Trump anajuta na kulia kuhusu Iran

Trump anajuta na kulia kuhusu Iran

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,698
Reaction score
7,884

Mashambulizi ya Iran yamejeruhi takriban wanajeshi 100 ndani ya wiki mbili - Pentagon​

f

Chanzo cha picha,Getty Images
Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, imesema takriban wanajeshi 100 wa Marekani wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Iran ndani ya kipindi cha wiki mbili zilizopita, hali inayoashiria kuongezeka kwa mvutano kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa mujibu wa Pentagon, majeruhi wengi walitokana na mashambulizi yaliyolenga vituo vya kijeshi vya Marekani katika Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, wizara hiyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu aina au ukubwa wa majeraha waliyoyapata wanajeshi hao.

Awali, Pentagon ilithibitisha kuwa wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa katika mashambulizi yaliyoihusisha Iran.
Taarifa hiyo inakuja baada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran, IRGC, kutangaza kufanya mashambulizi katika maeneo ya Bahrain, Kuwait na Jordan, ambapo baadhi yake yalisababisha vifo vya wanajeshi watatu wa Marekani.
 
Back
Top Bottom