza.

“Awamu ya kwanza inatarajia kugharimu kati ya Dola 15 milioni za Marekani (zaidi ya Sh33 bilioni) hadi Dola 20 milioni (zaidi ya Sh44 bilioni). Utekelezaji wake tayari umeanza tangu Februari Mosi na baada ya siku 90 tutaendelea na maeneo mengine tulivyoyapa kipaumbele,” amesema Francis.

CHANZO:MWANANCHI

My Take:
CCM katika ilani yake ya uchaguzi 2015-2020 ilahidi kuongeza idadi ya watumiaji wa internet. Suala hili limetajwa katika ilani ya Ccm ukurasa wa 80 kipengele J.

(j) Kuongeza idadi ya watumiaji mitandao (internet)
kutoka milioni 9.0 mwaka 2015 hadi kufikia milioni
20.0 mwaka 2020.[B\]
Haya ma internet cable tena kutoka kampuni ya serikali sio ya kuipendelea sana maana siku mkizingua maandamano wanazima tu...
 
Unakuja mbio kama vile ahadi ni ktu cha ajabu ndani ya serekali ya ccm. Ukija hapa ukumbuke kuna ahadi ya 50m@kijiji na bado haijatekelezwa. Tuliahidiwa kwamba gas ikifika Dar itasambazwa majumbani, lakini hii leo wala hakuna anayethubutu kuongelea hilo. Hivyo ukija hapa jukwaani uwe makini.

NB: Nje ya mada, tulikubaliana ikifika mwisho wa mwezi wa tatu utaleta maendeleo ya ujenzi wa viwanda kila mkoa na mahali hivyo viwanda vilipo kila mkoa ili tukajionee wenyewe. Kumbuka ni viwanda 100 kila mkoa. Nakukumbusha huu ni mwisho wa mwezi wa pili. Hakikisha unaanza kukusanya taarifa hizo za awali kwa wakuu wa wilaya na mikoa kwani kuna watu makini tunafuatilia. Hapa ndio tutaanza kujua mwelekeo halisi wa awamu hii ya tano.
Hahaha....!!! Mie naomba nipite tu na kwakuwa naishi kijijini nilizingoja sana hizo chenji bado sijaziona.

Back
Top Bottom