True story kumhusu ndugu yangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

True story kumhusu ndugu yangu.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Judgement, Jan 29, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mpendwa my fellow Jf membar, awali ya yote nakuomba unipe macho na maskio na uvumilivu wako uisome hii story.
  Kwa kuyahifadhi majina halisi ya wahusika, nitatumia majina ya kubandika.
  Mzee Karama alikua muhamiaji hapa Tanzania katika miaka ya 70"s. Hakua raia wa nchi hii.
  Alikuja Tz kwa dhumuni la kutafuta maisha.
  Akiwa hapa nchini, Mz. Karama alikutana na Shangazi yangu wakapendana na hatimae ndoa.
  Maisha yao yaliwapatia watoto wa 5 kati ya hao wa kike watatu na wa kiume wawili.
  Mfuatano wao mtoto wa kwanza hadi wa tatu wa kike ndiyo walifuatana na wa4 na wa5 walimalizia uzao.
  Katika miaka ya 80"s Mz. Karama aliihamisha familia yake yote kwao, nchi aliyotoka.
  Kuanzia Shangazi na watoto wote, mistake aliyofanya Mz Karama ni kutofanya utaratibu kisheria kwa kanuni za uhamiaji za uraia wa familia yake, kwakua watu wa familia yake hawakutambulika katika nchi hiyo.
  Hivyo familia ya Mz Karama ikawa inaishi kinyume na sheria.
  Mwaka mmoja kupita tangu wahamie Shangazi yangu akafariki na akazikwa hukohuko.
  Miezi 6 kupita tokea shangazi afe, binti wa kwanza Riza akaolewa, na mume aliemuoa Riza nae hakua raia wa nchi hiyo waliohamia, alikua ni raia toka nchi jirani na hiyo.
  Hivyo baada ya kuolewa Riza alihamia huko kwa mumewe, ambako alikumbana na maisha magumu kwani shughuli ya mumewe ilikua ni kilimo, ufugaji na kwa kua palikua ni kijijini sana miundo mbinu ilikua ya shida, vitu kama utafutaji kuni maji ndiyo ilikua changamoto kwa Riza.
  Kwenye mji wa Mz Karama wakabaki Bebiy na Mariyamu na wale wa kiume wadogo.
  Katika story hii niliyemlenga ni Bebiy bint wa 3 kuzaliwa.
  Babiy alipata kibarua Super market, alifanya kazi kiujaujanja siku akisikia fununu ya msako wa wahamiaji haramu hatoki.
  Kwa kua Bebiy alikua ni makini na capacity yake ya uelewa pale kazini, muda si muda akapewa usupervisor.
  Hilo liliwauma baadhi ya staff wenzake, na kati ya staff wale mmojawao waliishi jirani, na alikua akiijua familia ya Karama haina uhalali wa uraia.
  Huyo jirani yake staff alimchoma Bebiy kwa maofisa uhamiaji, na Bebiy akakamatwa na polisi, badae kotini kisha Prison.
  Bebiy alihukumiwa jela miaka miwili, kule gerezani akakuta mpango ni kila room wafungwa wawili,
  chumba alichopangiwa Bebiy alimkuta mdada ambae alikua ana mtoto mdogo wa kiume wa mikononi. Kama ilivyo kawaida wakaanza kuulizana haya na yale, kwanza wakajikuta wote wanaongea kiswahili.
  Kumbe na yule mdada nae kosa alilofungiwa, ni kosa kama la Bebiy la uraia, ni bahati ilioje ufungwe nchi ya mbali na ukutane na mfungwa mwenzio mnaongea lugha moja ?.
  Yule mdada alimwambia Bebiy yeye na mme wake walihamia hapo wakitokea Zanzibar, na walihamia bila kanuni za sheria.
  Na tangu akamatwe mumewe imebidi atorokee kwenye miji mingine tofauti na huo.
  Wiki mbili baada ya hapo mdada akaanza kuumwa, kuumwa kukazidi ikalazimu kitengo cha magonjwa hapo prison kimpeleke hospitali kubwa nje ya gereza.
  Mdada yule kabla hajapelekwa hosp alimkabidhi Bebiy mtoto, akavua Herini, Bangili, Mkufu, vyote vya dhahabu na kijikaratasi chenye No ya simu ya mumewe Baba wa huyo mtoto aliekua akiitwa J.
  Akiwa analengwa machozi mama J alimwambia Bebiy kwamba hategemei kurudi gerezani akiwa hai. (namnukuu)
  "Ndg yangu Bebiy nakuachia mtoto nakuachia na rasilimali kidogo Mungu alizoniwezesha kua nazo, mlee huyo mtoto awe mwanao, sina namna nyingine ya kufanya ukijaaliwa kumaliza kifungo jaribu kumtafuta Babaake J , anaitwa Mr. Tiba, na kwa tatizo lolote la mtoto ama ataugua au vinginevyo unaweza ukauza chochote katika hivyo vipuli vitakusaidia mbele ya safari." (mwisho kunukuu)
  wote machozi yakawamwagika mama J, akachukuliwa na gari ya jela na kupelekwa hosp na kupita siku 3 mama J akafariki, habari zikafika gerezani za msiba Bebiy akalia sana na akashukuru Mungu.
  Mwaka mmoja, baadae askari mmoja wa gereza akaanza kumtongoza Bebiy huku akimuhadaa kua akiwa atamkubalia basi anao uwezo wa kumfanyia mpango Bebiy akatoka jela kwa kupitia misamaha ya kiongozi wa nchi.
  Bebiy hakuyumbishwa na hilo, alimkatalia huyo askari mzee mpango wake.
  Bebiy alikomaa akamaliza kifungo chake.
  Na wakati Bebiy anaingia gerezani palikua na form ya kujaza ambapo ktk hiyo form kuna kipengele cha kujaza uraia wako unatoka nchi gani.
  Bebiy alijaza anatoka ile nchi jirani alipoolewa dadaake Riza, hivyo siku amemaliza kifungo alipakiwa kwenye gari la serikali hadi nchi ile ya jirani, akiwa na mwanae J aliyempata jela, ikumbukwe miezi mi3 nyuma kabla Bebiy hajamaliza kifungo Mz Karama alifariki.
  Bebiy baada kubatwa hapo kilichoanza kumsaidia No ya simu ya dadaake Maryamu alikua nayo kichwani, hivyo alitafuta duka la sonara akauza bangili moja, kisha akatafuta callbox na kumpigia kumpa habarize.
  Then akamuomba Mariyamu ampe No za simu za Riza, akapewa na akampigia Riza.
  Haikua rahisi Bebiy kufika huko kwani palikua ni umbali (kama Mtwara na Bukoba).
  Ilimlazimu Bebiy kubadili magari ma3 kumfikisha huko. NITAENDELEA N
   
 2. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,849
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ngoja Kwanza Nikale.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,215
  Likes Received: 1,625
  Trophy Points: 280
  Story yenyewe ngumu kuifuatilia it is too anonymous! Ungekuwa uantaja nchi za mfano manake mara nchi jirani, mara nchi rafiki ya jirani ya Riza! Kha! Na mie nimeskia njaa sasa!
   
 4. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtoto gerezani?sijaelewa kwanini hakumuacha kwa baba'ke?.ngoja nikale
   
 5. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 493
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hadithi nzuri sana naomba uimalizie muda huu tafadhali.
   
 6. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 4,285
  Likes Received: 1,194
  Trophy Points: 280
  kwani inaruhusiwa kuingia jela na vipuri sio unaandikisha ndo unaviacha ili ukitoka upewe?
   
 7. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  mtafute Lizzy,nae mtunzi mzuri sana atakushauri namna ya kuandika!!yaani nimesoma mpk kichwa kinawaka moto kama ukuta unakwaruzwa na bati
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,293
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Duh mpaka nasinzia...
   
 9. M

  Madodi Senior Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 181
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  jamaan naombwni panadol nimeze ili niendelee na kusoma hii hadithi
   
 10. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,168
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa Tz huruhusiwi lakn kwa wenzetu hatujui may be wanaruhusu.
   
 11. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  story nzuri, we tutajie tu izo nchi hatutawatafuta hao ndugu zako
   
 12. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kwa sheria ya Tanzania inawezakua hairuhusiwi , bt kwa nchi nyingine kama hiyo ni ruhusa.
   
 13. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nchi waliozaliwa ni Tanzania, wakahamia Jeddah (S. Arabia) na nchi aliyoolewa Riza ni Yemen.
   
 14. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,272
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  taja nchi basi ata za uongo,afu fanya haraka umalizie.lakini,kwani uyo bebii alishindwa nini kurudi bongo baada ya kifungo?
   
 15. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mh. Baba wa mtoto alitoroka kukamatwa. Na mtt anaenyonya kifuani always hua attached na mama yake hakuna mama m'badala labda mama mzazi afe. Aidha storty nimeifupisha kutokana na kuokoa tym ya wasomaji, palifanyika taratibu za kisheria kufikia Bebiy kupewa atone power ya kuondoka na mtt ambae hakua wake.
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,929
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  Stori inaonesha kuwa hata Mzee Karama aliwapeleka nchi ambayo alikuwa ni mgeni pia. Kwa hayo majina, na jinsi nnavyozijuwa nchi za Kiarabu (nakisia ni nchi za Kiarabu kwa majina). Nnavyoizijuwa nchi za Kiarabu ni kuwa, ikiwa kweli Mzee Karama hapo alipowapeleka hao watoto na yeye ni kwao basi wasingekuwa wageni hata kidogo na wasingeishi kwa kujificha.

  Waarabu wana kitu kinaitwa "Sheikh" au Mzee wa kabila na hao hawakubali damu yao ipotee na ihangaike kama ni kweli mtu wa hapo. Mifano hai mingi sana tunayo ya watu wa Yemen na Oman ambao ndio wengi walihamia hapa Tanzania.

  Oman katika miaka ya 70s na 80s walikuwa na Sheikh wao hapo msikitini kwao kitumbini, ambae ilikuwa ukitaka kwenda Oman, hata kama hujazaliwa huko bali wazee wako walikuwa na asili yahuko hata iwe ni mababu wa tano, mradi una "tree" ya ukoo, basi walikuwa wanakufanyia facilities za kukupeleka, nawajua wengi sana waliokwenda kwa njia hii.

  Yemen, hawa mpaka leo ukienda ubalozini kwao kkwa kutaka kwenda huko, kama una asili ya huko wanakuambia uende kwa watu waliowafanya kama ma "sheikh" wao hapa Tanzania, wao kwa kuwa wameshakuwa wenyeji hapa Tanzania na maarufu, kama hawakujui, basi wataulizia watu tofauti wa asili yao na wakisha hakikisha ni kweli una asili ya huko basi watakufanyia urahisi katika hiyo safari.

  Sasa Judgement kama majina yao unayaficha basi hata majina ya nchi waliokwenda? Ukitaja majina tunaweza kukupa ushauri ni nini wafanye kama bado wanahitaji msaada. Wengine inakuwa ni hawaelewi tu baadhi ya mambo yanakuwaje ndio hufikia kuwa na matatizo yasiyo kuwepo.

  Labda ungetaja majina ya nchi ili tusasambuwe hadithi yako.

  Nawajua baadhi ya Watanzania wasio na asili ya Oman lakini wamepata Uraia wa huko kupitia hawa ma "sheikh" kwa kusaidiwa tu.

  Ukitaka kujuwa jinsi Yemen kabila na hawa wazee zinavyofanya kazi, muulize Jabiri Shikamkono, "Mola Dawila". Kama anapitia humu anaelewa nnachokisema.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,929
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  Si unaona hapo, nna uhakika huyo Mzee Karama , hapo Saudia alikuwa si kwao, nae alikuwa ni muhamiaji haramu.

  Msaudi hususan mwenye asli ya Jiddah, hawezi kabisa kuhangaika, wao wana "system" ya "Umdah" ambae huyo mzee angekuwa ana asili ya hapo, lazima angemjuwa Umda wake na huyo Umdah asingekubali kabisa apate taabu.

  Kati ya Watanzania nnao wajua wenye asili ya Jiddah ni kina Jidawi (wa Zanzibari), hawa ni ukoo maarufu sana Zanzibar na hakuna asiyewajua, ingawa wamechanganya damu "nadhani na wangazija" na watoto wengine wameolewa na kuoa makabila tofauti, lakini asili yao ni watu wa Jiddah na ndio maana wanaitwa "Jidawi". Hawa hata waende leo Ubalozini wakaoneshe roots za na family tree, basi watafanyiwa kila kitu chao kiwe sahali na watapokelewa kwa mikono miwili.

  Nna uhakika Mzee Karama alikuwa ni illegal immigrant hapo Jeddah, Saudi Arabia.

  Kama bado wapo Saudia na wanahitaji msaada wowote hapo, tafadhali ni PM ntakujulisha wafanye nini na waonane na nani.
   
 18. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  uko juu sana FF,nikiwa na shida kama hizo lazima nikutafute.
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,929
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  Huyo hakukaa Jela kama mfungwa, huyo alikaa jela ya "deportation" ya wahamiaji haram, ambao wenyewe huita "tarhil" (deportation) na kuchelewa kwake ilikuwa ni kukosa nauli na au kutokujuwa asafirishwe wapi mpaka alipoamuwa apelekwe Yemen. "illegal Immigrants hawana hukumu ya kufungwa, huwa wanawekwa kungoja safari na ndio maana akakutana na "illegal immigrant" mwingine humo ndani.

  Na angekuwa na nauli na amesha amuwa wapi kwao, basi hapo asingekaa hata kidogo.
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,929
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  Anytime, nimeishi sana nchi za Kiarabu, karibu zile nchi za Gulf zote, kuanzia Yemen, Oman, Saudia, Kuwait, UAE, Qatar, Bahrain na zingine nimezitembea sana. Gozi lilikuwa "consultant" la mambo ya telecommunications huko, kwa hiyo alikuwa ana hamahama sana hizo nchi kutokana na shughuli zake, na mimi karibu hizo nchi zote nimefanya kazi, zingine part time zingine full time.

  Hapo Jeddah anapopasema nilishawahi kuwa "part time" mkalimani wa hizo sehemu za kusafirishia "illegal immigrants" kwa hiyo kwa kesi kama yake nnaijuwa sana.
   
Loading...