Tsh Milioni 225 zimetolewa na Serikali Kuu Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu Jimbo la Manonga, Igunga, Tabora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

MHE. SEIF GULAMALI: "MILIONI 225 KWA AJILI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU JIMBO LA MANONGA, TABORA

Mbunge wa Jimbo la Manonga, Mhe. Seif Khamis Gulamali amesema kuwa tayari wamepokea fedha Shilingi Milioni 225,000,000/= kutoka Serikali Kuu za Ujenzi wa Nyumba za Waalimu na kukamilisha Maboma.

1. KATA YA USWAYA, Chalamo Shule ya Msingi imepokea Milioni 50,000,000/= Ujenzi wa nyumba ya Mwalimu

2. KATA YA IGOWEKO, Selegei Shule ya Msingi imepokea Milioni 50,000,000/= Ujenzi wa nyumba ya Mwalimu

3. KATA YA CHOMA, Shule ya Msingi Chamalendi imepokea Milioni 25,000,000/= Ukamilishaji boma la vyumba 2 Madarasa lililojengwa Nguvu za wanachi

4. Shule ya Msingi Chibiso imepokea Milioni 25,000,000/= Ukamilishaji wa Boma la vyumba2 Madarasa lililojengwa na Mbunge na wananchi

5. KATA YA MWASHIKU, Shule ya Msingi Matinje imepokea Milioni 25,000,000/= Ukamilishaji wa boma la vyumba 2 vya madarasa lililojengwa na Wawekezaji MASHILI LTD

6. KATA YA SUNGWIZI, Shule ya Msingi Sungwizi imepokea Milioni 25,000,000/= Ukamilishaji wa Vyumba 2 vya madarasa vilivyojengwa na Fedha ya mapato ya Minara ya simu na nguvu za wananchi

7. Shule ya Msingi Ncheli imepokea Milioni 25,000,000/= Ukamilishaji wa vyumba 2vya Madarasa vilivyojengwa na Mbunge na wananchi

Aidha, Mhe. Seif Khamis Gulamali amesema, Daraja la Mto Mazila Kijiji cha Mwina Kata ya Igoweko Ujenzi wake unaendelea hatua kwa Hatua na kusema ni imani yake wanakwenda Kutatua changamoto ya Barabara hii ambayo inaenda Simbo na Inaenda Kata ya Igunga.

Mhe. Seif Khamis Gulamali ametoa Shukurani kwa Serikali ya Rais wa JMT, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kuendeleza Kuwapatia fedha ili kutatua changamoto za wananchi wa Jimbo la Manonga, Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora.

WhatsApp Image 2023-04-07 at 18.56.17.jpeg

WhatsApp Image 2023-04-07 at 18.56.18.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom